Uchaguzi 2020 CCM acheni kujipa Moyo, CHADEMA walijiandaa na Uchaguzi muda mrefu. Siri hii hapa...

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
211
1,000
Kwa hakika ni WanaCCM wachache sana wanaojua kuwa CHADEMA NI MSINGI lilikua ni zoezi operation ya chama nchi nzima na lilikua na lango la kuhakiki wanachama wake nchi nzima ngazi zote kuanzia msingi, matawi hadi taifa. Zoezi hili lilifanikiwa 100%. CCM wengi hasa viongozi wake hawakujua lolote kuhusu hili na wala hawakujua kuwa hii operation iliongeza wanachama wengi na records za kila mkoa zipo.

CHADEMA kinasema kuwa kitashinda kwa sababu kupitia operation ya CHADEMA ni Msingi ilifanikiwa kwa 100% na hawa walioandikishwa wote kupitia zoezi hili ni wapiga kura wenye vitambulisho waliojiandikisha na wachache tu ambao hawakujisndikisha viongozi wa chama waliwafuatilia na kuhakikisha walijiandikisha.

CCM walikua bize kununua viongozi wachache hawakulijua hili. Hawa walioandikishwa kupitia CHADEMA ni msingi pekee wanatosha kuipa ushindi wa kura za urais achilia mbali mbali wagombea ubunge na udiwani.

Hii ndiyo faida ya kua na Chama ambacho viongozi wake ni wanamikakati na ni wasomi wabobevu. Naweza kusema hili watu wakachukulia mzaha lakini huu ndiyo ukweli.

Kazi iliyobaki ni CHADEMA kuongeza kura kutoka kwa wanachama wa CCM na wasiokua na chama kutoka majukwaa ambayo nayo mgombea Urais na makamu wake wanayamudu 100%.
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
11,465
2,000
2810
Tukutane hapahapa kupongezana na kupeana pole
Tanzania kwanza
Maendeleo hayana vyama
 

SOLOMO

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
258
225
Piga spana kwa Wasaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
hapo kwenye maneno "sisi watanzania" ondoa na weka maneno "mimi mtanzania"! ukifanya hivyo, utakuwa umeilinda heshima yako!
 

mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,308
2,000
Oct30 msikimbie tukutane hapa jukwaani kujadiri yakiyojiri baada ya uchaguzi
 

omegas

Senior Member
Jun 3, 2018
112
250
Wewe ni mwongo mkubwa chadema wamejiandaa wapi?? Kwetu hawana hata kiongozi mmoja na makao makuu ya mkoa sasa hayo mashina na matawi yako wapi? Tengenenzeni plopoganda zenu lakini ukweli utabaki kuwa ccm hakijapata upinzani wa dhati
 

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,895
2,000
Hiki chama kinaendeshwa kisayansi sana. Wamefanya kazi kubwa sana chini ya kapeti na kama kweli wana blue print ya wanachama wao basi uchaguzi huu ni wa moto sana.

Mungu Ibariki hii nchi iwe na uchaguzi wa amani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom