Mkuu unajua tofauti ya kuwa proactive na reactiveWatanzania jana wamekenua meno baada ya kipenzi chao Mheshimiwa Rais Kikwete kukidhi kiu yao ya kuvunjwa baraza la mawaziri na kusudio la kuwafikisha katika vyombo vya sheria waliohusika kufisadi mali za umma.
Hatua hiyo imezidi kukipaisha CCM na wakati huo huo kukiporomosha chama pinzani CHADEMA huku tukielekea 2015. Watanzania kutoka mashariki hadi magharibi, kaskazini mpaka kusini jana jioni walikuwa katika makundi wakisherekea hatua ya JK na kuipongeza CC ya CCM kuwa ina wapenda Tanzania na manufaa kwa Watanzania.
Poleni CHADEMA, tafuteni hoja nyingine, ya kuvunja baraza la mawaziri haina mshiko tena!