WARAKA BINAFSI JUU YA HARAKATI ZA UCHAGUZI MKUU TZ (Hasa nafasi ya Urais)
Nafuatilia sana mchakato huo kwa sbb kadhaa ikiwemo ... ni
#hatma yangu na Tanzania tuitakayo......#. Niliwah andika....... Ninaandika Tena....... ####SISIEM WAMESHINDWA KUONGOZA NCHI; ILA UPINZANI HAWAKO SERIOUS KUONGOZA NCHI ###
Ninamaana katika hili..... Ukiangalia tathmini ya "Tulipotoka.... Tulipo na tunapokwenda" ni dhahiri hatupigi hatua sawasawa na Mabadiliko na Wakati... Yaani TUMEDUMAA ... Kama bajeti yetu ya 2005 ilikuwa trillion 7 na Shilingi ikiwa ni Tsh. 650/= kwa Dollar ..... Leo.... Bajeti trillion 22 Dollar ni Tsh. 2630/=..., ukiconvert utakuta bajeti ya 2005 ni kubwa Kuliko ya Leo..... Ona Mfumuko wa Bei.... Ulifika Hadi 19.8%..,,,, wakati baada ya vita ya Uganda Mfumuko ulifika 20% mwalimu Nyerere akatangaza# kufunga mkanda# ..... Ila watawala wa Leo hawatoi suluhisho stahiki kwa kila tatizo linapotokea... wanachukua mkopo wa Trillion 8 kutoka China ili kuongeza thamani ya Shilingi (Sijui kanuni hii inatoka wapi??? ). UGONJWA NI NCHI KUSHINDWA KUUZA BIDHAA ZA NDANI NJE BALI KUBAKI INAPOKEA BIDHAA KUTOKA NJE ... Pima Hali ya umasikini imezidi KUWA kubwa kwa umma licha ya MTU mmoja mmoja kuonekana Kupanda Kwani hoja ni kuwa... Sehemu yenye Mfumuko wa bei wanaoumia zaidi ni wale wenye kipato kidogo ...... Hali ya huduma kwenye taasisi za Umma imeporomoka..... Uadilifu...... Umeporomoka....... Nk... Ni baadhi ya CHANGAMOTO AMBAZO ZINGINE ZIMEGEUKA NA KUWA MATATIZO sio CHANGAMOTO TENA....
....... Kwa nini Wanyarwanda wameamua kubadili vifungu vya katiba vinavyomruhusu Paul kagame aingie Tena kwenye kinyang'anyiro ..... UWAJIBIKAJI.... HUDUMA WAPATAZO.... Nimepata uthibitisho Wapo mawaziri wa Kagame Ambao wanavuliwa nyadhifa zao..... Jukwaani kwenye ziara..... In our land people are not serious....... Nimekaa vijijin ktk utumish WANGU kwa takriba miaka 10..... Nafahamu namna ambavyo ndugu zetu vijijin wanateseka..... Sijasimuliwa nimeishi nao.....
NINI KIFANYIKE????? Watanzania... Hawahitaji MABADILIKO ; Watanzania.... Wanahitaji.. MABADILIKO YENYE TIJA #
Tuna mifano mingi ya TIJA...... Libya wamefanya Mabadiliko ya kukurupuka...... Ila...... TIJA haijaonekana na Baadhi wameanza kujuta ......
Kenya wamefanya Mabadiliko...... TIJA kidogo imeonekana...... Obviously kwa ukanda wa A/M.. Kutajwa na WB kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati..... Sio ndoto .... Uhuru is my role model..... Nimefuatilia mdahalo wa Uganda Entrepreneurs na midaharo kadhaa... nimeiona IQ yake.....
WATANZANIA Tuna njaa ya Mabadiliko...... Ila yawe na TIJA....
VIPI MAGUFULI AU UKAWA....
