CCM kabla ya uteuzi wa Makonda ilikuwa imelala na kibaya zaidi ilikubali kirahisi kupokwa kazi za siasa na Serikali

Tao

Member
Nov 10, 2018
95
157
Leadership is not about authoritative role we hold in an organisation,rather it is about the choice of actions we prefer to take.

Donald McGannon

Ndani ya muda mfupi tokea alipoteuliwa kuwa Katibu wa Nec itikadi na uenezi taifa,Ndugu Paul Christian Makonda ameweza kufanya mambo ambayo wenzake ndani ya Chama hasa wajumbe wa secretariat ya taifa wameshindwa kufanya kwa miaka mitatu

Nitayataja mambo hayo kwa uchache.

1 Ameamsha CCM iliyokuwa imelala
CCM kabla ya uteuzi wa Makonda ilikuwa imelala na kibaya zaidi ilikubali kirahisi kupokwa kazi za siasa na serikali, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Chama chenyewe.

Hii inatokana na sababu kuu mbili,kwanza ni baadhi ya viongozi wakuu kutokuwa na mvuto na pili ni kwasababu Chama kilijiweka mbali na matatizo na changamoto za wananchi.

2. Amerudisha imani na matumaini ya Wananchi kwa kanda ya ziwa kwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan
Makonda ameondoa dhana potofu iliyokuwa imejengeka kwa baadhi ya wananchi wa kanda ya ziwa kuwa kanda hiyo imetengwa na serikali ya awamu ya sita kimaendeleo na kisiasa kutokana na hisia potofu kuwa miradi ya maendeleo ikiwemo iliyokuwa imweanzishwa na Hayati JPM ukiondoa Daraja la Busisi inahujumiwa na kwamba watu wa kanda ya ziwa wanapokonywa uongozi ndani ya Chama na serikali.Hotuba za Makonda alizozitoa kanda ya ziwa na mapokezi yake yamerudisha matumaini huko Lake zone ambayo ndio mpini wa ushindi katika uchaguzi wa Rais.

3. Amerudisha ule uwezo wa CCM kuisimamia serikali yake
CCM ndiyo iliyounda serikali hivyo ina wajibu mkubwa wa kuisimamia.

Kabla ya ujio wa Makonda mawaziri na watendaji serikalini walikuwa wakifanya wanayotaka na Chama kikafyata mkia.

Hali hiyo imebadilika ghafla baada ya uteuzi wa Makonda kwani wazembe wanatajwa na kupewa maelekezo na Chama mbele ya umma.

Hiyo ndio iliyofanya CCM iendelee kuaminiwa na wananchi na ninafananisha ujio wa Makonda na ule ujio wa Mzee Kinana alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015

4. Amekuwa kiuingo muhimu katika kufanikisha ushindi wa Dr Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu ujao 2025 kama Mwenyezi Mungu atampa uhai

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr Samia Suluhu Hassan inafanya mambo mengi mazuri kwa wananchi katika vita dhidi ya umaskini na kukuza uchumi lakini wananchi wengi hawajaelimishwa ipasavyo kutokana na ukweli kuwa wasaidizi wa Dr SSH hawamsemei ipasavyo bali wanajisemea wao wenyewe tofauti na ilivyokuwa wakati wa uongozi wa Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli.

Makonda anamsemea vilivyo Bosi wake vilivyo na kama moto huo utaendelea ni hakika atapata ushindi wa kishindo 2025.
 
Katika matamko yote anayoyatoa ni lipi limetekelezwa? Maiti zinazozuiliwa kwenye Mochwali mbalimbali katika Mahospitali ya Serikali kwa kudaiwa gharama za matibabu zimeachiwa ili Ndugu wakazike?

Wagonjwa mbalimbali waliopona lakini wanashikiliwa na Hospitali mbalimbali za Serikali kwa kudaiwa gharama za matibabu wameachiwa warudi majumbani kwao?
 
Katika matamko yote anayoyatoa ni lipi limetekelezwa??maiti zinazozuiliwa kwenye Mochwali mbalimbali katika Mahospitali ya Serikali kwa kudaiwa gharama za matibabu zimeachiwa ili Ndugu wakazike??wagonjwa mbalimbali waliopona lakini wanashikiliwa na Hospitali mbalimbali za Serikali kwa kudaiwa gharama za matibabu wameachiwa warudi majumbani kwao??
Haya ndio maneno sasa, haswa je maiti zote zimepewa ndugu wakazike? Au ni usanii tu wa kutatua kisa kimoja kama anatatua tatizo la kifamilia?

Hapo ilikuwa asemee nchi nzima kuwa ni marufuku kuzuia maiti au mgonjwa asiekuwa na hela hospitali
Umepiga mule mule kama wanaelewa na waelewe la sivyo waendelee kuwaburuza mafala
 
Kwahiyo chama chote Cha CCM makonda ndo mkombozi. Na bila makonda serikali na CCM yote walikuwa Kama hawapo bhasi tuna Safari ndefu kupiga hatua kama taifa.
 
Leadership is not about authoritative role we hold in an organisation,rather it is about the choice of actions we prefer to take.

Donald McGannon

Ndani ya muda mfupi tokea alipoteuliwa kuwa Katibu wa Nec itikadi na uenezi taifa,Ndugu Paul Christian Makonda ameweza kufanya mambo ambayo wenzake ndani ya Chama hasa wajumbe wa secretariat ya taifa wameshindwa kufanya kwa miaka mitat...
uko rada mbaya sana 💪👌
 
Leadership is not about authoritative role we hold in an organisation,rather it is about the choice of actions we prefer to take.

Donald McGannon

Ndani ya muda mfupi tokea alipoteuliwa kuwa Katibu wa Nec itikadi na uenezi taifa,Ndugu Paul Christian Makonda ameweza kufanya mambo ambayo wenzake ndani ya Chama hasa wajumbe wa secretariat ya taifa wameshindwa kufanya kwa miaka mitatu

Nitayataja mambo hayo kwa uchache.

1 Ameamsha CCM iliyokuwa imelala
CCM kabla ya uteuzi wa Makonda ilikuwa imelala na kibaya zaidi ilikubali kirahisi kupokwa kazi za siasa na serikali, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Chama chenyewe.

Hii inatokana na sababu kuu mbili,kwanza ni baadhi ya viongozi wakuu kutokuwa na mvuto na pili ni kwasababu Chama kilijiweka mbali na matatizo na changamoto za wananchi.

2. Amerudisha imani na matumaini ya Wananchi kwa kanda ya ziwa kwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan
Makonda ameondoa dhana potofu iliyokuwa imejengeka kwa baadhi ya wananchi wa kanda ya ziwa kuwa kanda hiyo imetengwa na serikali ya awamu ya sita kimaendeleo na kisiasa kutokana na hisia potofu kuwa miradi ya maendeleo ikiwemo iliyokuwa imweanzishwa na Hayati JPM ukiondoa Daraja la Busisi inahujumiwa na kwamba watu wa kanda ya ziwa wanapokonywa uongozi ndani ya Chama na serikali.Hotuba za Makonda alizozitoa kanda ya ziwa na mapokezi yake yamerudisha matumaini huko Lake zone ambayo ndio mpini wa ushindi katika uchaguzi wa Rais.

3. Amerudisha ule uwezo wa CCM kuisimamia serikali yake
CCM ndiyo iliyounda serikali hivyo ina wajibu mkubwa wa kuisimamia.

Kabla ya ujio wa Makonda mawaziri na watendaji serikalini walikuwa wakifanya wanayotaka na Chama kikafyata mkia.

Hali hiyo imebadilika ghafla baada ya uteuzi wa Makonda kwani wazembe wanatajwa na kupewa maelekezo na Chama mbele ya umma.

Hiyo ndio iliyofanya CCM iendelee kuaminiwa na wananchi na ninafananisha ujio wa Makonda na ule ujio wa Mzee Kinana alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015

4. Amekuwa kiuingo muhimu katika kufanikisha ushindi wa Dr Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu ujao 2025 kama Mwenyezi Mungu atampa uhai

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr Samia Suluhu Hassan inafanya mambo mengi mazuri kwa wananchi katika vita dhidi ya umaskini na kukuza uchumi lakini wananchi wengi hawajaelimishwa ipasavyo kutokana na ukweli kuwa wasaidizi wa Dr SSH hawamsemei ipasavyo bali wanajisemea wao wenyewe tofauti na ilivyokuwa wakati wa uongozi wa Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli.

Makonda anamsemea vilivyo Bosi wake vilivyo na kama moto huo utaendelea ni hakika atapata ushindi wa kishindo 2025.
Naunga mkono hoja, tunampongeza Makonda kwa amsha amsha, ila tumemshauri aende taratibu, mwenda pole hajikwai. Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!
P
 
Naona unajaribu kumfunga kamba za viatu Makondo kama yeye alivyomfungaga Ridhi1 na akaonekana, pigana ndugu ajira nazo nchi hii ni ngumu mno bora kuonekana zoba mwisho wa siku unaweza onekana maisha yakabadilika, kilalakheri mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom