CCM amueni kati ya hawa wawili

CCM amueni kati ya hawa wawili

Mtoa mada dont underestimate Magufuli. Huyu jamaa kama umemgundua si mtu wa porojo, ni vitendo tu. Amejizuia sana kutoa hotuba za mbwembwe. Lakini utendaji wake tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye baraza la mawaziri hakuna mtanzania atakayeusahau. Sina hakika na January lakini kama ikibidi wabaki wawili basi ni Muhongo na Magufuli. Udhaifu mkubwa wa Muhongo (ambapo anazidiwa na magufuli) ni kwamba Prof. hana uzoefu na chaguzi, hajawahi kugombea hata udiwani (maana ni mbunge wa kuteuliwa), sasa moja kwa moja kwenye urais, hii inaweza kuwa changamoto kwake.
Magufuli ni mzuri pia kaka. Ninachompendea ni kuwa ni mtu ambaye yuko straight na ukimwambia asimamie anasimamia ipasavyo.
Ila kosa kubwa sana la magufuri ni kutoitumia nafasi aliyopewa na demokrasia vizuri. Nifafanue hapa, unapotangaza nia sio tu unatangaza kwa wana CCM, hii dunia imebadirika sana sasa ni lazima utumie nafasi uliyopewa na demokrasia kujieleza vizuri kwa sababu siku ya mwisho utapigiwa kura na watanzania wote. Alitakiwa at least atuambie maono yake na fikra zake juu ya Tanzania tunayoitaka. Dunia ya sasa watu wako makini sana wanaogopa kuuziwa mbuzi kwenye gunia.

Kitu kingine ambacho ni changu binafsi ni kuwa namuona magufuri hana vision nzuri. Hii mimi ninaithibitisha kwa jinsi alivoshindwa kuishauri serikali yake vizuri kuhusu ujenzi wa barabara za kuingia mji mkuu wa kibiashara hapa Tanzania Dar es salaam. Embu angalia ujenzi wa barabara za morogoro,bagamoyo na kilwa ndugu yangu. Kwangu mimi binafsi nilidhani angeitumia exposure yake vizuri hata kushauri zile barabara zijengwe kwa 3 or 4 lines kila moja kwa mfumo wa super highways. Hii sio tu kupunguza msongamano wa magari ila pia kupendezesha mji na kuufanya uwe na hadhi inayostahili.(napenda kusisitiza hili ni langu binafsi)
 
Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania utakubaliana na mimi kuwa nchi hii imekuwa ikikosa viongozi wazuri kwa sababu tu ya rushwa , ushabiki usio na maono na upenzi tu.

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza watangaza nia wa chama cha mapinduzi na nafikiri kama hauendeshwi na siasa za ushabiki,upenzi, wivu,chuki na fedha utakubaliana na mimi kuwa wagombea wenye maono na wanaotakiwa kuwekwa na kupambanishwa na chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi huu ni Prof Muhongo , January Makamba.

Hapa ninaelezea wagombea walioonyesha kuwa na maono mazuri ya Tanzania tuitakayo huko mbeleni na wamejipambanua vizuri kimpakakati kwenye kuyafikia maono yao kwenye HOW. Nasema hivi kwa sababu nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu wa siasa za Marekani na sehemu za ulaya na nilichokuja kugundua kwa wale binadamu wenzetu ni kuwa wanaangalia sana how utakavoenda kutekeleza sera zako na sio tu uzuri wa sera. Na hapa ndo nchi nyingi za kiafrika tumekuwa tunafeli siku zote kwa sababu hatuwapimi wagombea kwa njia na mikakati yao ya kutekeleza sera zao bali uzuri tu wa sera zao na uwezo wao wa kuyazungumzia matatizo ya wananchi.

Najua wapenzi wa watangaza nia wengine mtanisema vibaya ila naomba tu leo niwajadili hawa na kutoa hitimisho mwishoni juu ya nani wa kupewa bendera ya chama chao ili akiwakilishe kwenye uchaguzi mkuu.

Kusema ukweli hawa wagombea wote wameonekana kuwa watu wa facts na reality na sio porojo na maneno matamu tu. Wote kwa pamoja wamejitanabaisha kuwa sio watu wa maneno maneno bali ni issues tu.wote kwa pamoja wamejionyesha kuwa wana maono mazuri na wanatumia vizuri exposure yao katika kuitengeneza Tanzania ijayo.

Wote wanaonekana hawana mda na mtu wala visasi na mtu kitu ambacho ni kikubwa sana kwa chama cha mapinduzi kwa wakati huu na ujao. Ka kifupi kama mtu alisikiliza hotuba ya kingunge wakati lowassa anatangaza nia Arusha na maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na Membe wakati anatangaza nia huko kwao Lindi atakubaliana na mimi. N I ukweli usiopingika kuwa endapo team lowassa watashika nchi kuna watu lazima watakimbia nchi na likewise Membe akishika nchi ni lazima upande wa pili watafute sehemu ya kwenda. Na kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania utagundua ugomvi wa hizi timu mbili ndo zimeupa shida sana utawala wa sasa.

Napenda kumalizia kwa kuonesha wapi ambapo mimi naona Prof Muhongo amemzidi bwana January Makamba. Sehemu pekee ambayo Prof Muhongo amemzidi January Makamba ni kwenye uwezo wa kuongoza, kusimamia mambo kwa weredi wa hali ya juu na utendaji kwa ujumla.

Sisemi hivi ili kumsifia tu Prof Muhongo ila kila mtu anakubali kuwa huyu Prof amekaa kwenye system kwa miaka miwili tu ila alivoisimamia Tanesco hasa kwa miradi ya usambazaji vijijini hadi kufikia asilimia 38 wakati anaondoka huu ni utendaji wa kutukuka na kipekee sana unaomfanya astahili kupewa tuzo ya heshima na raisi. Pili ni alivosimamia sekta ya gesi kwa kipindi hiki kifupi huku akikataa kuwapa watu wababaishaji vitalu na kusimamia upatikanaji wa schoralships kwa watanzania wengi inasemekana zaidi ya 100 kwa ajili tu ya kuifanya nchi ije kuwa na wataalam wa kusimamia hii sekta(hapa napenda kumfananisha na kagame anavofanya Rwanda).

Hizo ndo sifa ambazo Prof Muhongo anaonekana kumzidi January Makamba na January anaitaji kupewa mda kidogo ili aweze kuprove how strong he is kwenye huo upande.

Napenda kusisitiza kuwa watu wa kambi zingine mtanisamehe sana,wengi wagombea wenu wnapata popurarity only kwa kuisemea rushwa tu na kupambana na wala rushwa ila sio kwenye vision ya kuitengeneza Tanzania imara kwenye uchumi na mikakati ya kutekeleza sera zao na kuifikia iyo vision.

Nilisema kwenye post moja humu kuwa CCM iandae timu imara ya kufanya kazi na Prof MUHONGO na kwa kuanzia mwampe Salim Ahmed Salim kuwa makamu wake. Leo napenda kutoa ushauri kwa Prof mwenyewe kuwa Mungu akikubariki uingie magogoni mambo ya nje mpeleke January akajijenge zaidi, na January najua utasoma hii post naomba sana ufanyie kazi ilo eneo nililokuomba ulithibitishe kwa watanzania ili mda ukifika Prof akistep down upewe kijiti uendeleze vision bora kwa taifa la Tanzania.

MUNGU ibariki TANZANIA na WATANZANIA WOTE.

MUNGU wabariki Prof Muhongo na January Makamba.

hongera binafsi nakupongeza kwa sababu umejitahidi kuandika na huo ni mtazamo wako kwahiyo haufatwi ila haupingwi, kimsingi sidhani kama watanzania wanahitaji kiongozi ambaye yupo kwenye system ya uongozi kwa miaka mingi kwa sababu hata hao wapo (ambao wamekaa mda mrefu ila ni mafisadi) wanahitaji kiongozi ambaye ana weledi, uwezo wa kutatua changamoto zao ntanukuu mh january makamba kwenywe kitabu chake cha Maswali 40 na majibu 40 kuwa ''Kama una maana ya kukomaa kwa maana ya kuzifahamu kero za Watanzania na uwezo wa kuzipatia majawabu, jibu pia ni ndio, nimekomaa. Na tena sio
kuyafahamu majawabu ya siku zote bali maarifa mapya yanayoendana na
karne hii mpya. Kama ni kukomaa kwa maana ya kuwepo kwenye siasa kwa
miaka mingi, sina hakika Watanzania wanatafuta kiongozi ambaye kwa miaka
40 ameshiriki kuuweka mfumo tunaoulalamikia.
Kama ni kukomaa kwa maana ya busara, hekima na uwezo wa kufanya
maamuzi sahihi, jibu pia ni ndio, nimekomaa. Sina rekodi ya kuropoka,
kutukana, kuhamaki, kushambuliana na watu na kufanya maamuzi ya
papara. Najua uzito wa dhamana ya uongozi.
 
Kama sijakosea, hivi si huyu Muongo, sorry Muhongo, wakati watanzania wenye uwezo walipimuomba washirikishwe katika biashara ya gesi akakataa na kuwakejeli kuwa watanzania wanauwezo tu wa kushiriki katika biashara za kuuza juice na njugu. Baadae akakimbilia Canada kusaini mikataba na wazungu. Sasa mtu kama huyu ambae hana sera za maksudi za kuwainua wazawa atawezaje kuwa Rais wao!!

Achana nae huyo. Kazoea kuwa boi wa wazungu. Hivi ile kazi yake ya kuangalia miamba duniani aliyopewa na wazungu baada ya kutimuliwa uwaziri imeishia wapi???

alielezea ni kwanini hawawezi kuchimba kuwa ghalama za uendeshaji ni kubwa ukilinganisha na matajili wetu WA bongo akiwa MENGI
 
Nategemeaga sana critical analysis inayotoa majibu murua kutoka kwa members wa hii forum ila nikipataga majibu kama haya ndo naumiaga kwa kweli ndugu.
Hizo kashfa mnazozisema ni zipi na zenye uthibitisho gani? Alafu hizi tabia za kuwadharau watanzania eti hawafuatilii na kuyajua mambo ndo mana nasema kila siku Mungu atuhurumie. lets take mfano huu tu tuseme jamii forums ina wafuatiliaji zaidi ya laki 5 mikoa mbalimbali na wote wanafuatilia huu mjadala humu. hao watu hawana marafiki? hao watu hawana watu wnaojadili nao mambo ya siasa za tanzania na mustakabali wa taifa kwa ujumla???
Alafu with all confidence unasema angeachana na mambo ya siasa? yaani nawe umeona kuwa huyu alipigwa tu zengwe na unaona kuwa alionewa alafu unasema kabisa aachane tu na siasa pamoja na alivo potential.
kwa mitazamo kama hii ndugu yangu tusije kumlaumu kikwete alivosema hajui kwa nini tanzania ni maskini kwa sababu hii inaprove kuwa tunatabia mbaya ya kuendekeza siasa kutawala maisha yetu na kutotumia resources zetu vizuri na ndo mana tunakuwa maskini kila siku. Na tusipoangalia tutakuwa maskini kwa fikra hizi hadi Mungu anakuja kuchukua ulimwengu wake.

Huo mfano uliyoutoa utabaki kuwa hivyohivyo ni mfano tu,lakini kiuhalisia Jf haipo hivyo kama wengi wanavyofikiri. Wanachokijua wananchi ni kwamba huyo jamaa ana kashfa ya ufisadi na hadi amejiudhuru kutokana na jambo hilo. Sasa sie humu kubishana kuwa huyo jamaa alifisadi kweli ama si kweli haitosaidia chochote huo ndio ukweli ulivyo. Lakini pia mie sijasema kwamba aachane kabisa na mambo ya siasa ila nimesema kuwa aachane na hiyo nafasi ya urais.
 
Sasa ndugu yangu kama hilo ndo tatizo ni jukumu letu mimi na wewe kuwaelimisha Watanzania wenzetu juu ya ukweli halisi kwa maslahi mapana ya taifa letu na wananchi kwa ujumla. Tumeshaona kuwa tumeletewa mtu na Mungu wa kutuvusha basi hatuni budi kuwaambia wenzetu ambao bado walipofushwa na wale watu wabaya ukweli halisi na kuuambia umma wa watanzania wenzetu kuwa the time is now ya kumtumia huyu mtu. La sivo tutaendelea kuwa vilevile tu.
 
Ni January pekee aliye msafi na muadilifu, mchapakazi asiye kwenye kashfa
Twendeni na Jmakamba... 1434036523813.jpg
 
Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania utakubaliana na mimi kuwa nchi hii imekuwa ikikosa viongozi wazuri kwa sababu tu ya rushwa , ushabiki usio na maono na upenzi tu.

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza watangaza nia wa chama cha mapinduzi na nafikiri kama hauendeshwi na siasa za ushabiki,upenzi, wivu,chuki na fedha utakubaliana na mimi kuwa wagombea wenye maono na wanaotakiwa kuwekwa na kupambanishwa na chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi huu ni Prof Muhongo , January Makamba.

Hapa ninaelezea wagombea walioonyesha kuwa na maono mazuri ya Tanzania tuitakayo huko mbeleni na wamejipambanua vizuri kimpakakati kwenye kuyafikia maono yao kwenye HOW. Nasema hivi kwa sababu nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu wa siasa za Marekani na sehemu za ulaya na nilichokuja kugundua kwa wale binadamu wenzetu ni kuwa wanaangalia sana how utakavoenda kutekeleza sera zako na sio tu uzuri wa sera. Na hapa ndo nchi nyingi za kiafrika tumekuwa tunafeli siku zote kwa sababu hatuwapimi wagombea kwa njia na mikakati yao ya kutekeleza sera zao bali uzuri tu wa sera zao na uwezo wao wa kuyazungumzia matatizo ya wananchi.

Najua wapenzi wa watangaza nia wengine mtanisema vibaya ila naomba tu leo niwajadili hawa na kutoa hitimisho mwishoni juu ya nani wa kupewa bendera ya chama chao ili akiwakilishe kwenye uchaguzi mkuu.

Kusema ukweli hawa wagombea wote wameonekana kuwa watu wa facts na reality na sio porojo na maneno matamu tu. Wote kwa pamoja wamejitanabaisha kuwa sio watu wa maneno maneno bali ni issues tu.wote kwa pamoja wamejionyesha kuwa wana maono mazuri na wanatumia vizuri exposure yao katika kuitengeneza Tanzania ijayo.

Wote wanaonekana hawana mda na mtu wala visasi na mtu kitu ambacho ni kikubwa sana kwa chama cha mapinduzi kwa wakati huu na ujao. Ka kifupi kama mtu alisikiliza hotuba ya kingunge wakati lowassa anatangaza nia Arusha na maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na Membe wakati anatangaza nia huko kwao Lindi atakubaliana na mimi. N I ukweli usiopingika kuwa endapo team lowassa watashika nchi kuna watu lazima watakimbia nchi na likewise Membe akishika nchi ni lazima upande wa pili watafute sehemu ya kwenda. Na kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania utagundua ugomvi wa hizi timu mbili ndo zimeupa shida sana utawala wa sasa.

Napenda kumalizia kwa kuonesha wapi ambapo mimi naona Prof Muhongo amemzidi bwana January Makamba. Sehemu pekee ambayo Prof Muhongo amemzidi January Makamba ni kwenye uwezo wa kuongoza, kusimamia mambo kwa weredi wa hali ya juu na utendaji kwa ujumla.

Sisemi hivi ili kumsifia tu Prof Muhongo ila kila mtu anakubali kuwa huyu Prof amekaa kwenye system kwa miaka miwili tu ila alivoisimamia Tanesco hasa kwa miradi ya usambazaji vijijini hadi kufikia asilimia 38 wakati anaondoka huu ni utendaji wa kutukuka na kipekee sana unaomfanya astahili kupewa tuzo ya heshima na raisi. Pili ni alivosimamia sekta ya gesi kwa kipindi hiki kifupi huku akikataa kuwapa watu wababaishaji vitalu na kusimamia upatikanaji wa schoralships kwa watanzania wengi inasemekana zaidi ya 100 kwa ajili tu ya kuifanya nchi ije kuwa na wataalam wa kusimamia hii sekta(hapa napenda kumfananisha na kagame anavofanya Rwanda).

Hizo ndo sifa ambazo Prof Muhongo anaonekana kumzidi January Makamba na January anaitaji kupewa mda kidogo ili aweze kuprove how strong he is kwenye huo upande.

Napenda kusisitiza kuwa watu wa kambi zingine mtanisamehe sana,wengi wagombea wenu wnapata popurarity only kwa kuisemea rushwa tu na kupambana na wala rushwa ila sio kwenye vision ya kuitengeneza Tanzania imara kwenye uchumi na mikakati ya kutekeleza sera zao na kuifikia iyo vision.

Nilisema kwenye post moja humu kuwa CCM iandae timu imara ya kufanya kazi na Prof MUHONGO na kwa kuanzia mwampe Salim Ahmed Salim kuwa makamu wake. Leo napenda kutoa ushauri kwa Prof mwenyewe kuwa Mungu akikubariki uingie magogoni mambo ya nje mpeleke January akajijenge zaidi, na January najua utasoma hii post naomba sana ufanyie kazi ilo eneo nililokuomba ulithibitishe kwa watanzania ili mda ukifika Prof akistep down upewe kijiti uendeleze vision bora kwa taifa la Tanzania.

MUNGU ibariki TANZANIA na WATANZANIA WOTE.

MUNGU wabariki Prof Muhongo na January Makamba.
January anamaono yepi? Wa tz hatupo serious
 
Usisahau

*****************

Kupiga kura
Diamond Platnumz kategori 3 (tatu) - Best MALE, Best COLLABORATION na Best LIVE and Vanessa 1(moja) -- Best FEMALE

ingia kwa link hii chini

http://mama.mtv.com/voting/

Bonyeza bonyeza VOTE usichoke

******************
 
Mkuu Lord denning, nakubaliana na wewe, ila kati ya hao uliowasikiliza, jee ulimsikia Mwigulu?!. Mimi nimewasiliza wote, Prof. Muhongo was real good tatizo lake ni kujitapa mno kuwa he is the only one!, uongozi ni team work, mtu anayejitapa kuwa he is the only one, anakuwa na tatizo la umimi, hivyo ndio the type watakaomake the worst dictators!. Mfanano na Tofauti kati ya Muhongo na Magufuli, wote wawili can make the worst dictators this country has ever had, both wanatoka Kanda ya Ziwa, makabila ya majisifu, kujitapa na madharau, tofauti ni Muhongo ni kichwa cha ukweli tatizo lake ni too boastful na too arrogance mwenye dharau kupitiliza!, wakati Magufuli ni mtu mwenye hasira na katili wa kuweza kuwapotezea wabaya wake into thin air bila thinking twice wala conscious!.

January alijipanga vizuri na kuongea kwa ma poze ya kiobama obama ila sio realist, he was only paying lip services. Kama hukumsikiliza Mwigulu, tembelea hapa!.Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!.

Paskali
Mkuu Lord denning nilikuwa nafanya tuu rejea kumhusu mtu wako huyu!.

Paskal
 
Back
Top Bottom