CCM amueni kati ya hawa wawili

CCM amueni kati ya hawa wawili

kama ni mfuatiliaji wa siasa za tanzania utakubaliana na mimi kuwa nchi hii imekuwa ikikosa viongozi wazuri kwa sababu tu ya rushwa , ushabiki usio na maono na upenzi tu.

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza watangaza nia wa chama cha mapinduzi na nafikiri kama hauendeshwi na siasa za ushabiki,upenzi, wivu,chuki na fedha utakubaliana na mimi kuwa wagombea wenye maono na wanaotakiwa kuwekwa na kupambanishwa na chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi huu ni prof muhongo , january makamba.

Hapa ninaelezea wagombea walioonyesha kuwa na maono mazuri ya tanzania tuitakayo huko mbeleni na wamejipambanua vizuri kimpakakati kwenye kuyafikia maono yao kwenye how. Nasema hivi kwa sababu nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu wa siasa za marekani na sehemu za ulaya na nilichokuja kugundua kwa wale binadamu wenzetu ni kuwa wanaangalia sana how utakavoenda kutekeleza sera zako na sio tu uzuri wa sera. Na hapa ndo nchi nyingi za kiafrika tumekuwa tunafeli siku zote kwa sababu hatuwapimi wagombea kwa njia na mikakati yao ya kutekeleza sera zao bali uzuri tu wa sera zao na uwezo wao wa kuyazungumzia matatizo ya wananchi.

Najua wapenzi wa watangaza nia wengine mtanisema vibaya ila naomba tu leo niwajadili hawa na kutoa hitimisho mwishoni juu ya nani wa kupewa bendera ya chama chao ili akiwakilishe kwenye uchaguzi mkuu.

Kusema ukweli hawa wagombea wote wameonekana kuwa watu wa facts na reality na sio porojo na maneno matamu tu. Wote kwa pamoja wamejitanabaisha kuwa sio watu wa maneno maneno bali ni issues tu.wote kwa pamoja wamejionyesha kuwa wana maono mazuri na wanatumia vizuri exposure yao katika kuitengeneza tanzania ijayo.

Wote wanaonekana hawana mda na mtu wala visasi na mtu kitu ambacho ni kikubwa sana kwa chama cha mapinduzi kwa wakati huu na ujao. Ka kifupi kama mtu alisikiliza hotuba ya kingunge wakati lowassa anatangaza nia arusha na maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na membe wakati anatangaza nia huko kwao lindi atakubaliana na mimi. N i ukweli usiopingika kuwa endapo team lowassa watashika nchi kuna watu lazima watakimbia nchi na likewise membe akishika nchi ni lazima upande wa pili watafute sehemu ya kwenda. Na kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za tanzania utagundua ugomvi wa hizi timu mbili ndo zimeupa shida sana utawala wa sasa.

Napenda kumalizia kwa kuonesha wapi ambapo mimi naona prof muhongo amemzidi bwana january makamba. Sehemu pekee ambayo prof muhongo amemzidi january makamba ni kwenye uwezo wa kuongoza, kusimamia mambo kwa weredi wa hali ya juu na utendaji kwa ujumla.

Sisemi hivi ili kumsifia tu prof muhongo ila kila mtu anakubali kuwa huyu prof amekaa kwenye system kwa miaka miwili tu ila alivoisimamia tanesco hasa kwa miradi ya usambazaji vijijini hadi kufikia asilimia 38 wakati anaondoka huu ni utendaji wa kutukuka na kipekee sana unaomfanya astahili kupewa tuzo ya heshima na raisi. Pili ni alivosimamia sekta ya gesi kwa kipindi hiki kifupi huku akikataa kuwapa watu wababaishaji vitalu na kusimamia upatikanaji wa schoralships kwa watanzania wengi inasemekana zaidi ya 100 kwa ajili tu ya kuifanya nchi ije kuwa na wataalam wa kusimamia hii sekta(hapa napenda kumfananisha na kagame anavofanya rwanda).

Hizo ndo sifa ambazo prof muhongo anaonekana kumzidi january makamba na january anaitaji kupewa mda kidogo ili aweze kuprove how strong he is kwenye huo upande.

Napenda kusisitiza kuwa watu wa kambi zingine mtanisamehe sana,wengi wagombea wenu wnapata popurarity only kwa kuisemea rushwa tu na kupambana na wala rushwa ila sio kwenye vision ya kuitengeneza tanzania imara kwenye uchumi na mikakati ya kutekeleza sera zao na kuifikia iyo vision.

Nilisema kwenye post moja humu kuwa ccm iandae timu imara ya kufanya kazi na prof muhongo na kwa kuanzia mwampe salim ahmed salim kuwa makamu wake. Leo napenda kutoa ushauri kwa prof mwenyewe kuwa mungu akikubariki uingie magogoni mambo ya nje mpeleke january akajijenge zaidi, na january najua utasoma hii post naomba sana ufanyie kazi ilo eneo nililokuomba ulithibitishe kwa watanzania ili mda ukifika prof akistep down upewe kijiti uendeleze vision bora kwa taifa la tanzania.

Mungu ibariki tanzania na watanzania wote.

Mungu wabariki prof muhongo na january makamba.


moja ya vitu alivobugi huyo 'le profeseri muongo' eti akipewa nchi ataiongoza kwa uchumi wa gesi na kila mwananchi atakuwa na bomba mbili, moja la gesi na moja la maji...hahaha how is this possible????
 
moja ya vitu alivobugi huyo 'le profeseri muongo' eti akipewa nchi ataiongoza kwa uchumi wa gesi na kila mwananchi atakuwa na bomba mbili, moja la gesi na moja la maji...hahaha how is this possible????
Sikiliza vizuri hotuba yake wakati anatangaza nia ndugu ndo utaelewa vizuri.
 
Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania utakubaliana na mimi kuwa nchi hii imekuwa ikikosa viongozi wazuri kwa sababu tu ya rushwa , ushabiki usio na maono na upenzi tu.

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza watangaza nia wa chama cha mapinduzi na nafikiri kama hauendeshwi na siasa za ushabiki,upenzi, wivu,chuki na fedha utakubaliana na mimi kuwa wagombea wenye maono na wanaotakiwa kuwekwa na kupambanishwa na chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi huu ni Prof Muhongo , January Makamba.

Hapa ninaelezea wagombea walioonyesha kuwa na maono mazuri ya Tanzania tuitakayo huko mbeleni na wamejipambanua vizuri kimpakakati kwenye kuyafikia maono yao kwenye HOW. Nasema hivi kwa sababu nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu wa siasa za Marekani na sehemu za ulaya na nilichokuja kugundua kwa wale binadamu wenzetu ni kuwa wanaangalia sana how utakavoenda kutekeleza sera zako na sio tu uzuri wa sera. Na hapa ndo nchi nyingi za kiafrika tumekuwa tunafeli siku zote kwa sababu hatuwapimi wagombea kwa njia na mikakati yao ya kutekeleza sera zao bali uzuri tu wa sera zao na uwezo wao wa kuyazungumzia matatizo ya wananchi.

Najua wapenzi wa watangaza nia wengine mtanisema vibaya ila naomba tu leo niwajadili hawa na kutoa hitimisho mwishoni juu ya nani wa kupewa bendera ya chama chao ili akiwakilishe kwenye uchaguzi mkuu.

Kusema ukweli hawa wagombea wote wameonekana kuwa watu wa facts na reality na sio porojo na maneno matamu tu. Wote kwa pamoja wamejitanabaisha kuwa sio watu wa maneno maneno bali ni issues tu.wote kwa pamoja wamejionyesha kuwa wana maono mazuri na wanatumia vizuri exposure yao katika kuitengeneza Tanzania ijayo.

Wote wanaonekana hawana mda na mtu wala visasi na mtu kitu ambacho ni kikubwa sana kwa chama cha mapinduzi kwa wakati huu na ujao. Ka kifupi kama mtu alisikiliza hotuba ya kingunge wakati lowassa anatangaza nia Arusha na maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na Membe wakati anatangaza nia huko kwao Lindi atakubaliana na mimi. N I ukweli usiopingika kuwa endapo team lowassa watashika nchi kuna watu lazima watakimbia nchi na likewise Membe akishika nchi ni lazima upande wa pili watafute sehemu ya kwenda. Na kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania utagundua ugomvi wa hizi timu mbili ndo zimeupa shida sana utawala wa sasa.

Napenda kumalizia kwa kuonesha wapi ambapo mimi naona Prof Muhongo amemzidi bwana January Makamba. Sehemu pekee ambayo Prof Muhongo amemzidi January Makamba ni kwenye uwezo wa kuongoza, kusimamia mambo kwa weredi wa hali ya juu na utendaji kwa ujumla.

Sisemi hivi ili kumsifia tu Prof Muhongo ila kila mtu anakubali kuwa huyu Prof amekaa kwenye system kwa miaka miwili tu ila alivoisimamia Tanesco hasa kwa miradi ya usambazaji vijijini hadi kufikia asilimia 38 wakati anaondoka huu ni utendaji wa kutukuka na kipekee sana unaomfanya astahili kupewa tuzo ya heshima na raisi. Pili ni alivosimamia sekta ya gesi kwa kipindi hiki kifupi huku akikataa kuwapa watu wababaishaji vitalu na kusimamia upatikanaji wa schoralships kwa watanzania wengi inasemekana zaidi ya 100 kwa ajili tu ya kuifanya nchi ije kuwa na wataalam wa kusimamia hii sekta(hapa napenda kumfananisha na kagame anavofanya Rwanda).

Hizo ndo sifa ambazo Prof Muhongo anaonekana kumzidi January Makamba na January anaitaji kupewa mda kidogo ili aweze kuprove how strong he is kwenye huo upande.

Napenda kusisitiza kuwa watu wa kambi zingine mtanisamehe sana,wengi wagombea wenu wnapata popurarity only kwa kuisemea rushwa tu na kupambana na wala rushwa ila sio kwenye vision ya kuitengeneza Tanzania imara kwenye uchumi na mikakati ya kutekeleza sera zao na kuifikia iyo vision.

Nilisema kwenye post moja humu kuwa CCM iandae timu imara ya kufanya kazi na Prof MUHONGO na kwa kuanzia mwampe Salim Ahmed Salim kuwa makamu wake. Leo napenda kutoa ushauri kwa Prof mwenyewe kuwa Mungu akikubariki uingie magogoni mambo ya nje mpeleke January akajijenge zaidi, na January najua utasoma hii post naomba sana ufanyie kazi ilo eneo nililokuomba ulithibitishe kwa watanzania ili mda ukifika Prof akistep down upewe kijiti uendeleze vision bora kwa taifa la Tanzania.

MUNGU ibariki TANZANIA na WATANZANIA WOTE.

MUNGU wabariki Prof Muhongo na January Makamba.

Nakuunga mkono mtoa mada
 
January na muhungo ni kati ya walioenda nnje ya utaratibu na dawa yao ni kukatwa tu
Ndugu hadi leo unaamini unatakiwa uletewe kiongozi usiyejua mtazamo wake na fikra zake ni zipi juu ya taifa lako na maisha yako kama mwananchi??? Basi si bora tungebaki kwenye one party system tu.
Alafu hadi watu makini kama waliokuzwa na chama kama balozi augusto Mahiga nae kajitokeza na kujieleza. na pia mzee kingunge anayekijua chama vizuri ameshiriki mtu wake akitangaza nia na kujitangaza sera zake sasa unaamini kuwa iyo ni hoja nzito ya kumdisqualify mtu potential ili kuiongoza nchi yako?
 
Tatizo watu tunashindwa kuelewa,kutoa hotuba nzuri hata Rostam Aziz anaweza jitokeza na kutangaza nia kwa kuandaa hotuba nzuri,kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti,naona kuna mwana jf anajalibu kuaminisha watu kuwa Mwiguru kwa sababu ameongea vizuri basi awe Raisi wetu,,kama hivyo ndivyo basi nchi hii imaweza pia ongozwa na watengeneza hotuba wa viongozi,,
 
Sasa umeandika nini? Unabeba mawe mgongoni? hayawezi kubadilika kuwa watoto ndugu.Pole!
 
Binafsi namuona January makamba ni zaidi ya urais namfananisha na Ahmed salum katika ubora wake
 
Binafsi namuona January makamba ni zaidi ya urais namfananisha na Ahmed salum katika ubora wake
January ni hazina na yuko vizuri sana ndugu. Sehemu pekee ninayoona tumpe mda na autumie vizuri huo mda ni kwenye eneo la usimamizi wa mambo na utendaji wa mambo katika uweredi wa hali ya juu( kwa sababu leadership tu sio kigezo hata uwezo kwenye management nao ni muhimu sana)
 
umakin n muhm juu ya swala hili
Kweli kabisa ndugu. Huu ulikuwa ni wakati wa wananchi kukaa na kusali kumwambia Mungu afanye yake katika hili. Ila tunajikita kwenye ushabiki tu usio na maono, wivu, chuki na siasa za fedha na kuchafuana.
Mungu aiangalie Tanzania kwa kweli.
 
January ni hazina na yuko vizuri sana ndugu. Sehemu pekee ninayoona tumpe mda na autumie vizuri huo mda ni kwenye eneo la usimamizi wa mambo na utendaji wa mambo katika uweredi wa hali ya juu( kwa sababu leadership tu sio kigezo hata uwezo kwenye management nao ni muhimu sana)

Uongozi ni dhamana haja ni kutumikia nafasi unayopewa sio kutumika namuamini Jmakamba kama mtu wa kusimamia kile anachokiamini pia ni mpangaji mzuri na mtekelezaji mwenye uweledi na stahaa sio mtu wa kuzungumza sana.
Aina yake hittler wa ujerumani good orator and implementor
 
Huyu kweli ni wa kupewa hongera tu kwa kuandika, hivi ana underestimate nguvu ya ukawa eeh, yaani kusimamisha Muhongo au Makamba ni bora hata uchaguzi tusifanyike tu kuokoa hizo fedha, tunamwachia tu Dr.Slaa aende zake Magogoni
hao ni marais wa ccm siyo marais wa watanzai jaman mbona hamuelewi kiongozz wa wa kweli yupo ukawa
 
Bwana mwandishi sijakuelewa kidogo, huyu bwana Muhongo si ndo yule mwenye kashfa ya Escrow, yule aliyetajwa kuwa ni profesa wa kwanza muongo kuwahi kutokea, aliyelazimishwa na bosi wake ajiuzuru. Acha kuwadanganya CCM wapoteze kiti. Na huyu January si ndo yule yumo kwenye mambo ya Usho.. Tanzania kweli tumefika pabaya hatuna kiongozi kabisa anayejipambanua miongoni mwa watu kuwa na sifa za kuwa Raisi. Eeee baba wa Taifa tuombee
 
hao ni marais wa ccm siyo marais wa watanzai jaman mbona hamuelewi kiongozz wa wa kweli yupo ukawa
Kwa kweli kati ya vitu vilivyonisikitisha ni kwa jinsi Ukawa wanavoendesha mambo yao sasaivi.
Ndugu zanguni Ukawa huu ulikuwa ni wakati muafaka narudia tena muafaka kwa nyie kuwaonyesha watanzania kwanza ni kwa jinsi gani mlivo na demokrasia ya kweli na sio ya maneno tu(ndani ya vyama) na pili ni kwa jinsi gani mlivyo na resources za kutosha ndani ya vyama vyenu. Kusema kweli imenisikitisha sana kwa NCCR tulitangaziwa tu fulani kapitishwa, hata hatujui alipambanishwa na kina nani na walikuwa ni watu wa namna gani na wana fikra gani na maono gani juu ya Tanzania. kwa CUF ndo tunasikia kwanza Lipumba anatangaza jumapili na hatuna uhakika kwma kuna mtu atapambana nae. Kwa chama kikuu cha upinzani nasikia ndo kuna Slaa tu na hana mpinzani. NDUGU ZANGU hili ni kosa kubwa sana hasa katika dunia ya leo. Sina uhakika vitengo vyenu vya intellensia vinafanya kazi gani kwa sababu vingeweza tu kuwashauri kuwa hata mtengeneze watu kadhaa wasio na sifa ndani ya vyama vyenu na mkawapambanisha live mbele ya watanzania na kuwapata hao mnaowachukulia kama ndo wenye haki ya kugombea nafasi ya juu kabisa nchini.( Hii alikuwa anafanya hata Mobutu wakati ule zaire).
Sasa hiyo ni weakeness kubwa sana kwa ukawa na napenda kusema hata mkija na sera zipi kwa hizo elements tu mtashindwa kuwashawishi watanzania.
Uzuri wa demokrasia ndo huo, kuwa unakuwa na watu wengi wanaopewa nafasi sawa na siku ya mwisho mnaamua yupi ni bora kati ya wote. Mfano ni kwa kama ilivo kwa CCM saivi, mwanzoni ilikuwa ni Lowassa na Membe na wengine kwa karibu sitta, sumaye na wassira. Ila walipoamua kuipa nafasi demokrasia na tumewasikiliza wote ndo hapa kama wengine tumewaona Prof Muhongo na January Makamba kuwa ni bora na ndo wanaoitajika kwa taifa la Tanzania.
 
Bwana mwandishi sijakuelewa kidogo, huyu bwana Muhongo si ndo yule mwenye kashfa ya Escrow, yule aliyetajwa kuwa ni profesa wa kwanza muongo kuwahi kutokea, aliyelazimishwa na bosi wake ajiuzuru. Acha kuwadanganya CCM wapoteze kiti. Na huyu January si ndo yule yumo kwenye mambo ya Usho.. Tanzania kweli tumefika pabaya hatuna kiongozi kabisa anayejipambanua miongoni mwa watu kuwa na sifa za kuwa Raisi. Eeee baba wa Taifa tuombee

Duh ndugu yangu nimelielezea sana hilo suala kwenye pages zingine,fuatilia juu uko nawe utajua kuwa upo wapi. Kwa kifupi nikuulize tu Muhongo ndo mwenye escrow kivipi??? Ndo alieanzisha akaunti ya esrow? AU alieratibu issue uya escrow????
Ni ripoti ipi ya uchunguzi imesema ivo??? au labda kwenye wafaidika wa fedha tuambie labda nae alikuwepo???? aliwekewa sh. ngapi kwa account gani??? au kwa kukiuka maadili labda uliona jina lake tume ya maadili??????
 
Nazani nilikua wa kwanza kupendekeza hapa with title; "Napendekeza Muhongo Uraisi Tz", Ila kwa kua wakati ule wachangiaji wengi walileweshwa na sakata la Escro, few could see me through. Naungana na mtoa mada mia kwa mia, kama ukijivua ushabiki na mihemko ya kimakundi utaweza ona mbali kwamba Muhongo ndiye mtu sahihi tunayemhitaji leo hii kushika nafasi ya uraisi.
 
Nazani nilikua wa kwanza kupendekeza hapa with title; "Napendekeza Muhongo Uraisi Tz", Ila kwa kua wakati ule wachangiaji wengi walileweshwa na sakata la Escro, few could see me through. Naungana na mtoa mada mia kwa mia, kama ukijivua ushabiki na mihemko ya kimakundi utaweza ona mbali kwamba Muhongo ndiye mtu sahihi tunayemhitaji leo hii kushika nafasi ya uraisi.

Kusema kweli hata mimi kabla nilikuwa namkubali Muhongo kwa upande wa utendaji na weredi wake tu. Ila nilipokuja kumsikiliza nakumbuka nilitamani hata kulia machozi nikasema tulikuwa wapi kuitumia hii resource. Ingawa kwa makamba tangu mwanzo lilisoma kitabu chake nikajua hapa kuna kitu kwa watanzania.
 
moja ya vitu alivobugi huyo 'le profeseri muongo' eti akipewa nchi ataiongoza kwa uchumi wa gesi na kila mwananchi atakuwa na bomba mbili, moja la gesi na moja la maji...hahaha how is this possible????

january makamba siku ya kutangaza nia aliweka wazi kuhusu suala la gesi kwamba miaka kumi ijayo gesi itakuwa bado haijatoka kinachofanyika sasa ni miundo mbinu tu
 
Wanzania tuamuitaji rais aina ya MAGUFULI bac,wakijichanganya tu ccm imeeat kwao.
 
Back
Top Bottom