UKAWA..... naipenda sana idea yao ya Ndoa "Muungano" Japo Muungano wao ni wa Mashaka.... Mimi ni mchokoz... Uchaguz wa S/mitaa nilikaa na dereva wa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba Bar kwa dkk 5,,,, nikamuuliza..... Vp... Unahis.... Vyama hivi kuna ..... Dhamira ya dhati imeviunganisha au kuna sababu nyingine????..... Akajibu ; ndani yao Wapo wana Mabadiliko wa Kweli na pia Wapo..... Wanaotia shaka...... Akatolea mfano wa Ilala ktk Chaguzi hizo... KUWA kuna nafasi za mitaa UKAWA walikubaliana atasimama wa CUF...... Baadae CDM wakasimamisha..... Nikashuhudia... Siku kadhaa kabla ..... Pro Lipumba.... Anapokuwa anafunga mkutano aliwaita viongozi wote wa UKAWA...... Lakin Mbowe hakufanya hayo... Japo sio sharia Ila LAZIMA TUYAISHI TUNAYOYAAMINI.... Ni lazima...... Kuyatenda tu au kuyawaza haitoshi (To live the talk and not walk the talk or talk the talk)
NAAMINI PIA.... In politics.... There is neither permanent friend nor permanent enemy..... JUST A MISSION ACCOMPLISHEMENT
Ili chama kisimame lazima kufuata kanuni ya ukuaji wa MBUYU.... Ndio wamachotakiwa kufanya.... Kuwa bora juu matawi yawe kiasi Ila chini.... Shina na mizizi Iwe MARADUFU....
Msiseme naisifu SISIEM but.... Chin ndio kuna wananchi...... Hivi Kaliua kuna M/Kit wa KIJIJI..... X... Kashinda uenyekiti juz Leo karudisha kadi.... Kwa hoja KUWA viongozi wa juu walikuja kuwapa ahad KUWA hakutakuwa na michango.... Ila wametelekezwa.... Miradi ya maendeleo haiendi......
Mifano iko mingi.... Lazima Vyama viwezeshe mamlaka za chini..... Je, chama kipi kimeendesha semina za uongozi baada ya VIONGOZI wao kushinda........ Nitajie?????
Ndugu ZANGUNI.... Kuchukua nchi sio lelemama.... Kama kucheza SHIKOLOBO...
Lazima watu wa toil... Vyama vyetu vya UPINZANI lazima viende kisasa..... Vijikite kwenye TAFITI....... Na sio kila wakati Agenda za Uchaguz.... Na namna ya kushinda.....
(Nina sabb za msingi kwa nn Vyama hivyo viliungana..... Ila muda hauniruhusu.... Ni mada kamili pia)
VIPI machali Kweli kaondoka kwenda ACTIIIII????? Kama Kweli minong'ono imeanza ya kumtoa kasoro..... Hivi Kama Kweli nae ana kasoro na wale Wengine.... Basi kwenu hakuna msafi......
Hoja ya Mgombea Urais lazima apate Makamu kutoka Chama husika..... Na pia Je, tukishinda Uchaguz au tulipo.... Mgawanyo wa VITI MAALUM KWA ASILIMIA mtakazo pata.... HILI SIO JIPYA...... Mwenyekiti wa TUME YA UCHAGUZ alitahadharisha...... Hakuna chama hicho.... Pia Vyama vyote vina wanasheria..... Hivyo havikujua mapema.....???? Nadhani walikuwa na la kufanya mapema Ila ttz...... IMANI YA PALE WALIPO BADO HAIKO SAWASAWA....
VIPI MAGUFULI ..... Tutegemee kipya .....????
SAMAKI MMOJA AKIOZA.... Ni wote.... Ila..... Narudia Ila.... Mgaagaa na upwa Hali wali mkavu.....
Ni bora MAGUFULI Kuliko aliowamwaga... Na hii ni faida kwa CHAMA CHAO NA KUPUNGUZA MAKUNDI YAO .... Magufuli ana kashfa..... Ila angalau Kuliko Wengine miongoni mwao (Japo hakuna kashfa ndogo)....
Kwani...... Pamoja na KUWA..... Wizara aliyopo inapimika kwa urahis.... (Urefu wa Barabara.... Unaweka futi kamba )..... Uuzaji wa Nyumba za shirika unadaiwa kukiuka kanuni za Ubinafsishaji.... Pia ubora wa Barabara zake unatupa utata..... Ila kashfa alizonazo ni Chembe ukilinganisha na KINA VIJISENTI ... Magufuli alipata sifa kupitia Vijisent baada kushusha bei za Barabara kutoka Bilioni 1.2 kwa km Hadi kufika Million 800..... Tofauti na mtangulizi wake..... Tumeshuhudia wachina wakipata shida juu yake..... Kafanya yanayomtosha Mwl. Magufuri Kuliko Mahar*** Wengine.... Mana penye Mia hapakosi haramia....
SITAACHA KUSEMA UKWELI..... Naipenda nchi yangu Tanzania..... Naitakia mema wakati wote..... Wenu KAPOLISI..... I stand to be corrected..