CCM KUMDHALILISHA DC ni sawa?

Nashindwa kuelewa, CCM wanasema ati CDM wamemdhalilisha DC, lakini wao wanasambaza picha za DC akiwa anapelekwa kama Mhalifu.Unajua Mnafiki utamjua haraka sana. Hawa viongozi wa juu wa CCM wanawadharau sana wananchi na wote walio chini yao. Haiingii akilini kwa mtu kama waziri kuwaonyesha wananchi picha za mtu akiwa amevuliwa nguo, nadhani angeelezea mkasa tu ingetosha!Kwa upande mwingine, kwa vyovyote vile atapata huruma ya washabiki wa CCM tu, kwa watu ambao wanajua kuwa DC anakula hela ya walipa Kodi wakati ni kada wa CCM ndio watafurahia na kuona kuwa CDM ni chama makini kwani wana nguvu hata ya kumkamata DC kuliko CCM na polisi wake wanaoshindwa kuwakamata wahalifu. Hivyo CCM inabidi wabadilike na kuwajali wananchi kuliko kukumbatia makada wake wahalifu.Tumeona ile Meli iliyozama huko ZNZ wamiliki hawajachukuliwa hatua, na kesi inapugwa danadana kwa sababu mmiliki mmoja ni mbunge wa CCM.....wananchi wakijua haya wataelewa unafiki wa CCM mana hawajali maisha ya mwananchi wa kawaida kwa kukumbatia makada wake....Nawapongeza CDM kwa kuonyesha kuwa mbele ya sheria hakuna mkubwa!Source: Mwananchi today
Mbona watanzania wendi tu wanadhalilishwa kila siku na wengine kuuawa, hii ya DC ina nini special? Kwani yeye sio mtu.
 
Mkuu,

Utakuwa unakosea sana wewe na wenzako. Kama hospital, wanaweza wakafikiri kuwa labda ni baada ya ajali ya mabomu.

Picha nzuri ni zile za WAATHIRIKA wa Chemicals huko Mara kwenye migodi. Tena waseme kuwa na hapo Igunga jamaa wataanza kutumia muda wowote, labda CDM washinde na mbunge wao kuzuia hayo mambo.

Waseme kuwa huyo jamaa wa CCM ameshuhudia watu wakiathirika na hizo chemical huko Mara na hadi leo hajafanya kitu.

2.JPG
3.JPG



https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/56294-hatari-mgodini-north-mara-chukua-hatua-4.html


Sasa hivi nimempigia simu kiongozi wa CDM katika kampeni huko Igunga na kumpa wazo hilo, na amesema ataliwakilisha kwa wenzake ili waone kama itafaa nao kutumia picha za wajawazito wanaodhalilishwa katika nchi yao yenye utajiri mkubwa.
 
Mkuu,

Utakuwa unakosea sana wewe na wenzako. Kama hospital, wanaweza wakafikiri kuwa labda ni baada ya ajali ya mabomu.

Picha nzuri ni zile za WAATHIRIKA wa Chemicals huko Mara kwenye migodi. Tena waseme kuwa na hapo Igunga jamaa wataanza kutumia muda wowote, labda CDM washinde na mbunge wao kuzuia hayo mambo.

Waseme kuwa huyo jamaa wa CCM ameshuhudia watu wakiathirika na hizo chemical huko Mara na hadi leo hajafanya kitu.

2.JPG
3.JPG



https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/56294-hatari-mgodini-north-mara-chukua-hatua-4.html

Kwani huyo DC alikuwa kama hivi?
 
josephine.jpg mtu mmoja anasema eti Tanzanian are confused na sikupenda kuambiwa hivyo lakini nafsi zinatusuta.
Hivi zicha za maiti za maandamano ya Arusha pamoja na mwanamke aliyepigwa na polisi akivuja damu mwili mzima watu hawakuzionyesha na badala yake wanaona in suala la maana kuonyesha picha eti za mtu aliyevuliwa hijab nk!!!!
 
Nashindwa kuelewa, CCM wanasema ati CDM wamemdhalilisha DC, lakini wao wanasambaza picha za DC akiwa anapelekwa kama Mhalifu.
Unajua Mnafiki utamjua haraka sana. Hawa viongozi wa juu wa CCM wanawadharau sana wananchi na wote walio chini yao. Haiingii akilini kwa mtu kama waziri kuwaonyesha wananchi picha za mtu akiwa amevuliwa nguo, nadhani angeelezea mkasa tu ingetosha!

Kwa upande mwingine, kwa vyovyote vile atapata huruma ya washabiki wa CCM tu, kwa watu ambao wanajua kuwa DC anakula hela ya walipa Kodi wakati ni kada wa CCM ndio watafurahia na kuona kuwa CDM ni chama makini kwani wana nguvu hata ya kumkamata DC kuliko CCM na polisi wake wanaoshindwa kuwakamata wahalifu. Hivyo CCM inabidi wabadilike na kuwajali wananchi kuliko kukumbatia makada wake wahalifu.

Tumeona ile Meli iliyozama huko ZNZ wamiliki hawajachukuliwa hatua, na kesi inapugwa danadana kwa sababu mmiliki mmoja ni mbunge wa CCM.....wananchi wakijua haya wataelewa unafiki wa CCM mana hawajali maisha ya mwananchi wa kawaida kwa kukumbatia makada wake....
Nawapongeza CDM kwa kuonyesha kuwa mbele ya sheria hakuna mkubwa!

Source: Mwananchi today

Waache waumane,sisi tunasonga!!
 
Back
Top Bottom