CCM inadandia hoja nzito za upinzani, alianza Kikwete mwaka 2010 na kima cha chini cha mshahara. Huenda hawajui hata kuandaa ilani yao!

dikteta2020

JF-Expert Member
Aug 14, 2018
595
3,990
Kwa mantiki hii ipo sasa haja ya moja kwa moja kuipumzisha CCM, kwanini?

Kama mtakumbuka kuwa, mwaka 2010 Rais mstasfu Jakaya Kikwete alikuwa na mgogoro mkubwa sana na Katibu mkuu wa TUCTA wa wakati huo Nicholas Mgaya. Mgogoro huo ni kuwa bwana Mgaya alikuwa anashinikiza wafanyakazi kima chao kiwe Tshs laki tatu na thelathini kwa kina cha chini. Kikwete alijiapiza kuwa kiasi hicho hakilipiki na akasema kama mtu hataki basi aache kazi. Saga likaendelea huku kila mmoja akikaza uzi.

Ukaja uchaguzi mkuu akasimama Slaa kwa upande wa Chadema na Kikwete kwa upande wa CCM. Slaa akiwa Jangwani akasema kuwa serikali yake itawalipa wafanyakazi mshahara wa kima cha chini kama walivyotaka. Mgaya naye akasema TUCTA itawaelekeza wafanyakazi mtu wa kumchagua.

Japo ilani ya CCM wakati ule haikuelezea kabisa suala la kima cha chini cha mshahara kuongezwa, ila Kikwete akalazimika kuongeza mshahara kipindi cha kampeni hadi kufikia kima cha chini wafanyakazi walichokuwa wanahitaji. Mbona aliongeza? Huko kutokulipika kulilipika vipi?

Mwaka 2015 sera ya elimu bure nayo hivyo hivyo wakaidandia juu kwa juu. Mwaka huu tayari wameshadandia hoja ya kuajiri na bima ya afya kwa wote.

Lipo jambo la msingi la kujifunza
Huenda na kwa uhakika wa evidence hizi tunawapa nchi waongoze watu wasio stahili. Huenda hii ndiyo ikawa chanzo kikubwa kabisa cha nchi yetu kulemaa. Ni lazima turudi na tujiulize kama kweli hii CCM isiyojua hata kuandaa ilani na kuishia kudandia hoja, ina uhalali wowote wa kuongoza Tanzania?

Mbali na kuwa awamu hii wametoa wapinzani kibao na kuwaingiza kwao, bado wameshindwa jambo lile lile ambalo limekuwa likiwashinda miaka nenda rudi.

Tunahitaji kuwaza na huenda hawa wanaoshinikiza tupige kura kwa Magufuli wanapigania njaa zao, ndiyo maana hawana hoja yoyote ile! Tujihadhari miaka mitano ni mingi na mengi kutokea hapo kama tutakosea basi mabaya yatakuwa mengi zaidi na kama tutapatia basi mazuri yatakuwa mengi zaidi.
 
Back
Top Bottom