benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,503
- 2,980
Wakati fulani mwaka 2018, aliyekuwa rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akizungumza katika kongamano la kujadili hali ya siasa na uchumi alisema
"SERIKALI YAKE HAINA MPANGO WA KUANZISHA UPYA MCHAKATO WA MAGEUZI YA KIKATIBA KWA SABABU KUNA MASUALA MENGINE YENYE KIPAUMBELEKWA SERIKALI"
Rais Magufuli alisema wazi kuwa hategemei kutenga fedha kwa ajili ya watu kula wakakae bungeni kujadili katiba, na akasisitiza kuwa hata kama kuna mtu (Wahisani) wako tayari kuipa Tanzania fedha kwa ajili ya mchakato wa Katiba basi pesa hizo zitolewe zikajenge Reli.
Huo ndio ulikuwa msimamo wa Hayati Dkt Magufuli ambapo ni dhahiri kuwa aliamini Katiba sio mwarubaini wa kila kitu
Miaka takribani Minne baadae, mwaka 2022, Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kila jitihada kurejesha hali ya utengamano wa Kitaifa. Amekutana na makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani ambao wengine walikimbia nchi na wengine walikuwa gerezani
Kubwa zaidi ni utayari wake wa kuruhusu mawanda ya kidemokrasia kuendelea kutanuka pamoja na Serikali na Chama chake CCM kuweka wazi kuwa milango ya mchakato wa kupata Katiba Mpya iko wazi hivyo kwa sasa itafutwe namna bora ya kufufua mchakato wa kupata katiba mpya ambao ulianza mwaka 2011 na kukwama mwaka 2014
Pamoja na mengi lakini kwa hili Rais Samia Suluhu Hassan anastahili pongezi kwani ni wazi angeweza kuwa na maamuzi kama ya mtangulizi wake lakini yeye ameamua kuruhusu kuanza kwa mchakato huu muhimu kwa Taifa na ni matumaini yetu, Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu, itatupatia Katiba Mpya Watanznia.
Mungu Ibariki Tanzania.