Baada ya majina ya wagombea kupitishwa, sasa umezuka mtindo wa kila jimbo, kila kata kulazimisha mapingamizi ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa. Huu ni uzembe na uhayawani wa chama kikongwe. Miaka zaidi ya 50 bado CCM mnawaza kukataa kushindana!
Kuna majimbo yalishatangaza wagombea, rasmi nao sasa wanalazimisha kuwe na mapingamizi nje ya muda wa kisheria; ni pamoja na jimbo kama Ukerewe ambalo tayari kuna mauaji! Misungwi ambako kuna mgombea nako kunalazimishwa kusiwe na mpinzani wa CCM. Morogoro mjini huko waliwahi watu wakapigwa mamilioni kujiondoa.
CCM hii ni aibu. Hata wizi unahitaji akili, sasa CCM ni mbinu bila hata akili kwa kujidai ni mbinu ya kisiasa. Kama mlipitisha wagombea wasiokubalika, tulieni wananchi watoe hukumu.