CCM inadilishe jina la chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM inadilishe jina la chama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanamabadiliko, Nov 3, 2010.

 1. m

  mwanamabadiliko JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 340
  Trophy Points: 80
  CCM wanapaswa kutafuta jina lingine, maana lilianza wakati ule wa chama kimoja na wanalitumia kurubuni wajinga ili wapate kura. kuanzia mfumo wa vyama vingi walipaswa kulibadili mana hili jina lilikuwa la watanzania wote.

  Pia mali na viwanja vya mpira vilivyopatwa wakati wa chama kimoja wavirudishe kwa wananchi mana hata mashabiki wa chadema ni wananchi, wasitaifishe mali ya umma kuwa ya chama kwa kisingizio cha multipatism. lasi hivyo na sisi upinzani tutalitumia jina hilo na bendera mana ni mali ya wananchi na si individual kama CCM.

  NI LAZIMA WATAFUTE JINA LAO KUWAKILISHA HAO MAFISADI NA WEZI HII ITASAIDIA KUFANYA MABADILIKO KTK NCHI

  :A S cry::A S cry: nalia kwa uchungu
   
 2. Sanja

  Sanja JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Kuna mapinduzi ya aina tofati katika maisha ya binadamu ya kila siku.Lakini hapa nitaomba mnisaidie kwenye upande wa siasa na utawala wa nchi hasa Tanzania. Hivi ikitokea (inawezekana kutokea kwani sisi ni binadamu kama wengine ambao yanawatokea)yatakayo badili utawala uliopo na baada ya hapo kikaundwa chama cha siasa kinachoendana na kitendo cha mapinduzi kinachoitwa chama cha mapinduzi kinachojumuisha wanamapinduzi watawala katika mazingira ya siasa na uhalisia wa jina nini mtizamo/maoni yako. Inawezekana kuna vyama vingine vyenye majina yanayotokana na kitendo/vitendo fulani ambavyo vinaweza kufanywa na makundi mengine na bado vikasajiriwa.
  Maoni yangu ni vyama vya namna hii viwe vinauendelezo wa jina linalotokana na kitendo na mlengo wao,mfano Chama cha mapinduzi ya Kijani, Chama cha watetea haki za wananchi, na n.k
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Chama kuitwa chama cha mapinduzi na kikasajiriwa kwa jina hilo inachanganya.

  Kuna mapinduzi ya aina tofati katika maisha ya binadamu ya kila siku.Lakini hapa nitaomba mnisaidie kwenye upande wa siasa na utawala wa nchi hasa Tanzania. Hivi ikitokea (inawezekana kutokea kwani sisi ni binadamu kama wengine ambao yanawatokea)yatakayo badili utawala uliopo na baada ya hapo kikaundwa chama cha siasa kinachoendana na kitendo cha mapinduzi kinachoitwa chama cha mapinduzi kinachojumisha wanamapinduzi watawala katika mazingila ya siasa na uhalisia wa jina nini mtizamo/maoni yako. Inawezekana kuna vyama vingine vyenye majina yanayotokana na kitendo/vitendo fulani ambavyo vinaweza kufanywa na makundi mengine na bado vikasajiriwa.
  Maoni yangu ni vyama vya namna hii viwe vinauendelezo wa jina linalotokana na kitendo na mlengo wao,mfano Chama cha mapinduzi ya Kijani, Chama cha watetea haki za wananchi, na n.k


  Fanyia kazi niliyohighlight...​
   
 4. Sanja

  Sanja JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Kikasajiriwa=kikasajiliwa, mazingila=mazingira,kinachojumisha=kinachojumuisha. Bila shaka nimesahihisha na tunaweza kuendelea
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Sanja.
  Unapotaka kusahihisha unaweza kufanya hivyo kwenye original post yako, ukiwa ume/sign in utaiona post yako na chini utaona kitufe cha edit, itatokea katika kisanduku kama kile ulichotumia kupost original, utafanya masahihisho halafu unabonyeza kitufe cha save changes.
   
 7. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,457
  Likes Received: 1,383
  Trophy Points: 280
  Wakuu naeleza kwa kifupi sana chanzo cha Chama Cha Mapinduzi kuishiwa sera. Ni jina...... Toka kianzishwe hata jina lake siyo zuri! Kinaonekana kuwa si chama cha mrengo wowote kwa maana ya jina ku-reflect dira ya chama. Kinazungumzia "mapinduzi". Ni mapinduzi gani hayo? Sasa hivi mambo ya harakati za ukombozi yalikwisha isha na sasa ni kuwa na sera za kuleta maendeleo kwa wananchi. Sasa hapa CCM walipokibatiza chama jina hilo walikuwa na mawazo ya harakati za kiukombozi-kombozi tu.
  Na ndiyo sababu mafisadi wameweza kujipeneza na kuingia bila shida maana mrengo wa chama haujulikani wala sera. Hata jina pia halijulikani linahusiana vipi na watanzania kimantiki.
  Ili kiweze kutekeleza azma yake ya kujivua gamba inatakiwa hata jina la chama libadilishwe!!!
  Ni hayo tu wakuu.
  Nawaomba mchangie hoja.
   
 8. W

  Wangama guy Senior Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siyo tu kibadilishwe jina, kifutiliwe mbali katika uso wa dunia. Miaka 50 kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi hii. Tanzania siyo nchi maskini hata kidogo! Rasilimali nyingi zinaishia kunufaisha kikundi kidogo tu cha mafisadi, huku wananchi wengi wakiishi katika lindi la umaskini mkubwa! ahha ... kwanza nikiendelea kusema naweza kupata kichefuchefu!
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Arumeru mambo yanaendaje huko?
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nani wakubadilisha jina hilo?
   
 11. F

  FUSO JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  nyie na hoja zenu bana-- wamewaambia wanajikoboa magamba ili chama kijizae upya -- sasa hata zoezi hili halijakamilika nyie mnakuja na jingine -- jamani hebu wapeni muda wa kutosha magamba mengine magumu kukoboka, yahitaji maji yawe ya moto saana.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nashauri kiitwe chodema ili kuwachanganya wananchi,
  kwa sbb hakuna namna ya kukiponyesha.:lol::eyebrows:
   
 13. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Cjui wanataka Kumpindua nani tena hapa......Mapinduzi ya viwanda....mmh! Ilikuwa Ulaya. Tanzania Mapinduzi ninayoyafahamu aliongoza John Okelo kule visiwani....kwa kweli hili jina Lina utata cjafahamu mwalimu JULIASI alilenga nini maana hata hamu ya kufuatilia hili chama sinaga......nahofia tu wasije siku wakapigwa chini na Upinzani ndio waTANZANIA tukajua maana Halisi ya JiNa Hili. mmh!
   
 14. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jina pekee sio linalo elekeza sera ya chama bali hata katiba yake hivi ilivyo haina mwelekeo wa kuelekeza Taifa kwenye maendeleo. Kama katiba ya Tanzania inavyo bidi kubadilishwa na kadhalika katiba ya CCM nayo inabidi kubadilishwa. Na ikibadilishwa kutakuwa hamna haja ya kuvuwa magamba. Hayo magamba ni kukifanya chama kiwe cha kurithisha majukumu na uongozi. Kinyume na hivi, ni bora kifutwe kabisa.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwani si walishabadilisha na kukiita chama cha magamba au?
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  uko sahihi kabisa mkuu kwani bila kitu kama hicho kutokea Tz haitaweza kusema imejikomboa
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Washaonyesha dhahiri hawataweza kujikoboa na sasa wameamua kujiunga na hao magamba ktk kufisadi
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Labda mapinduzi yenyewe ni wao kupinduliwa na chama kingine au jeshi kushikiliwa na dola
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Umenifanya nicheke.... Uchaguzi wa mwaka jana kule Karatu walifikiri Dr wa ukweli atagombea ubunge, ili kuwachanganya wananchi CCM wakamweka mtu anayeitwa Dr Willbard Slaa wakati yule original ni Dr. Wilbroad Slaa, kwa hiyo si ajabu kwa akili hizi za kina Mwigulu unaweza sikia CCM wamependekeza iitwe CHODEMA.
   
 20. W

  William wa Ukweli Member

  #20
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wazo huru lenye nia ya kuipandisha chati CCM.

  Dhana ya utumizi wa neno 'Mapinduzi' kwa sasa imepitwa na wakati, neno 'Makini' likitumika badala yake, litasaidia sana kuungwa mkono na wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao, mwaka 2015. Sambamba na mabadiliko haya, kuwepo na mkakati maalum wa kupata safu mpya ya uongozi wa juu wa chama ngazi ya taifa baadae mwaka huu.

  Chama Makini + Viongozi waadilifu = Taifa lenye Maendeleo.
   
Loading...