CCM Arumeru Mashariki tujipange vema, bundi yupo mtini

CCM Arumeru Mashariki tujipange vema, bundi yupo mtini

Kwani sio kweli kuwa nasary anahongwa maviwanja na wazungu Wa doli,anatumbua mfuko Wa jimbo, amehongwa gari aina ya harrier . Wanameru nimewadharau pamoja na matuhuma yote haya bado wanaipigia chadema kura

Bora huyo huyo,kuliko nyie ESCROW account ,EPA,MEREMETA,RICHMOND,mmemaliza vyote sijui wajukuu zenu mtawwambiaje.Hakika watataka kujua vichwa vyenu vilikuwa NAZI au UBONGO wa kawaida.
 
...

Mosi nimesema hayo kutokana Nami nilikuwepo kwenye kila ziara za chama na kujionea mwenyewe changamoto tunazopata hasa kwa kundi la vijana ambao wanaonyesha dalili za kutupinga na kuonyesha ishara ya vidole viwili kila pahala.

...

Tena vijana wamewaheshimu sana ninyi magamba; siku watakapoanza kuwaonesha kidole kimoja ndio mtakuwa mmepotea jumla; shukuruni kwa hiyo "heshima" japo kiduchu.
 
Jipe moyo nasary tutamngoa kwa nguvu zote hata kwa fimbo ya Chuma.

Mh!Ni kweli mtamng'oa toka vijiji 0-vijiji 115,sidhani kajipangeni.Na safafri hii bi BVR machine,sijui mtawaleta wa Meru toka Kenya.
 
Si nilisikia CDM Arumeru inakata roho,sasa imefufufka lini?Duh,haya ndiyo matatizo ya kumdanganya Prof wa Kichina.

Mkuu Tetty

Umewasikia wana CCM wanasema hawana imani na Kinana, Mwigulu na Nape maana walifanya ziara mtaa kwa mtaa, matokeo yake CCM wamepoteza mitaa zaidi hususani mahali palipofikiwa na wakuu wao hawa.

Hivyo, usijeshangaa wakisema hawana imani na mwenyekiti wa CCM Taifa. Kuna chama tena humo?
 
umezunguuuka, kumbe nia yako no kuipongza CDM. mdogo mdogo unajongea. Karibu
 
Kwani sio kweli kuwa nasary anahongwa maviwanja na wazungu Wa doli,anatumbua mfuko Wa jimbo, amehongwa gari aina ya harrier . Wanameru nimewadharau pamoja na matuhuma yote haya bado wanaipigia chadema kura

Ungeongeza na jitihada alizofanya za kuwapatia maji ya bomba wananchi wa maeneo mbalimbali ambao hawakuwahi kuwa na maji hayo kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita.Ungeongeza pia na Ofisi ya mbunge inayofanya kazi badala ya ile iliyokuwa imetanda buibui na haikuwahi kuhudumia hata makada km wewe licha ya wananchi wa kawaida.Nassary amekuwa akitoa mawazo chanya kwenye vikao vya Halmashauri,ila midiwani yenu ikiongozwa na Mang'unde imekuwa ikipinga bila sababu ya msingi.Siko tayari kuliona jimbo la arumeru mashariki likirudi kwa manyang'au ccm.Na kwa hivyo basi,Mungu akitupa Uhai,nakuja meru mwakani kuidelete kabisa ccm,nitahakikisha madiwani wote wanatoka CDM,na km Nassari tu anawapelekesha hivyo,Mungu asaidie nije huko maana mziki wangu ni zaidi yake,lazima mkae.Msalimu Dr.Daniel Pallangyo,wakili msomi na Lecturer wangu enzi hizo
 
Mkuu Tetty

Umewasikia wana CCM wanasema hawana imani na Kinana, Mwigulu na Nape maana walifanya ziara mtaa kwa mtaa, matokeo yake CCM wamepoteza mitaa zaidi hususani mahali palipofikiwa na wakuu wao hawa.

Hivyo, usijeshangaa wakisema hawana imani na mwenyekiti wa CCM Taifa. Kuna chama tena humo?

