CCM amueni kati ya hawa wawili

CCM amueni kati ya hawa wawili

Duh ndugu yangu nimelielezea sana hilo suala kwenye pages zingine,fuatilia juu uko nawe utajua kuwa upo wapi. Kwa kifupi nikuulize tu Muhongo ndo mwenye escrow kivipi??? Ndo alieanzisha akaunti ya esrow? AU alieratibu issue uya escrow????
Ni ripoti ipi ya uchunguzi imesema ivo??? au labda kwenye wafaidika wa fedha tuambie labda nae alikuwepo???? aliwekewa sh. ngapi kwa account gani??? au kwa kukiuka maadili labda uliona jina lake tume ya maadili??????

Mkuu teyari huyo mtu anakashfa hayo maswali unayoyauliza wewe humu kama njia ya kuthibitishiwa ufisadi wake sidhani kama watanzania(wapiga kura) wote wanafuatilia au kuyajua hayo,huyo jamaa kwa wananchi huku wanamtambua ni mtu mwenye kashfa ya ufisadi hivyo Jf haitosaidia kumfanya wananchi kumuelewa tofauti na sasa wanavyomuelewa. Bora angeachana na mambo ya urais kutokana na hiyo kashfa na hatokuwa wa kwanza kuamua hivyo.
 
Kusema kweli hata mimi kabla nilikuwa namkubali Muhongo kwa upande wa utendaji na weredi wake tu. Ila nilipokuja kumsikiliza nakumbuka nilitamani hata kulia machozi nikasema tulikuwa wapi kuitumia hii resource. Ingawa kwa makamba tangu mwanzo lilisoma kitabu chake nikajua hapa kuna kitu kwa watanzania.

Hivyo ndiyo lazima awe rais ili tuweze kumtumia?
 
Muhongo namkubali saana lakini kinachonipa wasiwasi ni vile vikauli vyake vya kujibeba bungeni kipindi cha sakata la Escrow pamoja na kuziita nyaraka za Kafurila ni karatasi za kufungia maandazi mwishowe ukweli ukajulikana .swali langu mtu kama huyu kweli anafaa kuwa mtawala wa hii nchi?
Hapa bado matengenezo yanaitajika

Jamaa ana dharau za wazi kabisa na kujiona hakosei ktk mambo yake sijui akiwa mkuu wa nchi itakuwaje!!
 
Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania utakubaliana na mimi kuwa nchi hii imekuwa ikikosa viongozi wazuri kwa sababu tu ya rushwa , ushabiki usio na maono na upenzi tu.

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza watangaza nia wa chama cha mapinduzi na nafikiri kama hauendeshwi na siasa za ushabiki,upenzi, wivu,chuki na fedha utakubaliana na mimi kuwa wagombea wenye maono na wanaotakiwa kuwekwa na kupambanishwa na chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi huu ni Prof Muhongo , January Makamba.
MUNGU ibariki TANZANIA na WATANZANIA WOTE.

MUNGU wabariki Prof Muhongo na January Makamba.
Mkuu Lord denning, nakubaliana na wewe, ila kati ya hao uliowasikiliza, jee ulimsikia Mwigulu?!. Mimi nimewasiliza wote, Prof. Muhongo was real good tatizo lake ni kujitapa mno kuwa he is the only one!, uongozi ni team work, mtu anayejitapa kuwa he is the only one, anakuwa na tatizo la umimi, hivyo ndio the type watakaomake the worst dictators!. Mfanano na Tofauti kati ya Muhongo na Magufuli, wote wawili can make the worst dictators this country has ever had, both wanatoka Kanda ya Ziwa, makabila ya majisifu, kujitapa na madharau, tofauti ni Muhongo ni kichwa cha ukweli tatizo lake ni too boastful na too arrogance mwenye dharau kupitiliza!, wakati Magufuli ni mtu mwenye hasira na katili wa kuweza kuwapotezea wabaya wake into thin air bila thinking twice wala conscious!.

January alijipanga vizuri na kuongea kwa ma poze ya kiobama obama ila sio realist, he was only paying lip services. Kama hukumsikiliza Mwigulu, tembelea hapa!.Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!.

Paskali

Muhongo namkubali saana lakini kinachonipa wasiwasi ni vile vikauli vyake vya kujibeba bungeni kipindi cha sakata la Escrow pamoja na kuziita nyaraka za Kafurila ni karatasi za kufungia maandazi mwishowe ukweli ukajulikana .swali langu mtu kama huyu kweli anafaa kuwa mtawala wa hii nchi?
Hapa bado matengenezo yanaitajika

Jamaa ana dharau za wazi kabisa na kujiona yupo sahihi kwa kila jambo sijui akiwa mkuu wa nchi itakuwaje!!!
 
Katika watia nia wa ccm mpaka sasa profesa muhongo amefunika hilo halina swali, tatizo ccm ya mafisadi wanahitaji mtu kama muhongo? Jibu ni rahisi, hatakiwi. Wao wanataka vilaza kama kina lowassa na membe. Kuhusu January makamba, huyu mwizi wa mitihani galanos hadi akafutiwa mtihani wa taifa anaenda wapi? Halaf unavyosema apelekwe mambo ya nje ili akomae halaf aje atutawale, hivi wewe una akili timamu wewe? Umeona sisi watanzania ni mazezeta ya kutawaliwa na ccm dahari!!? Hapo ndo nimekudharau
 
vipi kuhusu usiri wa mikataba? hasa wa gesi... vipi kuhusu majigambo ya elimu na kuja kutaja matokeo ya mbunge kwakuwa kakosoa wazo lakooo amkeni..
 
Mkuu teyari huyo mtu anakashfa hayo maswali unayoyauliza wewe humu kama njia ya kuthibitishiwa ufisadi wake sidhani kama watanzania(wapiga kura) wote wanafuatilia au kuyajua hayo,huyo jamaa kwa wananchi huku wanamtambua ni mtu mwenye kashfa ya ufisadi hivyo Jf haitosaidia kumfanya wananchi kumuelewa tofauti na sasa wanavyomuelewa. Bora angeachana na mambo ya urais kutokana na hiyo kashfa na hatokuwa wa kwanza kuamua hivyo.
Nategemeaga sana critical analysis inayotoa majibu murua kutoka kwa members wa hii forum ila nikipataga majibu kama haya ndo naumiaga kwa kweli ndugu.
Hizo kashfa mnazozisema ni zipi na zenye uthibitisho gani? Alafu hizi tabia za kuwadharau watanzania eti hawafuatilii na kuyajua mambo ndo mana nasema kila siku Mungu atuhurumie. lets take mfano huu tu tuseme jamii forums ina wafuatiliaji zaidi ya laki 5 mikoa mbalimbali na wote wanafuatilia huu mjadala humu. hao watu hawana marafiki? hao watu hawana watu wnaojadili nao mambo ya siasa za tanzania na mustakabali wa taifa kwa ujumla???
Alafu with all confidence unasema angeachana na mambo ya siasa? yaani nawe umeona kuwa huyu alipigwa tu zengwe na unaona kuwa alionewa alafu unasema kabisa aachane tu na siasa pamoja na alivo potential.
kwa mitazamo kama hii ndugu yangu tusije kumlaumu kikwete alivosema hajui kwa nini tanzania ni maskini kwa sababu hii inaprove kuwa tunatabia mbaya ya kuendekeza siasa kutawala maisha yetu na kutotumia resources zetu vizuri na ndo mana tunakuwa maskini kila siku. Na tusipoangalia tutakuwa maskini kwa fikra hizi hadi Mungu anakuja kuchukua ulimwengu wake.
 
Jamaa ana dharau za wazi kabisa na kujiona hakosei ktk mambo yake sijui akiwa mkuu wa nchi itakuwaje!!
? Na huko kujiona kwake hakosei kumekuathiri kivipi kama mtanzania na taifa lako kwa ujumla???
Haya tuseme dharau zake nazo zimekuathiri kivipi wewe kama mtanzania wa kawaida na taifa lako kwa ujumla???
 
Mkuu nakubaliana na wewe, ila kati ya hao uliowasikiliza, jee ulimsikia Mwigulu?!. Mimi nimewasiliza wote, Prof. Muhongo was real good tatizo lake ni kujitapa mno kuwa he is the only one!, uongozi ni team work, mtu anayejitapa kuwa he is the only one, anakuwa na tatizo la umimi, hivyo ndio the type watakaomake the worst dictators!.Tofauti kati ya Muhongo na Magufuli, wote can make the worst dictators this country has ever had, bali Magufuli kanyamaza, Muhongo kajitapa!.

January alijipanga vizuri na kuongea kwa ma poze ya kiobama obama ila sio realist, he was only paying lip services. Kama hukumsikiliza Mwigulu, tembelea hapa!.Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!.

Pasco

Ndugu yangu pasco mwigulu nilimsikiliza vizuri sana. Ni mzuri pia ila kuna kitu nimekiona hapa kwake. bado exposure yake ni ndogo sana ndo mana hata kutangaza kwake nia kulikuwa na elements za kuattack. Hicho ni kitu kibaya sana na kilimuangusha Mitt Romney mwaka 2012 alipojaribu kulitumia tukio la shambulizi la ubalozi wa marekani nchini Libya kuzicritisize sera za obama. lile lilikuwa kosa na wamarekani walimuadhibu.
Siku zote a smart politicians halaumu,anaonyesha njia. siku zote a smart politicians anaelezea uwezo wake na fikra zake kwenye kutackle challenges za watu. Sio kusema kwa sababu tu umekulia kimaskini basi utaweza kuziondoa shida za umaskini kwa watanzania.
Hapa anahitaji kumature kidogo.
kwa muhongo alikuwa anaongea facts na sio kujitapa. Alikuwa anasema kuwa ni kweli dunia ya sasa ni sayansi na teknolojia na yeye ndo anahizo njia za kutumia sayansi na teknolojia kututoa hapa. Alikuwa anaonyesha kuwa ni lazima kujenga uwezo wa uchumi na mambo mengine ndo yatafuata na akasema ni lazima ukitaka kujenga uchumi uwe na watafiti wengi na ili kuprove ilo ilibidi aonyeshe ni kwa jinsi gani alivo na iyo karama kwa kutoa statistics mbalimbali.
Nikwambie kitu PASCO, nchi hii tunapenda sana porojo,maneno maneno, uvivu na ushabiki na hayo yote tisa kumi kulalamika. Lazima tupate mtu in the top seat wa kubadirisha iyo mindset kwa watanzania na watu wa kubadirisha iyo mindset ni watu wa kuwaambia ukweli na kuwaonyesha kuwa muache maneno na mfanye ivi. bila hivi nakuhakikishia tutaishia kuwa masikini hadi mwisho wa dunia.
 
Katika watia nia wa ccm mpaka sasa profesa muhongo amefunika hilo halina swali, tatizo ccm ya mafisadi wanahitaji mtu kama muhongo? Jibu ni rahisi, hatakiwi. Wao wanataka vilaza kama kina lowassa na membe. Kuhusu January makamba, huyu mwizi wa mitihani galanos hadi akafutiwa mtihani wa taifa anaenda wapi? Halaf unavyosema apelekwe mambo ya nje ili akomae halaf aje atutawale, hivi wewe una akili timamu wewe? Umeona sisi watanzania ni mazezeta ya kutawaliwa na ccm dahari!!? Hapo ndo nimekudharau
Sipendagi kuongea vitu nisivo na uhakika navyo ndugu. Ndo mana hilo swala la January sikuamua kuliweka kwenye mada yangu
 
vipi kuhusu usiri wa mikataba? hasa wa gesi... vipi kuhusu majigambo ya elimu na kuja kutaja matokeo ya mbunge kwakuwa kakosoa wazo lakooo amkeni..
kuweka mikataba kuwa siri ni sera ya Muhongo???? Alafu mbona suala la mikataba lilishamalizwa na bunge??? au hauko updated ndugu????
Ni majigambo gani hayo aliyoyatoa na aliyatoa wakati gani???? au wakati anamjibu yule jamaa wa simanjiro???
Embu iweke kwa upande wako, wewe ni waziri na una uhakika unafanya mambo ya maslahi ya taifa na wananchi wake, inaibuka scandal bungeni na unajua hauhusiki na iyo scandal ila kuna syndicate tu imejipanga kutumia ushawishi wao kwenye bunge na media fulani kukuchafua tu na kukufanya uondoke kwenye nafasi yako uliyokuwa unaitumia kuwapigania watanzania, alafu mbunge mmoja anajaribu kukutolea maneno ya dharau na kashfa huku wewe unajua kuwa kumbe nae ni wa kuunga uunga tu. utafanyaje?????
 
