Kwenye gazeti la Mwananchi la jana Jumatano tarehe 05/12/2012 kuna habari zinahohusu Uchaguzi wa kuziba nafasi ya wazi kwa Mwenyekiti wa Kjiji cha Igima Kata ya Igima Tarafa ya Mdandu huko Njombe. Katika uchaguzi huu Mgombea wa Chadema ndugu Haruna Mligo alipata kura 471 dhidi ya 393 za mgombea wa CCM ndugu Jelly Jombe. Kwa matokeo hayo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho ndugu Zakayo Matimbwe alimtangaza Mligo (Chadema) kuwa mshindi wa Uenyekiti wa serikali ya kijiji.
Hata hivyo siku moja kabla ya uchaguzi usiku wa Manane Katibu mwenezi wa CCM Kata ya Igima ndugu Titus Kiswaga (pichani) alikula kichapo cha nguvu baada ya kukutwa akifanya kampeni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi (kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi). Hata hivyo kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Njombe ndugu Alatanga Nyagawa a.k.a lutondwe (ni member wa JF) akiongea na vyombo vya habari anasema Mr Kiswaga alipigwa baada ya kufumaniwa na Mke wa mtu.
Ajabu ni kwamba CCM wanataka kutumia tukio hili ili kupora ushindi huo wa Chadema. Kwa kushirikiana na Polisi Njombe wamemtaka Mwenyekiti Mteule (ambaye hajaapishwa) awatafute wote waliohusika na tukio hili la kupigwa kwa Kiswaga na kuwakabidhi kwa polisi. Wana JF na wadau wengine wa demokrasia tupige kelele kuhusu ubakaji huu wa demokrasia unaotaka kufanyika.