Huyo mbona walishasema siku nyingi!!!!!!!!Huoni hata wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wetu alipita kwa mbinde na mizengwe ya kutishana.Huko ndiko Rushwa imehalalishwa,inaitwa ZAWADI aka TAKRIMA au shukurani kwa mpiga kura kabla hajapiga.Acha kabisa.Bila RUSHWA hakuna CCM
 
Ni sawa na kuondoa mlima meru na kuupeleka babati. Wana Arumeru Mashariki tumesema Nasari is enough! Peleka chama chako cha ukoo kwenu! Narendu!

Kimeru sikijui ila "narendu" Ha haaaaaaaaaaa
 
Huyo mbona walishasema siku nyingi!!!!!!!!Huoni hata wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wetu alipita kwa mbinde na mizengwe ya kutishana.Huko ndiko Rushwa imehalalishwa,inaitwa ZAWADI aka TAKRIMA au shukurani kwa mpiga kura kabla hajapiga.Acha kabisa.Bila RUSHWA hakuna CCM

Ha ha ha

Muhimu zoezi la kuing'oa CCM, futa delete kabisa linaendelea vizuri nchi nzima. Andaa kura yako ya hapana kuikataa katiba pandikizi ya ukandamizaji hapo mwezi wa nne mwakani. Nguvu ya umma ndio kimbilio letu.
 
Hawa MAJANGILI yanajua kinachokuja ndiyo maana wanadilidali kutuletea MACHINE,japo za kichina zije tu.Yaani nadhani siku ya kwanza lazima niwe mlangoni mwa mwandikishaji,hata msimamizi awe Mwamunyange!:cheer2:
 
Huyo mbona walishasema siku nyingi!!!!!!!!Huoni hata wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wetu alipita kwa mbinde na mizengwe ya kutishana.Huko ndiko Rushwa imehalalishwa,inaitwa ZAWADI aka TAKRIMA au shukurani kwa mpiga kura kabla hajapiga.Acha kabisa.Bila RUSHWA hakuna CCM

Watamtafuta mchawi hawatamwona, ukweli ni kwamba wamechuja
 
Wadau nawasalimu sana.

Ccm ni chama makini na chenye dola na wananchi Wa Meru mashariki wametupa ushindi ambao nitauita ushindi mwembamba kwa minajili ya matokeo yote yaliyohesabiwa kwa kuona kuna dalili ambazo inionyesha kuna kazi ngumu mwakani katika uchaguzi mkuu 2015.

Mosi nimesema hayo kutokana Nami nilikuwepo kwenye kila ziara za chama na kujionea mwenyewe changamoto tunazopata hasa kwa kundi la vijana ambao wanaonyesha dalili za kutupinga na kuonyesha ishara ya vidole viwili kila pahala.

Bundi ametua mtini kwa haya matokeo chini:

1: vijiji Ccm- 56
Chadema-34

2: vitongoji Ccm - 217
Chadema- 115

Nb: ikumbukwe kuwa chadema hawakuwa na kijiji na kitongoji hata kimoja.

Natoa ushauri kwa timu yote ya kamati ya siasa Meru tusikate Tamaa wala kurudi nyuma mwakani nia ya kumuondoa huyu nassary ipo pale pale

Nawasilisha tujipange kimakakati

Mtazamo...!!!! Tayari CDM imeshajiwekea mizizi hata vijijini..!!! Kwa namna nyingine CDM inaweza sasa kuongoza nchi kwani tayari kila sehemu ya nchi kuna wanachama...!!!!! Hongera CDM kwa kujenga chama kuanzia ngazi ya kijiji...!!!!!
 
Hawa MAJANGILI yanajua kinachokuja ndiyo maana wanadilidali kutuletea MACHINE,japo za kichina zije tu.Yaani nadhani siku ya kwanza lazima niwe mlangoni mwa mwandikishaji,hata msimamizi awe Mwamunyange!:cheer2:

Sana tu, na teknolojia tushaijua kabla ya uandikishwaji kuanza hachakachuliwi mtu hapa. Expiry date ya CCM ilikuwa 2010 sasa hivi wapo way overdue watu wanatumia bidhaa iliyokwisha muda wa matumizi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom