CCM jitengeni na kundi la Wasiojulikana

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Kabla ya vyama sisi sote ni watanzania.

Moja ya imani za CCM ni kuwa binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

Tumefikaje huku kwenye kuuwana, kutekana, kutesana, kupotezana, kubambikiziana kesi na yote yenye ukakasi huu?

Ilikuwaje kina Sabaya wakatambulika kama vijana wazalendo pamoja na matendo yao maovu?

IMG_20211026_051336_047.jpg

Kundi la watu wasiojulikana ni halisi, lipo na rasmi limejipenyeza katika utawala wa nchi hii. Pole pole kalitambua kama parallel power na kuwa kwa sababu ya kundi hilo, CCM wala hamsikilizwi tena katika uendeshaji wa nchi.

Si kweli kuwa kundi hili linawatumia ninyi kama koti tu, la kufichia madhambi yao? Si kweli kuwa nyie mko kimya kwa sababu ya vipande 30 vya pesa linavyowapa baadhi yenu?

Hamuioni chuki inayomea nchini kwa sababu ya kundi hili? Nanyi mmeridhia kufungamanishwa pamoja na kundi la wauwaji hawa?

Kulifumbia macho kundi hili ni kukubali kuwa mshirika wa haramu zake.

IMG_20211026_051305_676.jpg

Kulifumbia macho kundi hili hakutawaacha salama siku zote.

Ushauri wa bure kwenu kama nchi hii mnaipenda, basi jitengeni na kundi hili.

Kufanya hivyo hadharani kutawapa uhalali wa kujivua madhambi yao.

Kila mmoja na akaubebe msalaba wake mwenyewe.
 
Tunakubaliana CCM haishindi uchaguzi wowote kwa kura za watanzania, "ushindi" wake unatokana na ushirika usio na hekima kati yake na wasiojulikana, polisi, tume ya uchaguzi, kura feki kwenye mabegi meusi n.k

Ukiwatenganisha CCM na wasiojulikana maana yake unataka kuwafuta kwenye ramani ya siasa za Tanzania, hata wale walioko huko CCM "wanaota" urais wanajua watatimiza ndoto zao kwa msaada wa wasiojulikana, sio wapiga kura kwani walishatuasa; "hata tusipowachagua, wao ndio watatangazwa washindi".
 
Tunakubaliana CCM haishindi uchaguzi wowote kwa kura za watanzania, "ushindi" wake unatokana na ushirika usio na hekima kati yake na wasiojulikana, polisi, tume ya uchaguzi, kura feki kwenye mabegu meusi n.k

Ukiwatenganisha CCM na wasiojulikana maana yake unataka kuwafuta kwenye ramani ya siasa za Tanzania, hata wale walioko huko CCM "wanaota" urais wanajua watatimiza ndoto zao kwa msaada wa wasiojulikana, sio wapiga kura.

Mkuu kwa mwenye hekima, ni heri fedheha kuliko kuwa sehemu ya ufedhuli. Ni heri kuukosa urais kama kinachohitajika kuupata ni kuuwa, kutesa, kuteka, kupoteza au kubambikizia watu kesi.

Tofauti yake itakuwa nini na kusaka utajiri na viungo vya binadamu kama kafara?

Nirekebishe kidogo hapo kwenye mahusiano yasiyo na hekima.

List nzima uliyoitaja hapo inakamilika kwa sababu wasiojulikana wamejipenyeza au kupenyezwa huko polisi, tume, mahakamani nk:

Kama CCM siyo adui, mchawi wetu ni nani?

"Inasemekana wajumbe wake hao wako kila mahali na katika kila idara wanayoiita nyeti. Si mahakamani, polisi hadi JF. Kina Sabaya ni baadhi yao. Wameigeuza nchi kuwa yenye huzuni na vilio badala ya kuwa yenye furaha na bashasha."
 
Mikono ya maccm yote imejaa damu hivyo hakuna atakayethubutu kumnyooshea kidole mwenzie. Yote ni mauaji hayo.

Pamoja na yote mkuu shweitan peke yake ndiyo kesha nyimwa nafasi ya toba.

Kujitenga nao haiwezi kuangaliwa kuwa ni sawa na kuendelea kuambatana nao.

IMG_20211025_173023_914.jpg

Kama vipi wasiojulikana waanzishe chama chao.
 
Mkuu kwa mwenye hekima, ni heri fedheha kuliko kuwa sehemu ya ufedhuli. Ni heri kuukosa urais kama kinachohitajika kuupata ni kuuwa, kutesa, kuteka, kupoteza au kubambikizia watu kesi.

Tofauti yake itakuwa nini na kusaka utajiri na viungo vya binadamu kama kafara?

Nirekebishe kidogo hapo kwenye mahusiano yasiyo na hekima.

List nzima uliyoitaja hapo inakamilika kwa sababu wasiojulikana wamejipenyeza au kupenyezwa huko polisi, tume, mahakamani nk:

Kama CCM siyo adui, mchawi wetu ni nani?

"Inasemekana wajumbe wake hao wako kila mahali na katika kila idara wanayoiita nyeti. Si mahakamani, polisi hadi JF. Kina Sabaya ni baadhi yao. Wameigeuza nchi kuwa yenye huzuni na vilio badala ya kuwa yenye furaha na bashasha."
Kwao siku hizi kuongoza no sio kuongoza, ni kutawala, hawatawali wananchi, wao wanatafuta madaraka ili wapate 10% kwa manufaa yao na familia zao, wabebane wao kwa wao kwenye kula keki ya taifa, vyeo vikubwa serikalini wapewe watoto wao; na mwisho waibe wapate ya kuhonga ili kutimiza ndoto zao za kuwa viongozi wa nchi mbele ya safari.

Halafu wenye midomo [ Katiba Mpya ] wote mnawekwa gerezani kwa kesi za uongo ili wapate nafasi nzuri ya kufanya mambo yao, na ikibidi wanahonga vyeo majaji ili watoe maamuzi ya kuwafurahisha wao, tupo kwenye circle moja chafu sana tunahitaji miujiza tujinasue hapa tulipo.
 
Sabaya amefungwa kwa sasa sijui unataka kitu gani mkuu au dhamira inakusuta?

Twende na Mbowe sasa, haki itendeke naye apate haki yake.
 
na walivyo wengi wanaweza kushinda

Wakipigiwa ukelele kama wa mwizi nao wanapiga ukelele huo vidole wakimnyooshea CCM, JK na hata Samia. Wao nyuma ya pazia.

Kumulikwe nyuma ya pazia kila mtu akajishindie mechi zake.

Waanzishe chama wana uzoefu wa wizi, uuwaji, utekaji, na kubambikia watu kesi na hata hukumu - watashinda wakawe sole power.

Katiba hairuhusu parallel power.
 
Wakipigiwa ukulele kama wa mwizi nao wanaupiga ukelele huo vidole wakimnyooshea CCM, JK na hata Samia. Wao nyuma ya pazia.

Kumulikwe nyuma ya pazia kila mtu akajishindie mechi zake.

Waanzishe chama wana uzoefu wa wizi, uuwaji, utekaji, na kubambikia watu kesi na hata hukumu - watashinda wakawe sole power.

Katiba hairuhusu parallel power.
Kitakuwa chama kama Taliban
 
CCM ni kikundi cha hovyo sana. Hakijawahi kuwa chama tangu Mwalimu Nyerere alipong'atuka rasmi kama Mwenyekiti wake.
 
Ccm ni kikundi cha hovyo sana. Hakijawahi kuwa chama tangu Mwalimu Nyerere alipong'atuka rasmi kama Mwenyekiti wake.

Hata enzi za Sodoma na Gomora watu walipokuwa wachafu wa matendo kuliko maelezo, wasafi wachache walikuwapo.

Ushahidi wa wazi, Nuhu na binti zake wakaiepuka hasira kali ya Mola.

CCM kama hili si genge lao kweli kama anavyo lalama Polepole of recent, wajitenge hadharani na kundi hili la kihalifu sasa.

Hala hala kabla ya hatari.
 
Polepole ni kajitu kanafiki sana! Hutakiwi kukaamini kwa 100%
 
CCM ndio mratibu wa magenge yote ndani ya nchi hii,wametufanya mateka na kuondoa furaha nchini,watu wanaishia kwa wasiwasi na chuki, ukigeuka huku police, ukigeuka huku tume ya uchaguzi,ukigeuka huku wasiojulikana, ukigeuka huku msajili wa vyama, wote hao ni mbeleko ya CCM
 
Mkuu kuna CCM na kundi la watu wasiojulikana.

Nikimnukuu pole pole yuko wazi. "Kuna parallel power ambapo sasa hata CCM hawashirikishwi kwenye kuendesha nchi
"

IMG_20210911_000004_180.jpg

Nyuma ya usukani kuna anayejua Lijenje Ben Azory walipo. Anawajua waliotaka kumwua Lissu.

Hao ndiyo wenye kura za kwenye mabegi. Ndiyo wabambikaji kesi na ndiyo wabambika hukumu pia.

Wapo kwenye idara zote wanazoziita nyeti zikiwamo polisi, mahakama, nk hadi JF.

Uzuri kama mapaka nyau yenye kengele shingoni hawawezi kujificha hata kwa yaliyomo tu kwenye mabandiko na maoni yao.

Watu hawa ni waovu sana. Wauwaji, watekaji, watendaji na wapoteza watu.

CCM iko huru kuendelea kujifungamanisha nao au kuwakana hadharani, kwani malipo ni hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom