CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

wala hatusikii la mtu kijijini kwetu hatujaisikia ACT tena hatuitaki kwani Zito Haaminiki, Ukiungana naye mbele atakusaliti na kukuuza kwa ccm.si kosa lake ndivyo alivyozaliwa kuwa kigeugeu
Dawa ya moto ni moto mkuu
 
Nimejaribu kufuatilia kwa kina nini hasa watanzania wanahitaji, nimegundua kwamba, wengi walikuwa na tumaini na Ukawa, lakini baada ya kutokea migongano ya kimaslahi ukawani(kila chama kutaka kutoa rais) , wananchi wameachwa njia pande, pia kukosekana kwa siasa za uwazi(transparency) kwenye vyama vikuu vya upinzani(chadema & CUF) kumevunja kabisa matumaini ya wengi

Mahaba yamekupofusha pole kwa kufuatilia usisahau kujiandikisha kwenye B V R
 
Mamlaka yenye kudhulumu watu, kuwaonea watu, kuua watu bila sabab, kuwashtaki viongoz wa upinzan kwa lengo la kuwakatisha tamaa na kuwaogopesha wananchi isirudishe nyuma vita yetu ya ukomboz wa kiuchumi kijamii na kiutamaduni. popote pale ulipo mtanzania mzalendo pigana kuhakikisha ccm inaondoka madarakan.
 
hakika nawaambia ndugu zangu watanzania wapenda aman na maendeleo ya taifa letu ccm imefikia the point of no return dhambi waliyotenda haivumiliki. vijana wachumia tumbo na opportunist nawaomba muache kuchelewesha ukomboz wa nchi yetu. kundi lingine walimu waache ulofa wa kijinga kampen zipigwe mashulen kuwaambia vijana ukweli na kuchukua hatua madhubuti mana hao (walimu) wanatumika kama dodoki hasa kipindi hk cha uchaguz
 
Kwa kweli kwa hapa tulipofika watanzania tusema ccm sasa basi kwa sababu hawana uwezo wa kutupeleka mbele zaidi ya hapa. tunahitaji mawazo mapya yatakayotusaidia kutoka hapa tulipo na kwenda mbele.

Hii ccm imeshindwa problems can not be solved by the same people who have the same thinking capacity.
 
Nimekua nikiletewa maono mbalimbali lakin mara nyingi huwa nanyamaza lakini kwa haya yenye faida kwa taifa hili inabidi kuwasaidia watu wanao taka mabadiliko.

Ni wiki moja tu tangu niandike humu kuhusu kukatwa jina cc.sasa ni hivi mwenge ndio shida unafunga fahamu kwa wale wote walio wepesi.
 
Kwa jinsi mlivyotusababishia matatizo makubwa hapa nchini ikiwemo migogoro mikubwa ya ardhi,kudorora kwa uchumi na rushwa inayozidi kushamiri,sikutarajia kuwaona mkishadadia kurudi tena Ikulu.Kuweni na huruma,kwa kuwa ninyi mmeshindwa ebu waachieni wengine watuongoze
 
Chama cha mafisadi (CCM)
Weka mbali na raia wema wa Tz
 
muonekano wa marekani hufanana na akili za raia wake,the same muonekano wa tanzania hufanana na akili za watanzania
 
Ungekumbuka kwamba karibia woote unawataka ndio hao hao wametokea humohumo CCm.

Kama wizi woote tu wanataka kwenda kula
 
Augustino Ramadhani
Profile:
Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.
Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.
Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.
Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.
Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.
Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.
Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.
Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.
Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.
Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.
Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.
Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool.” nimeikopi tu...
 
Ungekumbuka kwamba karibia woote unawataka ndio hao hao wametokea humohumo CCm.

Kama wizi woote tu wanataka kwenda kula

Potelea pote,lakini kuendelea na hawa jamaa walio prove failure,ni kuendelea kujiangamiza,thamani ya shilingi inazidi kushuka,ufisadi kila kona ya nchi,elimu duni kwenye shule za serikali,pamoja na huduma mbovu ktk hospitali za serikali.Naomba wajiondoe tu,tumechoka
 
Tunategemea Ukombozi wa pili kutoka kwa mkoloni wa kijani upo njiani.Ninaamini kuwa maisha bora itakuwa sio nadharia bali ni uhakika viva ukawa.
 
Back
Top Bottom