CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

Sawa Mr.kolola nimekusoma
Nataman kuendelea ila bando limekata,uchumi wa kati wengine hatujafika bado😄
Kwenu publicity matter a lot lakini kwa Me, kitanda ndicho mwisho wa lami. Ulishasikia msemo kuwa ‘mwanaume roho yake hailali anapolaza kiwiliwili chake bali hulala inapolala k anayoipenda sana’ . Hivyo tulivyo tofauti kimaumbile hata kimtizamo. Mchepuko unaonipenda kwa dhati ni wa maana kuliko mwanamke wangu wa ndoa ya kikatoliki asiyenithamini.
 
Mimi kwa maoni yangu hili ni jambo binafsi sana, unamzuiaje mtu kuweka shada la maua kwenye kaburi? afu uhalisia ni kuwa huyo mume alikuwa katika harakati za kimahakama kuivunja ndoa.all in all ndugu yangu Shaka angejikita zaidi kwenye ajenda za kitaifa, huko tunaskia hela zinapigwa tu mawizarani,mpaka Rais au waziri mkuu ndio avumbue hayo maovu,wakati kuna mawaziri,maPS, wakurugenzi na watendaji kibao.hili ninaona ndio la kuvalia njuga ,muda ni mfupi sana na matatizo ya wananchi bado ni mengi sana,hivyo chama kiisimamie serikali yake kwelikweli hasa katika uwajibikaji na utekelezaji wa ilani ili kupunguza adha wa wananchi.
nawasilisha
 
Ni majina tu ya kiislamu, mume Omary na mke anaitwa Aziza; hila nadhani wote ni wakristo (not certain about the wife religion though).

Catherine ni public figure lakini ili swala ni private, mke wa marehemu anayo haki ya kutema nyongo na kimada (Catherine) alikuwa na haki ya kumzika mtu aliekuwa akiishi nae.

Kwa mila zetu ni mambo ya kifamilia kwa watu wa nje kufuatilia zaidi ni umbea tu.

Huyo Shaka if anything anatakiwa kuwaonya tu ugomvi wao usiende public tena; but both women have the right to grieve in their own rights.
Katika ndoa ya kikatoliki hiyo sheria ya kusema malaya, kimada, kahaba inamtambua katika kipengele kipi? Yaan anagrieve wapi? Kimpango gani? Kahaba naye ana haki ya kuomboleza? come on. Yaan hata angelala naye miaka 10 hata 100 bado ni kahaba as long ad marehem bado hakumtaliki mkewe ndoa. Kwanza katoliki hatuvunji ndoa tunaita kutengana. Msiba wa babu yangu yule mwanamke aliyezaa naye kabla ya ibada aliutwa mbele akaulizwa unafanya nini hapa mbele? Uko kama nani hapa? Unakaaje hapa kwenye sehem ya familia? Hana majibu. Akaambiwa hukupaswa kuwa hapa. Nyanyuka mara moja. Na usionekane hapa. Na kama ndivyo kakae nyuma kabisa kama waombolezaji wengine. Na bado baada ya msiba aliendelea kuitwa patokiani. Kila mtu afate sheria za imani yake. Hutaki kaa pembeni
 
Kama alihama akiwa na akili timamu Magige kosa lake nini?
Dawa ya wanawake viburi kama huyo mnayemtaja ni MATALA tu. Halafu kulia lia kinafiki si waume tukifa tutakuja kukuonana wabaya ipo siku atafufuka mtu ooooh

Magige ana Haki kuonyesha hisia zake. 2 yrs in a single bed naked mnaliona dogo.

Ngoja dawa ni kuandika mirathi hata kwa micheuko na kuirithisha tu tena naiweka kisheria zaidi
Ule wa mengi si ulikua kisheria pia? Na si walikua wamechuma na mke? Kama unadhan ni rahisi hivyo hayaa kajaribh tu. Zaidi uwatese wanao kisaikolojia. Labda kwa mwanamje mjinga mjinga
 
Nakuunga mkono, tuache kuwanyanyasa hao wanaotuhifadhi wake zetu wakitutesa. Magige nimemheshimu sana alikuwa na Upendo wa kweli. Kitendo cha kutupa ua kilionesha huyo mwanamke ni jeuri na hakuwa anampenda Marehemu
Upendo wa kweli akaenda kufumaniwa na bwana mwiningine mpaka marehemu apate heart attack?
 
Tena nasema yule aziza ni mstaarab sana nampa heko,yule magige angekutana na kichwa kilicho resi hata hilo shada asingeweka
Pumbavu zake kabisa,eti kisa mbunge!napata picha ndo ningekua mimi mbona show angeifurahia huyo mbunge
Yaan ningenpasuaaaaaaaaa.... na maua yaleee. Sema mpasue ila damu zake zisikurukieee. Matatizo mapya hayo
 
Wewe una mke.....??
... tena mzuri kweli kweli! Rejea post yako niliyo-quote; unauliza kama ninaweza kuhudhuria msiba wa mwanaume ambaye nilikuwa natembea na mkewe huku huyo mumewe (marehemu kwa sasa) akiwa anajua? Jibu langu ni huyo mwanaume kwa sasa si marehemu? Nitahudhuria.

NOTE: this is for illustration purposes only; siwezi kutembea na mke wa mtu.
 
Wanamchukulia hatua kwani alienda pale kuiwakilisha CCM?

Mimi nilidhani jeshi la polisi ndio lingedeal naye kwa kosa la 'trespassing'
Yes. Polisi walikua watu w akwanza kudeal naye.

Pili, chama kinapaswa kumchukulia maadili kwakua kuna misingi na kanuni za kuyaishi anayopaswa kuishi kama mwanachama wa chama cha mapinduzi na mbunge anayewakilisha wanamama na watoto bungeni kwa kutunga na kutetea sheria zao. Yeye anayaishi?
 
Kweli kabisa Mkuu. Tatizo kubwa ninalo liona ni kuwa wanawake wengi wa mjini hawataki kutengeneza wanaume zao wanao watakao wawe. Wao Wana taka mwanaume 'ready made and successfull'. Wengi wa type hiyo kiukweli they are already taken. Hapa ndiyo shida inaanzia. Hawataki mwanaume wa kuanza naye from the scratch.
Mwaaah
 
Afadhali maana katika hali kama ile, familia ya Marehemu ilitakiwa kutake charge si mke ambaye kila mtu alijua hakuwa anaishi na Marehemu!
Wewe ndo hujaelewa anasema katarina alishanyooshwa zamani za kale kulekule kaburini mbali na kushangilia kwamba ameshinda vita. Ama hujaona clip? Yeye na mashankupe menzake wanasema wameshinda. Kulikua na vita? Awajibishwe.
 
Amekwisha likoroga vya kutosha; kama ana akili hatafuata ushauri wako wa kidangaji!!! Mbunge ni lazima awe kioo kwa jamii, hivyo kujitoa ufahamu na kufanya mambo ya kukiaibisha chama kilichompa dhamana ya kukiwakilisha bungeni haikubaliki kimaadili!!!
Yes you are very RIGHT MBUNGE NI KIOO CHA JAMII. na kwa mujibu wa mila desturi na maadili ya JAMII YA WATANZANIA MKE ZAIDI YA MMOJA NI RUKSA!!! Na msibani hazuiwi mtu kuingia.
 
Serikali nijuavyo ina ukubali "mfumo zinaa" maana mahawara wakikiwa pamoja miezi kadhaa (sina uhakika )wanaheesabika ni wake wa ndoa Kiserikali.

Kama ndio hivyo, kwanini na yeye si mke Kiserikali? CCM si ndio yenye dhamana ya kuendesha serikali, sasa mnapatwa mchechetu wa nini akinsa Shaka?


Kubalini tu matokeo au ufuteni mfumo zinaa uliopo nchini.
Mfumo zinaa upo kweli. Unahalalishaje 'ke na 'me waishio pamoja kwa miezi 6 au zaidi kuwa ni mke na mume!? Yaani hata kama mimi nina mke halali, kwa ndoa halali ya Kikristo,nikaishi na mwanamke mwingine kwa muda wa miezi 6 au zaidi,eti huyo "automatically" anakuwa mke wangu!!! Inakuwajee niwe na wake wawili!!???
 
Back
Top Bottom