Mkuu MwanaCCM,
JF si kama ipo against CCM, wanaokufyatukia ni watanzania wenzako. Unatakiwa kuelewa watu wetu (watanzania wenzetu) walivyo, sisi pamoja na kuwapa uhuru wa kujadili mijadala anuai hatupendi kuwaingilia sana.
Tunaheshimu sana mtizamo wako na swali lako naamini umelileta kwakuwa unahitaji kupata msaada.
Kuna watu waliochangia kwa namna ya kukukatisha tamaa na wengine wakikwambia ONDOKA. Tunakushauri USIWASIKILIZE, aidha tumeifuta michango yao na tunasikitika kwa hilo kwani si msimamo wetu. JF si mali ya CCM wala CHADEMA. Hivi ni vyama vya siasa tena ambavyo wakati wowote kimojawapo kinaweza kuchukua dola na kingine kikawa cha upinzani wakati wowote kulingana na wapiga kura wanavyoamua kila baada ya miaka mitano.
ONYO (kwa baadhi ya watu):
IKOME mara moja tabia ya kuwa mnamnukuu mtu na kuandika neno moja CRAP, hii ni dharau ya wazi, haipendezi na si uungwana kwa nchi yetu Tanzania. Kama huna hoja ya kujibu hoja flani kaa kimya au nenda hoja nyingine ambayo unaamini unaweza kujibu au kushiriki kikamilifu. Si lazima kuongeza idadi ya posts kama hazimsaidii mtu zaidi ya kufurahisha genge tu.
IKOME tabia ya kuwambia watu walio na mtizamo tofauti na wako kuwa WAMETUMWA au WAONDOKE; kama wao wametumwa wewe hujatumwa? Kwanini uwambie waondoke? Uliwakaribisha wewe? Ni tabia ambazo tunaona zinaanza kuota mizizi, hatutavumilia hali hii, si ya kiungwana hata chembe, hata kama ni unazi ni kuvidhalilisha vyama mnavyoshabikia vionekane vinaungwa mkono na watu wasiopenda kukosolewa!