CCM wafanya Mizengwe kwenye ushindi wa CHADEMA Kijiji cha Igima-Wanging'ombe

Polisi wanadhulumu kupita upeo. Mimi ninaijua fika kesi ya mjane ambae mpangaji wake kavunja sheria. Polisi wakapokea hongo nzuri kwa mpangaji wakamchukua mjane na kumweka rumande sasa ni miezi mitano inapita. Watoto wake ni wadogo wanazunguka mtaa bila mama wala baba. Wanalia machozi ya damu usiku na mchana kwani wanajua mama yao hana kosa lolote lile. Kama una ndugu yako polisi mshauri angaalie sana penye mjane na yatima kwani hata Biblia inasema hao usiwaguse. Maadili ya mtanzania yanashuka kwa kasi kubwa. Viongozi wetu na vyombo vya usalama wamegeuka wezi, wanyang'anyi, na wauaji wakubwa. Tujiulize tangu lini m/kiti mteule wa kijiji akageuka kuwa polisi? Tumemsahau Nyerere na maadili mema aliyoijengea Tanzania. Tumemkaribisha shetani nyumbani kwetu na sasa tunavuna matunda ya kazi yeke.
 
Back
Top Bottom