CCM nilikuunga mkono lakini kwa upuuzi huu sasa basi

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Siku chache zilizopita nilitoa maoni yangu kutathmini awamu hii ta tano. Niliandika kuwa pamoja na kuchukizwa na na baadhi ya mambo lakini namuunga mkono Magufuli. Niliandika pia siamini kama Rais anaweza kuyajua mambo yote ya moja kwa moja pale anapoingia madarakani, mambo mengine hujifunza akiwa ofisini. Kwahiyo, nilikuwa tayari kumuunga mkono Magufuli nikiamini kuwa atajifunza kutokana na makosa.

Kwa bahati mbaya nilifanya makosa. Kwanza, nataka kumweleza Magufuli kuwa kwasababu nilikuwa namuunga mkono haina maana nilikuwa nauchukia upinzani. Nathamini mchango wao na naamini kama serikali ikiachiwa ifanye inavyotaka bila kukosolewa itajisahau na kufanya mambo ya hovyo.

Pili, mambo wanayofanyiwa wapinzani hivi karibuni siyafurahii na siwezi kuvumilia upuuzi huu.

Link hapo chini kinaonyesha maoni yangu siku chache zilizopita nikimmunga mkono.

Magufuli nakuunga mkono lakini kuwa makini kwenye kipindi chako cha pili
 
Kuna msemo unasema kuwa SIASA NI MCHEZO MCHAFU.swala watu wanataka ushindi
 
Kwanza umejichanganya sana na hatuelewi nini unazungumza. Kiambatanisho kinasema unamuunga mkono Magufuli lakini meseji mpya unazungumzia CCM halafu tena vitu wanavyofanyiwa wapinzani hauviweki wazi ni vipi. Wewe ni zero plus. Siyo lazima kuanzisha thread mzee.
 
Pole, si kila mtu ataona ubaya wa Magu, au uzuri wake, hivyo ndivyo ilivyo asili ya binadamu!
 
CCM ni kikundi cha hovyo sana. Ujangili ni wao, Ufisadi ni wao, Uhujumu uchumi ni wao, wizi wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka, ushirikina na kurogana mchana kweupe, unafiki, uzandiki, ugaidi, mauaji, utekaji, vurugu, nk vyote ni vyao!

Hivi hiki kikundi kinachoitwa CCM kina jema lolote lile, hata moja tu kwa Watanzania kweli? Ifikie wakati Watanzania tuamue kwa kauli moja kuwaondoa hawa Wakoloni Weusi kwa njia yoyote ile. Ikibidi hata kwa kutumia Nguvu ya Umma.
 
Siku chache zilizopita nilitoa maoni yangu kutathmini awamu hii ta tano. Niliandika kuwa pamoja na kuchukizwa na na baadhi ya mambo lakini namuunga mkono Magufuli. Niliandika pia siamini kama rais anaweza kuyajua mambo yote ya moja kwa moja pale anapoingia madarakani, mambo mengine hujifunza akiwa ofisini. Kwahiyo, nilikuwa tayari kumuunga mkono Magufuli nikiamini kuwa atajifunza kutokana na makosa...
Nakumbuka post yako ile..naikumbuka sana ..nilisahau tu kukuwekea hii picha

downloadfile-1.jpg
 
Kama unalipenda taifa letu kwa dhati kabisa bila unafiki huwezi muunga mkono magu kamwe, chini ya magu umoja wa taifa letu unakufa, chuki inatamalaki.lissu ni mzalendo wa kweli

Mkuu

Nakushauri uache kupoteza nguvu kazi yako kwa kushabikia vitu vya kipuuzi kabisa.

Tupunguze mahaba kwenye vitu halisia!
 
Mkuu

Nakushauri uache kupoteza nguvu kazi yako kwa kushabikia vitu vya kipuuzi kabisa.

Tupunguze mahaba kwenye vitu halisia!
Kwangu huo ndo ukweli, ingawa sikuzuii kumshabikia Huyo jpm wako, kiongozi muda wrote anagawa watu kwa tofauti zao.Naamini kulipenda taifa lako ni pamoja na kutenda haki kwa wrote.magu kashindwa
 
Mbowe asipokuwa katili hiyo wilaya atashindwa kufanya kampeni uchaguzi huu wote. Kila anataka kuhutubia ahakikishe ameshaanda watu wa vita liwalo na liwe. Kosa kubwa sana alifanya kuacha kuhutubia walipomshusha jukwaani Mara ya kwanza.

Halafu walivyo kuwa wajinga eti CHADEMA wanatembea na shehena ya Mawe kwa nini fujo hazitkutokea Mikoa na Wilaya nyingine alikopita Lisu?
 
Hii video nimeingalia vizuri hawa machalii wanatumika vibaya mbaya zaidi wanaowatuma wanashindwa hata kuwapa chakula angalau wali na ndondo, Ukiwangalia machoni wananjaa hadi sura zao zimepoteza nuru wamekaririshwa maneno ya kuongea siajabu wamewaada kua watawapa ubwabwa wakimaliza kazi waliowatuma vijana tusikubali kutumiwa kama ndomu.
malipo ubwabwa ndondo
 
Ukiamua kuwa baridi kuwa baridi tu ukiamua kuwa Moto kuwa Moto.

Kumuunga mkono Huyo dikteta na kusema unamchukia anayofanya haimake sense
 
Siku chache zilizopita nilitoa maoni yangu kutathmini awamu hii ta tano. Niliandika kuwa pamoja na kuchukizwa na na baadhi ya mambo lakini namuunga mkono Magufuli. Niliandika pia siamini kama Rais anaweza kuyajua mambo yote ya moja kwa moja pale anapoingia madarakani, mambo mengine hujifunza akiwa ofisini. Kwahiyo, nilikuwa tayari kumuunga mkono Magufuli nikiamini kuwa atajifunza kutokana na makosa.

Kwa bahati mbaya nilifanya makosa. Kwanza, nataka kumweleza Magufuli kuwa kwasababu nilikuwa namuunga mkono haina maana nilikuwa nauchukia upinzani. Nathamini mchango wao na naamini kama serikali ikiachiwa ifanye inavyotaka bila kukosolewa itajisahau na kufanya mambo ya hovyo.

Pili, mambo wanayofanyiwa wapinzani hivi karibuni siyafurahii na siwezi kuvumilia upuuzi huu.

Kiambatanisho hapo chini kinaonyesha maoni yangu siku chache zilizopita nikimmunga mkono.
Wasalimie huko uendako. Wengine wengi tu tumebaki kama kipindi kile cha Lowassa.

TUKUTANE OKTOBA 28!
 
Back
Top Bottom