Hesabu za ushindi wa majimbo 3 hizi hapa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
2,000
UPO uwezekano mkubwa kwa wagombea watakaosimamishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka ushindi katika kinyang’anyiro cha ubunge katika majimbo matatu.

Majimbo hayo ni ya Songea Mjini mkoani Ruvuma, Singida Kaskazini mkoani Singida na Longido mkoani Arusha. Tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Januari 13, mwakani kuwatarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa wabunge kwa majimbo hayo matatu. Uchaguzi huo utafanyika sambamba na wa madiwani katika kata sita, ambazo hazikuchagua madiwani katika uchaguzi uliofanyika Novemba 26, mwaka huu.

NEC ilitangaza majimbo hayo kuwa wazi baada ya wabunge wake, Leonidas Gama (CCM) wa Songea Mjini kufariki dunia hivi karibuni na Lazaro Nyalandu (CCM) kufukuzwa uanachama na CCM na kupoteza nafasi zake zote ikiwemo ubunge kabla ya kuhamia Chadema. Aidha ushindi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Longido, Onesmo Nangole, ulitenguliwa na Mahakama na hivyo kuilazimisha NEC kuitisha uchaguzi mwingine.

Kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo zitatarajiwa kuanza Desemba 21 na kukamilika Januari 12, mwakani, siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo unaotarajiwa kuandika historia ya uwepo wa vyama vingi vya siasa nchini kutokana na upepo unavyovuma hivi sasa. Uimara wa CCM majimboni Ni wazi kuwa hesabu ya kwanza itakayotumiwa na CCM itakuwa ni uimara wake katika majimbo hayo matatu ya Songea Mjini, Singida Kaskazini na Longido ukilinganisha na vyama vingine vya siasa hususani washindani wake wa karibu Chadema.

Songea Mjini Jimbo la Songea Mjini linapatikana mkoani Ruvuma, mkoa ambao unayo majimbo tisa ya uchaguzi, mengine yakiwa ni Nyasa, Tunduru Kaskazini, Tunduru Kusini, Peramiho, Madaba, Namtumbo, Mbinga Mjini na Mbinga Vijijini, majimbo ambayo yote hivi sasa yapo chini ya CCM. Aidha jimbo hilo linaundwa na kata za Matogoro, Bombambili, Mshangano, Subira, Mletele Mjini, Lizaboni, Msufini, Ruhuwiko, Majengo, Ruvuma, Mfaranyaki na Matarawe, likiwa na wapigakura 95,435.

Urahisi wa Jimbo la Songea Mjini kwa CCM na ugumu wake kwa upinzani unatokana na sababu za kihistoria ambapo Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano ambayo haijawahi kuwa na wabunge kutoka vyama vya upinzani tangu siasa za vyama vingi zirejeshwe nchini mwaka 1992 na uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo kufanyika mwaka 1995. Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Dodoma, Mtwara, Pwani, Ruvuma, Tabora.

Singida Kaskazini Kwa upande wa Jimbo la Singida Kaskazini lililopo mkoani Singida, ni moja kati ya majimbo manane yaliyopo mkoani humo. Jimbo la Singida Kaskazini linaundwa na kata za Ikhanoda, Ilongero, Kinyeto, Maghojoa, Makuro, Merya, Mgori, Msisi, Mtinko, Mudida, Ngimu na Ughandi, likiwa na wapigakura 106,208. Singida ni moja mikoa ambayo ni ngome ya CCM kutokana na chama hicho kupata ushindi wa kishindo tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi.

Mbali ya Singida Kaskazini, majimbo mengine ya mkoani Singida ni Singida Mjini, Iramba Mashariki, Iramba Magharibi, Manyoni Magharibi, Manyoni Mashariki, Singida Mashariki na Singida Magharibi. Nguvu ya CCM inajidhihirisha wazi kutokana na kutoa wabunge saba kati ya wabunge wanane, huku Chadema ikishikilia jimbo moja tu la Singida Mashariki kupitia kwa Mbunge wake Tundu Lissu.

Jimbo la Longido Jimbo la Longido lipo mkoani Arusha, mkoa ambao unayo jumla ya majimbo ya uchaguzi saba, mengine yakiwa ni Monduli, Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Arusha Mjini, Karatu na Ngorongoro, ukiwa na jumla ya wapigakura 831,827. Jimbo la Longido linaundwa na Kata za Engarenaibor, Gelai Lumbwa, Gelai, Meirugoi, Kitumbeine, Longido, Matale, Namanga, Ol –molog na Tingating, likiwa na jumla ya wapigakura 41,941 huku likiwa mpakani mwa mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga.

Kabla ya matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani wa hivi karibuni, Mkoa wa Arusha ulikuwa unajitanabaisha kama ngome kuu ya chama cha Chadema kutokana na wagombea wake kutoa upinzani mkali kwa wagombea wa CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Katika uchaguzi huo, Chadema iliweza kushinda katika nafasi ya ubunge kwa majimbo sita na kubakiza jimbo moja tu la Ngorongoro ambalo ndilo lililochukuliwa na CCM.

