CCM Mwisho wake kuwepo kama chama tawala ni 2020

Inaweza ikawa kweli maana huyu jamaa noma aliomba Corona ije Tz ikaja,hivyo na hili linaweza likatokea kweli.
 
"CCM mwisho wake kuwepo"

"CCM mwisho wake ..., kama chama tawala"

Ni kati ya hayo mawili.

Kwa maoni yangu, CCM kama chama ilikwishaondoka siku nyingi.

Kilichopo ni jina tu la chama hicho linalotumiwa na wenye maslahi yao kutimiza matakwa yao.

Kati ya hao wanaolitumia jina ni:
1. Mwenyekiti, ambaye sasa ndiye CCM yenyewe

2. Wenye maslahi yao wanapitia kwenye jina hilo, CCM waendelee kupata manufaa yao binafsi, hata kama jina limebinafsishwa kwa Mwenyekiti

Ukweli ni kwamba sasa hivi hakuna chama kinachojisimamia kama chama na kuwa na uwezo wa kuamua jambo mhimu linalohusu maslahi ya nchi.
Msukumo upo kusimamia maslahi ya makundi hayo hapo juu. Hilo la pili, linategemea fadhira za mwenye chama.

Wanaojiita wanachama wa CCM, hasa huko vijijini na kwingineko, imebaki kutumia mazoea tu na ushabiki wa ki-Simba na Yanga, ndio unaoshikilia waendelee kujitambulisha hivyo.
Kweli aisee, CCM ya sasa ni CCM ya Mwenyekiti (Magufuli) na si CCM ya wanachama. Nikimanisha kuwa wanachama hawawezi amua jambo lolote likafanyiwa kazi isipokuwa matakwa ya Mwenyekiti tu ndio yanageuka kuwa matakwa ya wanachama!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati nasema niache tu hata kuchangia maana mada kama hizi za ukichaa au za digree ya 32 au ulofa katika ubora wake mimi sijui, sijui ni matumaini wanayojipaga Ufipa hata kama mtu ajaende shule na hajui kufanya tafiti hawezi kuandika ujinga kama huu, alafu vijana wa ufipa wanatiririka kuchangia utafikiri mazuzu, hii ni aibu sana si kwa Ufipa na upinzani lakini kwa taifa hata sisi tunaona aibu sana eti kisa mitandao iko wazi basi unatoka na hisiha zako za kilofa unaandika tu.
Unaijua CCM wewe?

Kama maandamano mlishindwa, sera za kupambana na ufisadi mlishindwa, mambo ya maendeleo mnapinga sasa mnafikiri watanzania hawa wajinga hawasikii ulofa wenu, alafumnasema CCM mwisho 2020 huu si upumbafu wa kujilisha upepo.

Kwanini mmekuwa wajinga kiasi hiki, mlipokea mfumo wa vyama vingi hili kuwa malofa(mmekili) au mlipokea mfumo wa vyama vingi hili kupinga kilakitu hata kama ni chema kwa taifa. Kwanini mnawaza kwenda Ikulu wakati hamna sifa hata moja ya kuwafikisha huko. Vyama vyote vya upinzani wenyeviti wanahisia za umiliki wa vyama vyao sasa iweje tumpe mtu 1 nchi kwa maslai yake binafsi na nduguzake itawezekana kweli?Kwani sababu ya kwanza ya kuletwa kwa mfumo wa vyama vingi ni kubadirishana vijiti sasa tuwaamini kwa lipi wakati Freeman anakaa mika zaidi ya 20 katika kiti?
Mimi nasema kama hamkubadilika hivi mlivyo hata mzikili bila nguo hamtoiona Ikulu hadi Yesu hatakaporudi katika nchi ya Watanganyika na Wanzinzibari.
 
Naomba niombe Radhi kwa kuleta dini kidogo kwenye ili maandiko yetu Waislamu yanasema ukiona japo Baya linafanyika unatakiwa uliondoe ukishindwa likataze ukishindwa kbs onyesha kuchukia juu jambo ilo lipi hapa Mh Rais ameonyesha kati ya hayo...
Mkuu Rubawa, hayo unayoyasema mimi pia nayapitia, baada ya lile swali la Ikulu, kuna watu wanafanya mambo ya kiajabu ajubu as if wametumwa na yeye, kwasababu wanajua huwezi kupata access kuuliza, lakini through circumnavigating, nimeweza kubaini hao watu hawajatumwa na Magufuli, tena usikute hata Magufuli mwenyewe hajui nini watu wake wanawafanyia dhulma kubwa watu in his name!.

Kwenye wateule wake, unaweza kukuta sii kweli
Mh rais Magufuli amewapa wateule wake madaraka makubwa ya kudhurumu na kunyanyasa kwa kisingizio cha kutumwa na rais, hivyo wewe kudhani ni kweli wametumwa na rais Magufuli hivyo kudhania kuwa Mh rais Magufuli anajua dhuluma zote juu yako, kumbe in reality rais Magufuli hajamtuma yoyote kufanya dhulma zozote na hivyo hajui chochote kuwa huku chini kuna watu wana nyanyasika.

The best way kuujua ukweli ni kufanya cross checking kwa kutumia njia inayoitwa circumnavigating ikishindikana, then unatumia direct.

Kuna mambo mengi mabaya wanamhisi ni rais Magufuli, lakini ukweli sio yeye na wala hajui kitu.

Mfano kuna watu wanadhani lile tukio la zile pyu pyu pale Dodoma ni yeye, kumbe sio yeye wala hakujua kitu, ila...

Mambo mengine ni too sensitive tuyaache yapite ila yote yana mwisho haya.
Pole kwa yote.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaki kusema mengi kwanini kinaenda kufa ila hoja kubwa ni toka baba wa taifa afariki CCM kimekuwa kikitawala kwa ujanja ujanja na propaganda

Kikubwa zaidi hawamu ya 5 imekizika kwa kupuuza wananchi wanataka nini kiufupi ccm haifanyii kazi matakwa ya watanzania walio wengi ili swala linaenda kuwaondoa madarakani kimchezo mchezo.

Wale mliokwapua pesa za umma muanze kuzilejesha bila kusahau mliokuwa mnafanya maovu mjindae kweli kweli.

Naapa kwa jina la baba la mwana na roho mtakatifu ccm haitarudi madarakani kwa sababu ya ubishi na mtakuja kukumbuka maneno yangu mlikuwa na muda wa kujirekebisha ila kibri kibri mjiandae kisaikolojia.

This is what people or rather citizens of Tz term as “DAY-DREAMING”!!
 
Sitaki kusema mengi kwanini kinaenda kufa ila hoja kubwa ni toka baba wa taifa afariki CCM kimekuwa kikitawala kwa ujanja ujanja na propaganda

Kikubwa zaidi hawamu ya 5 imekizika kwa kupuuza wananchi wanataka nini kiufupi ccm haifanyii kazi matakwa ya watanzania walio wengi ili swala linaenda kuwaondoa madarakani kimchezo mchezo.

Wale mliokwapua pesa za umma muanze kuzilejesha bila kusahau mliokuwa mnafanya maovu mjindae kweli kweli.

Naapa kwa jina la baba la mwana na roho mtakatifu ccm haitarudi madarakani kwa sababu ya ubishi na mtakuja kukumbuka maneno yangu mlikuwa na muda wa kujirekebisha ila kibri kibri mjiandae kisaikolojia.
Una matatizo makubwa kichwani mwako! Wahi kwa Daktari.
 
Mkuu una uhakika na mada yako au umeandika tu ili kujaza servers za JF>??>>>>>>
 
Sitaki kusema mengi kwanini kinaenda kufa ila hoja kubwa ni toka baba wa taifa afariki CCM kimekuwa kikitawala kwa ujanja ujanja na propaganda

Kikubwa zaidi hawamu ya 5 imekizika kwa kupuuza wananchi wanataka nini kiufupi ccm haifanyii kazi matakwa ya watanzania walio wengi ili swala linaenda kuwaondoa madarakani kimchezo mchezo.

Wale mliokwapua pesa za umma muanze kuzilejesha bila kusahau mliokuwa mnafanya maovu mjindae kweli kweli.

Naapa kwa jina la baba la mwana na roho mtakatifu ccm haitarudi madarakani kwa sababu ya ubishi na mtakuja kukumbuka maneno yangu mlikuwa na muda wa kujirekebisha ila kibri kibri mjiandae kisaikolojia.
This is chimpumu not beer.
 
Mawazo uliyo nayo wewe leo ndio mimi pia nilikuwa nayo kabla ya July,2017, Baada ya kupata kibarua cha kuwa National Sales Manager wa kampuni kubwa binafsi ya usambazaji bidha za matumizi mbali mbali ya nyumbani, ilinipa fursa ya kutembelea karibu Wilaya zote na hasa miji mikubwa na midogo karibu maeneo yote ya Tanzania.

Nimejifunza mengi katika mzunguuko huo ambao nakaribia miaka 3, hali hiyo imenibadilisha sana na nilivyokuwa nafikiri kabla kuhusu kukubalika kwa vyama hasa vyama vya upinzani kulinganisha na CCM, kwa ushuhuda wa matembezi ya kikazi nilibadilisha muono wangu. Hatuna mgombea wa kuitikisha CCM kwa nafasi ya Urais labda kwa ushabiki. Tuna kazi ngumu sana ya kufanya na tunahitaji kufanya kazi ya kutosha.
Nina wasi wasi kuwa hata wabunge wa majimbo wanaweza wakapungua sana. Sidhani hata kumtikisa Mkulu tutaweza labda afanye blanda kubwa ambayo itamwodolea imani wapiga kura.

KWA MFANO: Ukisema hana uwezo wa kujieleza vizuri au kuelezea masuala ya kitaifa na kimataifa vizuri, MAJIBU....walikuwepo waongeaji wazuri sisi walitusaidia nini, sisi tunataka kazi na tunataka matokeo tuu na sasa tunaona jaribu kutembea nchi nzima inajengwa leo hii.

Ukiwaeleza jamaa amebana sana upande wa siasa
MAJIBU.. sasa kazi yetu ya kulima siasa inatusaidia nini?
Walioko vijijini wanaona tufauti ndogo sana ya mapato kati ya siku za nyuma na kulinganisha na leo. Hasa ukitilia maanani mazao yao mengi ya kilimo wanayauzwa na wanapata pesa labda kwa mazao machache ya biashara.

Kuna mengi ningechangia humu, lakini kwa kifupi elimu ya demokrasia bado sana miji mingi midogo na vijijini. Ngoja wazoee umeme, maji, barabara, na hospitali mpya zilizojengwa nina hakika baada ya kuzoea, mahitaji yao yatakua na hapo ndipo wataanza kuigeukia CCM kwa kuhitaji mambo mengi Zaidi..

Na wenzetu CCM wameweka watu wao katika kila ngazi ya utawala kuanzia nyumba kumi.

UPINZANI BADO TUNA KAZI KUBWA YA KUFANYA. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Acha uongo kila mtu anafanya hizo field ,kwanzaa huko vijijini wanasema huyu baba achatu ,nimawakala wangapi wapembembejeo huko mikoani wamezulumiwa helazao ,wengi wamekufa kwa presha namadeni .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM itashinda hata kwa goli la mkono-Nape Nnauye 2015
Mtoa mada ukishiba ugali ni bora uhesabu nywele zako kuliko kuota ndoto kama hizi.

Nzi wa kijani itachukua miaka mingi sana kutoka madarakani hasa upinzani huu wa Lipumba na wale ambao walimfukuza Zitto Kabwe kisha wakampokea Lowassa.

Kutamba kote huku ni kwa sababu ya uhakika mlio nao wa kutumia Usalama wa Taifa kubadilisha matokeo na kuyaweka mnavyotaka kwa nguvu ya dola, si kwa nguvu ya vote.

Jeuri yote hii ni kutokana na kiburi cha kudhani kuwa CCM ni chama cha Mungu: eti kitakaa madarakani milele. Ni ulevi wa madaraka mnayohodhi kwa nguvu, na kiburi cha kujiona mnajua kila kitu. MTAANGUKA saa msiyoijua. Na baada ya hilo anguko HAMTAONEKANA tena.

Kiburi hutangulia mauti. Mmedhulumu na kuishi kwa damu na jasho la watanzania kwa zaidi ya nusu karne. Hata mizimu yenu na matambiko yenu yanajua, kwamba Mungu wa mbinguni huchoshwa na dhulma ya wenye majivuno na kibri.

MTAONDOKA NA SI MUDA MREFU. Jitahidini tu kuwa wanyeyekevu, ili siku yenu ya dhiki ikifika, mtendewe kwa huruma kuliko mnavyowatendea wenzenu sasa.

Pure FACTS.
 
Jiandikisheni Uandikishaji unaendelea nawahakikishia serikali ya Ccm inaanguka mwezi october tokeni mjiandikishe kwa wingi maana mwaka huu hakuna uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi na ikipatikana Magufuli hana chake.
 
Hahah
Chadema wakishashiba mbege bwana

Ccm haiwezi kukabidhi Nchi kwa wahuni haitotokea, hatuwezi kumdhalilisha Nyerere
 
Sitaki kusema mengi kwanini kinaenda kufa ila hoja kubwa ni toka baba wa taifa afariki CCM kimekuwa kikitawala kwa ujanja ujanja na propaganda

Kikubwa zaidi hawamu ya 5 imekizika kwa kupuuza wananchi wanataka nini kiufupi CCM haifanyii kazi matakwa ya watanzania walio wengi ili swala linaenda kuwaondoa madarakani kimchezo mchezo.

Wale mliokwapua pesa za umma muanze kuzilejesha bila kusahau mliokuwa mnafanya maovu mjindae kweli kweli.

Naapa kwa jina la baba la mwana na roho mtakatifu CCM haitarudi madarakani kwa sababu ya ubishi na mtakuja kukumbuka maneno yangu mlikuwa na muda wa kujirekebisha ila kibri kibri mjiandae kisaikolojia.

Hicho kiapo chako mungu atakitema kama mate tu, atakiona kama kimetoka kwa shetani.
 
Jiandikisheni Uandikishaji unaendelea nawahakikishia serikali ya Ccm inaanguka mwezi october tokeni mjiandikishe kwa wingi maana mwaka huu hakuna uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi na ikipatikana Magufuli hana chake.
Kwa chadema hii ambayo hata wabunge wanamdharau mwenyekiti wao akisema twende kushoto wao wanaenda kulia ndio waikutoa ccm?

Au kuna upinzani gani mwingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom