CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

hii post imeonekana ni ya kitambo saana but imeeleza ukweli mtupu maana UKAWA ambayo tuliona kama ndo mkombozi wa wengiimegubikwa na uchu pamoja na tamaa kubwa ya madaraka na kwa hali hii watawaachia tena CCM miaka mitano jambo ambalo kwa wanaharakati na wakerketwa kama mimi cjalifurahia hata kidogo......Prof Lipumba kujienguo kuiongoza CUF ni udhaifu mkubwa kwake na kwa ukawa kiujumla huku Dr SLAA kukaa mbali na utaratibu wote wa UKAWA ni kuonyesha utengano ambao hautaleta ushindi wa maana sana 2015......CCM nao wataitumia fursa hii kujinadi vizuri kwa watanzania ambao tunapaswa kupimwa akili tutakapoichagua tena ccm
 
chadema sasa ni mti unaokua nakuchanua ila ccm unapurukutisha majani haijulikan kama utakufa kabisa au utachipua mii naona wabadilishe jinala chama wajipange upya
 
Chadema chadema chadema chadema ukawa ukawa ukawa ukawa lowassa lowassa lowassa duni duni duni,ushindi ushindi ushindi 2015 , 2015,2015 ni wahakika hakika hakika
 
Inasikitisha sana kuona viongozi wa ccm na makada wake wakitumia nguvu nyingi sana kuwashawishi
wanachi wakipe ridhaa chama chao kwa mara nyingine tena huku wakiwabembeleza wanchi ambao wamekuwa hawana thamani kwao baada ya kumalizika uchaguzi.

Ccm wamekuwa hodari wa kusahau jinsi walivyowadhalilisha wananchi kwa kuwaona hawafai pale walipopendekeza katiba waliyodhani ingewaongoza vema na kuwa chachu ya maendeleo yao na nchi kwa ujumla.matokeo yake waliipiga teke na kuwatolea hata maneno ya kejeli wananchi waliopendekeza rasimu hiyo ya katiba
leo wanajfanya kwambakuna chama kngine kilichokuwa kitwala sasa wanaomba idhaa ya wananchi
kujakusahisha makosa ya chama hicho wamesahau kwamba ccm ni ile ile.sasa watanzania wanawaambia kama wamesahau au kujisahulsha wapumzike
 
Sisi malofa wapumbavu na mbumbumbu tumeamua mabadiriko ni lazina.
ccm wamelewa madaraka na wametapanya mali ya nchi
 
Ndio maana tunaitwa malofa na wapumbavu.wanatuambia ccm ni ile ile bado hatushtuki.ccm mbele kwa mbele. Ukishawapa kura hawarudi nyuma
 
Mimi nyumbani kwangu kuanzia watoto mpaka mke wangu ni vichekesho jamani kama mwanangu wa kiuume utamskia baba lowasa safi anaonesha dole gumba, magufuli anakwambia kimeo cjui usemi ule anautoaga wapi cjui wandugu
 
Duh Pasco uko vizuri hii post ni ya muda mrefu lakini mie ndio naiona leo,Nakupa hongera.Kwa vile mie ni bingwa wa kutoa like nilijipanga kutotoa like mpaka tarehe 26/10 lakini hii imebidi nitoe.Kwa kiasi fulani yale ulotamka ndio yanaendelea lakini kwa sasa hali imebadilika sana na Mzito kabwela na Dr.Mihogo hawapo tena.Ni mtihani mkubwa lakini kuna kila dalili za ukawa kuchukua nchi.Nitarudi tena 26/10 kutoa like.
 
Dah...umegonga mule mule..so SAD
Hata Mimi CCM ni chama changu lakini kwa kweli CCM inashindwa kusimamia misingi ya haki na utawala bora ili raia wake waendelee, dhuluma ya ardhi ni kibao, wazazi wangu wote wamekufa na kesi za ardhi na mpaka Leo ni kitendawili. wizi mtupu serkalini, usiende polisi au mahakama au hspitali . Shule nalipa toka vidudu, michango , michango , michango. Wenye pesa ni wafanya kazi serikalini, na mishahara Yao wala siyo mi kubwa, vijana Hawana kazi, mpaka unasikia uchungu, Michezo imekufa, DSM hakuna viwanja, watoto wameamua kuanzisha jogging. Clubs wakimbie barabarani, Barabara zenyewe nyembamba, unaogopa Kama mtoto, yupo salama. Mimi naamini tukikaa nje ya madaraka miaka mitano tutarudi na chama imara. Leo tukishinda tena subiri kura za maoni miaka mitano mambo Yale Yale
 
Kama watanzania wangekuwa na kumbukumbu ccm ilitakiwa ishinde viti 10, tu vya ubunge na mgombea wao alitakiwa awe nyuma ya wagombea wawili ktk kiti cha uraisi,tatizo letu watanzania tunasahau mapema,...yaani ktk kipindi kifupi tumesahau sakata la escrow na jinsi wabunge na viongozi wa chama walivuokuwa wanahaha kulififisha,tumesahau oparation ya tokomeza ilivyodhalilisha utu wetu,tumesahau jinsi serikari ilivyoshughulikia swala la mafuta kwa wanaochakachua ikaona kuliko kuwanyang'anya leseni wachakachuaji bora ipandishe bei mafuta ya taa ili ikaribiane na mafuta ya magari bila kujali mtanzania wa kawaida anayetumia kibatali,...nk .....kwa kweli yapo mambo mengi ambayo ccm hawapaswi kuyafanya kama watawala wanaowapenda wananchi wake.........wakati wa mabadiliko ni huu.
 
Tunapenda kudanganywa na elfu mbili mbili na chumvi.Acha tuendelee kunyonywa mpaka tupate akili
 
Wanabodi,
Nikiwa hapa Dom, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde,

Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kanda ya ziwa, nimewaona ni wa kawaida tuu, hivyo nimefikia jibu moja la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, lingechaguliwa!

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu japo kipo juu, lakini bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa.
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.
Jee Chadema sasa imeishajipanga na iko tayari kukabidhiwa nchi hapo October 25?.

Pasco
 
Back
Top Bottom