Hata hivyo hatua ya CCM kuweza kuchukua kata zote nane katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa mwezi Novemba kunatoa picha ya ujio wa CCM mpya mkoani humo. Ushindi wa kishindo wa madiwani Hesabu ya kwanza itakayotumiwa na CCM ni kutumia ushindi mkubwa ambao chama hicho kilijipatia katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika 43, kama chachu ya kuendeleza ushindi kwa kunyakua majimbo hayo matatu na kata sita zilizobakia. Katika kata hizo 43, CCM ilishinda kata 42, huku ikipoteza kata moja ya Ibhigi iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya iliyochukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

CCM ilishinda katika kata za Morieti, Ambureni, Musa, Ngabobo, Maroroni, Leguruki, Makiba na Moita mkoani Arusha, Mbweni, Kijichi na Saranga za Dar es Salaam, Chipogolo mkoani Dodoma, Bukwimba mkoani Mwanza, Senga mkoani Geita, Kitwiru na Kimala mkoani Iringa. Nyingine ni Bomambuzi, Mnadani na Weruweru mkoani Kilimanjaro, Chikonji na Mnacho mkoani Lindi, Nangwa mkoani Manyara, Kiroka na Sofi mkoani Morogoro, Milongodi, Chanikanguo na Reli mkoani Mtwara, na Kijima na Muhandu mkoani Mwanza.

Zipo pia kata za Sumbawanga Mjini, Lukumbule, Kalulu, Muongozi mkoani Ruvuma, Siuyu mkoani Singida, Nyabubinza mkoani Simiyu, Ndarambo mkoani Songwe, Nata na Urambo mkoani Tabora, Majengo, Mamba na Lukuza mkoani Tanga. Nguvu hiyo ya CCM katika kata hizo miongoni mwake zikiwa katika mikoa ya Arusha, Singida na Ruvuma ambako utafanyika uchaguzi huo mdogo wa ubunge na udiwani ni dalili kuwa CCM imejiimarisha zaidi ukilinganisha na vyama vingine vya siasa miaka miwili tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo upinzani ulikuwa na nguvu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema ana uhakika wa ushindi wa kishindo katika majimbo hayo yote matatu kama ambavyo chama hicho kilivyoshinda kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani katika katika kata 42 kwa asilimia 97.67.

Alisema kimsingi Jimbo la Singida Kaskazini tayari lilikuwa chini ya himaya CCM isipokuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho Nyalandu alijizulu baada ya kushindwa kwendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli. Aidha, alisema katika Jimbo la Songea Mjini ambalo nalo lilikuwa chini ya CCM, mbunge wake Gama aliyefariki hivi karibuni, alianza kufanya kazi nzuri ya kujenga maendeleo ya jimbo hilo chini ya Ilani ya chama hicho.

Akizungumzia Jimbo la Londigo, Polepole alisema katika uchaguzi wa mwaka 2015, chama hicho kilihujumiwa kwa upande wa upinzani kufanya kampeni zisizo za kistaarabu jambo lililofanya Mahakama kutengua ushindi wa mgombea aliyeshinda baada ya CCM kufungua kesi.

Alisema ana uhakika wa ushindi wa kishindo katika majimbo hayo yote matatu kama ambavyo chama hicho kilivyoshinda kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani katika katika kata 43 kwa asilimia 97.67. Kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Katibu Mkuu taifa wa chama hicho, Dk Evarist Mashinji, alisema chama kitatoa taarifa kuhusu utaratibu waliouweka wa kuwapata wagombea wa kuwania majimbo hayo kwa kuwa kwa sasa ndio wako kwenye kikao wakijadiliana suala hilo.
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,969
2,000
Manyo'anokho! Unaandika kama unafukuliwa expansion joints za nyuma huko Lumumba! Eti Tabora haijawahi kutoa mbunge wa upinzani tangu kuanza kwa siasa ya vyama vingi! Manyo'anokho! Hivi ni lin
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,445
2,000
Manyo'anokho! Unaandika kama unafukuliwa expansion joints za nyuma huko Lumumba! Eti Tabora haijawahi kutoa mbunge wa upinzani tangu kuanza kwa siasa ya vyama vingi! Manyo'anokho! Hivi ni lin
Aisee hadi 2020 mbona mtajambishwa sana.
 
Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
16,704

.....
.....huu muda ulioutumia bora unge panda nyanya
 
abdallah chongono

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
351
250
Ila kama ushindi wa HAKI mungu atakuwa nao ILA kama ni wa rushwa hatodumu ni mabalah maana kilichoingia kwa haramu hakuna neema za mungu hilo pia mlielewe naona watu wanapenda siasa kuliko dini
 
Magimbi

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
1,401
2,000
Kama tume ilichaguliwa na Serikali yangu ya CCM basi wapinzani mkae mbali na uchaguzi huu..lakini kama ni tume yetu Mkurugenzi wetu..polisi wetu nawashauri wapinzani mkae pembeni. Tutashinda kwa gharama yeyotee ile..hapa kazi tuu.
 
MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,370

Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Mtwara naTabora kuna wabunge wa UPINZANI
 
leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
1,982
2,000
Hivi ni gazeti gani ume quote eti? Mbona unalificha hilo gazeti lisilojua hata wale wabunge wawili walio wekwa ndani Moro Lijualikali na mwenzake wanatoka mkoa gani!
Halafu kweli nilikuwa nimesahau mbunge Mag Sakaya wa Tabora anatoka CCM
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema ana uhakika wa ushindi wa kishindo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom