CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,511
2,000
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa umoja wa wanawake wa chama hicho Mkoa wa Arusha wakiongozwa na mbunge wa viti maalum, Catherine Magige.

Mbunge huyo jana Alhamisi Mei 27, 2021 alikwenda makaburini yalikokuwa yakifanyika mazishi ya mfanyabiashara Kuzula Madoda inayedaiwa kuwa ni mchumba wake. Madoda alifariki dunia Mei 24, 2021 na ameacha mke, Aziza Msuya na watoto.

Kitendo cha Catherine kwenda makaburini kiliibua hali ya sintofahamu kutokana na watu waliokuwa naye kuvunja geti na kuingia katika makaburi hayo ya familia.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na katibu wa itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka leo Ijumaa Mei 28,2021 inaeleza kuwa CCM inaheshimu katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na katiba ya CCM na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," inaeleza taarifa hiyo.

PIA, SOMA Pole Catherine Magige, hii iwe fundisho kwa wadada maarufu nchini

=====

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige.

CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi
28 Mei 2021
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,970
2,000
Unafiki tu, hawa nao si ccm je wao ni bora zaidi ya magige?
Makonda
Sabaya
Hapihapi
Nk
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,534
2,000
"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM,"
Mmechukua maamuzi sahihi vinginevyo chama kingeonekana kinajengwa na kundi la wahuni wasiozingatia mipaka yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom