Mara wamsimika Makonda na kumpa jina la Manyama, aagiza bodaboza ziachiliwe, Mizigo ya magendo itozwe kodi na iachiliwe

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,395
9,676
Ukiona mkoa wa Mara unafanya jambo hili ujuwe wewe ni kidume kwelikweli. Kule hakunaga chawa.

Ngoja tuone mwisho wa Makonda.

Akabidhiwa kifimbo cha Nyerere.

======

MAKONDA AAGIZA BODABODA ZIACHILIWE

"Ninafahamu ya kwamba zipo bodaboda zilizotumia fursa ya mpaka kufanya biashara za magendo hilo halipingiki na mimi ni msema ukweli lakini wapo Wananchi ambao wameendelea kufanya shughuli zao katika kusongesha maisha yao na hili sio la kupinga"

"Sasa Maelezo ya CCM na Mkuu wa Mkoa upo hapa Mhe. Mtanda upo hapa, na nimemsikia Mhe. Waitara anasema nimpigie simu Waziri wa Fedha, sasa hili swala wala sio la kupiga simu ni maelekezo tu ya Chama Cha Mapinduzi, kuanzia sasa leo tarehe 14 hadi ifikapo kesho tarehe 15 pikipiki zote zilizokamatwa Silali warudishiwe pikipiki zao na kama kuna mali zilizokamatwa watozwe kodi warudishiwe mali zao na kuanzia hapo utaratibu wa kisheria ufuate mkondo wake, wapeni fursa watu wafanye biashara kama ni bodaboda alipe kodi, ushuru achukue bidhaa auze, CCM Oyeee"

Cde. Paul Makonda
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Wananchi wa Tarime Mkoani Mara , leo tarehe 14 Novemba, 2023.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#TunaendaNaMama
 
Mkoa wa mara wamsimika makonda na kumpa jina la Manyama.

Ukiona mkoa wa Mara unafanya jambo hili ujuwe wewe ni kidume kwelikweli. Kule hakunaga chawa.

Ngoja tuone mwisho wa Makonda.

Akabidhiwa kifimbo cha Nyerere.
Kwa hiyo unataka kuwapa ujumbe wana JF kwamba Komredi PCM anatakiwa kuwa na harufu ya nyama muda wote huku zingine zikining'inia mdomoni na mikononi?

Nini maana ya 'MANYAMA' katika makabila haya ya mkoa wa Mara?
1. Kurya
2. Jaluo
3. Jita
4. Kerewe
5. Zanaki
6. Simbiti
7. Ikoma
8. Ikizu
9. Kwaya
10. Suba na
11. Sizaki?

*Kati ya makabila tajwa hapo juu atakuwa amesimikwa na Wajita waliochanganya na Wakurya
 
Ukiona mkoa wa Mara unafanya jambo hili ujuwe wewe ni kidume kwelikweli. Kule hakunaga chawa.

Ngoja tuone mwisho wa Makonda.

Akabidhiwa kifimbo cha Nyerere.
Eti Mara 'hatunaga uchawa' aliyekudanganya ni nani? Umesahau tukio la Kangi Lugola kumtukuza Jiwe kwa kumpa hadhi ya Yesu? Hadi ikapelekea Magufuli kuitwa 'Mheshimiwa Mungu'? Au Kangi Lugola hatokei Mara?
 
Back
Top Bottom