CCM: Dk. Slaa na wenzake wadandia kinguvu mazishi ya Mwangosi, Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Dk. Slaa na wenzake wadandia kinguvu mazishi ya Mwangosi, Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Sep 5, 2012.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  CCM Blog: DK. SLAA NA WENZAKE WADANDIA KINGUVU MAZISHI YA MWANGOSI, MBEYA

  VIONGOZI wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa, wametuhumiwa kulazimisha kinguvu, kushiriki mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten, mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.

  Marehemu Mwangosi aliyefariki katika vurugu, zilizobababishwa na CHADEMA eneo la Nyororo, alizikwa Jumanne ya wiki hii, katika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe huku kundi kubwa la wafuasi wa CHADEMA, likihudhuria mazishi hayo.

  Inaelezwa licha ya kuambiwa msiba huo siyo wa kisiasa, hivyo hawatakiwi viongozi hao wala wanachama wa CHADEMA, lakini walilazimisha kushiriki kwa nguvu, na hata mwili wa marehemu ulipowasili Tukuyu mjini ukitokea mkoani Iringa, walilazimisha kuingia kinguvu kwenye gari hilo.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, Francis Godwin, alisema kuwa tangu wakiwa mjini Iringa, aliwatangazia wazi CHADEMA kuwa msiba huo unawahusu waandishi wa habari na siyo wanasiasa.

  "Tulianza kukwaruzana tangu hatujaondoka mjini Iringa, kwani wakati tunatangaza taratibu za kusafiri, nilitumiwa ujumbe na viongozi wa CHADEMA, kuwa nitangaze msafara huo utaongozwa na Dk.Slaa, lakini niliwakatalia kuwa huo siyo msiba wa mwanasiasa bali ni mwanahabari hivyo hilo halitawezekana" alisema Godwin.

  Godwin alisema aliwaeleza wazi viongozi wa CHADEMA, kuwa kama wanataka kwenda kushiriki mazishi hayo basi ni vyema watafute taratibu nyingine za kufika wilayani Rungwe, lakini siyo kung'ang'ania waongozane na mwili wa marehemu, kitu kilichowakera viongozi hao.

  Aliongeza kuwa walishangazwa walipofika Tukuyu mjini, kundi la vijana wafuasi wa CHADEMA walilifuata gari walilokuwemo waandishi wa habari kutoka mkoa wa Iringa ambamo ndipo mwili wa marehemu Mwangosi ulikuwemo na kuamua kuingia kinguvu.

  Kwa mujibu wa Godwin, walipojaribu kuwakataza vijana hao wa CHADEMA, iwapo kuna mtu atawakatalia kuingia basi watambue wazi kuwa damu itamwagika hali iliyowafanya washindwe kuwazuia kwa kuogopa kuanzisha vurugu zisizo na msingi.

  Aidha, katika kuonyesha kukerwa na hali hiyo iliyojitokeza, akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Busoka, wilayani Rungwe, Godwin alisema hakuwahi kusikia marehemu Mwangosi akisema kuwa yeye ni mwanachama ama mfuasi wa chama chochote cha siasa.

  Godwin alisema:"Ninachokifahamu mimi ni kuwa marehemu Mwangosi, alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa, hivyo hatutegemei msiba huu kuanza kuingizwa itikadi za kisiasa".

  Aliongeza kwa kulitaka Jeshi la polisi kuwa hata kama marehemu Mwangosi, alifanya kosa lililopelekea akutwe na mauti hayo alipaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na siyo kufa aina ya kifo hicho cha kufa kwa bomu la machozi.

  Katika kuonyesha kuwa kauli hizo ziliwachoma CHADEMA, Dk.Slaa aliposimama kuzungumza na wananchi, alisema anachofahamu yeye ni kuwa msiba hauna rangi, kabila wala dini.

  Dk.Slaa aliongeza hivyo anapenda kutumia nafasi hiyo kukemea kauli za ubaguzi zilizotolewa, kwani CHADEMA wameenda kushiriki msiba huo kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na marehemu.

  "Wakati tunaondoka mkoani Iringa kuja huku Rungwe-Mbeya, kuna kitu kilitokea ambacho kilitukwaza na sitapendi kukizungumza hapa…nimemjua marehemu Mwangosi alikuwa mtu wa haki na alikuwa akipinga vitendo vya kifisadi" alisema Dk.Slaa.

  Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati wa mazishi, Dk.Slaa alimfuata Godwin na kumueleza kuwa amemsamehe kwa yote aliyoyafanya hali ambayo ilimlazimu naye (Godwin), kumjibu kuwa hajafanya kosa lolote linalostahili asamehewe.
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  (nimeikuta huko lakini ina ukweli?) ukifika chini bofya
  NEWZZ:DR.SLAA ALIVAMIA MSIBANI,AKAIDI AGIZO LA WENYE MSIBA  [​IMG]

  chanzo:habari mpasuko blog

  Blogu ya Wananchi: NEWZZ:DR.SLAA ALIVAMIA MSIBANI,AKAIDI AGIZO LA WENYE MSIBA

 3. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Inatafutwa mada ya kupotosha focus tuu hapo; wananchi roho zinatuuma kwa mauaji haya ndo bolded heading kwa msimu huu nani kahudhuria na nani kavamia au kaalikwa kwa sasa sio kipaumbele; wananchi wapenda haki na amani tunataka vitendo hivi vikome FINAL

  Longolongo zimetosha..................
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tayari Msiba wa Mwangosi umekuwa biashara hivi Godwin Francis ni mwanafamilia mpaka azuie watu fulani kumzika au kaambiwa atapewa ukuu wa wilaya akifuata maagizo ya polisi mjinga sana huyo kijana kama anadhani anaweza akachukua nafasi ya familia watoto na mke kupanga watu wa kuwahani
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kuvamia msiba??
   
 6. m

  markj JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  yale yale ya balali! shame on them, we are tanzanians bana, hatuna manbo yakuzuiana kwenye misiba.
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Msiba hauna mwenyewe..........!
   
 8. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Huu nao ni upuuzi mwingine.... linapokuja suala la msiba hakunaga itikadi, kama wanachadema walishirIki msiba walishiriki kama watanzania wengine walioguswa na msiba huo mambo ya kubaguana msibani huo ni upuuzi uliokomaa kama watanzania bado hatujafika huko ndo maana hata CDM walipofiwa na mbunge wao wana CCM walikuwepo kama watanzania wengine walioguswa na msiba huo.
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Ule wa steven kanumba pia jk alivamia
   
 10. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CDM wakiacha kushiriki wanasema wamewatelekeza, wakishiriki wanasema wamedandia. Sasa wewe Godwin umeshiriki kama nani? tangu lini msiba unapotokea kuna kualikana? Kama marehemu aliuawa wakati anafuatilia habari za CDM, utawaambiaje kuwa CDM wasishiriki?
   
 11. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Kwani msiba huwa una kadi za mwaliko? Mbona hizi propaganda sizielewi! Hebu tumieni ubongo mnapo posti vitu humu!
   
 12. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Dah! Mnavyotapatapa mtafikiri mko "leba". Mtaongea yote nyakati hizi za mwisho.
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CCM bwana...!Msiba hauna mwenyewe.
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hivyo vijamaa vya Channel 10 hamna kitu.....

  Kama tumerogwa tunapoacha maswala ya utu na kuleta utumbo tunaoamini ni siasa... huu ni wehu!!

  Niliangalia kipande cha tukio pale, baada ya marehemu kulipuliwa na polisi kuutelekeza mwili ni wananchi waliubeba mwili na kuuweka kwenye gari la M4C.... Hao waandishi walikuwa wapi??

  Katika kanuni za utu mlitaka wale watu ambao ni wanachama wa CDM (kwa bahati mbaya sana kwenu) wafanyaje?

  Tunaendelea kuwa taifa la wajinga kila leo.

  Hata kwenye kuzikana pia ni nongwa?

  Lakini mmejiuliza ni nini mngesema kama Dr angepanda gari na kurudi Dar??
  Ukwaju ndugu yangu hayo maswali sikuulizi wewe, nawalenga hao wapuuzi na hoja zao mbilikimo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,300
  Likes Received: 3,038
  Trophy Points: 280
  Yan msiba nao umekuwa mtaji khaa.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Siasa za Tanzania zimeanza kuwa kama za jirani zetu wa hapo Kenya. Kwa Kenya kila pahala ni siasa: Mwanasiasa akienda kanisani kusali lazima apate wasaa si kwa ajili ya kuhubiri injili, la ni kuhubiri siasa na kujipigia debe. Mwanasiasa akihudhuria msiba lazima apate nafasi atoe neno na si neno la kumuombea marehemu bali neno la kujipigia debe kisiasa.
   
 17. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naona kama Nape anataka kuchukua nafasi ya mke wa marehemu vile! Maana kila kitu cha Mwangosi anajaribu yeye na vibaraka wake kutaka kukizungumzia pamoja na kwamba ni ukweli ulio utupu ni serikali ya ccm ndio iliyomuua Mwangosi.
   
 18. papason

  papason JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Wee mleta maada una lako jambo! Yaani unatuletea udaku wa blog za wamagamba!
  Kwa leo nakustahi......
  vinginevyo ningekuharibia siku...
   
 19. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni upuuzi kujadili kuwa nani kavamia msiba. Sidhani kama ndugu wa marehemu watakaposoma habari kama hizi. Tujali utu wa mwenzetu walau hata kwa kiwango cha chini. Hao wanaoanzisha mada za nani kavamia msiba haina maana zaidi ya kuonesha ujinga na upumbavu wetu.
   
 20. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Umepata pa kutokea i.d.i.o.t.a
   
Loading...