CCM jitengeni na kundi la Wasiojulikana

Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,244
2,000
Kabla ya vyama sisi sote ni watanzania.

Moja ya imani za CCM ni kuwa binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

Tumefikaje huku kwenye kuuwana, kutekana, kutesana, kupotezana, kubambikiziana kesi na yote yenye ukakasi huu?

Ilikuwaje kina Sabaya wakatambulika kama vijana wazalendo pamoja na matendo yao maovu?

View attachment 1986970

Kundi la watu wasiojulikana ni halisi, lipo na rasmi limejipenyeza katika utawala wa nchi hii. Pole pole kalitambua kama parallel power na kuwa kwa sababu ya kundi hilo, CCM wala hamsikilizwi tena katika uendeshaji wa nchi.

Si kweli kuwa kundi hili linawatumia ninyi kama koti tu, la kufichia madhambi yao? Si kweli kuwa nyie mko kimya kwa sababu ya vipande 30 vya pesa linavyowapa baadhi yenu?

Hamuioni chuki inayomea nchini kwa sababu ya kundi hili? Nanyi mmeridhia kufungamanishwa pamoja na kundi la wauwaji hawa?

Kulifumbia macho kundi hili ni kukubali kuwa mshirika wa haramu zake.

View attachment 1986971

Kulifumbia macho kundi hili hakutawaacha salama siku zote.

Ushauri wa bure kwenu kama nchi hii mnaipenda, basi jitengeni na kundi hili.

Kufanya hivyo hadharani kutawapa uhalali wa kujivua madhambi yao.

Kila mmoja na akaubebe msalaba wake mwenyewe.
Eti watu wasiojulikana,kumbe hawakutakiwa wajulikane,kwa kulewa majukumu waliyokuwa wamepewa, walifanya yao binafsi pia
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,448
2,000
Eti watu wasiojulikana,kumbe hawakutakiwa wajulikane,kwa kulewa majukumu waliyokuwa wamepewa, walifanya yao binafsi pia

Baada ya kufariki baba wa taifa watu waliokuwa na jukumu la kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa kama jukumu lao pekee walipanua uwanja kwa maslahi yao.

Badala ya kuwafanyia tathmini zaidi wateuliwa wa nafasi mbalimbali wakaanza kujipenyeza wao kwenye nafasi zote nyeti.

Kansa ikaanza kumea. Hawakuwa na mamlaka ya kukamata. Wakaanza kukamata, kutesa, kupoteza na hata kuuwa.

Hawakuwa na mamlaka ya kutisha mtu, wakaanza kubambika kesi na kushinikiza rushwa.

Hawakutakiwa kutambulika katika zaidi ya yule mkuu wao katika wilaya. Mambo yakageuka ikawa unanijua mimi nani? Baa ndiyo usiseme..

Sumaye, Pinda wakawa wakaingia PM, Kingai akawa RPC na Sirro IGP. Pana mlango wa kutokea hapo?

Waliokuwa walinzi nje wakawa vibosile ndani. Nani amfunge paka kengele?

Abarikiwe sana bwana Zacharia mwamba wa kanda ya ziwa usiotikisika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom