CCM: Dk. Slaa na wenzake wadandia kinguvu mazishi ya Mwangosi, Mbeya

CCM Blog: DK. SLAA NA WENZAKE WADANDIA KINGUVU MAZISHI YA MWANGOSI, MBEYA

VIONGOZI wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa, wametuhumiwa kulazimisha kinguvu, kushiriki mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten, mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.

Marehemu Mwangosi aliyefariki katika vurugu, zilizobababishwa na CHADEMA eneo la Nyororo, alizikwa Jumanne ya wiki hii, katika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe huku kundi kubwa la wafuasi wa CHADEMA, likihudhuria mazishi hayo.

Inaelezwa licha ya kuambiwa msiba huo siyo wa kisiasa, hivyo hawatakiwi viongozi hao wala wanachama wa CHADEMA, lakini walilazimisha kushiriki kwa nguvu, na hata mwili wa marehemu ulipowasili Tukuyu mjini ukitokea mkoani Iringa, walilazimisha kuingia kinguvu kwenye gari hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, Francis Godwin, alisema kuwa tangu wakiwa mjini Iringa, aliwatangazia wazi CHADEMA kuwa msiba huo unawahusu waandishi wa habari na siyo wanasiasa.

“Tulianza kukwaruzana tangu hatujaondoka mjini Iringa, kwani wakati tunatangaza taratibu za kusafiri, nilitumiwa ujumbe na viongozi wa CHADEMA, kuwa nitangaze msafara huo utaongozwa na Dk.Slaa, lakini niliwakatalia kuwa huo siyo msiba wa mwanasiasa bali ni mwanahabari hivyo hilo halitawezekana” alisema Godwin.

Godwin alisema aliwaeleza wazi viongozi wa CHADEMA, kuwa kama wanataka kwenda kushiriki mazishi hayo basi ni vyema watafute taratibu nyingine za kufika wilayani Rungwe, lakini siyo kung’ang’ania waongozane na mwili wa marehemu, kitu kilichowakera viongozi hao.

Aliongeza kuwa walishangazwa walipofika Tukuyu mjini, kundi la vijana wafuasi wa CHADEMA walilifuata gari walilokuwemo waandishi wa habari kutoka mkoa wa Iringa ambamo ndipo mwili wa marehemu Mwangosi ulikuwemo na kuamua kuingia kinguvu.

Kwa mujibu wa Godwin, walipojaribu kuwakataza vijana hao wa CHADEMA, iwapo kuna mtu atawakatalia kuingia basi watambue wazi kuwa damu itamwagika hali iliyowafanya washindwe kuwazuia kwa kuogopa kuanzisha vurugu zisizo na msingi.

Aidha, katika kuonyesha kukerwa na hali hiyo iliyojitokeza, akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe, Godwin alisema hakuwahi kusikia marehemu Mwangosi akisema kuwa yeye ni mwanachama ama mfuasi wa chama chochote cha siasa.

Godwin alisema:”Ninachokifahamu mimi ni kuwa marehemu Mwangosi, alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, hivyo hatutegemei msiba huu kuanza kuingizwa itikadi za kisiasa”.

Aliongeza kwa kulitaka Jeshi la polisi kuwa hata kama marehemu Mwangosi, alifanya kosa lililopelekea akutwe na mauti hayo alipaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na siyo kufa aina ya kifo hicho cha kufa kwa bomu la machozi.

Katika kuonyesha kuwa kauli hizo ziliwachoma CHADEMA, Dk.Slaa aliposimama kuzungumza na wananchi, alisema anachofahamu yeye ni kuwa msiba hauna rangi, kabila wala dini.

Dk.Slaa aliongeza hivyo anapenda kutumia nafasi hiyo kukemea kauli za ubaguzi zilizotolewa, kwani CHADEMA wameenda kushiriki msiba huo kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na marehemu.

“Wakati tunaondoka mkoani Iringa kuja huku Rungwe-Mbeya, kuna kitu kilitokea ambacho kilitukwaza na sitapendi kukizungumza hapa…nimemjua marehemu Mwangosi alikuwa mtu wa haki na alikuwa akipinga vitendo vya kifisadi” alisema Dk.Slaa.

Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati wa mazishi, Dk.Slaa alimfuata Godwin na kumueleza kuwa amemsamehe kwa yote aliyoyafanya hali ambayo ilimlazimu naye (Godwin), kumjibu kuwa hajafanya kosa lolote linalostahili asamehewe.

Kama Dr Slaa alidandia mbona alipewa nafasi ya kuhutubia?
 
Si vizuri kuwakataza kwa sababu marehemu alikuwa mfuasi wa CDM kwa moyo wake wote. Alishirikiana na wenzake kukijenga chama kila ilipobidi.
Kule Tanga walipopigwa chenga na familia walipotezea kwa sababu marehemu hawamjui na itikadi yake hawaijui.
 
Pro-Chadema kila siku mnapiga kelele kuwa JK anapenda kwenda kujipendekeza kwenye misiba, vipi tena Dr Slaa anavamiia msiba wa watu au marehemu alikuwa kada wa Chadema...RIP Mwangosi.

watu wengine bwana.
 
Huwezi ukakataza watu wasije kwenye msiba ikiwa wakati msiba sio wako.

Na lazima ukubali kama sio CDM na slaa kufika iringa basi mwagosi angekua hai

neno la leo "nyota yako ikingaa imengaa tu na nyota yako ikififia imefifia tu"
 
Ccm fanyen yenu nyie kwa sasa mnanuka achen propaganda zenu mnataka kutumia msiba kama mtaji, kwan huyo godwin ni nan au mwanafamilia? Dk. Slaa katoa uban milion 2 yeye godwin katoa ngapi? Achen hizo tunasema watzee hatudanganyiki.
 
Msiba hauvamiwi! Vinginevyo ingeshatungwa sheria wafiwa washiriki peke yao na rambi rambi zisingekuwapo.kushiriki msiba ni mira na desturi ya watanzania.hatudanganyiki,karibu kunakucha tusirudi nyuma
 
Mbona kama ndugu wa rehemu walikuwa hawataki uwepo wa kiongozi yeyote wa cdm mbona kuhusu kusomesha mtoto hawajapinga?


Kweli ccm wanatapa tapa na Dr asinge kwenda wangesema wametelekeza msiba!
 
Mbona kama ndugu wa rehemu walikuwa hawataki uwepo wa kiongozi yeyote wa cdm mbona kuhusu kusomesha mtoto hawajapinga?


Kweli ccm wanatapa tapa na Dr asinge kwenda wangesema wametelekeza msiba!

Mkuu watoto wa marehemu watasomeshwa na Dr Slaa? Ebu tujuze mkuu.
 
Tatizo lenu ninyi sisiem kuanzia mkuu wenu wakaya kama mmezaliwa bb na mama mmnja! Akili zenu,fikra zenu,mitazamo yenu inafanana,mbaya zaidi mnaambukiza hadi wajukuu wenu.hakika ipo siku mtalia na kusaga meno!
 
Duuuh! Kumbe huu msimba mmeshindwa kuwaonga wafiwa ili waikache cdm! Ukiona njama mnazo jaribu zina kwama ujue mwisho wa policcm umekaribia!

Imechoma hiyo kama mnapenda misiba Muhimbili, Mwanyamala, kila siku watu wanakufa mbona amjaenda kuzika, mmeusafiria msiba kutoka Dar mpaka Iringa.
 
Imechoma hiyo kama mnapenda misiba Muhimbili, Mwanyamala, kila siku watu wanakufa mbona amjaenda kuzika, mmeusafiria msiba kutoka Dar mpaka Iringa.

Kwahiyo una imply kwamba hawakufahamiana na Mwangosi?Kauli yako inaonyesha hutaki kujishughulisha kufikiri.
 
Ni kweli kabisa kiongozi! Tuliuona mwili wa marehemu upo kwenye gari la M4C na jamaa mmoja anafukuzia nzi. Wale polisi majeruhi tayari walikuwa wamekimbizwa hospitali na ma-defender yao. Hatukuliona gari la waandishi wa habari pale; Usikute walikuja kwa lifti ya M4C.
 
Back
Top Bottom