CCM: Dk. Slaa na wenzake wadandia kinguvu mazishi ya Mwangosi, Mbeya

Pro-Chadema kila siku mnapiga kelele kuwa JK anapenda kwenda kujipendekeza kwenye misiba, vipi tena Dr Slaa anavamiia msiba wa watu au marehemu alikuwa kada wa Chadema...RIP Mwangosi.

Mkuu Ritz,
Dr. Slaa kapagawa dhambi ya unafiki inamsuta, mbona hakwenda Tanga kumzika Ally (R.I.P)? mbona hakwenda Singida si anadai msiba hauna dini wala kabila? hivi huyu haponi kweli? kauli zake anaezielewa mwenyewe.

Chama
Gongo la mboto DSM- safarini Brussels
 
Nimemkumbuka Mugabe alizuiwa kwenda Ulaya lakini wakati wa msiba wa pope alienda kuhudhuria alipoulizwa na waandishi wa habari alitamka kuwa waafrika hata wakigombana wakati wa msiba husitisha ugomvi wao. Hata hivyo msiba ni wa familia na si wa taasisi hivyo kila mtu anauhuru wa kuhudhuria labda kama ndugu wangezuia jambo ambalo silitegemei kutokea hapa Tanzania.
 
Lazima tukumbuke kuwa kuna aina nyingi za kuomba. Matonya (R.I.P) alitumia mtindo wa kipekee.Alilalia mgöngo na kuweka bakuli tumbon.GODWIN amechagua njia hii kuomba kwa CCM
 
Mmemua mwangosi muichafue cdm, mmechafuka mmetukanana jana mwema na nchimbi laana haitowacha milele pamoja na kuendeleza tabia za kununua watu kwenye msiba 2015 hamponi
 
Ccm mnagombania mpaka msiba???
Kesho tena mtaua mwingine ili mtumie mazishi kujinadi.
Hakika kuitetea ccm inahitaji uwe na akili ya maiti.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu Ritz,
Dr. Slaa kapagawa dhambi ya unafiki inamsuta, mbona hakwenda Tanga kumzika Ally (R.I.P)? mbona hakwenda Singida si anadai msiba hauna dini wala kabila? hivi huyu haponi kweli? kauli zake anaezielewa mwenyewe.

Chama
Gongo la mboto DSM- safarini Brussels

Mkuu chama,
Hivi kutoka Dar es Salaam mpaka Iringa, au kutoka Dar es Salaam mpaka Tanga wapi mbali?
 
Last edited by a moderator:
Kwani CCM walipanga mpango mzima kuanzia kuuwa hadi kuzika wawe wao wenyewe???
 
Huu nao ni upuuzi mwingine.... linapokuja suala la msiba hakunaga itikadi, kama wanachadema walishirIki msiba walishiriki kama watanzania wengine walioguswa na msiba huo mambo ya kubaguana msibani huo ni upuuzi uliokomaa kama watanzania bado hatujafika huko ndo maana hata CDM walipofiwa na mbunge wao wana CCM walikuwepo kama watanzania wengine walioguswa na msiba huo.

Miproccm ni kama mijivi,inataka kutupeleka kwenye siasa za zanziba ya miaka ya 2000?ya kutozikana?
 
ccm wamefilisika kisera, kimtizamo
kwa mtu msomi na mwenye busara hawezi kuandika upuuzi kama huu.
 
Hakuna anayemlaumu JK kuhudhuria misiba bali anacholaumiwa, kama kiongozi wa nchi mwenye mamlaka, kuwa mwepesi sana kwenda kuhudhuria misiba na kutoa pole lakini ni mgumu sana wa kuchukua hatua za kuzuia vifo. Ikifikia mahali chama kinaona wananchi fulani eti kwa sababu ya itikadi zao au dini zao au makabila yao au jinsia yao, hawastahili kushiriki misiba au majanga kwa kudhania wakifanya hivyo au wataongeza kuungwa mkono au kupata umaarufu, basi chama hicho ni dhahiri kitakuwa cha kishetani kinachoongozwa na shetani. Watu wa Mungu, siku zote kwenye misiba na majanga hushikamana. JK alienda kwenye msiba wa Regia Mtema, kuna mtu aliuliza? Hakukuwa na wana-CCM, wana CUF, wana NCCR, wasio na vyama, wakristo kwa waislam, wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume, watu wa makabila mbalimbali, n.k? Kama hilo liliwezekana kwa Regia, kwa nini iwe tofauti kwa Daudi? CCM waache uwendawazima, Watanzania hatutaki kuona tofauti zinapaliliwa wakati wa misiba wala majanga. Tofauti zetu ni pale tunapotembea, lakini mwisho wa maisha yetu wote tunafanana, tunazikwa katika ardhi moja, wote twageuka mavumbi/udongo. CCM wamepalilia udini, sasa wanataka hata tusizikane?

Pro-Chadema kila siku mnapiga kelele kuwa JK anapenda kwenda kujipendekeza kwenye misiba, vipi tena Dr Slaa anavamiia msiba wa watu au marehemu alikuwa kada wa Chadema...RIP Mwangosi.
 
Huwezi kuusafiria msiba ambao una uhusiano nao kama Dr Slaa anapenda kuzika mbona Dar kuna misiba mingi kaicha kaenda huko mbali.

Huyu aliyeleta ujinga hapa kwenye forum ni Nape na akili fupi kama za kenge. Nimemsikia pia leo kwenye redio ya Clouds akitoa pumba zake akisema CHADEMA haikutii amri ya polisi na haraka haraka nikajua huyu mtot hana akili na siyui alikuwa anawezaji kujibu maswali ya "concept" kama alipitia chuo! Mwingine ni IGP ndiye mwenye matatizo ambaye anatekeleza maagizo ya Wassira na Lukuvi. Ma-RPC wanakuwa tayari wameishaelewana na Ma-kamanda wa CDM ikikaribia jioni baada ya IGP kupewa amri toka CCM anawapigia ma-RPC kutekeleza ujinga. Alifanya hivi Arusha, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Iringa na n.k. Kwa personality ya IGP aliyokuwa nayo toka enzi namfahamu akiwa Commissioner wa Interpol hakuwa mtu wa kuamrisha na wajinga wa CCM naye akatekeleza bila kutafakari au kuwashauri watekeleze.
Watanzania wanajua kuwa kisingizio cha sensa kilishapita na CCM waliendelea na kampeini zao huko Zenji, eti leo namsikia Nape akisema suala la kusitisha shughuli za kisiasa hazikuhusu Zanzibar! Je Nape anataka kutwambia kuwa tayari Muungano umeisha vunjika? Umevunjwa na CCM? Naomba maoni wapenzi watanzania.
 
huwezi kuusafiria msiba ambao una uhusiano nao kama dr slaa anapenda kuzika mbona dar kuna misiba mingi kaicha kaenda huko mbali.

jf gold member ????????????????????????????????????????????????????????????
 
Wanataka wahudhurie ili waonekane watetezi wa wananchi kumbe ndio wanaosababisha vifo hivyo kwa kulazimisha mikutano. Leo channel 10 nimeona live habari ya slaa kwamba watahakikisha nchi haitawaliki. Ni dhahiri yanayojitokeza ni mwendelezo wa kutaka nchi isitawalike. Kaeni mkijua watanzania tunapenda amani, ni bora ulalie uji kwenye amani kuliko kula soseji kwenye. Ewe Mwenyezimungu tuepiushe na balaa la wana CDM.
 
Mkuu chama,
Hivi kutoka Dar es Salaam mpaka Iringa, au kutoka Dar es Salaam mpaka Tanga wapi mbali?

Kwa hesabu za Dr. Slaa Tanga mbali kamanda kazikiwa Rungwa lakini ilikuwa ni kama vile anapiga tripu ya Temeke- Ilala

Chama
Gongo la mboto DSM- safarini Brussels
 
Back
Top Bottom