CCM KUMDHALILISHA DC ni sawa?

mozze

Senior Member
Aug 27, 2010
185
28
Nashindwa kuelewa, CCM wanasema ati CDM wamemdhalilisha DC, lakini wao wanasambaza picha za DC akiwa anapelekwa kama Mhalifu.
Unajua Mnafiki utamjua haraka sana. Hawa viongozi wa juu wa CCM wanawadharau sana wananchi na wote walio chini yao. Haiingii akilini kwa mtu kama waziri kuwaonyesha wananchi picha za mtu akiwa amevuliwa nguo, nadhani angeelezea mkasa tu ingetosha!

Kwa upande mwingine, kwa vyovyote vile atapata huruma ya washabiki wa CCM tu, kwa watu ambao wanajua kuwa DC anakula hela ya walipa Kodi wakati ni kada wa CCM ndio watafurahia na kuona kuwa CDM ni chama makini kwani wana nguvu hata ya kumkamata DC kuliko CCM na polisi wake wanaoshindwa kuwakamata wahalifu. Hivyo CCM inabidi wabadilike na kuwajali wananchi kuliko kukumbatia makada wake wahalifu.

Tumeona ile Meli iliyozama huko ZNZ wamiliki hawajachukuliwa hatua, na kesi inapugwa danadana kwa sababu mmiliki mmoja ni mbunge wa CCM.....wananchi wakijua haya wataelewa unafiki wa CCM mana hawajali maisha ya mwananchi wa kawaida kwa kukumbatia makada wake....
Nawapongeza CDM kwa kuonyesha kuwa mbele ya sheria hakuna mkubwa!

Source: Mwananchi today
 
Ccm wapo tayari hata kuua ili walinde maslahi yao. Yule mama anatumiwa kama mtaji wa siasa naye hajijui.
 
taratibu kidogo...twende tartibu....

kwamba umesoma Mwananchi ndo ukaja na hizi hoja, au hii ni habari kwenye gazeti la Mwananchi?

anyhow, ulichokiandika kina mashiko kwa sababu kama sasa tunakwenda kwa ushahidi wa picha, na sisi Chadema tuna picha za mgombea wa CCM akiwa amevaa kufuli la mwanamke aliyefumaniwa naye, tuzioneshe kwa wananchi?
 
Hii Habari imeandikwa na Mwananchi, lakini picha zilishatumika hata kabla ya mwananchi kuandika. Reference imewekwa hapa kama chanzo cha habari kwa undani.

anyhow, ulichokiandika kina mashiko kwa sababu kama sasa tunakwenda kwa ushahidi wa picha, na sisi Chadema tuna picha za mgombea wa CCM akiwa amevaa kufuli la mwanamke aliyefumaniwa naye, tuzioneshe kwa wananchi?

Kama mkakati wa kisiasa, CDM wakionyesha picha za mwana CCM akiwa kafumaniwa ni nzuri na itakuwa na impact kuliko wanayofanya CCM kuonyesha picha za Kada wao, tema DC, akiwa anaburutwa kama muhalifu. Technically CCM wanajionesha hawawezi kutawala mana kama Chama pinzani wana uwezo wa kumkamata DC kama mhalifu basi CDM ndio wana jeuri ya kuchukuwa madaraka.

Kwa mimi nadhani, CDM wangeweza kusambaza picha kama hizo za viongozi wa CCM wakiwanyanyasa wananchi, kwa jinsi wanavyolala bungeni, wanavyofuja mali za wananchi etc. CCM watachanganyikiwa mana wananchi watazidi kuamka!
 
Nimesikitishwa sana na jinsi ccm wanavyotumia picha ya dc kuomba kura za huruma hasa kwa kina mama, je hawaoni kuwa ni kumdhalilisha zaidi huyo mama? Nawasilisha
 
Kama mkakati wa kisiasa, CDM wakionyesha picha za mwana CCM akiwa kafumaniwa ni nzuri na itakuwa na impact kuliko wanayofanya CCM kuonyesha picha za Kada wao, tema DC, akiwa anaburutwa kama muhalifu. Technically CCM wanajionesha hawawezi kutawala mana kama Chama pinzani wana uwezo wa kumkamata DC kama mhalifu basi CDM ndio wana jeuri ya kuchukuwa madaraka.

Kwa mimi nadhani, CDM wangeweza kusambaza picha kama hizo za viongozi wa CCM wakiwanyanyasa wananchi, kwa jinsi wanavyolala bungeni, wanavyofuja mali za wananchi etc. CCM watachanganyikiwa mana wananchi watazidi kuamka!

Kwenye red: Nimeipenda hiyo na ndiyo maamuzi magumu yanayotakiwa -- yaani onyesho la uthubutu wa kufanya yale CCM huwa inashindwa kuyafanya hadi nchi hii inaenda hovyo hovyo.
 
wasambaze na picha zinazo onyesha akinamama wajawazito wakiwa wamelala chini kwa kukosa vitanda
 
Huyu DC ni mteule wa rais, Mbunge ni mteule wa wananchi.. Hata wafanye hila gani bado wanajisumbua tu. wabunge wako juuu.
 
chadema kwa kweli ni chama cha majambazi na wahuni, kamwe hawawezi kuchukua jimbo la igunga na wala nchi hii
 
wasambaze na picha zinazo onyesha akinamama wajawazito wakiwa wamelala chini kwa kukosa vitanda

Yessss....Chadamea nao wasambaze picha hizo za wanawake wajawazito wanaolala chini kwenye mawodi. Hapo CCM itakuwa imekwisha kabisa jeuri yake na itaangukia pua. Wezi na majambazi wakubwa, na ndiyo maana uchaguzi wa 2010 waliporomoka vibaya, wakaokoloewa na NEC.
 
chadema kwa kweli ni chama cha majambazi na wahuni, kamwe hawawezi kuchukua jimbo la igunga na wala nchi hii

Mkuu mbona uko hapa muda sana .Kwa hii comment yako unachangia kuijenga JF na kuifany mahali maalum pa great thinkers ?
 
Yessss....Chadamea nao wasambaze picha hizo za wanawake wajawazito wanaolala chini kwenye mawodi. Hapo CCM itakuwa imekwisha kabisa jeuri yake na itaangukia pua. Wezi na majambazi wakubwa, na ndiyo maana uchaguzi wa 2010 waliporomoka vibaya, wakaokoloewa na NEC.

Sasa hivi nimempigia simu kiongozi wa CDM katika kampeni huko Igunga na kumpa wazo hilo, na amesema ataliwakilisha kwa wenzake ili waone kama itafaa nao kutumia picha za wajawazito wanaodhalilishwa katika nchi yao yenye utajiri mkubwa.
 
Mimi huwa napata taabu sana kuhusu hawa viongozi wa CCM, kila siku inayofuata nao uwezo wao wa kufikiri unazidi kushuka kwanini? kuna mtu kanipa habari kuwa jana Komba na Mukama kidogo wazichape kavukavu jee ni kweli?
 
Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 kuna DC alilambwa mtama na kukwidwa na wanachama wa CCM wale waliomtenda DC huyo walichukuliwa hatua gani
 
Matendo madogo madogo yanayoigharimu CHADEMA, najua ni ushabiki tu, ila ndani yao nadhani wanajuta kwa ujinga huu, gharama yake ni kubwa mno. Viongozi wa CDM wanashaurika, juzi Mheshimiwi Lissu alikaa na wazee kutafuta jinsi kusafisha sura ya chama mbele za wananchi hasa Igunga...ninyi wapuuzi endeleeni kujifurahisha na ujinga wenu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom