CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Ndugu wanajamvi,

Katika hotuba yake ndani ya Bunge la Katiba mjini Dodoma hivi karibuni, Rais Kikwete, pamoja na mengineyo, alinukuliwa akisema kwamba – muungano wa serikali tatu uliopendekezwa katika rasimu ya katiba haufai kwa kuwa ni ‘mfumo legevu na utawaongezea wananchi mzigo’. Rais Kikwete pia alienda mbali na kueleza kwamba:

Sisi katika Chama Cha Mapinduzi, tunaamini mfumo wa Serikai Mbili, ndio murua na rahisi kutekelezeka.

Hapa Rais Kikwete alikuwa akimaanisha mfumo wa serikali mbili ambao CCM imesema “itauboresha”, kama njia ya kuondoa kero za muungano zilizodumu kwa zaidi ya miaka 30. Kufuatia hotuba hii ya Rais Bungeni, huu ukawa ndio msingi wa hoja za kile kilichoitwa “Maoni Ya Wengi” ndani ya bunge maalum la Katiba. Na ni msimamo huu wa “Maoni ya Wengi” ambao pia ukapelekea upande mwingine wa hoja, ulioitwa “Maoni ya Wachache”, hatimaye kuamua kujiondoa katika bunge hili, chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa nia ya kwenda kuwaeleza wananchi jinsi gani waliojiita “wengi” bungeni walivyoamua kupuuza maoni ya wananchi kuhusiana na rasimu ya katiba.’

Kama tutakavyojadili, Muungano wa Serikali Mbili “Zilzoboreshwa”, kama unavyopigiwa kampeni na CCM, hautaimarisha Muungano na hautamaliza malalamiko, lawama na shutuma za kero za Muungano. Badala yake, Serikali mbili “zilizoboreshwa”, zitavunja na kuuzika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mjadala wetu umegawanyika katika sehemu kuu tatu.

Sehemu ya kwanza tutajadili:
· Muundo Wa Serikali.
· Madaraka ya Viongozi.
· Muundo Wa Bunge.

Hapa tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa yataenda kuvunja muungano.

Sehemu ya pili tutajadili:
· Mapato na Matumizi Ya Kuendesha Muungano.
· Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mikopo, na Misaada.
· Mapendekezo ya Baraza la Mapinduzi kuhusu masuala ya kuyaondoa katika Orodha ya mambo ya Muungano.

Vile vile, tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili “zilizoboreshwa” yataishia kuvunja muungano.

Na Sehemu ya TATU tutajadili:
· Sheria Za Ndani na Nje ya Muungano.
· Mgongano wa Kikatiba.
· Kuzinduka kwa Utaifa kwa pande zote mbili za Muungano (Tanganyika na Zanzibar). Muungano.

Hapa pia tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili “zilizoboreshwa” yataenda kuvunja muungano.


SEHEMU YA KWANZA

MUUNDO WA SERIKALI, MADARAKA YA VIONGOZI NA MUUNDO WA BUNGE

Katika hotuba yake bungeni, Rais Kikwete aliwahimiza wajumbe wa Bunge la Katiba juu ya umuhimu wa kuwaenzi Waasisi wa Muungano (Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume), kwa vile wao ‘walitaka na walituachia mfumo wa serikali mbili’. Wanaojiita “Maoni Ya Walio Wengi” Bungeni, ambao wanapigia chepuo mfumo wa serikali mbili “zilizoboreshwa” wanafahamu kwamba – muundo wa muungano ulioachwa na waasisi wetu ulikuwa ni ‘muungano wa NCHI MOJA, yenye SERIKALI MBILI. Zanzibar ilikuwa ni SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO. Hiyo ndio hali ya Muungano ambayo Mwalimu Nyerere alipofariki kumi na tano iliyopita. Leo hii Zanzibar sio tu kwamba tayari imeshaondoa mambo mengi ya msingi juu ya “muungano”, bali pia, kwa mujibu wa marekebisho ya kumi ya Katiba (2010), Zanzibar haitambuliwi tena kama ni “sehemu” ya muungano, bali inatambulika (Kikatiba) kama “nchi kamili”, yenye bendera yake, wimbo wake wa taifa, na amiri jeshi mkuu.

Pamoja na Muungano sasa kuwa na Nchi MBILI, SERIKALI MBILI, CCM bado inasema kwamba serikali mbili hizi “zitaziboreshwa”, huku chama kikipendekeza kwamba – katika katiba ijayo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano (ambae leo hii ni Dr. Bilal), anyang’anywe mamlaka aliyokuwa nayo ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, na badala yake, mamlaka hayo yahamie kwa Rais wa nchi jirani ya “Zanzibar”. Kwa maana nyingine, chini ya serikali mbili “zilizoboreshwa” na CCM, Rais wa nchi jirani ya “Zanzibar” atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa Rais wa Muungano kwa masuala ya Zanzibar, lakini pia atakuwa ni mmoja wa viongozi wakuu wa nchi (Tanzania). CCM haisemi lolote kuhusu kiongozi atakayekuwa msaidizi wa Rais wa Muungano katika masuala ya Tanganyika (ukipenda, sema - Tanzania Bara).

Mkataba wa Muungano (1964) uliweka utaratibu ambao – Rais wa Muungano wa NCHI Moja, alikuwa na wasaidi wake wakuu wawili – Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar (Marehemu Karume), na Makamu wa Pili wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika (Marehemu Kawawa).

Chini ya Katiba Mpya, CCM inapendekeza kwamba – Rais wa Zanzibar afanywe kuwa Makamu wa Rais wa Muungano bila ya kujalisha Rais wa Muungano anatokea upande upi wa Muungano. Kwa kufanya hivyo, CCM inadai kwamba – hali hii itamwongezea Rais wa Zanzibar - “madaraka na hadhi” ndani ya serikali ya Muungano na pia nje ya nchi.
MGOGORO UTAKAOJITOKEZA KUTOKANA NA MAPENDEKEZO YA RAIS WA ZANZIBAR KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

Chini ya mfumo huu wa serikali mbili “zilizoboreshwa”, CCM haisemi iwapo Rais ni mmoja - yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano, ni kiongozi gani ndiye atakayesimamia Mawaziri watakaokuwa wanasimamia mambo ya Tanzania Bara katika mfumo huu wa serikali mbili “ulioboreshwa”. Pamoja na kuendelea kupigia debe serikali mbili “zitakazoboreshwa”, CCM bado imeendelea kukaa kimya juu ya ufafanuzi wa masuala muhimu (kiutekelezaji), kwa mfano, - katika mazingira ya Zanzibar kuwa ni “nchi” kamili, yenye “mamlaka” kamili, ikitokea kwamba Rais wa Muungano anatokea upande wa pili wa muungano (Zanzibar), JE:

· Rais huyu kutoka nchi jirani ya “Zanzibar” atasimamia masuala yasiyo ya muungano - ya upande unaoitwa “Tanzania Bara”, ndani ya Jamhuri ya Muungano, kwa mamlaka yepi?

· Iwapo Rais wa Muungano atatokea panapoitwa “Tanzania Bara”, Rais huyu wa Muungano atakuwa na mamlaka yepi ya kusimamia mambo ya “Tanzania Bara” wakati yeye atakuwa amechaguliwa na wananchi wa pande zote mbili za muungano?

· Zipo wapi ‘pande mbili’ za muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika?

CCM haina muda wa kutoa majibu kwa maswali haya muhimu. Kutokana na hali hii, serikali mbili “zilizoboreshwa”, hazitaboresha muungano bali zitajenga mazingira ya kuvunja muungano. Hii ni kwa sababu:

Tuseme Rais wa Muungano anatokea upande wa nchi jirani ya “Zanzibar”, ambaye chini ya mfumo wa serikali mbili ambao CCM inadai utakuwa “umeboreshwa”, Rais wa Zanzibar pia atakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM inapendekeza kuwa iwe hivyo bila ya kujali Rais wa Muungano atatokea upande upi wa Muungano. Kitakachotokea ni kwamba - siku moja, Rais wa Muungano na Makamu Wa Rais Wa Muungano, wote watakuwa wametokea nchi jirani ya “Zanzibar”. Kwa maana hii, inachokifanya CCM, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, CCM inaweka mazingira ambayo Zanzibar hawataweza tena kutoa Rais wa Muungano. Hii ni kwa sababu:

Kama tulivyoona, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Rais wa Zanzibar “automatically”, atakuwa pia ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM ikimsimamisha mgombea Urais wa Muungano kutokea nchi jirani ya “Zanzibar”, nchi ambayo pia automatically itatoa makamu wa Rais wa Muungano, chini ya mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, wapiga kura kutoka upande wa inayoitwa “Tanzania Bara”, upande ambao una wapiga kura zaidi ya 90% ya wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano, wengi ya wapiga kura hawa kutoka “Tanzania Bara”, hawatakubali kumchagua mgombea wa urais (CCM) kutokea nchi ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake pia anatokea huko huko “nchini” Zanzibar. Madhara yake ni yepi?

Ni kwamba – chini ya mfumo wa Serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Zanzibar ianze kusahau kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitachofuatia ni Zanzibar kuanza kulalamika kwamba wanabaguliwa, wanonewa, wananyimwa haki ndani ya Jamhuri ya muungano, kwahiyo waachwe “Wapumue”. And interestingly enough, watakaongoza katika kutoa hoja hizi ni wale wale wazanzibari ambao Islaml Jusa alisema kwamba walipofika Dodoma “Waliufyata”. Ni wale wale ambao leo wanapinga kwamba wao sio “wasaka tonge”. Katika kundi hili, hatutashangaa kuja kuona viongozi kama Balozi Seif Iddi, Mohamed Seif Khatib, Hamad Rashid Mohamed, na wengine wakija unga mkono hoja hii. Hatujui bado, lakini haitashangaza! Hali hii haitadumisha au kuboresha Muungano bali itauvunja Muungano.

Kwa upande wa inayoitwa “Tanzania Bara”, iwapo Mgombea Urais wa Muungano atatokea nchi jirani ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake “automatically” pia atatokea Zanzibar, watakaoongoza katika kupinga hali hii haitakuwa watu wengine bali wale wale makada wa CCM ambao leo ndani ya bunge la katiba wanajiita “Maoni ya Walio Wengi”, wanaotetea mfumo huu huu wa serikali mbili “zilizoboreshwa”. Fitina zilizomkumba Dr. Salim Ahmed Salim 2005 hazitafua dafu kwa fitina zitakazojitokeza katika mazingira tunayojadili hapa. Wana CCM ambao watakuwa katika makundi ya kutafuta Rais wa Muungano wataendesha kampeni kubwa kupinga uongozi wa Muungano kwenda kwa “nchi jirani katika kofia zote mbili za juu – Rais wa Muungano na Makamu wa Rais wa Muungano.

Aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya, wanachoambiwa Wazanziri na CCM ni kwamba - chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa, Wazanzibari wajiandae kuwa ni “wasindikizaji” tu wa Uongozi katika Jamhuri ya Muungano. Pia CCM nayo ijiandae kutupiwa lawama na malalamiko mapya juu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar. Mbegu ya kuvunjika kwa muungano itaanza kuchepuka.


Inaendelea bandiko linalofuatia…

cc - Nguruvi3, @FJM,@ tpaul, @Mag3, @JokaKuu, @Mwigulu Nchemba, @Nape Nnauye, @MwanaDiwani,@zomba, @Ritz, @ZeMarcopolo, @Gamba la Nyoka, @Mtanganyika , @Mzee Mwanakijiji, @Pasco, @Kitila Mkumbo, @EMT, @MTAZAMO, @Kobello,@Jasusi, @zumbemkuu, @Mimibaba, @Zakumi, @Invisible, Tumaini Makene, @Yericko Nyerere, @FaizaFoxy, @Dingswayo, @Makusudically, @Tumaini Makene, @Nicholas, @Mtu wa Pwani, @jmushi1, @Mwita Maranya, @Ngongo, @zumbemkuu, Zitto, @Mzawa Halisi, Barubaru, Mindi, Kiganyi, @Communist, Dr. F. Ndungulile, Ezekiel Maige, Anna Tibaijuka, HKigwangalla, candidscope, tpaul, Tetty, TIMING, chama
 
Last edited by a moderator:
MUUNDO WA BUNGE

Katika maboresho yake ya serikali mbili, CCM inapendekeza kuwepo Kwa MABUNGE MATATU (chini ya serikali mbili), kwa kuongeza Bunge la tatu litakaloitwa "Baraza La Wawakilishi la Tanzania Bara". Jukumu la chombo hiki litakuwa ni kusimamia masuala ya Tanzania Bara pekee, tofauti na sasa ambapo masuala haya yanasimamiwa na Bunge la Muungano ambalo, wabunge kutoka nchini jirani ya Zanzibar pia ni sehemu ya bunge hili la Muungano. CCM inapendekeza kwamba – wakati Bunge la Muungano litakapo kuwa linajadili mambo ya muungano, wabunge wote – kutoka Tanzania Bara na nchi jirani ya Zanzibar, watashiriki katika majadiliano. Lakini pale mijadala juu ya masuala ya Tanzania bara pekee itakapoanza, wabunge kutoka Zanzibar hawataruhusiwa kushiriki katika mijadala hiyo. Kwa maana nyingine, mijadala juu ya "Tanzania Bara" itakapoanza ndnai ya Bunge, hii itawapa Wabunge kutoka nchi jirani ya Zanzibar, fursa ya - nikiazima maneno ya Nguruvi3, "KUTALII".

Lipo suala lingine muhimu katika kile CCM inachokiita "maboresho ya serikali mbili". Bunge la Muungano litakuwa na Spika na Naibu Spika. Spika atatokea sehemu moja ya muungano, na naibu wake atatokea sehemu ya pili ya muungano. CCM inapendekeza kwamba wakati wa vikao vinavyohusu mambo ya Tanzania bara, Spika au Naibu Spika atakayetokea Tanzania Bara ndiye atakaye endesha kikao hicho.

MGOGORO UTAKAOJITOKEZA

Utaratibu huu wa kuanzisha Baraza la Wawakilishi la Tanzania Bara ambalo litasimamia masuala ya Tanzania bara, hautatekelezeka chini ya mfumo wa Serikali Mbili zitakazo boreshwa na CCM. Hii ni kwa sababu, kitendo cha kuwazuia wabunge kutoka wa Zanzibar kushiriki mijadala isiyohusu masuala ya muungano ni kutengeneza mgogoro mwingine mkubwa. Hii ni kwa sababu:

  • Chini ya mfumo wa serikali mbili ulioboreshwa, HAKUNA MAMBO YA TANZANIA BARA PEKEE YAKE. Badala yake, Yapo MAMBO YA ZANZIBAR, NA MAMBO YA MUUNGANO. Basi!.

Chini ya serikali mbili, wananchi wa Tanzania Bara wasahau kuwa na chombo kitakacho wawakilisha kwa dhati – yani Bunge. Hii ni kwa sababu, chini ya kitakachoitwa "Bunge la Tanzania Bara/Baraza la wawakilishi la Tanzania Bara", maamuzi ya bunge hili yanayohusu mambo ya Tanzania Bara hayatakuwa na Serikali ya kuyasimamia au kuyatekeleza. Badala yake, utekelezaji wake utayeyuka ndani ya serikali ya muungano na kupoteza fedha nyingi sana za walipa kodi. Hali hii itazua migogoro mikubwa ndani ya muungano kwa sababu uwepo wa "Bunge la Tanzania Bara" bila ya "Serikali Ya Tanzania Bara", maana yake ni kwamba hakuna mtu au chombo chochote ambacho kitawajibika/wajibishwa moja kwa moja iwapo yale yanayopitishwa au yanayoamulia na bunge la Tanzania Bara, hayatatekelezwa!

CCM kuwaanzishia wananchi wa TANZANIA BARA lao kwa maana ya - "Bunge la Tanzania Bara" bila ya kuwaanzishia Serikali ya Kufanya kazi na Bunge hili kutawafungua akili na macho wananchi wa Tanzania bara juu ya nini ambacho watetezi wa serikali tatu walikuwa wanakijengea hoja. Hali hii itapelekea wananchi wengi wa "Tanzania Bara" kuanza kudai serikali yao ya Tanganyika (ukipenda, ita Tanzania Bara). Hii ni kwa sababu, hata kupitia elimu zao za sekondari, elimu ambayo sasa imeanza kutambulika kama ni Elimu Ya Msingi kwa kwa wananchi wote, elimu waliyopata na ambayo inaendelea hata leo ni kwamba - Duniani kote, BUNGE ni moja ya mihimili mikuu mitatu ya dola, mihimili mingine miwili ikiwa ni SERIKALI NA MAHAKAMA. Wananchi wa Tanzania Bara wataanza kuhoji - kwanini tuna Bunge la Tanzania Bara lisilokuwa na Serikali yake? Maamuzi wa bunge hili kwa maana ya sera mbalimbali za maendeleo zinasimamiwa na nani? Hapo ndio wataanza kuelewa Profesa Lipumba alikuwa anamaanisha nini aliposema bungeni kwamba – kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la DFID la Uingereza, 35% ya fedha zinazotengwa katika bajeti ya muungano kila mwaka wa fedha, hazifanyi kitu chochote cha maana kwa wananchi. Kwa maana nyingine, fedha hizi hazileti ufanisi wowote katika uchumi kutokana na mfumo mbovu wa utawala.

BARAZA LA MAWAZIRI

Kama tulivyojadili, chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa, CCM inataka kuleta Mabunge mawili ndani ya bunge la Muungano: (1) Bunge la Muungano na (2) Bunge la Tanzania Bara. Bunge la kwanza (la Muungano) litajumuisha wabunge kutoka Tanzania bara na wale kutoka nchi jirani ya Zanzibar ambao watakuwa wanajadili masuala ya muungano, Bunge la pili (Bunge la Tanzania Bara) ni lile ambalo pale majadiliano juu ya masuala ya Tanzania bara peke yake yatakapoanza, wabunge kutoka nchi jirani ya Zanzibar wataruhusiwa kwenda kutalii au hata kurudi nchini kwao kwa muda.

Mabunge mawili ndani ya Bunge la Muungano ni jambo ambalo halitekelezeki. Hii ni kwa sababu, bunge la Tanzania Bara halitakuwa na maana yoyote bila ya uwepo wa baraza lake la mawaziri pamoja na kiongozi wake wa serikali (bila ya kujalisha kiongozi huyu ataitwa Rais, Waziri Mkuu, Gavana, n.k). CCM haitoi ufafanuzi katika maboresho haya ya serikali mbili, wale Mawaziri wa "Tanzania Bara" ambao hawatokuwa Mawaziri wa Muungano, wakati wa vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili masuala ya Muungano, Mawaziri hawa wasiokuwa wa muungano watakuwa na nafasi gani katika baraza hilo la mawaziri wa muungano.

Pia CCM haitoi ufafanuzi kwamba ikiwa Muungano utakuwa na Rais mmoja, ni kiongozi gani atakaye kuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri watakaosimamia mambo ya Tanzania bara. Vile vile, ikitokea Rais wa Muungano atatokea nchi jirani ya Zanzibar, CCM haitoi maelezo Rais huyu atasimamia masuala ya Tanzania bara kwa mamlaka yepi. Pia, iwapo Rais wa Muungano atatokea upande wa Tanzania Bara, CCM haielezi Rais huyu atasimamia masuala ya Tanzania Bara (yasiyo ya Muungano) kwa mamlaka yepi wakati atakuwa amechaguliwa na pande zote mbili za Muungano - wananchi wa Tanzania Bara na Wananchi wa nchi jirani ya "Zanzibar".

Maswali kama haya majibu yake yapo wazi kabisa katika rasimu ya Katiba, rasimu ambayo CCM inaipinga. Ni vigumu kuelewa kwanini CCM haoini kwamba "haiwezekani pakawa na pande mbili za muungano bila ya uwepo wa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. CCM kuendelea kukataa uhalisia huu, ni kuweka mazingira ya kuvunja muungano, sio kuboresha muungano, hata kama CCM itaziboresha "serikali mbili" kwa kiasi gani.

Inaendelea bandiko linalofuatia...
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA PILI

· Mapato na Matumizi Ya Kuendesha Muungano.
· Mambo ya Nje, Mikopo na Misaada.
· Zanzibar na Mamlaka Kamili.

SUALA LA VYANZO VYA MAPATO

Moja ya sehemu muhimu za maboresho ya serikali mbili za CCM inahusisha kufunguliwa kwa "Akaunti ya pamoja" ya fedha zitokanazo na mapato ya vyanzo vya muungano. CCM inapendekeza uwekwe utaratibu wa kisheria utakaotekeleza uendeshaji wa akaunti hiyo na kuweka mgawanyo wa mapato kwa pande mbili za muungano. Hili ni jambo gumu kutekelezeka chini ya serikali mbili hata kama "zitaboreshwa" namna gani. Ndiyo maana, pamoja na hiyo "Akaunti ya pamoja" kufunguliwa karibia miaka ishirini (20) iliyopita, bado malalamiko juu ya suala la mgawanyo wa mapato yapo pale pale. Hata katika hotuba yake kuadhimisha miaka 50 ya muungano, Rais Kikwete amekiri kwamba kero hii bado haijapatiwa ufumbuzi.

CCM inatakiwa itoea majibu kwa swali kwamba:

  • Chini ya Serikali Mbili, mapato ya muungano yatatokea wapi wakati hakuna chombo cha kusimamia mapato ya aina hiyo kwa "Tanzania Bara"?
Kilichopo chini ya serikali mbili ni: Mapato ya Muungano (Tanganyika na Zanzibar) chini ya TRA, na mapato ya Zanzibar (chini ya ZRA). Kwisha!.


MGOGORO UTAKAOJITOKEZA CHINI YA SERIKALI MBILI ZILIZOBORESHWA

Chini ya mfumo huu, kutazuka mgogoro ambapo wananchi wa "Tanzania bara" wataanza kuzuia nchi jirani ya Zanzibar, isiwe inatumia fedha zisizo ihusu.Wananchi wa upande wa Zanzibar, nao pia wataendelea kulalamika kwamba wanadhulumiwa mapato yao. Yote haya ni kwa sababu, chini ya mfumo wa serikali mbli, hakuna chombo cha kusimamia mapato ya Tanzania Bara ambacho kitatenganisha mapato ya Muungano, na Mapato Ya Tanzania Bara. Chombo hiki hakiwezi kupatikana kwa vile CCM imekataa kuunda serikali itayayosimamia mapato haya - Serikali ya Tanganyika(ukipenda, iite serikali ya Tanzania Bara). Hatima ya mgogoro huu ni kuvunjika kwa muungano.

SUALA LA MATUMIZI

Chini ya Serikali mbili "zilizoboreshwa", matumizi ya rasilimali za muungano, mchango wa shughuli za muungano, mgawanyo wa mapato ya muungano na mchango wa Zanzibar katika masuala ya muungano, yote haya yataendelea kuwa masuala tata. Hii ni kwa sababu, mfumo huu utaendeleza uwepo wa "wizara mchanganyiko" zinazoghughulikia mambo ya muungano na yale ambayo yataendelea kuitwa "mambo yasiyo ya muungano". Tuchukulie mfano wa Wizara ya
Elimu. Wizara hii sio ya Muungano (kwa maana ya elimu ya msingi na sekondari ni masuala ya Tanzania Bara pekee). Lakini pia suala la elimu ya juu, hili ni la Muungano, na linasimamiwa na wizara hii hii ambayo sio ya Muungano. Mfano mwingine ni wa – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Wizara hii ni ya Muungano, lakini ni wazi kwamba jeshi la kujenga taifa (JKT), hili sio suala la muungano bali ni la Tanzania Bara peke yake. Zanzibar pia wana kitengo kinachofanana na hiki cha Tanzania bara ambacho wanakiita "jeshi la kujenga uchumi" (JKU), lakini pia hivi sasa, Zanzibar ina vikosi vyake vya ulinzi ambavyo Rais wa Zanzibar ndiye amiri jeshi mkuu.

MGOGORO UTAKAOJITOKEZA

Tukichukulia tu suala la ‘Ulinzi", chini ya mfumo wa serikali mbili ulioboreshwa, wapiganaji wetu watakuwa na kazi ya ziada na isiyowahusu – kulinda mipaka ya nchi jirani ya Zanzibar kwa gharama za walipa kodi wa Tanganyika. Vile vile, wapiganaji wetu wataendelea kumpigia Rais wa Jamhuri ya Muungano "mizinga" kila atakapokuwa nchi ya jirani (Zanzibar), huku pia wakiendelea kufanya hivyo Rais wa Muungano anaporudi kwake "Tanzania Bara". Hii ni kazi nyingine ya ziada kwa wapiganaji wetu. Hivi karibuni, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba (Jaji Warioba), amenukuliwa akisema kwamba tume ilipokea maoni kutoka kwa wapiganaji wetu kwamba ‘wamechoka' kumpigia Rais wa Muungano "mizinga", pande zote mbili za muungano. Bila ya uangalifu, ipo siku wapiganaji wetu wataanza kulalamikia juu ya ugumu wa kulinda mpaka wetu na nchi ya jirani ya "Zanzibar" kutokana na sababu mbali mbali zitakazotokana na Zanzibar kuzidi kupata mamlaka kamili. Majeshi yetu yakifikia hatua hii, serikali mbili hazitaboresha Muungano, bali zitavunja muungano.

CCM haielezi chini ya serikali mbili "zilizoboreshwa", mambo yasiyo ya muungano yatasimamiwa na serikali gani, hasa MAENDELEO YA UCHUMI maendeleo ya uchumi. Chini ya Serikali mbili, hakuna chombo cha kusimamia mambo yasiyo ya muungano. Kila suala ambalo halihusiani na Zanzibar litaendelea kuwa ni suala la muungano, bila ya kujalisha kama suala hilo ni la Tanzania Bara peke yake.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977) inaeleza wazi kwamba serikali ya muungano ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia mambo yoye ya muungano na mambo yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanzania Bara. Kwa maana hii, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa, Serikali ya Muungano itaendelea kusimamia sekta za Uchumi, Elimu, Maji, Afya, Kilimo, Ujenzi, Nishati, Maliasili na utalii, uchukuzi, n.k. Hata kama Zanzibar itaruhusiwa Kukopa na kufanya mipango yake ya maendeleo, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa, utekelezaji wake kwa Zanzibar utakuwa bado utajaa utata. Hii ni kwa sababu, Zanzibar itaendelea kuwa chini ya Tanzania bara ambayo itakuwa imevaa koti la muungano. Ni muhimu kwa Zanzibar kufahamu kwamba - hakuna mazingaombwe yatakayo wachomoa kwenye utawala wa Tanzania bara chini ya serikali mbili, hata kama CCM itaziboresha Serikali hizi mbili kwa kiwango gani.


Inaendelea…
 
MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, MIKOPO, MISAADA, ORODHA YA MAMBO MENGINE YASIYO YA MUUNGANO KWA ZANZIBAR

Awali, tulijadili kwamba hata Zanzibar ikiruhusiwa kukopa, bado suala la maendeleo ya UCHUMI kwa Zanzibar litakuwa na utata chini ya mfumo wa serikali mbili. Tulisema kwamba hii inatokana na Katiba ya JMT (1977) kutamka kwamba serikali ya muungano ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia mambo yoye ya muungano na mambo yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanzania Bara. Kwahiyo, hata kama Zanzibar itaruhusiwa Kukopa na kufanya mipango yake ya maendeleo, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa, utekelezaji wake kwa Zanzibar utakuwa bado ni wa shida kwa sababu Zanzibar itaendelea kuwa chini ya Tanzania bara ambayo itakuwa imevaa koti la muungano ikiendelea kusimamia Maendeleo Ya Uchumi.

Mwaka 2004, Baraza La Mapinduzi Zanzibar lilitoa Ripoti yake juu ya matatizo na kero za muungano na kuweka utaratibu wa kuziondoa (2004). Chini ya ripoti hii, Zanzibar inaelekeza serikali ya muungano kuondoa katika mambo ya muungano masuala yafuatayo: Mafuta na gesi asilia, elimu ya juu, posta mawasiliano, biashara za nje, ushuru wa bidhaa, takwimu, utafiti, ushirikiano wa kimataifa, leseni za viwanda, bandari, usafiri wa anga, polisi na usalama wa taifa.

Vile vile. Zanzibar wanataka kuruhusiwa kujiunga na mashirika ya kimataifa kama vile OIC, Benki ya Dunia, IMF, n.k. Kwa mujibu wa mapendekezo ya CCM, Serikali mbili zilizoboreshwa zitairuhusu Zanzibar kujiunga na OIC.

MGOGORO UTAKAOJITOKEZA

Mengi ya masuala haya ambayo Zanzibar inataka yaondolewe katika orodha ya mambo ya muungano, ndiyo masuala hayo hayo ambayo Rais Kikwete katika hotuba yake Bungeni alikaririwa akisema kwamba chama chake (CCM) "hawana matatizo nayo". Kutokuwa na matatizo juu ya masuala haya ndio kitu ambacho CCM inaita "Maboresho ya Serikali Mbili".


  • Lakini nani asiyeona kwamba kuruhusu Zanzibar kuwa na mamlaka kamili katika maeneo ya – Posta, mawasiliano, takwimu, usafiri wa anga, utafiti, uteuzi wa mabalozi wa nje, polisi na usalama wa taifa, ni kuiruhusu Zanzibar kujiondoa katika muungano?
  • Zanzibar wakipewa mamlaka juu ya masuala haya, watakuwa na "motivation" gani ya kuendelea kuwa chini ya mfumo mbovu wa "Serikali Mbili" ambao kwa miaka 50 wamekuwa wakilalamika kwamba hauwatendei haki?
  • Nani asiyeona kwamba kuwapa Zanzibar mamlaka kamili katika maeneo haya chini ya serikali mbili ni kuchochea kuni wa moto wa madai ya upande wa Tanzania Bara kutaka nao wapate serikali yao kamili ya "Tanganyika" (ukipenda, ita Tanzania Bara)?

Serikali mbili zilizoboreshwa pia zinalenga kuruhusu Zanzibar kuwa na sarafu yake huko mbeleni. Lakini ukweli unabakia wazi kwamba:

  • Haiwezekani Zanzibar ikaunda sarafu yake halafu bado ikaona haja ya kuwa ndani ya muungano;
  • Haiwezekani Zanzibar ikawa na benki kuu yake (Central Bank) halafu bado ikaona haja ya kuwa kwenye muungano;
  • Zanzibar yenye mamlaka kamili kujiunga na jumuiya za kimataifa au kujifunga na mikataba mingine ya kimataifa, haitaona umuhimu wa kubakia katika muungano;

Hii ni kwa sababu, masuala yote haya ndio nguzo kuu za Muungano wowote ule. Ukiondoa masuala yote haya, muungano hauta kuwa na maana tena. Kuipa Zanzibar mamlaka kamili juu masuala haya na kusema ni maboresho ya serikali mbli hakutaimarisha muungano kama CCM inavyodai, bali kutavunja muungano. Hii ni kwa sababu - Katika hali ya sasa, Muungano unashikiliwa na Zanzibar. Muungano haushikiliwi na Tanzania Bara kwa sababu haipo kama Tanzania Bara, badala yake imevaa koti la Muungano. Hivyo, kitendo cha kuipa Zanzibar mamlaka yote haya chini ya mfumo wa serikali mbili ni kuiacha Tanzania bara peke yake kwenye muungano.

TUANGALIE SUALA LA MAFUTA NA GESI

Katika hotuba yake Bungeni, Rais Kikwete alitamka kwamba Zanzibar watarudishiwa suala la mafuta na gesi ili lisiwe tena ni suala la muungano. Rais Kikwete akasema kwamba, sababu za kufanya hivyo ni za kiuchumi – kwa maana ya kwamba kama ilivyokuwa kwa zao la karafuu, Zanzibar pia inahitaji mafuta na gesi yake kwa ajili ya kuendesha uchumi wake. Rais akaenda mbali zaidi na kufananisha rasilimali hizi za Zanzibar (gesi, mafuta na karafuu), na rasilimali za Tanzania bara (Dhahabu, Kahawa, Pamba n.k). Kwa matamsho haya ya Rais Kikwete, zipo implications mbili kubwa na muhimu:

1. Kwanza, mwaka 1964, uamuzi uliotolewa ulikuwa kwamba - vitu vyote ambavyo vilikuwa ni vya Tanganyika vikabidhiwe kwenye serikali ya Muungano. Kwahiyo, kwa upande wa Tanzania Bara, kabla ya kauli hii ya juzi ya Rais Kikwete, hapakuwa na kitu kinachoitwa cha "Tanzania Bara", bali vya muungano. Kauli ya Kikwete ni kusema kwamba - Sasa watanzania bara wameachiwa wapumue kwani wamepatiwa rasilimali zao ambazo kwa miaka 50 zilikuwa kwenye kapu la muungano linalohusu Tanzania Bara na Zanzibar. Tofauti na Tanzania bara, kwa upande wa Zanzibar, mwaka 1964, vitu karibia vyote vya Zanzibar vilibakia kuwa ni vya Zanzibar kasoro "Mafuta na Gesi". Hatuna uhakika kama makofi ya wajumbe wa BLK kwa Rais Kikwete yalilenga kushangilia ushindi huu wa mwanzo wa watanganyika (ukipenda waite watanzania bara).

2. Implication ya pili ya maneno ya Kikwete kwenye BLK ni kwamba - chini ya serikali mbili zilizoboreshwa, CCM na Serikali yake sasa wameanza kutambua mshirika mwingine wa muungano ambaye alikuwa anaficha chini ya zulia (Tanganyika). Kwa maneno ya Rais, kirasilimali, sasa Jamhuri ya Muungano imegawanywa katika makundi makuu mawili: Rasilimali zilizopo Nchi ya Zanzibar (Karafuu, mafuta, gesi n.k), ambazo sasa zitasimamiwa na zanzibar chini ya mamlaka yake, na nchi nyingine ambayo bado kuitaja kuna kigugumizi (Tanganyika) ambayo, kama ilivyo kwa Zanzibar, nayo pia itasimamia Rasilimali zake (Dhahabu, Makaa ya Mawe, Almasi, Kahawa, Chai, Pamba, n.k) chini ya mamlaka yake.

Kwa kauli ya Rais, ingawa Tanganyika bado haitajwi, lakini haitachukua muda mrefu kabla ya wananchi wake kuanza kushinikiza uzinduzi wa serikali yake ili sasa rasilimali hizi zianze kusimamiwa kikamilifu na Serikali yake, na sio serikali ya Muungano kama ilivyo sasa chini ya serikali mbili. Isitoshe, hadi leo, mipaka ya Tanganyika bado inaendelea kuwa ni mipaka ile ile ya Tanzania Bara.

Kitendo cha waasisi wa muungano kufanya Rasilimali hizi mbili muhimu za gesi na mafuta kuwa ni za muungano kiliweka alama muhimu sana ya muungano wa NCHI MOJA – kwa maana kwamba pande zote mbili kushirikiana kwa pamoja. Kuruhusu Zanzibar waendelee kivyao na suala la mafuta na gesi nje ya muungano kumefungulia milango Zanzibar kudai kila kitu kilichobakia. Again, kinachoshikilia muungano ni Zanzibar, sio Tanzania Bara. Kitendo cha kuruhusu Zanzibar kujifunga na mikataba ya kimataifa na kuendeleza mahusiano ya kimataifa kama "Zanzibar" maana yake ni kuanza kuitenganisha na serikali ya muungano (Tanzania Bara/Tanganyika) katika jumuiya za kimataifa.