Ndugu yangu pasco mwigulu nilimsikiliza vizuri sana. Ni mzuri pia ila kuna kitu nimekiona hapa kwake. bado exposure yake ni ndogo sana ndo mana hata kutangaza kwake nia kulikuwa na elements za kuattack. Hicho ni kitu kibaya sana na kilimuangusha Mitt Romney mwaka 2012 alipojaribu kulitumia tukio la shambulizi la ubalozi wa marekani nchini Libya kuzicritisize sera za obama. lile lilikuwa kosa na wamarekani walimuadhibu.
Siku zote a smart politicians halaumu,anaonyesha njia. siku zote a smart politicians anaelezea uwezo wake na fikra zake kwenye kutackle challenges za watu. Sio kusema kwa sababu tu umekulia kimaskini basi utaweza kuziondoa shida za umaskini kwa watanzania.
Hapa anahitaji kumature kidogo.
kwa muhongo alikuwa anaongea facts na sio kujitapa. Alikuwa anasema kuwa ni kweli dunia ya sasa ni sayansi na teknolojia na yeye ndo anahizo njia za kutumia sayansi na teknolojia kututoa hapa. Alikuwa anaonyesha kuwa ni lazima kujenga uwezo wa uchumi na mambo mengine ndo yatafuata na akasema ni lazima ukitaka kujenga uchumi uwe na watafiti wengi na ili kuprove ilo ilibidi aonyeshe ni kwa jinsi gani alivo na iyo karama kwa kutoa statistics mbalimbali.
Nikwambie kitu PASCO, nchi hii tunapenda sana porojo,maneno maneno, uvivu na ushabiki na hayo yote tisa kumi kulalamika. Lazima tupate mtu in the top seat wa kubadirisha iyo mindset kwa watanzania na watu wa kubadirisha iyo mindset ni watu wa kuwaambia ukweli na kuwaonyesha kuwa muache maneno na mfanye ivi. bila hivi nakuhakikishia tutaishia kuwa masikini hadi mwisho wa dunia.
Mkuu kiukweli kwa Prof. Muhongo, umeni convince, ila sidhani kama vikao vya CCM vitakuwa conviced, kwa sababu kwa siasa zetu, watu hawapendi facts bali tunapenda sana porojo, longo longo, maneno maneno, fitna, zengwe, hivyo mtu ukiwa mpiga domo mzuri, unakubalika zaidi kuliko best brains,truthfulness na facts!.

Ila pia Prof. Muhongo ni too arrogant!, watoa kura wa Tanzania wanajiona kumpigia kura mtu ni just a favour na sio right, hivyo katika kuombwa kura, wanataka wabembelezwe na kutongozwa kwa vihongo vidogo vidogo, na hata ikibidi bora wadanganywe kuliko kuambiwa ukweli!.

Hivyo sasa wishful choices zangu za the best president ni

  1. Prof. Mhongo.
  2. Dr. Magufuli
  3. Mwigulu Nchemba
Ila pia lazima tukubali tunaishi kwenye CCM era, reality ya CCM has never picked the best, but the most preferential candidate wa kuwaletea ushindi wa kishindo bado ni

  1. Edward Ngoyai Lowassa (Kupendwa na watu)
  2. Benard Membe (1st family choice)
  3. Makongoro Nyerere,(revival of Nyerere's legacy).
Tuendelee na safari ya uchambuzi!.

Pasco

[h=3][/h]
 
Nimekupata zaidi ya vizuri. ILA kwa mustakabali wa Tanzania nzuri tuitakayo huko mbeleni lazima tupige magoti na kusali Mungu awafungue macho na awape maono hata hao CCM. Tunaitaji kubadirika na kufika pale wote tunapotaka kufika. Ni MUNGU tu kwa maombi yetu sisi watanzania atakayewafanya CCM waamue kwa maslahi mapana ya Tanzania na Watanzania.
Pamoja sana ndugu.
 
Sasa hivi ni zamu ya Lowasa,hao wengine wasubiri muda wao ukifika tutawafikiria

Zamu kwani tuko kwenye foleni ya maji Hapa!!!!! Watanzania tujitahidi kuwa serious kwenye issues! Kwa mawazo madogo kama haya ni ndoto kupiga hatua ya maendeleo
 
Mtoa mada dont underestimate Magufuli. Huyu jamaa kama umemgundua si mtu wa porojo, ni vitendo tu. Amejizuia sana kutoa hotuba za mbwembwe. Lakini utendaji wake tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye baraza la mawaziri hakuna mtanzania atakayeusahau. Sina hakika na January lakini kama ikibidi wabaki wawili basi ni Muhongo na Magufuli. Udhaifu mkubwa wa Muhongo (ambapo anazidiwa na magufuli) ni kwamba Prof. hana uzoefu na chaguzi, hajawahi kugombea hata udiwani (maana ni mbunge wa kuteuliwa), sasa moja kwa moja kwenye urais, hii inaweza kuwa changamoto kwake.
 
Mkuu jamaa toka kaingia wizara ya nishati na madini nasikia Deni LA tanesco limeongezeka Sana.....
 
Mkuu jamaa toka kaingia wizara ya nishati na madini nasikia Deni LA tanesco limeongezeka Sana.....

Mkuu huyo aliyesema(aliyekwambia) deni limekuwa alikupa takwimu kabisa kuwa limekuwaje yaani kutoka sh.kadhaa hadi kadhaa? limekuwa kutokana na sababu gani? Na huko kukua kulitokana na kitu gani?????
Huitaji kuwa na akili sana au hata kwenda shule ili kuielewa siasa ya Tanzania ikoje.
 
Back
Top Bottom