Kwanza nakusikitikia....kama nilivyokueleza hapo mwanzo,Urais ni Taasisi, na sio mtu mmoja mmoja.
Naona unapenda sana kupata raisi kwa presentations....hilo sio sifa ya kujua ubora wa kiongozo.....tambua ukitaka rais wa namna hiyo....yupo mchagiaji humu alikupa mfano wa kuwa marais wa hivyo unaweza kuwapata 300 UDSM.
Unapokuja kwenye suala la Muhongo...unachozungumza wewe ni simulizi ulizozipata....kipi alichokifanya Muhongo
kinachokugusa moja kwamoja?? Hizi ni siasa.
Muhongo keshaonyesha udhaifu, kwenye sakata la escrow, na ndio maana kajiuzuru.
Makamba na familia yake hawawezi kusema loloye kwa kina Lowasa na Rostam na timu yao ya wapigaji....maana wamefadhiliwa familia nzima.
Tafuita kiongozi mwenye kuweza kutatua matatizo yaliyopo kwa sasa....kati ya hao uliowataja HAMNA.
Tunahitaji kiongozi atakaeweza kutatua tatizo kubwa tulilonalo watanzania nalo ni UFISADI...kati ya uliowataja HAMNA
Maana walikumbatiwa na mfumo uliopo, nao wataukumbatia hata wakitoka.
fikiri, acha ushabiki
Nimegundua tatizo lililopo hapa ni kuwa umeshindwa kunielewa ninachomaanisha ninaposema aina ya kiongozi wa juu ina determine ubora na uchapakazi wa timu inayomzunguka kama unavosema taasisi.
Ngoja nikupe mfano Kagame anapoteuaga mawaziri huwa wanaaandikiana mikataba kuwa wewe waziri utafanya haya na haya ndani ya mda fulani na huo mda unsapofika waziri anakaa nae na wanaangalia kila kitu kudetermine kama waziri amefanikisha yale aliyoahidi ndani ya mda husika. Hiyo inamaanisha nini?? Labda nikusaidie, inamaanisha kagame ana vision yake, na anapomteua waziri wanakubaliana kabisa kuwa ili tufike hapa ndani ya mda fulani fanya haya na haya na ni lazima u deliver usipodeliver basi anakuondoa. So hapa kiongozi kama kagame ameleta impact kwenye system yake nzima.
Soma vizuri mada kuu kwa nini nimewasifia January na Muhongo??? Sio kwa presentations zao tu ila ni kwa kuweza kuonyesha ni wapi kama nchi tumekuwa na tatizo na kwa kuonyesha vizuri kabisa wana mikakati gani na watafanyae ili kufika hapo.
Sikuishia hapo tu nimeenda mbali zaidi kwa kuonyesha wapi naona prof amemzidi January na nimesema January afanye nini ili kuweza kuuthibitishia umma wa watanzania.
Labda nikusaidie ndugu yangu tuseme hujui Muhongo kafanya nini????? Au ndo lile tatizo alilosema la uvivu kwenye jamii yetu linakusumbua??? sasa basi nenda kaulize takwimu za usambazaji umeme vijijini na maeneo mengine zilikuwaje tangu tupate uhuru na kabla muhongo hajaingia wizara ya nishati na madini,alafu uliza zimepanda kiasi gani kwa kipindi cha miaka miwili tu aliyokaaa pale???
Kingine ndugu unajua kuwa ameweka mikakati na kuitekeleza ya kuwapeleka vijana wa taifa lako nje ya nchi kusomea mambo ya gesi na mafuta na kwa sasa inasemekana wapo zaidi ya 100 ili kulifanya tu taifa lako lije kuwa na wataalamu wa hii sekta kwa ajili ya kuusimamia huu uchumi wa hii sekta huko mbeleni??? sasa hayo kayafanya ndani ya miaka miwili tu aliyokaa kwenye system unataka afanyaje tena?????
Umeongelea kuhusu tatizo la ufisadi nakuomba tu ndugu yangu uliza tanesco alifanyaje au kama ukishindwa kamuulize wakili fulani anaitwa mguu aliyegeuza tanesco kitega uchumi chake. Au ukishindwa hapo kamuulize jamaa fulani ivi alitaka vitalu vya bure akafanya udalali.
Unasema kuwa alionyesha udhaifu kwenye sakata la escrow labda useme ni upi huo kwa ushahidi upi na ripoti ipi ambao hata leo tunaweza kumshtaki kwa uzembe na kuliingizia hasara taifa????
Ndugu yangu nikuambie kitu dunia ya sasa sio ya bla bla ni ya facts, watu wanaenda na facts siku izi ndo mana hata juzi umeona fbi waliamua kuingia field kuanza kuthibitisha kuwa fifa kuna rushwa kwa sbabu wenzetu wazungu wanatuzidi hapo,wao wanaenda na facts na sio bla bla, sasa wewe unasema rostamu anafadhili familia ya January bila kuweka ushahidi. unatakiwa uweke ushahidi hapa na sio wa kutunga ili watu wakuelewe na sio kuongea tu.