CCM tawi la Marekani, swali dogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM tawi la Marekani, swali dogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaCCM, Oct 14, 2010.

 1. M

  MwanaCCM Senior Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwenu TAWI LA CCM-MAREKANI,

  Natambua wapo baadhi ya watu hapa JF ambao ni wana CCM katika tawi la Marekani.

  Naomba kuuliza swali langu dogo kuhusu TAWI LA CCM-MAREKANI.

  Hili tawi la CCM-MAREKANI ni la watu wa Houston tuu? Kwasababu sikujua hata kuwa kuna tawi la CCM hapa USA mpaka juzi mshikaji wangu akaniambia anaenda kwenye mkutano. Cha kushangaza hakuna watu wengine wa state nyingine wanaofahamu kuhusu hili tawi.

  Sasa cha kushangaza zaidi nikauliza kuhusu viongozi, eti viongozi wote pia nao wanakaa HOUSTON, halafu washikaji.

  SWALI LANGU NI HILI:

  HIKI NI CHAMA CHA CCM-HOUSTON AU MAREKANI ZIMA?

  Kwasababu huwezi kusema TAWI LA CCM-MAREKANI kama wanachama wengi wa CCM-USA hawajui hata kama kuna TAWI. Sijawahi ona sehemu yoyote kuna tangazo limewekwa hata kusema kuna mkutano au tunachangua viongozi.

  Mimi ni mwanachama wa CCM ila sitambui kiongozi wa CCM-MAREKANI hata mmoja na siwajui. Na najua watu wengine pia watakubali hili swala. Kama hicho chama kweli kina NIA ya kujumuisha wanachama wa CCM-MAREKANI kwanini tusiwe na viongozi state zingine pia? Huu mimi naita ubinafsi wa madaraka.

  Naomba wote tushirikiane sio kuwa na ubinafsi wa madaraka na kuweka washikaji wote wawe viongozi.

  CCM JUU, JUU ZAIDI

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
   
 2. M

  Mboko JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kidumu kwako na sio kwa wote.

  Nasikitika sana kuona ati watu wanaandika oooh ufunguzi wa Tawi la CCM hovyo,i hate to hear that.Nahisi watu kama nyie ndo baba zenu Mafisadi na kama si hivyo kuna kitu ndo maana kila leo oooh tunawatangazia ufunguzi wa Tawi la CCM somewhere mimi mwenyewe nimechoka na watu kama nyie na CCM yenu yaani mpaka mwaka huu nyie bado tu na CCM.

  Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka
   
 3. Azadirachta

  Azadirachta Senior Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani mzee wa Vermont anahusika na hili!
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  Swali la kijinga.
   
 5. M

  MwanaCCM Senior Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe unayesema hii ni mada ya kijinga, sasa kutukana kwako kunasaidia nini? Na kama ni mada ya kijinga kwanini upotenze hata muda wako kujibu hapa. Ni swali nimeuliza na nataka jibu, KUULIZA SI UJINGA AU?
   
 6. M

  MwanaCCM Senior Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa umetukana umeambulia nini au umefurahi? Jamani ni swali tuu au na wewe ni hao watu wa Houston kwenye hicho chama. JAMIIFORUMS ni sehemu ambayo mtu yoyote anaweza weka hoja kama umeuzika nenda kwenye mada nyingine sio lazima usome hii.
   
 7. M

  MwanaCCM Senior Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama watu wa jamii forum wamepokea hii mada na kuweka humu basi ni ya maana na kuna watu wanataka jua kama huoni umaana wake potea wewe.
   
 8. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Umetumwa na Miraji wewe si bure.
   
 9. M

  MwanaCCM Senior Member

  #9
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  . Acha majungu kama unashida zako binafsi na huyo miraji mufate. Who is miraji anyways? Jibu swali acha longolongo.
   
 10. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good job!
  Vote CCM
  Vote JK
  Can't wait for the CCM victory night party at the embassy in DC!!
  We gonna party all night:A S thumbs_up:
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  WENZIO HUKO WALITOKA NA WAKO KWENYE GHILIBA MPYA ZA:-

  Mwenzetu "MWANA CCM" hawa mafisadi walikupotezea wapi maana yaelekea hizo sera zao mpya hata huna habari zao..........POLE SANA
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Enyi mliojaaliwa na mnaofaidi matunda ya uhuru peke yenu kwa kuwa mmepata nafasi za kiupendeleo kwenda huko marekani na kwingineko, sisi huku nyumbani tumekichoka hucho chama na tuna mpango wa kukimwaga mwaka huu.

  Wakati nyie mnakula kuku huko marekani na kusoma ktk mavyuo ya nguvu sisi huku tunakula mlo mmoja na watoto wetu wanakaa chini ktk shule zisizo na maticha. Mafisadi wametukaba koo kila kona kupata fedha za kuwasomeshea nyie watoto zao huko marekani.

  Endelezeni tawi lenu huko lakini mkirudi mjue kabisa tumeishajanjaruka na hamtapata fursa mlizoahidiwa za kuendeleza ukolono mamboleo, ukoloni mbaya sana wa mwafrika dhidi ya mwafrika mwenzie.
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mko marekani then mnashbikia Ccm. Tulidhani mngekuwa na uzalalendo kidogo kwa hawa maskini mlioacha huko chini udhalimu wa hiyo Ccm yenu
   
 14. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hili ndilo tatizo kubwa limalotukabili sisi wanaadam. Sikatai kuwa Mwenyezimungu katuumba na kitu kinaitwa kusahau. Ila sijawahi kuona mtu aliewahi kusahau Kuendesha baiskeli hata kama atakaa miaka 100 bila kuiendesha ila siku ikiipatia nafasi hatakua hata ktk level ya ulena ila atakua rider mzuri tu.....

  hapa Nyumbani CCM wanajivunia kwa kujenga shule za kata, so far mgombea urais wa CCM kesha ahidi Meli nne na Pantoni ""(Piga hesabu Meli nne zaweza somesha wanafunzi wangapi)"" sijui ngapi kwa wananchi wanaokaa karibu na maziwa au vivuko..... na ni hivi juzi tu kaahidi nyingine huko Ziwa Nyasa. lakini kumbuka nchi hii elimu bado ni duni kuanzia shule hizo za kata mpk vyuo vikuu. Shule za msingi za vijijini hali bado ni mbaya kuanzaia kimazingira mpk kielimu hapa namaanisha kuwa na walimu wa kutosha na vitabu vya ziada na kiada.....Pamoja na msaada wanaopata toka kwa makapuni ya simu kama Zain, Tigo na Vodacom lakini bado hali ni mbaya...

  Mnaweza kuona ni sawa koz ubalozi wa TZ marekani unang'aa sana lakini usiende mbali tazama na ofisi za serikali ya TZ pale Holili na Tarakea then fananisha na za Kenya pale pale utagundua kuwa Upo nje ya nchi....Hili ni dogo ukilinganisha na jamaa anavyowabeba wale ambao ni mafisadi na hata baadhi yao wana kesi ila anawaita swafi... Hapa wanaandaa kitu gani mara baada ya kuitwaa nchi?????

  Rudia kusoma matukio ya Richmond, Radar, Ndege ya Rais, Mikataba ya Madini, EPA(Kagoda), Deep Green NK....Then fanya maamuzi sahihi si kwa kujiangalia wewe unaekaa upepo unapovuma ila kutuangalia sisi tuokaa na wezi wanaotutambia, sisi tunaoteseka kwa ajali za mara kwa mara, sisi tunaotumia 6hrs kwenda na kurudi kutoka kazini.......

  Sikulazimishi kuchagua chama ila nakuomba ufanye maamuzi sahihi koz unajua kabisa hicho ni chama cha Kibinafsi thus why u r not in the loop......THINK...................
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Azadirachta, nadhani ulimaanisha Mt.Vernon ni mahali poa kwa wabongo wengi wana ushirikiano sana watu wa hapo na mpaka kuna wazee wetu pale, ila pia kuna aina tatu za hawa wana CCM wa matawi ya ughaibuni.
  1. CCM Damu- ni kundi la wana CCM ambao wanaipenda CCM kwa dhati, ni watoto wa viongozi, wamezaliwa CCM na hata liwake jua, inyeshe mvua, hawataiacha CCM kamwe na watafia CCM.
  3. Wafaidika-hili ni kundi la wale wanaofaidika na uwepo wa CCM madarakani, wanaipenda CCM just for convenience kwa sababu CCM imewafikisha hapo walipo, hawa sio commited sana, wengi ni wafanya biashara, watatumia fedha zao kuifadhili CCM sio kwa sababu wanaipenda sana, bali kulinda status quo zao, CCM ikipigwa chini, convenience inaisha, wataitosa.
  3.Waganga njaa- Hawa ndio kundi kubwa zaidilikijumuisha ma loosers kibao ambao wanaikumbatia CCM wakitafuta opportunities za kutokea, hawa wanachoipendea CCM ni njaa zao tuu, CCM ikipigwa chini, wataachia ngazi na utaanza kusikia matawi ya Chadema ughaibuni.
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  unfortunately hii imetoka kwako mtu ambaye kidogo nilikuwa nadhani unaweza kuvumilia tofauti za kisiasa, nina swali dogo tu kwako,unaweza kuniambia wewe upo kwenye kundi gani kati ya hayo(kwenye whatever political view uliyonayo)?
   
 17. M

  MwanaCCM Senior Member

  #17
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe Burn ukokundi gani? Mimi niko la kwanza.
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya sifiti kwenye hizo kategorizi za Pasco, hilo la kwanza pia si baya kwani kuzaliwa na wazee wa CCM ni bahati, fikiria ungekuwa ni mtoto wa mzee wa CHADEMA maana ungerithi ubishi, matusi, vitisho na kumiliki madanguro.
   
 19. M

  MwanaCCM Senior Member

  #19
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 5, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi sio mtoto wa fisadi au kigogo bali nawatu wangu ndani ya chama
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Safi unajuana na watu wa maana hivi fikiria ungekuwa na watu wako CHADEMA, ingekuwa ni mtu kama marando aliyetayari kutoa kitu chochote kwa pesa.
   
Loading...