mfanyakazfake
Member
- Feb 14, 2023
- 17
- 34
Ccmchipukizi maana yake nii?
Wana faida gani kwa chama?
Kwanini wawe watoto wengi wa viongozi na watu mashuhuri ndani na nje ya chama na sio mtoto wa mkulima na mfugaji?
Je, mtoto wa mkulima na mfugaji huko Nanjilinji, kantalamba, ng'alita, kishumundu, Gamboshi, nshamba na huko kwingineko ambako watoto wa wakulima na wafugaji wanapatikana ambao pengine wana uwezo mkubwa wa kiuongozi kuliko hata hawa tulionao, je mchakato uliwafikia hawa watoto kweli?
Je, mchakato wa ccm chipukizi una mazingira sawa au ndo mwenye kamba ndefu ndo atakula pakubwa zaidi?
Kama ndo tunaenda kwa kufahamiana, je ccm na nchi ya Tanzania ndio kusema inaenda kuwa mali ya watu au familia chache miaka michache ijayo?
Naona baada ya mchakato vijembe na majigambo kutoka kwa wazazi wa watoto waliochaguliwa vinatamalaki ndo kusema kulikua na vita kubwa sana kwenye mchakato mzima au ndo wanajaribu kutuambia nini hao viongozi wetu?
Je, CCM na serikali yake mko tayari kuwaona chadema na vyama vingine wakianzisha hizo chipukizi? Na kama mko tayari ruhusuni muone halafu baada ya miaka 5 mfanye tathmini kama bado mtakua na chama au gari bovu ambalo kila mtu hatamani kulipanda tena, watoto smart wanatoka familia duni ambazo ccm haikuona umuhimu wao, huko ndo chadema na ACT wazalendo watabeba vijana wao na sio hao wa kwenu watoto wa akina fulani?
Jifunzeni kipindi cha JPM alikiondoa chama kutoka kua chama cha familia fulani na kuwa chama cha watanzania wote na ndo ulikua mwanzo wa ccm kupendwa tena na watz, lakini kwa hiki mnachokifanya sasa hivi jiandaeni kisaikolojia hakina hatima nzuri kwa chama cha mapinduzi, kuna watu wenye nia ovu na mnawaruhusu agena zao kupenya ndani ya chama, chama kitakosa utulivu, chama kitagawanyika na chama kitakosa ushawishi kwa wananchi tena na ndo utakuwa mwanzo wa upande wa pili kupata nguvu kubwa zaidi na kujenga ushawishi tena kwani mnawatengenezea ajenda za kuwasema kwenye majukwaa yao.
Kupitia mchakato wa CCM chipukizi, chama cha mapinduzi mnajichimbia kaburi kwani mchakato umepandikiza chuki na makundi ndani ya chama na kwa wananchiwaliokua wamejenga imani kubwa kwenu na msipochukua tahadhari hili jambo litajibiwa 2024 na 2025 tujipe muda kwani muda ni mwalimu mzuri sana.