Uchaguzi 2020 CCM mnatia aibu kwa kulazimisha ushindi wa mapingamizi

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,864
Baada ya majina ya wagombea kupitishwa, sasa umezuka mtindo wa kila jimbo, kila kata kulazimisha mapingamizi ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa. Huu ni uzembe na uhayawani wa chama kikongwe. Miaka zaidi ya 50 bado CCM mnawaza kukataa kushindana!

Kuna majimbo yalishatangaza wagombea, rasmi nao sasa wanalazimisha kuwe na mapingamizi nje ya muda wa kisheria; ni pamoja na jimbo kama Ukerewe ambalo tayari kuna mauaji! Misungwi ambako kuna mgombea nako kunalazimishwa kusiwe na mpinzani wa CCM. Morogoro mjini huko waliwahi watu wakapigwa mamilioni kujiondoa.

CCM hii ni aibu. Hata wizi unahitaji akili, sasa CCM ni mbinu bila hata akili kwa kujidai ni mbinu ya kisiasa. Kama mlipitisha wagombea wasiokubalika, tulieni wananchi watoe hukumu.
 
Hili ni fundisho tosha kuwa CCM wanaogopa sasa kujiajiri ndiyo maana wapo tayari kutumia kila hila ili wapite bila kupingwa.

CCM wako tayari kukodi majambazi wapore fomu za wagombea wa upinzani ili wao wapite bila kupingwa; CCM wako tayari wamteke mgombea wa upinzani ili ashindwe kurudisha fomu ili wao wapite bila kupingwa; CCM wako tayari kuweka pingamizi feki ili wapite bila kupingwa kisa woga wa kujiajiri.

Kwa hiyo vijana wangu mliomaliza vyuoni akitokea kiongozi wa CCM anasema mjiajiri wakati wao wanyewe wako tayari kutoa roho ya mtu ili waepuke kujiajri msimsikilize ikibidi mtukaneni matusi ya ndani ya gagulo au boksa!!!!!!
 
Mbinu chafu ktk siasa ni kawaida, tatizo ni ubora wa wale wanaoleta mbinu chafu. Mbinu chafu za mtu mjanja ni tofauti sana na hawa akina Mheshimiwa fulani. Kinachofanyika sasa ni uchafu ambao hata jirani akisikia anaona tumeoza tangu kichwani hadi mkiani.

Btw. Nahisi kama wagombea wengi wa CCM akili haziko sawa au zimeharibiwa na movement ya mwaka huu. Sheria inazungumzia mgombea anayefariki je, anayepata tatizo la akili kabla ya uchaguzi inakuwaje?
 
Baada ya majina ya wagombea kupitishwa, sasa umezuka mtindo wa kila jimbo, kila kata kulazimisha mapingamizi ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa. Huu ni uzembe na uhayawani wa chama kikongwe. Miaka zaidi ya 50 bado CCM mnawaza kukataa kushindana!...

Mhe Tundu alimuwekea pingamizi Mhe Magufuli, Rais wa Tanzania, sasa kuna tatizo gani au dhambi gani kama the same trend cascades down to the lowest grade yaani mtindo huo ushuke kutoka ngazi za juu mpaka kwa madiwani/sheiya?? Acheni kulalama hiyo ndiyo trend(mwendo halali kwa wale waliojaza vibaya fomu zao!
 
Baada ya majina ya wagombea kupitishwa, sasa umezuka mtindo wa kila jimbo, kila kata kulazimisha mapingamizi ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa. Huu ni uzembe na uhayawani wa chama kikongwe. Miaka zaidi ya 50 bado CCM mnawaza kukataa kushindana!..
Rules are Rules, kama mtu kakosea kujaza fomu na apigwe pin
 
Baada ya majina ya wagombea kupitishwa, sasa umezuka mtindo wa kila jimbo, kila kata kulazimisha mapingamizi ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa. Huu ni uzembe na uhayawani wa chama kikongwe. Miaka zaidi ya 50 bado CCM mnawaza kukataa kushindana!..
CCM wamechoka kuiba.

Wameamua kunyang'anya na kupora.
 
Baada ya majina ya wagombea kupitishwa, sasa umezuka mtindo wa kila jimbo, kila kata kulazimisha mapingamizi ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa. Huu ni uzembe na uhayawani wa chama kikongwe. Miaka zaidi ya 50 bado CCM mnawaza kukataa kushindana!..

Tanzania tunakoelekea sio mbali nchi zilizo pata matatizo na vita duniani ni viongozi kulazimisha kubakia madarakani huku wakidhani yakitokea matatizo watabaki salama.

Haijawahi kutokea uhuni huu tokea siasa za vyama vingi viasisiwe Tanzania wapo viongozi walio tangulia kutoa angalau ushauri ? CCM imekua ikijitapa kila kukicha wamefanya maendeleo makubwa iweje leo waogope uchaguzi ?

Tunatowa angalizo kwa tume ya uchaguzi wasikubali kuiingiza nchi katika matatizo . Nchi ikichafuka haitakua rahisi kurejesha amani na sote tutaingia matatizoni lakini kwa kuanzia tutaanza na hawa wabunge ama madiwani wa kubebwa si tutakua nao mitaani ?

Uhuni huu haukubaliki kama hamuwezi siasa turudini kwenye mfumo wa chama kimoja .
 
CCM wamechoka kuiba.

Wameamua kunyang'anya na kupora.
mie naona bora upinzani kususia tu uchaguzi huu, hakuna namna watatangazwa washindi...sanasana wataachiwa majimbo mawili matatu tuu ya kuzugia...Jiwe ni katili hakuna mfano ndo maana alitaka kumtoa uhai JL na hakika karma itamlipa!!!.
 
Hivi Lissu hakuweka mapingamizi? Nadhani mchakato unaruhusu na yeye ndiye aliyeuanza kwenye uchaguzi huu kuweka mapingamizi dhid ya wagombea wenzake; sasa usipofanya kazi kwako usiulaumu utakapofanya kazi kwa wengine.
 
Tanzania tuna akili za kipekee. Tuna waheshimiwa wanaoupenda uheshimiwa kweli kweli, hata mahakamani wanakwenda kudai umewakosea heshima, ukivaa kaptula ofisi zao hurusiwi kuingia, ukiwa na rasta unafikiria mara mbili kama watakuelewa.
Lakini wanakaa vikao kupanga mipango ya kihuni, ili kesho na kesho kutwa wakutake uwaheshimu tena.
 
Mhe Tundu alimuwekea pingamizi Mhe Magufuli, Rais wa Tanzania, sasa kuna tatizo gani au dhambi gani kama the same trend cascades down to the lowest grade yaani mtindo huo ushuke kutoka ngazi za juu mpaka kwa madiwani/sheiya?? Acheni kulalama hiyo ndiyo trend(mwendo halali kwa wale waliojaza vibaya fomu zao!
Uko sahihi mkuu
 
Rev. Mtikila RIP naikumbuka kauli yake miaka ya 90 aliwahi kukiita chama fulani ni Chama Cha Majambazi hata sijui alimaanisha nini!!?
 
Kitu cha kushangaza kwangu ni hao wagombea ambao wanafurahi kupitishwa bila kupingwa.

Yote haya yana manufaa gani? Tangia mwanzo CCM wana wabunge wengi kuliko vyama vingine vya siasa ila nikiangalia naona yafuatayo:

1. Ushindi mkubwa wa CCM kulenga maeneo ya zamani ya wapinzani (maeneo ya upeo wa bahari pamoja na zanzibar na kaskazini Tanzania kama moshi, arusha) ni kubadilisha dynamics za wapiga kura mbeleni. Mambo ya kuiba kura na mengineyo yamepitwa na wakati maana kwa ukuaji wa technologia haiwezekani tena.

2. Dynamics za wapiga kura zikibadilika automatically watu wengi watakuunga mkono na pia ushindani hautakuwepo. Pamoja na hayo pia kuwakumbusha wananchi mambo mazuri CCM ambayo wameyafanya katika majimbo yao na yale majimbo yaliokosea ni kuwataarifu kama wabunge wenu wa vyama vengine hawakupiga kazi. Hii ni power of persuation, unakuta viongozi wengi tu wa serikali hua wanachomekea maneno wakienda kufanya ziara mbalimbali za kukagua miondombinu.

3. Unapopata wafuasi wako wote katika sehemu zote za serikali kuanzia ngazi ya chini mpaka juu kitu muhimu ambacho kama chama unanufaika ni kuboresha utekelezaji wako kwahiyo unakua unajua harakati zote za wananchi wako (intelligence) na pia katika bunge sera yoyote inapitishwa kwa kishindo namaanisha over 90%. Serikali yoyote inapenda kuwa na urahisi katika kupitisha mambo yake yote (na hayo yatakayokuja).

CCM kazi yao sio kurahisisha mambo ambayo vyama vingine inalalamika. CCM mantra yao ni kupata ushindi mkubwa na kuchukua viti vyote vya serikali na kuendelea kushika dola kwahiyo
sasa inabidi argument yako iwe vyama vya siasa vinginevyo vina mikakati gani?

Kama tatizo ni NEC? Je walitoa tamko lolote kabla na pia walikubaliana na wafanyakazi waliochaguliwa? Utekelezaji wa NEC ulikubalika? Etc.
 
mie naona bora upinzani kususia tu uchaguzi huu, hakuna namna watatangazwa washindi...sanasana wataachiwa majimbo mawili matatu tuu ya kuzugia...Jiwe ni katili hakuna mfano ndo maana alitaka kumtoa uhai JL na hakika karma itamlipa!!!.
Unaweza kususia mtu mwenye akili timamu lakini hawa na kiongozi wao, unaona dalili za aibu?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom