CCM wafanya Mizengwe kwenye ushindi wa CHADEMA Kijiji cha Igima-Wanging'ombe

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,928
2,000
Kwenye gazeti la Mwananchi la jana Jumatano tarehe 05/12/2012 kuna habari zinahohusu Uchaguzi wa kuziba nafasi ya wazi kwa Mwenyekiti wa Kjiji cha Igima Kata ya Igima Tarafa ya Mdandu huko Njombe. Katika uchaguzi huu Mgombea wa Chadema ndugu Haruna Mligo alipata kura 471 dhidi ya 393 za mgombea wa CCM ndugu Jelly Jombe. Kwa matokeo hayo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho ndugu Zakayo Matimbwe alimtangaza Mligo (Chadema) kuwa mshindi wa Uenyekiti wa serikali ya kijiji.

Hata hivyo siku moja kabla ya uchaguzi usiku wa Manane Katibu mwenezi wa CCM Kata ya Igima ndugu Titus Kiswaga (pichani) alikula kichapo cha nguvu baada ya kukutwa akifanya kampeni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi (kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi). Hata hivyo kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Njombe ndugu Alatanga Nyagawa a.k.a lutondwe (ni member wa JF) akiongea na vyombo vya habari anasema Mr Kiswaga alipigwa baada ya kufumaniwa na Mke wa mtu.

Ajabu ni kwamba CCM wanataka kutumia tukio hili ili kupora ushindi huo wa Chadema. Kwa kushirikiana na Polisi Njombe wamemtaka Mwenyekiti Mteule (ambaye hajaapishwa) awatafute wote waliohusika na tukio hili la kupigwa kwa Kiswaga na kuwakabidhi kwa polisi. Wana JF na wadau wengine wa demokrasia tupige kelele kuhusu ubakaji huu wa demokrasia unaotaka kufanyika.
 
Zimamoto

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
464
195
Kazi ya kutafuta wahalifu si ya mwenyekiti bali ni ya polisi. Wafanye kazi yao ya msingi na si kila siku kuua tu raia wasiokuwa na hatia.
 
Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,195
Kwenye gazeti la Mwananchi la jana Jumatano tarehe 05/12/2012 kuna habari zinahohusu Uchaguzi wa kuziba nafasi ya wazi kwa Mwenyekiti wa Kjiji cha Igima Kata ya Igima Tarafa ya Mdandu huko Njombe. Katika uchaguzi huu Mgombea wa Chadema ndugu Haruna Mligo alipata kura 471 dhidi ya 393 za mgombea wa CCM ndugu Jelly Jombe. Kwa matokeo hayo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho ndugu Zakayo Matimbwe alimtangaza Mligo (Chadema) kuwa mshindi wa Uenyekiti wa serikali ya kijiji.

Hata hivyo siku moja kabla ya uchaguzi usiku wa Manane Katibu mwenezi wa CCM Kata ya Igima ndugu Titus Kiswaga (pichani) alikula kichapo cha nguvu baada ya kukutwa akifanya kampeni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi (kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi). Hata hivyo kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Njombe ndugu Alatanga Nyagawa a.k.a lutondwe (ni member wa JF) akiongea na vyombo vya habari anasema Mr Kiswaga alipigwa baada ya kufumaniwa na Mke wa mtu.

Ajabu ni kwamba CCM wanataka kutumia tukio hili ili kupora ushindi huo wa Chadema. Kwa kushirikiana na Polisi Njombe wamemtaka Mwenyekiti Mteule (ambaye hajaapishwa) awatafute wote waliohusika na tukio hili la kupigwa kwa Kiswaga na kuwakabidhi kwa polisi. Wana JF na wadau wengine wa demokrasia tupige kelele kuhusu ubakaji huu wa demokrasia unaotaka kufanyika.

Mkuu Wangingombe si ndio kwa 'MKOMBOZI WA CCM" PHILIPO MANGULA au. Sasa kama watu wameanza Kuadabisha Nyumbani kwake kweli huyu Atamudu Mziki wa Mageuzi kweli?
 
sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
0
Hiyo haiingilian na ushindi kabisaa,nawala polisi hawana ubavu wa kutengua ispokua mahakama na wawe na ushahid wa kutosha.cdm wahuko msiwe nahofu chamachetu kinaongozwa na wanao ogopwa na magamba na tunaijua sheria na magamba wanatutegemea kwa msaada wa sheria.lasilimali watu tunayo magamba tulisha washika muda sana simnaona wanacheza mziki wetu?eti nao wana andamana nakaz yakuwaletea maendeleo hawaifany wanatumia kod zetu kujifichia
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,928
2,000
Mkuu Wangingombe si ndio kwa 'MKOMBOZI WA CCM" PHILIPO MANGULA au. Sasa kama watu wameanza Kuadabisha Nyumbani kwake kweli huyu Atamudu Mziki wa Mageuzi kweli?
Ni kijiji kama cha 3 hivi toka nyumbani kwa Mangula Imalinyi. Ni mwendo wa saa 1 tu kwa miguu
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,774
2,000
Yeye atawajuaje wakati yeye alikuwa mgombea hivi CCM hawana wanalofikiri
 
nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,956
2,000
Dah! Chadema wanaitesa sana ccm..mi sishangai hayo mambo kuku anapochinjwa lazima apaparike, kama anachinjwa na anakaa kimya hata anayemchinja atakosa raha make atahisi pengine amechinja kibudu, na kibudu hakiliwi..raha ya kui hinja ccm ni huko kuchanganyikiwa kwao baadae wataanza kuelewa kwamba ze kantry is slowly but fast silipingi awei from zea hands
 
Wile GAMBA

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
1,809
0
kuishia kupiga kelele kwenye mitandao hakuta saidi inabidi tupige hatua mbele ili wajue tumechoka na tabia zao chafu!
 
  • Thanks
Reactions: SG8

EMMANUEL NSAMBI

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
402
195
Mimi nawashangaa hapa Polisi.Kwani aliyesema kwamba jamaa amepigwa na watu wa chadema si wao?Si ina maana
wanawafahamu?
 
Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,124
2,000
Wameambiwa wafanye siasa wasitegemee vyombo vya dola lakini hawasikii.

...kusikia kwa KENGENGE(CCM) ni hadi atokwe na damu masikioni...na safari hii CDM tumeamua kupiga mbwa na mfugaji wake na tutamlizia kwa kuchoma kibanda 2014/2015...
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,794
2,000
Hivi hadi hapo bado tu kuna jeshi la polisi Tanzania? Si afadhali wabaki sungusungu tu? Kutafuta wahalifu kunamhusu nini raia? Alikuwa kwenye tukio? Huko ni kushindwa kwa serikali ya ccm.
 
Apr 3, 2012
30
0
Kwenye gazeti la Mwananchi la jana Jumatano tarehe 05/12/2012 kuna habari zinahohusu Uchaguzi wa kuziba nafasi ya wazi kwa Mwenyekiti wa Kjiji cha Igima Kata ya Igima Tarafa ya Mdandu huko Njombe. Katika uchaguzi huu Mgombea wa Chadema ndugu Haruna Mligo alipata kura 471 dhidi ya 393 za mgombea wa CCM ndugu Jelly Jombe. Kwa matokeo hayo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho ndugu Zakayo Matimbwe alimtangaza Mligo (Chadema) kuwa mshindi wa Uenyekiti wa serikali ya kijiji.

Hata hivyo siku moja kabla ya uchaguzi usiku wa Manane Katibu mwenezi wa CCM Kata ya Igima ndugu Titus Kiswaga (pichani) alikula kichapo cha nguvu baada ya kukutwa akifanya kampeni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi (kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi). Hata hivyo kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Njombe ndugu Alatanga Nyagawa a.k.a lutondwe (ni member wa JF) akiongea na vyombo vya habari anasema Mr Kiswaga alipigwa baada ya kufumaniwa na Mke wa mtu.

Ajabu ni kwamba CCM wanataka kutumia tukio hili ili kupora ushindi huo wa Chadema. Kwa kushirikiana na Polisi Njombe wamemtaka Mwenyekiti Mteule (ambaye hajaapishwa) awatafute wote waliohusika na tukio hili la kupigwa kwa Kiswaga na kuwakabidhi kwa polisi. Wana JF na wadau wengine wa demokrasia tupige kelele kuhusu ubakaji huu wa demokrasia unaotaka kufanyika.

Hii ni kali kweli kweli , hao ndio polisi wa Tanzania bana, aibu tupu!!! Sasa m/kiti wa watu anahusikaje na kupigwa kwa mpenda wake za watu!? polisi waache longolongo, wanataka kesi iende mahakamani mara tusikie mshindi amenyang'anywa ushindi.uchaguzi na kufumaniwa havina mahusiano, polisi wamwulize huyo Kiswaga awaonyeshe mwenye mke, hapa hakuna kumumunya maneno bana,hawa CCM na wake za watu nyakati za uchaguzi! ni hatari sana.
Hata kule Igunga mafumanizi yalikuwa hayo hayo.Siku ya uchaguzi itabidi tuweke ulinzi kwa wake zetu dhidi ya ccm.Wasipoacha hilo litabia watazidi kupoteza mvuto na ramani katika jamii.
 
chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,942
2,000
Hapo ndo tutauona uadilifu wa Mangula au naye ndo yule eeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, nyaishozi wanamuita Sosi
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
1,500
Kiswaga anafuata nyayo za Mwigulu Nchemba. Bahati mbaya Kiswaga yeye hakuwa na fuko la pesa la kuzima soooo!
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Inamaana hata ccm wale wa ngazi ya kata hawataki kushindwa? inamaana hii nchi imeoza basi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom