Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
HOT NEWS....CCM MWANZA KIMENUKA ,MBUNGE NDASA ATIMULIWA
KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, imemfukuza kwenye kikao, Mbunge wa Sumve wilayani humo, Richard Ndassa, kwa madai kwamba ameanza kuunda makundi na mgogoro kwa madiwani wa halmashauri hiyo, ili madiwani hao wamkatae mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa maslahi yake binafsi; imedokezwa.
Imeelezwa kwamba, Ndassa anatuhumiwa kuanza kuwarubuni baadhi ya madiwani wa CCM, ili wamkatae mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Zephania Masangu (CCM), na kwamba siku hiyo ya kikao cha kamati ya siasa kilichofanyika Novemba 3 mwaka huu, mbunge huyo alifukuzwa ndani ya kikao ili wajumbe waweze kumjadili kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kuanzisha mgogoro ndani ya halmashauri hiyo inayoongozwa na CCM.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mwanza Sitta Tumma anaripoti kuwa ,taarifa zilizoifikia mwandishi wa mtandao huu kutoka jijini Mwanza, Sitta Tumma, kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, zimeeleza kwamba, Ndassa ameanzisha harakati hizo za kutaka kumg'oa mwenyekiti huyo, ili aweke mtu anayemtaka yeye, kinyume cha taratibu na kanuni za chama, na kwamba siku hiyo ya kikao alitolewa nje na hakurudi hadi tena kikaoni.
Kwa mujibu wa habari hizo, kamati hiyo ambayo iliwaita na kuwahoji madiwani wake mmoja baada ya mwingine kuhusiana na mgogoro huo, inatarajia kutoa maadhimio yake Novemba 10 mwaka huu, na huenda ikamwadhibu vikali mbunge huyo pamoja na madiwani anaoshirikiana nao kupanga njama hizo chafu za kutaka kumng'oa mwenyekiti Masangu katika nafasi yake hiyo.
"Ndassa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya, lakini siku ya kikao alitimuliwa na hakurudi tena. Kisa cha kufukuzwa kwenye kikao hiki ni njama zake za kuanza kuwarubuni baadhi ya madiwani wa CCM ili wapitishe maazimio ya kumkataa mwenyekiti wa halmashauri kwa maslahi yake binafsi na jamaa zake.
"Kimsingi tunaiomba sana kamati yetu imwadhibu huyu Ndassa na ikiwezekana afukuzwe uanachama, maana ameanza kuigawa CCM. Ndassa hamtaki mwenyekiti wa halmashauri (Masangu), kwa vile anatetea sana maslahi ya wananchi wa Kwimba, na anapiga vita mambo ya kifisadi", kilisema chanzo kimoja cha habari kutoka ndani ya kamati hiyo.