Zanzibar wakishaondoka na mambo yote wanayotaka kuelekea mamlaka kamili, Serikali ya muungano itabakia kushughulikia mambo ya muungano peke yake, mambo ambayo kimsingi yatakuwa ni mambo ya Tanzania bara peke yake. Hii ni kufungua njia kwa Muungano kuelekea kwenye Kaburi lake. Muda sio mrefu, Zanzibar wata waaga Tanzania Bara na kuwatakia kila jema na lililojaa kheri.

Inaendelea…
 
SEHEMU YA TATU

SHERIA, MGONGANO WA KIKATIBA NA KUZINDUKA KWA UTAIFA KWA PANDE ZOTE MBILI ZA MUUNGANO

Awali tumeona Mapendekezo ya BLM (2004) juu ya orodha ya masuala ya muungano pamoja na jinsi gani kimsigni - CCM imekubali kuyatekeleza kama sehemu ya maboresho ya serikali zake mbili. Lakini kama tulivyokwisha jadili, mfumo huu ambao CCM umeipa jina "serikali mbili zilizoboreshwa", hautaboresha muungano kama CCM inavyofikiri, bali utauvunja muungano. Hii ni kwa sababu, maboresho hayo yanayokataa serikali ya Tanganyika, ambayo ndiyo itakayoipa Zanzibar mamlaka ya kweli, yatazidi kuipa Zanzibar fursa ya kuendelea kukiuka na kuivunja katiba ya Jamhuri ya Muungano, mabadiliko haya yatachochea mgawanyiko, yanaingilia mamlaka halali ya jamhuri ya Muungano, na yanaleta mgogoro mpya kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hatua ya CCM kuipa Zanzibar mamlaka tajwa chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa, ni sawa na kuipa Zanzibar "uhuru wa bandia". Hatua hii haitatatua kero zilizopo, na badala yake uhuru huu wa bandia wa Zanzibar utakuwa ni chachu ya wananchi wake kuzidi kutafuta "self determination", na hatimaye "kujitenga".

Muungano hauwezi kudumu iwapo moja ya nchi shiriki za muungano (Zanzibar) inajitambulisha kama nchi kamili ndani ya muungano kwa mujibu wa katiba yake, ina bendera yake, na ina wimbo wa taifa. CCM kulea haya yote ni kuweka mazingira ya kuvunjika kwa muungano, sio kuboresha muungano. Muda sio mrefu, mshirika mwingine wa muungano – Tanganyika nae atadai kupata haki zake kama zile ambazo mshirika mwingine (Zanzibar) amepatiwa. Na kwa vile serikali mbili zilizoboreshwa na CCM maana yake ni kukataa kuitambua Tanganyika, mvutano huu utaishia kufa kwa muungano.

Hitimisho la ripoti ya Baraza La Mapinduzi Zanzibar (2004) linasema kwamba:
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulianzishwa kwa kuzingatia msingi mkuu wa undugu na kuaminiana. Kwa tafsiri fasaha, muungano ni mashirikiano ya kijamii zilizo hai na hivyo hauna budi kuenziwa ili wananchi wasiuone muungano usioshuka kwenye vichwa vyao. Ni vyema kila mwananchi akajivunia muungano kwa kufaidika na matunda yake. Kwa hiyo, muungano ujitahidi kuzisaidia pande zote mbili katika kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.

Swali linalofuatia ni je – wananchi wa pande zote mbili za muungano watajivunia na kufaidika na matunda yake chini ya serikali mbili zilizoboreshwa? Tumeona jinsi gani kwa upande wa Zanzibar, viongozi wao wanavyohangaika kuhakikisha wanafanikisha hili kwa wananchi wake, lakini kwa upande wa Tanzania bara, hali haipo hivyo. Hali ndio itakayoua utanzania na badala yake kuchochea utanganyika muda sio mrefu.

Serikali mbili zilizoboreshwa, kama tulivyokwisha ona (zinazokosa Tanganyika), ni sawa na kuipa Zanzibar uhuru wa bandia, Hali hii itazidi kuchochea utaifa wa Zanzibar. Hauwezi kuipa Zanzibar mamlaka ya kujiamulia "mambo yake ya ndani" halafu ukaizuia kufanya hivyo kwa mambo yake ya nje - kwa mfano kuteua mabalozi wake na kuwa na kiti chake katika umoja wa mataifa. Pia hauwezi kuipa Zanzibar (mshirika mmoja wa muungano), mamlaka ya kujiamulia mambo yake "ya ndani", halafu usifanye hivyo kwa mshirika mwingine (Tanganyika). Huku ni kuchochea utaifa kwa watanganyika. Chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa, hakuna kitakachokuwa cha "Zanzibar Peke Yake". Ndani ya serikali mbili, badala yake kutakuwa na Zanzibar, na Tanganyika, lakini iliyovaa KOTI LA MUUNGANO. Koti liliwabana Zanzibar, na sasa limeanza kuwabana watanganyika. Chuki zitazidi kujengeka na kila upande utataka koti hili sasa livuliwe, pengine na kutupwa kabisa lisionekana tena.

Uhuru wa bandia wa kuipa Zanzibar mamlaka kamili bila ya kuwepo kwa Tanganyika sio suluhisho la kero za muungano. Zanzibar yenye mamlaka kamili itapatikana iwapo tu serikali ya Tanganyika itazinduliwa. Hakuna jinsi nyingine ya Zanzibar kupata "mamlaka kamili" kwani mamlaka kamili yamefunikwa na Koti la Muungano lililovaliwa na "Tanganyika".

Sasa ni dhahiri kwamba Zanzibari hawaitarudi nyuma na maamuzi yake Kikatiba (2010) yanayoitambua Zanzibar kama ni nchi kamili, hivyo kufanya muungano uliopo kuwa ni muungano wa nchi mbili, serikali mbili. Lakini inaendelea kujulikana wazi, hasa kwa wazanzibari (na waelewa wachache kutoka Tanzania Bara) kwamba hakuna muungano wa nchi mbili kuwa nchi moja bila uwepo wa Tanganyika. Bila ya Tanganyika, kilichopo ni nchi moja tu ya "Zanzibar", ambayo chini ya serikali mbili zilizoboreshwa, itaendelea kuporwa mamlaka yake ya utawala kwa koti la Muungano lililovaliwa na Tanganyika. Chini ya serikali mbili zilizoboreshwa zisizoitambua Tanganyika, wazanzibari wataendelea kulalamika kwamba wanaminywa, wanaonewa, wanadhulumiwa, wanafanyiwa hila. Watataka "waachwe wapumue".

Kama tulivyojadili, hotuba ya Rais Kikwete bungeni kutangaza kwamba Zanzibar ina uhuru wa kutumia rasilimali zake na Tanzania bara kufanya hivyo hivyo, ni ushahidi kwamba CCM na serikali yake ziliridhia uvunjwaji wa katiba ya Muungano, kulikofanywa na zanzibar (2010). Pengine ndio maana CCM na serikali yake imeendelea kukaa kimya juu ya suala hili. Viongozi wa CCM hawatoi tamko lolote kuhusu jinsi gani Zanzibar imevuruga mfumo wa muungano ulioachwa na waasisi wa muungano (nchi moja, serikali mbili). Badala yake CCM imebariki muungano wa nchi mbili, serikali mbili. Inawezekana CCM inaelewa kwamba Baraza La Wawakilishi lilishaweka msimamo juu ya hili, kwani baraza hilo lilipendekeza uwepo wa mamlaka huru ya muungano na kuwekwa wazi kwa "maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya "kila mamlaka" – kwa maana ya mamlaka ya Zanzibar, Tanganyika na Muungano. Ushahidi juu ya hili ni kwamba, Baraza la Wawakilishi halijazungumzia jambo lolote juu ya "Serikali mbili zilizoboreshwa". Kwahiyo, serikali mbili zilozoboreshwa itaendelea kuwa ni agenda ya CCM, ambayo imelazimishwa hadi miongoni wa wajumbe wa BLK wanaotokana na Chama hiki.

Baraza la wawakilishi halijataja popote juu ya maboresho ya serikali mbili, badala yake, BLW limesema kwamba:

Kwa sababu wazanzibari ni waumini wa muungano ambao haukuondoa na hautaondoa uwepo wa Zanzibar kama nchi, ni vyema katiba ijayo ya jamhuri ya muungano iweke wazi kuwa Tanzania ni Jamhuri ya Muungano. Hali hii itahakikisha kuwepo kwa maeneo maalum ya mamlaka ambayo Zanzibar ina uwezo nayo kama nchi (yani mamlaka ya Dola ya Zanzibar)."

Ikishatajwa Zanzibar kama nchi, maana yake ni kwamba nchi hiyo imeingia katika muungano na nchi nyingine ambayo Zanzibar inaitambua kuwa ni "Tanganyika". CCM haitaki kuitambua nchi hii.

CCM inayotetea mfumo wa serikali mbili "zilizoboreshwa" hawataki kuzungumzia hoja ya BLW, kwani chama kinaelewa fika kwamba Baraza la wawakishili, kamwe halitarudi nyuma katika uamuzi wake huu muhimu kwa mustakabali wake kama mshirika mmoja wapo wa Muungano. Na CCM inajua fika kwamba sio chama wala Serikali ya Muungano ambayo ina mamlaka ya kuizuia Zanzibar isijiamulie mambo yake. Mamlaka iliyobakia nayo ni kuwatukana wajumbe wa tume ya katiba, na kuwatisha wananchi kwamba serikali tatu zitaleta mapinduzi ya kijeshi.


Inaendelea sehemu ya mwisho…
 
SEHEMU YA MWISHO

Kama tulivyokwisha jadili, chini ya mfumo wa serikali mbili, hatua ya Zanzibar kuvunja Katiba ya Muungano iliyochukuliwa mwaka 2010 itazidi kuendelea kujitokeza. Kama ilivyokuwa wazi kwamba Serikali ya muungano haikuwa na ubavu wa kuizuia Zanzibar kufanya hivyo, vile vile, huko mbeleni, hakuna ushahidi wowote kwamba Serikali ya Muungano itakuwa na uwezo wa kuizuia Zanzibar isifanye hivyo tena.

Madaraka ya kisheria yaliyotungwa na Bunge la Muungano yaliyomo katika Katiba ya Muungano kuhusu mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kugawa nchi yatazidi kupuuzwa na Zanzibar siku hadi siku. Mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar (2010) ambayo sasa yanaitambua Zanzibar kama nchi kamili, ndiyo yaliyotoa mamlaka kwa rais wake kuigawa "nchi" hiyo katika maeneo mbali mbali ya kuitawala. Turudie kusisitiza kwamba, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa, hakuna atakayethubutu kuirudisha Zanzibar katika hili – sio CCM, wala Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Pengine CCM inatambua wazi kwamba kufanya hivyo kutawasha moto ambao haitaweza kuuzima. Ilichobakia kwa CCM ni kuondoka katika hoja, na badala yake kuwashambulia wakina Mzee Warioba kwa matusi, na pia kuwatishia wananchi kwamba wakichagua serikali tatu, jeshi litachukua madaraka ya nchi.

Kama tunavyoelewa, Zanzibar tayari wamehamishia madaraka na mamlaka ya serikali ya muungano kwenda kwao (Zanzibar). Lakini hili sio suala la kustaajabisha, kwani historia ni kitu cha ajabu sana, ina tabia ya kujirudia:

· Wananchi wa zanzibari bado wanakumbuka vizuri sana jinsi gani Bunge la Tanganyika mara tu baada ya muungano (1964), na bila ya idhini yao (Zanzibar), bunge hili lilivyojichukulia madaraka mkononi na kuifanya katiba yake (Tanganyika), kuwa katiba ya kudumu ya jamhuri ya muungano, kinyume na mkataba wa muungano (1964) ambao uliweka kipindi cha mwaka mmoja kama kipindi cha mpito.

· Wananchi wa Zanzibar bado wana kumbukumbu juu ya jinsi gani bendera ya Tanganyika ilivyobadilishwa kidogo rangi hapa na pale na kufanywa kuwa bendera ya Tanzania.

· Vile vile wanakumbuka jinsi gani nembo ya Tanganyika ilivyogeuzwa kuwa nembo ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ni kutokana na masuala haya, na mengine mengi, ndio maana Tume ya Katiba ikaja na mapendekezo ya serikali tatu ambayo yalilenga kupatia tiba donda dugu hili la miaka 50.

Badala ya makada wa CCM ndani ya bunge la katiba kung'ang'ania serikai mbili, busara zingewaongoza kujiuliza iwapo ni kweli wana CCM kutoka wataendelea kuunga mkono serikali mbili zilizoboreshwabaada ya kutoka Dodoma na kupanda boti kurudi nchini kwao - zanzibar.

CCM wanastahili kujiulize - iweje wana CCM kutoka Zanzibar waendelee kuunga mkono CCM juu ya serikali mbili zilizoboreshwa wakisharudi nchini kwao Zanzibar wakati kwa miaka 50, viongozi wa Zanzibar ndio wamekuwa walalamishi wakubwa dhidi ya mfumo wa muungano wa serikali mbili?

CCM ilitakiwa ifahamu siku nyingi sana kwamba, wajumbe wa BLK kutoka Zanzibar hawapo pamoja na CCM (Lumumba) katika suala hili la serikali mbili kwa dhati na moyo mmoja. Wajumbe wengi kutoka Zanzibar ni waumini wa serikali tatu, sio serikali mbili. Hata wale ambao leo wanatetea serikali mbili Dodoma, video mbalimbali zilizopo kwenye mitandao mbalimbali zinaonyesha wazi jinsi gani wanawalaghai Lumumba. Kwanini tunasema hivyo? Ni kwa sababu, iwapo kweli wajumbe wa Zanzibar wangekuwa wanaunga mkono kwa dhati msimamo wa CCM, basi:

1. Zanzibar wasingesema wao ni "nchini kamili" ndani ya Muungano."

2. Baraza la wawakilishi lisingepitisha azimio la kutaka mfumo wa serikali tatu.

3. BLW lisingeamuru sheria zote zinazotungwa na bunge la jamhuri ya muungano, kwanza zipate Baraka ya Baraza la Wawakilishi kabla hazijatumika Zanzibar.

4. Zanzibar isingemega vitu vya pamoja vya muungano - isingedai mamlaka kamili juu ya - mafuta na gesi asilia, elimu ya juu, posta mawasiliano, biashara za nje, ushuru wa bidhaa, takwimu, utafiti, ushirikiano wa kimataifa, leseni za viwanda, bandari, usafiri wa anga, polisi na usalama wa taifa.

5. Zanzibar isingedai kupewa bendera yake, wimbo wa taifa, vikosi vyake vya ulinzi na usalama, benki kuu yake, sarafu, mabalozi wake wa nje, na uraia wake.

6. Tusingesikia viongozi wa BLW wakilalamika kwamba umaskini wa Zanzibar unatokana na mfumo wa muungano wa serikali mbili.

7. Viongozi wa Zanzibar wasinge hoji yapo wapi mapato yao, yapo wapi mafuta na gesi yao.

8. Viongozi wa Zanzibar wasingetaka kuwapo mipaka ya utawala kati ya serikali ya muungano na serikali ya Zanzibar.

9. Viongozi wa Zanzibar wasinge geuza serikali ya Muungano kuwa ni mbia wa Zanzibar huku katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977) ikiendelea kutamka wazi kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano "ndiye mtawala wa Zanzibar".

10. Viongozi wa Zanzibar wasingejadili kwamba serikali inayotawala muungano ni serikali ya Tanganyika, na kuituhumu Tanganyika kwamba inanufaika na rasilimali za pamoja kuliko Zanzibar.

Tumefikia hapa kutokana na CCM kukataa kwa dhati kabisa kuizindua Tanganyika, ambayo ndiyo jawabu la sehemu kubwa ya kero za muungano zilizodumu kwa miaka 50.

Serikali Mbili zilizoboreshwa zitavunja muungano, na CCM wajiandae kutafunwa na dhambi ya kupinga mapendekezo ya tume ya katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba.

Tusemezane.
 
Uchambuzi Mzuri-Kama ni hivyo mbona hata ccm wanataka serikari tatu-UKAWA wajifanye kuwaunga mkono I believe watatwist kwenye S3
 
Mkuu Mchambuzi
Kwanza, nikushukuru kwa mjadala ambao wengi wameusahau.
Kila siku tunazungumzia S3 za tume ya Warioba.Tuliacha kuangalia upande wa pili nao ukoje.

Na hapa ni fursa kwa wale wa S2 kuja na maoni yatakayo clarify masuala kadhaa yanayojitokeza. Pengine hawatatokea kwasababu miaka 50 hawakuweza kuwa na majibu sijui wanawezaje kuja nayo

Hoja ya S2 zilizoboreshwa imejitokeza kwa namna taofauti. Ukweli unabaki, CCM na rasimu yao wanakubali maoni ya tume ya Warioba. Tatizo ni namna gani ya kufanya mambo nje ya template ya Warioba. Hapo ndipo wanakuja na hoja pungufu kama bunge la Tanzania bara.

Rasimu ya mafichoni ya CCM haielezi ni namna gani mbunge wa 'bunge la Tanganyika' atakuwa mbunge wa bunge la muungano. Bunge la Tanganyika(wanaliita Tanzania bara) halijulikani litakuwa na mamlaka ya mambo gani ambayo si ya muungano.

Kutengeneza bunge lisilojua mipaka ya mambo yake ni kutengeneza mgogoro mkubwa sana.
Rasimu ya CCM ieleze ni kipi ambacho ni cha Tanganyika ambacho wabunge wa Zanzibar hawaruhusiwi kuingia kujadili.

Bunge la Tanganyika(wanahofu, wanaita Tanzania bara) halijulikani chanzo chake cha fedha za uendeshaji.

Kama kitatoka JMT , BLW watakuja na hoja ya fedha za kuendesha baraza lao.
Je, hadi hapo hatutakuwa na S3 ? moja ya 'Tanganyika mafichoni, ya pili SMZ ambazo zote zitamtegemea JMT?

Bunge la Tanganyika(roho inagoma kusema Tanzania bara) litakuwa na mipango yake ya maendeleo.

Rasimu haielezi mipango hiyo itafikishwa na nani kwa kujadiliwa. Kwa mfano, waziri gani atapeleka mswada unaohusu mambo ya Tanganyika? Kama ni yule wa JMT, lalamiko la kuvaa koti la muungano litarudi kwa nguvu kubwa kuliko

Bunge la Tanganyika litapitisha matumizi ya Tanganyika kwa vyanzo gani vya mapato. Mchambuzi amesema TRA ni ya JMT, Tanganyika itakuwa na matumizi ya fedha kutoka mfuko upi.

Kama fedha ni za JMT, basi SMZ itakuwa na haki ya kupewa fedha kutoka JMT. Je, tutakuwa tume epuka hoja ya tume ya S3?

Ili bunge liweze kufanya kazi ni lazima liwe na mihimili mingine. Labda kwa uelewa mdogo, ningeomba mfano mmoja tu wa bunge lololote duniani linalofanya kazi bila kuwajibika, au chombo kingine kuwajibika kwalo.

Mipango iliyopitishwa na bunge la Tanganyika(bara kwa mujibu wa CCM) inapelekwa kwa nani kwa utekelezaji.Haya ni baadhi ya maswali yanayohusu bunge tu.

Ulinzi na usalama.
Kwa kuwa kuna rais mmoja wa JMT ambaye ni Amir jeshi mkuu wa majeshi, eneo lake la ulinzi ni pamoja na znz kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977.

Katiba ya Zanzibar ya 2010 inampa rais wa znz mamlaka hayo, hivyo kuwa Amir jeshi mkuu wa vikosi maalumu.

Linapotokea jambo la dharura kule znz ni nani anayetangaza hali ya hatari ikiwa Maamir jeshi wote wawili wana mamlaka sawa. Ni nani anayeamrisha majeshi ya pande zote mbili kukiwa na Amir jeshi anayepigiwa mizinga Dodoma na mwingine Zanzibar.

Mwaka 1984 wakati wa machafuko ya kisiasa znz, kulitungwa hoja ya znz kuvamiwa. JMT ikapeleka majeshi kuimarisha ulinzi. Viongozi wa znz wakasema wamevamiwa na JWT. Hoja yao haikuwa na nguvu kwasababu JWTZ ilikuwa ni mali yao pia hivyo hakukuwa na mtu kujiibia.

Kwa S2 ambazo zimeboreshwa kwa kutoa Maamir jeshi wawili, ikitokea hali ya dharura sijui itakuwaje. ZNZ ina uwezo wa kusema majeshi ya nchi jirani (JWTZ) yamepambana na vikosi maalumu na hoja ikawa na maana. Je, ndiyo maboresho hayo tunayohitaji?

Tutaangalia maeneo ya kiuchumi , maboresho yake na jinsi yatakavyoua muungano wa sasa wa S2 mara moja. Mfano, znz itawezaje kukopa ikiwa haina uwakilishi katika vyombo kama IMF n.k.
Na je nani tachukua dhamana ya ukopaji huo ikiwa resource za znz haiztakidhi vigezo vya ukopeshaji ?

Anna Tibaijuka, Dr F. Ndugulile HKigwangalla Paul Makonda Ezekiel Maige Mkandara
 
Duh sasa CCM naona wanatuletea mkorogo..
Mkuu Mchambuzi nina swali... Je ikitokea rais wa Muungano akafariki/au kuugua kwa muda mrefu ni nani atakahimu nafasi yake? Je ni makamo wa rais (Rais wa Zanzibar ambaye hakuchaguliwa na watanganyika (Bara) au ni Waziri mkuu ambaye hakuchaguliwa na wazanzibar (Maana nafasi ya rais wa Muugano ni muhimu kukahimiwa na kiongozi aliyechaguliwa pande zote za Muugano.

Swali la pili itakuwaje kama mgombea urais wa Muungano (tusema CCM) (Tanzania Bara) akapochaguliwa kwa kura nyingi bara. lakini kwa Zanzibar akapata kura chache saaaaana au hata hasipate kura kabisa na Mgombea urais wa Cuf apate kura za kutosha kutoka Zanzibar lakini kura pungufu Bara. Swali je nani atakuwa Rais wa Muungano maan rais wa Muugano inatakiwa akubaliwe sehemu zote.
 
Last edited by a moderator:
Duh sasa CCM naona wanatuletea mkorogo..
Mkuu Mchambuzi nina swali... Je ikitokea rais wa Muungano akafariki/au kuugua kwa muda mrefu ni nani atakahimu nafasi yake? Je ni makamo wa rais (Rais wa Zanzibar ambaye hakuchaguliwa na watanganyika (Bara) au ni Waziri mkuu ambaye hakuchaguliwa na wazanzibar (Maana nafasi ya rais wa Muugano ni muhimu kukahimiwa na kiongozi aliyechaguliwa pande zote za Muugano.
Alinda, nikiri kwamba sikulifikiria hili. Nadhani majibu uliyotoa ndio uhalisia wenyewe.
Nashukuru kwa angalizo hili muhimu.

Swali la pili itakuwaje kama mgombea urais wa Muungano (tusema CCM) (Tanzania Bara) akapochaguliwa kwa kura nyingi bara. lakini kwa Zanzibar akapata kura chache saaaaana au hata hasipate kura kabisa na Mgombea urais wa Cuf apate kura za kutosha kutoka Zanzibar lakini kura pungufu Bara. Swali je nani atakuwa Rais wa Muungano maan rais wa Muugano inatakiwa akubaliwe sehemu zote.

Nadhani chini ya mfumo wa sasa ambao ccm lazima wataendelea kuupigia chapuo ni kwamba - mshindi atakuwa ni yule mwenye simple majority katika jumla ya kura za zanzibar na Tanzania bara. Kwa maana hii, mshindi wa urais atakuwa yule atakayepata hata 50.01 percent ya kura zote, bila ya kutenganisha kura zilizopigwa Zanzibar na zile zilizopigwa Tanzania Bara.

Nadhani wenye uelewa zaidi wa mambo haya watatusaidia kutuelimisha humu.


Vinginevyo kama ulivyosema, mkorogo ni mkubwa sana.
Nguruvi3, mag3, FJM, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Ezekiel Maige, MwanaDiwani, Yericko Nyerere, JokaKuu, Ritz, Pasco, Ben Saanane


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hivi tunavyosema kuna mambo yana boreshwa kwa sisi wa Tanzania bara ni faida gani tutapata na hayo marekebisho zaidi ya kugawa pesa zaidi zaidi kwa Zanzibar, kuongeza mabalozi wa kutoka Zanzibar, Zanzibar wakipata mafuta yawasaidie wenyewe tu wakati kwenye mapato ya 4.5% wanayopata sasa kuna pesa ya gas na gold, Wabara haturuhusiwi kuwa na viwanja Zanzibar ni kuwapa Zanzibar tu kwa sisi hatupati kitu zaidi ya malalamishi ya kila siku.

Zanzibar ni asilimia tatu tu ya Watanzania wako 1.3M na Tanzania tuko 43M. Vilevile wna raisi wao, mawaziri wao, wabunge wao na serikali yao. Vilevile kuna wabunge huku kutoka Zanzibar kwenye bunge letu la kawaidi wanapata 4.5% ya mapato ambayo ni kubwa kuliko ididadi yao ya 3% na mchango wao kwenye uchumi ni 0% wanakipato cha $300M na matumizi ya $600M. Bado tunafikiria tuwape nini zaidi bado tunafikiria tufungue bunge lingine kwasababu yao tu, tuongeze serikali kwa sababu yao tu.

Tatizo letu Watanzania ni wanafiki hatuwezi kutatua matatizo ni kujidanganya danganya tu je kuna mtu anaamini kweli Wanzanzibari watarizika na chochote?!!Wanzanzibar wanataka kuwa kama nchi za kiarabu wasifanye kazi na wakae na kunywa chai na kuoa siku nzima haya mambo ya idadi ya serikali ni kuyeyushana tu ziwe mbili au tatu. Kama kweli wangekuwa wanataka maendeleo tungekuwa na serikali mmoja tu ndogo.

Haya mambo unayosema ni ya kisasa lakini hayana msingi kimandeleo, haya make sense yeyote ukiangalia vizuri kwani hatuwafahamu Wanzanzibari?
 
Hivi tunavyosema kuna mambo yana boreshwa kwa sisi wa Tanzania bara ni faida gani tutapata na hayo marekebisho zaidi ya kugawa pesa zaidi zaidi kwa Zanzibar, kuongeza mabalozi wa kutoka Zanzibar, Zanzibar wakipata mafuta yawasaidie wenyewe tu wakati kwenye mapato ya 4.5% wanayopata sasa kuna pesa ya gas na gold, Wabara haturuhusiwi kuwa na viwanja Zanzibar ni kuwapa Zanzibar tu kwa sisi hatupati kitu zaidi ya malalamishi ya kila siku.

Zanzibar ni asilimia tatu tu ya Watanzania wako 1.3M na Tanzania tuko 43M. Vilevile wna raisi wao, mawaziri wao, wabunge wao na serikali yao. Vilevile kuna wabunge huku kutoka Zanzibar kwenye bunge letu la kawaidi wanapata 4.5% ya mapato ambayo ni kubwa kuliko ididadi yao ya 3% na mchango wao kwenye uchumi ni 0% wanakipato cha $300M na matumizi ya $600M. Bado tunafikiria tuwape nini zaidi bado tunafikiria tufungue bunge lingine kwasababu yao tu, tuongeze serikali kwa sababu yao tu.

Tatizo letu Watanzania ni wanafiki hatuwezi kutatua matatizo ni kujidanganya danganya tu je kuna mtu anaamini kweli Wanzanzibari watarizika na chochote?!!Wanzanzibar wanataka kuwa kama nchi za kiarabu wasifanye kazi na wakae na kunywa chai na kuoa siku nzima haya mambo ya idadi ya serikali ni kuyeyushana tu ziwe mbili au tatu. Kama kweli wangekuwa wanataka maendeleo tungekuwa na serikali mmoja tu ndogo.

Haya mambo unayosema ni ya kisasa lakini hayana msingi kimandeleo, haya make sense yeyote ukiangalia vizuri kwani hatuwafahamu Wanzanzibari?

Mkuu Kamundu,
Kwahiyo una shauri nini, serikali
Moja? Tuvunje muunganoo? Kama una maanisha serikali moja, Iwapo serikali mbili zimekuwa ni kero kwa znz kwa miaka 50, serikali moja itaondoaje kero hizo?

Kwa upande wa bara, serikali moja haitakuwa na madhara sana kwao, hasa iwapo Zanzibar itarudi kuwa ni "sehemu ya jamhuri ya muungano", na sio "nchi kamili" kama ilivyo sasa. Lakini kwa upande wa znz, gharama za serikali moja ni kubwa sana, na zitavunja muungano siku inayofuatia, kwani tofauti na sasa ambapo Tanganyika imevaa koti la muungano, serikali moja sasa maana yake ni kwamba Tanganyika itavaa blanket kabisa na kuifunika znz. Hawatakubali hii, na ndio maana miaka 50 iliyopita, Mwalimu hakutaka hili, alijua madhara yake kwa Muungano.

Kuhusu Zanzibar kutegemea Tanganyika kujiendesha, hali hii ni matokeo ya ccm kung'ang'aniza serikali mbili. Hata kama znz itapewa ruksa kukopa (of which hatujui ni kwa collateral ipi kwa mujibu wa Nguruvi3 hapo juu), bado access to loans and AID kwa znz chini ya serikali mbili haitakuwa na effect ya maana kwa znz kama tulivyojadili awali.

Suluhisho hapa ikiwa kweli bado tunahitaji muuungano ni - kuifufua Tanganyika (serikali yake), na kupunguza masuala ya muungano - kwa mfano kwa mujibu wa rasimu ili kila upande ule kwa urefu wa kamba yake.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

..lets say wanaanzisha bunge dogo kwa ajili ya wa-Tanganyika, then what happens at the government level?

..je, kutakuwa na baraza la mawaziri wa Kitanganyika ndani ya baraza la mawaziri la muungano?

..au, kutakuwa na wakati mawaziri wa serikali ya muungano wenye asili ya Zanzibar hawashiriki majadiliano au vikao vinavyojadili mambo ya Tanganyika?


cc Mzee Mwanakijiji, Ritz, chama, NasDaz, Mdondoaji, gombesugu
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi hatuwezi kulazimisha muungano mimi naona ni kama tunahonga bila kujua sababu. Je kuna faida gani ya Muungano kwa Mtanzania wa kawaidi ambaye ni mkulima mikoani au hata mtu yeyote wa bara kuna faida gani ya muungano kwa sasa naomba mtu anieleze kwasababu sijasikia bado faida za muungano na huu si muungano ni kwasababu upande mmoja tu Zanzibar watu wake wana haki kote. Hivyo muungano ukivunjika sioni hasara kwa sisi wa bara hasa ukuzingatia Wanzanzibar wengi hawautaki muungano
 
Mchambuzi,

..lets say wanaanzisha bunge dogo kwa ajili ya wa-Tanganyika, then what happens at the government level?

Mkuu JokaKuu,

Bunge la Tanganyika (ukipenda Tanzania Bara) halitakuwa dogo bali kubwa kuliko mabunge mengine yote. Bunge la kuwakilisha zaidi ya 95pct ya watanzania utaliitaje bunge dogo? Unaposema dogo, una maana idadi ya wabunge au idadi ya wanaowakilishwa?

Nadhani pia una taarifa kwamba CCM inapendekeza majimbo mapya kwa ajili ya bunge la muungano, huku kwa upande wa znz, majimbo yale yale yaliyopo sasa yalete wabunge kwenye bunge la muungano, bunge ambalo, kuna wakati litaitwa la muungano, na wakati mwingine litaitwa la "Tanzania Bara".
Lengo hapa ni kujaribu kulifanya bunge la Tanzania bara liwe na sura ya uwakilishi wa wananchi wa Tanzania Bara. How? Hatujui.

Kuhusu what happens at gvnt level, nadhani jibu ni nothing.
Hii ni kwa sababu, bunge la Tanzania Bara halitakuwa na maana yoyote bila ya uwepo wa baraza lake la mawaziri pamoja na kiongozi wake wa serikali (bila ya kujalisha kiongozi huyu ataitwa Rais, Waziri Mkuu, Gavana, n.k).

Serikali mbili, mabunge matatu, mawili yakiwa ndani ya bunge la muungano. Hata watoto wetu wanaosoma juu ya mihimili ya dola watachanganyikiwa mashuleni. Hawataisha na maswali, itabidi waalimu wawajibu kwamba kuna mihimili ya dola na mihimili ya CCM, bila ya hivyo hawataelewa kabisa nini kimeikumba nchi yao.

..je, kutakuwa na baraza la mawaziri wa Kitanganyika ndani ya baraza la mawaziri la muungano?

..au, kutakuwa na wakati mawaziri wa serikali ya muungano wenye asili ya Zanzibar hawashiriki majadiliano au vikao vinavyojadili mambo ya Tanganyika?

Hakuna ufafanuzi kutoka CCM juu ya nini itakuwa ni nafasi ya mawaziri wa “Tanzania Bara” ambao hawatokuwa Mawaziri wa Muungano, hasa wakati wa vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili masuala ya Muungano. Tusisahau kwamba chini ya serikali mbili, hakuna mambo ya Tanzania Bara pekee yake bali yapo ya Zanzibar na ya Muungano, kwani Bara imevaa koti la muungano.

Pia CCM haitoi ufafanuzi kwamba ikiwa Muungano utakuwa na Rais mmoja - wa jamhuri ya muungano, ikiwa atatokea "Bara", je ni yeye ndiye atakuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri watakaosimamia mambo ya Tanzania bara? Kwa mamlaka yepi wakati kiti chake kitatokana na kura za nchi jirani ya Zanzibar pia?


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi hatuwezi kulazimisha muungano mimi naona ni kama tunahonga bila kujua sababu. Je kuna faida gani ya Muungano kwa Mtanzania wa kawaidi ambaye ni mkulima mikoani au hata mtu yeyote wa bara kuna faida gani ya muungano kwa sasa naomba mtu anieleze kwasababu sijasikia bado faida za muungano na huu si muungano ni kwasababu upande mmoja tu Zanzibar watu wake wana haki kote. Hivyo muungano ukivunjika sioni hasara kwa sisi wa bara hasa ukuzingatia Wanzanzibar wengi hawautaki muungano

Mkuu Kamundu,

Kwa mtazamo wako:

1. Kwanini wananchi walio wengi wa bara hawaguswi na hoja yako juu ya faida za muungano katika maisha yao ya kila siku?

2. Kwanini wapo wananchi wa Tanzania Bara ambao bado wanadhania serikali mbili ni bora kuliko serikali tatu?

3. Kwa mtazamo wako, kwa wananchi hawa, nini ni maana ya serikali moja? Mbili? Tatu? Kila moja maana yake ni nini katika maisha yao ya kila siku?

4. Kati ya serikali tatu, mbili au kuvunja muungano, kipi kina gharama kubwa kwa wananchi wa pande zote mbili kijamii na kiuchumi?

Nadhani unajua serikali moja haiwezekani, serikali mbili zinalazimishwa.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hii rasimu au mapendekiezo haya yalitolewa lini?
Kuna original document somewhere, au unaweza ukatuelekeza wapi uliiona?
cc. Mchambuzi

Haya ni mapendekezo ya chama juu ya rasimu ya katiba. Hivyo ndivyo ccm inapanga kuboresha mfumo wa serikali mbili. Nyaraka hiyo iliwasilishwa na Asha Migiro kwenye kikao cha NEC kuelekea Bunge La Katiba. Aliwasilisha haya kwa nafasi yake kama Katibu NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Je, was it a coincidence for her to be appointed Waziri Wa Sheria na Katiba? Tutajua mengi zaidi Bunge la Katiba liki "resume" baadae mwezi wa nane, 2014.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom