Hakika CHADEMA mnastahili pongezi, maana najua Sukununu kama mleta mada Tz walikuwa wengi lakini wamebadilika!! Vimebaki vichwa vya uyoga kama huyu vichache!! Kazeni mkanda msichoke!!
Historia inaonyesha ya kuwa CCM ndio chama peeke kilichodumu madarakani kwa muda mrefu hapa Africa Mashariki...Hii ni pongezi.Pia ni chimbuko la vyama viwili...Chama hiki kimeongoza kwa muda mrefu serikali yetu tukufu..Lakini kwa sasa kinapoteza mvuto kila uchao na ni kutokana na watu na sio mfumo....je kwa kuwa pia kimetokana na chimbuko la vyama viwil mbona kisibadilishe jina hususani kipengele cha mapinduzi ili kuleta ladha mpya katika siasa mpya za Tanzania?
Hata ikibadili jina haitasaidia kitu. Waliposema wanajivua GAMBA ndiyo ilikuwa nja sahihi. Ila GAMBA limegoma kuvuka, hivyo wamebakia na utendaji mbovu na kuwa pango la wanyang'anyi (MAFISADI). Wameendelea na kujinufaisha bila kumjali mwanannchi na wameshindwa kutekeleza sera za kumkomboa mwananchi. Kimekuwa chama cha kujinufaisha wao viongozi na kuleta uozo kwenye kila pande serikalini.
Chama cha Mapinduzi Maarufu kama CCM kipo mbioni kubadili jina ili kubadilisha taswira ya Chama hicho katika Jamii ya Watanzania. Watonyaji wanasema kwamba hii ndiyo karata ya Mwisho ambao chama hiki chenye umri mkubwa kuliko vyote hapa nchini kimeamua kuitumia baada ya mipango mikakati yote iliyotumika mpaka sasa kujihakikishia kuwa kinabaki madarakani 2015 kutozaa matunda kabisa.
Falsafa nyuma ya mpango huu ni kutumia jina jipya kukonga tena nyoyo za waTanzania ili 2015 waweze kushinda.
Licha ya kubadilisja jina Pia chama hiki kikongwe kitafanya mabadiliko machache ndani ya chama ili kurejesha imani kwa wa Tanzania
Mpango huu umekuja baada ya jitihada zote walizotumia kuua upinzani kutozaa matunda. Mtonyaji mmoja amesema kwa vyama kama NCCR, CUF waliishia ngazi za chini kabisa katika kuvimaliza kisiasa lakini kwa CHADEMA hali imekuwa tofauti. Hivyo baada ya external strategies kukwama wameamua watumie internal strategies kama kubadili jina. Hii ni pamoja na kujaribu kukinusuru chama na makundi hasimu yaliyopo ndani ya chama yanayotaka kuwania Urais mwaka 2015
Chanzo: Habari toka vyanzo vya kuaminika Dodoma White house na Lumumba Dar ambazo zimevuja na hazijathibitiswa na wasemaji maana ni toka vyanzo vya ndani sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.