CCM: Mwaliko maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Mwaliko maalum

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by JamiiForums, May 12, 2010.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,098
  Likes Received: 2,242
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Wakuu, mjumbe hauwawi. Mnakaribishwa sana
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kuchangia uchaguzi mkuu. Kila kitu kuomba omba tu.
   
 3. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu

  Naomba tangazo hili litolewe.

  watakutumaje wakati wao wana uwezo wa kutengeneza account hapa na kuweka tangazo;kwa vyovyote vile naamini umetumwa na umepewa pesa!

  na nawasihi sana wananchi mtakaosoma tangazo hili mlipuuzie;

  Kuendelea kuchangia pesa nyingi hizi kwa ajili ya matumbo ya watu na kudidimiza demkrasia na utu wa watu ni uzandiki.

  Ni sawa na kuchangia ili ndugu yako aendelee kuwa mtumwa.

  Sijawahi kusikia huyu mama amekusanya wachaga wenzie ili wachangie maendeleo ya Mkoa Wa Moshi,au suala la Barabara au kituo cha afya?

  sijawahi kumsikia Marealle akifanya hivi toka mwanzo,hii ni kwa kuwa anataka ubunge na ogopeni watu wanaotumia pesa ili kupata madaraka!

  Sijawahi kusikia CCM imechangisha pesa kwa ajili ya kuweza kuwaongezewa walimu Mishahara na posho zao!

  Mkuu hao Frotnline wamekulipa ili utoe tangazo hili basi umekosea sana..ungewaambia waje wajisajiri hapa na waliweke tangazo hili unless nitajua ndiyo mmeingia kwenye biashara (ubia) na hamtaweza kuwakwepa mafisadi kamwe!

  Siwakatazi ksuoma bali nawakataza kuchangia ila kama mnapenda kuona Mafisadi wanaendelea kushinda kwa kishindo basi endeleeni kuwachangia!

  Yes i have said,ACHANENI KABISA NA KUCHANGIA MAMBO YA OVYO NA NI BORA USOMOSHE NDUGU ZAKO MASIKINI WASIO NA UWEZO!

  Gembe!
   
 4. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama nilivyo sema kwenye thread ya (Ubunge Hai) Kuwa kuna harambee kubwa inaandaliwa na mama Vicki Swai ni harambee maalumu kwa jili ya jimbo la moshi mjini (sio kama wanavyoda wenyewe ) ikiwa na maana kwamba ni harambee ya kuchangisha fedha za kumuondoa mzee Ndesamburo kwenye jimbo la moshi mjini. Naona kazi imeanza rasmi sasa!
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  ishu siyo kumuondoa Ndesa

  Ndesa amekuwapo hapo muda mrefu sana ila bado wananchi wanapaza sauti za vilio vya shida..

  cha msingi ni seriklai kuongeza nguvu ya kusaidia maendeleo.

  Mie nashangaa sana ,hivi kama RAis anaweza kukusanya makapuni na matajiri kuchangia Pesa za kampeni kwanini basi asiwaombe wachangie kujenga baadhi ya barabara?au vituo vya Afya?

  Yaani mie nakereka kuchangia chama ambacho kinaongozwa na watu walioshindwa kulketa matumaini kwa watanzania..

  Maendeleo Zero na bado tuanendelea kuomba omba hadi nje..

  Nyani..wtf
   
 6. kizaizai

  kizaizai JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 2,740
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280
  Mbayuayu atapona kweli? :yuck:
   
 7. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #7
  May 12, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sioni sababu ya kuliondoa ili tangazo hapa, mbona ya Chadema ya napo we kwa hapa na wasiyo wausika hamsemi ya tolewe?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wizi mtupu na mh anaenda kuubariki!
   
 9. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Mie sijaongelea mambo ya CHADEMA na siyo mwanahcma wa CHADEMA.siku zote huwa mnapotea sana kwa kuzania kila anayeponda mabaya ya CCM ni CHADEMA.Jibu hoja na siyo kuleta vioja na kubwabwaja.

  Mie ni mtu mwenye Mlengo wa kushoto na hapa sikuangalia itikadi za chama chochote ila mstakabali wa taifa.

  Naomba Invisible kwa Heshima na kutumia jamiiformus kusupport jambo hili haututendei haki hata kidogo.Kwa taarifa yako ningekupinga hata kama Mkuu angeleta tangaz la CHADEMA.
   
 10. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #10
  May 12, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe ni nani humu ndani? maana naona unafundisha kazi watu sasa ? MODS wataliondoa endapo wataona kuna sababu ya kufanya hivyo .

  We endelea na mlengo wako wa kushoto hakuna aliyekuambia uwe kwenye mlengo wa kulia!
   
 11. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Mimi sijui ni kwa nini mnalumbana,hapa JF kila mmoja ana mtazamo wake na maoni yake na JF haiendeshwi kwa kufuata threads kama hizi za ondoa,husiondoe.Haya ni maoni yake na ya kwako
  Tusonge mbele
   
 12. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #12
  May 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kweli hilo Tangazo limetumwa na mtu anayeitwa Jamiiforums ni admin ina maana linabaraka zote toka kwenye uongozi wa jamiiforums na uongozi huo huo ndio ulitakiwa kutoa ufafanuzi kwako gembe hii ndio democrasia kama ikishindwa kutoa ufafanuzi basi itakuwa ni kuendelea kuandika historia mbaya na kama kweli limelipiwa basi utatakiwa kuhoji michango mengine ya watu wanaoitoa inaenda wapi na inakatwaje kodi
   
 13. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
 14. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Changamoto hizo
   
 15. k

  kaiya Member

  #15
  May 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wengine wanaamka asubuhi hawajui watakula nini? wengine wanaenda kutoa kiingilio elfu 50 kuingia kuchangia CCM. kweli vidole havilingani.
   
 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Si Tanzania tu bana......mbona Marikani wanachangia uchaguzi(kwa kuombaomba kama hivi)....Kama hutaki kuchangia waweza sepa vilevile...Hajalazimishwa mtu hapo ati...............
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Marekani wako dunia nyingine! Bibi yake Kabula pale karibu na kwa Mzee Luhende bado wanakunywa maji ya kwenye Malambo na akiugua analazwa chini na bila dawa!!!...kwani michango isifanyike kwa mambo endelevu? ie kuweka bomba za maji, Kujenga majosho, kuimarisha zahanati na vituo vya afya?
   
 18. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaaaaaa......lol......Ndo maana nikasema huo ni mwaliko.....anayetaka aweza kwenda na asiyetaka akasepa.......hajalazimishwa mtu.........Hizo ulizotoa hapo juu ni changamoto kwa CCM na chama chochote kitakachoingia madarakani...wazifanyie kazi...Pamoja Home B
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Niko gizani jamani hivi pesa nyingi inachangiaje kukomboa jimbo? Niondolee tongotongo
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,577
  Trophy Points: 280
  Mimi naipongeza Jamiiforums kuweka tangazo la CCM. Huu ni uthibitisho kuwa JF ni non partisan kwenye party politicts, ni impartial na ina play neutrality which is a good move.

  Tangazo kama hili lina neutralizes sentiments kuwa JF ni pro- Chadema. Wana Chadema wengi wamo humu kwa majina yao kwa vile wana feel wako free, wanaCCM kama Nape, pia waliingia kwa majina yao lakini wako kimya labda kwa hisia hizo hizo kuwa JF ni jukwaa la Chadema, tangazo kama hili ni uthibitisho tosha kuwa JF ni zaidi ya itikadi za vyama.

  Nakushukuru tena kwa mwaliko huu, wife wangu ni CCM damu, mimi nitamsindikiza na nitachangia kwa moyo wote ili kulinda amani ya familia na kusocialize.

  Natoa wito kwa wale wengine wasio na vyama kama mimi, kulipa 60,000/= dinner for two, Golden Tulip, is not a big deal, nitachangia kwa moyo mkunjufu sana, kwa vile siasa za Moshi, nazielewa fika, hata wakipata bilioni 100 ili kumng'oa Ndesa, watakuwa wanacheza makida makida, sio tuu CCM itaangukia pua, bali Mwenyekiti wao ataonekana kama Joti mbele ya umma wa Watanzania.

  Pole Rev Kishoka kutofautiana na wewe kwenye hili, sometime ili ushinde vita sio lazima kupigana front line kwenye uwanja wa mapambano, unaweza ku-infiltrate watu wako miongoni mwao na ukaishia kuwalipua from within, hivyo kuepusha kiwango cha casuality.

  Deal lote hili sio la Mama Swai, ni la kijana ambitious aliowaingiza CCM mkenge akijiaminisha Wachagga nao watauza utu wao kwa fulana na kofia pamoja na shibe ya siku moja!. Mama Swai anajua wazi Ndesa ni kisiki cha Mpingo ila kijana ni lobbyist mzuri, amemlobi mpaka Mkulu kutembeza bakuli, namhurumia watamtia aibu ya bure!.

  Ila baada ya kuboronga juzi alipowahutubia Wazee wa (CCM) Darisalaam, natumaini wamesha soma dalili za nyakati, hivyo wasaidizi wake watamshauri asiende.

  Kusipotokea mwana JF mwingine ambaye atakwenda, basi nitawajulisha kinachoendelea ingawa nadhani TV ya Mangi, itaonyesha live na sio TBC. Na kama itakuwa ni TBC, itabidi nishangae. Bila kusahau, MC wa CCM, ni yule yule Mtangazaji Maarufu kuliko watangazaji wote wa Redio za FM hapa jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla (naomba usibishe wala usiniulize), kwa jina maarufu la Kibonde, (ni jina tuu, sio Kibonde wa wale vibonde, shuleni alikuwa kipanga!)

  Karibuni Sana.
   
Loading...