CCJ waibukia kwa Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ waibukia kwa Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Mar 19, 2010.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Jamii (CCJ), Richard Kiyabo (kulia), akiangua kilio baada ya yeye na Katibu Mkuu wake, Renatus Muabhi, kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la hayati Baba wa Taifa, Mwalimu JK. Nyerere, Butiama mkoani Mara jana.


  *Wabubujikwa machozi kaburini kwake
  *Wahutubia hadhara, kadi kama njugu


  Viongozi hao walikutana na mkuu wa familia hiyo, Chifu wa Wazanaki, Japhet Wanzagi na mmoja wa watoto wa Mwalimu, Madaraka Nyerere.

  Viongozi wa CCJ waliotembelea familia hiyo ni Mwenyekiti, Richard Kyabo na Katibu Mkuu, Renatus Muabhi.


  Mbali na Chifu Wanzagi na Madaraka, mazungumzo hayo pia yaliwahusisha wazee mashuhuri wa kijiji cha Butiama.


  Katika mazungumzo hayo, Chifu Wanzagi alionekana kutoridishwa na jinsi sera ya ubinafsishaji ilivyoshindwa kuwaondoa Watanzania katika dimbwi kubwa la umaskini.


  Alisema kuwa ubinafsishaji huo ungefanyika wakati wa Mwalimu Nyerere, asingevumilia hali hiyo.


  Chifu Wanzagi alisema ingawa yeye ni mwana-CCM damu ambaye hawezi kukihama chama hicho kikongwe, lakini sera ya ubinafsishaji imeshindwa kabisa kuwasadia Watanzania kuondoka katika umaskini.


  "Mimi ni mwa-CCM, lakini kwa kweli sijui leo Mwalimu (Baba wa Taifa) angekuwepo angesema nini. Haiwezekani nchi ikatoa madini kwa watu wa nje, tena kwa bei poa huku wananchi wanaozunguka migodi hiyo wakikabiliwa na umaskini mkubwa, jambo hili linatusikitisha sana," alisema Wanzagi, ambaye pia ni msemaji wa familia hiyo.


  Alipongeza uanzishwaji wa chama hicho kwa kutambua kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuchagua kujiunga na chama chochote cha siasa chenye lengo la kuleta mabadiliko katika nchi bila kuathiri umoja wa kitaifa.


  Naye Madaraka alisema Butiama ni eneo la kila Mtanzania kwa kuwa ndipo alipozikwa Baba wa Taifa, hivyo kila mtu au chama cha siasa kina haki ya kufika na kutoa heshima katika kaburi la kiongozi huyo.


  "Butiama ni ya Watanzania wote, hivyo kila chama au mtu ana haki ya kufika kwa lengo la kuona kazi mbalimbali zilizofanywa na Baba wa Taifa wakati wa uhai wake, ambazo zimehifadhiwa katika makumbusho yake na kuona sehemu alipozikwa," alisema na kuongeza:


  "Tena bila ya ubaguzi wowote, kama mwenyewe alivyokuwa akituasa Watanzania leo na kesho kuwa wamoja na kabila lao ni Tanzania."


  Kyabo alisisitiza kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuhakikisha kinaenzi mema yote yalipiganiwa na Baba wa Taifa kwa maslahi ya Watanzania wote ingawa sasa yameonekana kusaulika.


  Alisema ndani ya CCJ, rushwa na ufisadi ni ajenda ya kwanza ambayo itasimamiwa kikamilifu.


  Alisema vitendo hivyo vilionekana wazi kumkera Baba wa Taifa kutokana na kusababisha kuwepo kwa baadhi ya watu wachache wanaonufaika na rasilimali za nchi huku idadi kubwa ya Watanzania ikiwa katika lindi kubwa la umasikini.


  "Leo tumekuja kuona mahali alipompumzishwa mwasisi wa Taifa la Tanzania ikiwa ni uzinduzi wa safari yetu ya nchi nzima kuelezea misingi yote iliyowekwa na Baba wa Taifa kwa nchi hii kwani CCJ inathamini kwa dhati michango hiyo, hiyo ndio sababu tumekuja kuwaeleza kuwa Mwalimu tutamtumia kila kona ya nchi yetu," alisema mwenyekiti Kyabo.


  Naye Muabhi alisema kushamiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi kunatokana na maamuzi ya viongozi wa CCM kukiuka misingi mizuri iliyoasisiwa na Baba wa Taifa kwa kuanzisha Azimio la Arusha ambalo walidiriki kuliua ili kupata mwanya wa kujineemesha.


  "Narudia kuwajulisha kuwa CCJ tunathamini sana misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa katika uongozi wa nchi hii, ndio maana tutatumia nguvu zetu zote kuirejesha kupitia CCJ baada ya wao kuua Azimia la Arusha, baada ya kubaini linawaumbua," alisema.


  Hata hivyo, viongozi hao walionekana kububujikwa machozi wakati wakiweka mashada ya maua katika kaburi la Hayati Mwalimu Nyerere, hali ambayo iliamsha simanzi kubwa kwa baadhi ya wananchi na wazee wa kijiji cha Butiama waliofika kuonana na viongozi hao.


  Baadaye viongozi hao walifanya mkutano wa faragha ndani ya nyumba ya Baba wa Taifa kati yao na Madaraka na Chifu Wanzagi. Hata hivyo, baada ya kukutana, wote walikataa kueleza kilichozungumzwa kwa zaidi ya nusu saa.Baada ya kutoa kijijini Butiama, viongozi hao wa CCJ walikwenda katika mtaa wa Bugharanjabho, Kata ya Buhare katika Manispaa ya Musoma na kutoa pole kwa familia tatu zilizokumbwa na mauji ya ndugu zao 17 waliouawa kikatili kwa kukatwa mapanga usiku wa Februari 16, mwaka huu.


  Na katika hatua nyingine, umati wa wakazi wa mjini hapa na vitongoji vyake, jana walijitokeza kununua kadi za CCJ wakati wa mkutano wa uzinduzi wa chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.


  Mkutano huo uliohutubiwa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya vijana, wafanyabishara na baadhi ya wananchi wa kawaida.


  Wananchi walikuwa wakiimba kuwa sasa ni wakati wa ukombozi kutokana na kujinasua kutoka katika makucha ya wakoloni.


  Aidha, katika mkutano huo, wananchi hao walimchagua Mwenyekiti wa muda wa CCJ mkoani Mara, Sospiter Manumbu, ambaye atasimamia shughuli zote za chama hicho ikiwemo kutafuta ofisi rasmi ya mkoa na kufungua ofisi za wilaya mkoani Mara.


  Licha ya mkutano huo kumalizika saa 12:00 jioni, bado kulikuwa na mamia ya wananchi waliokuwa wamefoleni katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo wakisubiri kununua kadi za chama hicho kipya.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Ni hatua nzuri,tukubaliane.Jukumu la kujenga upinzani wenye nguvu Tanzania ni letu sote.Vyama vingine vya upinbzani viangalie sera zao na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kupigania ukombozi wa kweli
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  huruma za mamba!!!!
   
 4. T

  The_Analyst JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 214
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Duh Hawa jamaaa wapo nyuma kweli.......... Yani ndo wanagundua hilo leo au ndo publicity??? :((
   
 5. P

  Pepe Rainer Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vyama kuonganisha nguvu ni ndoto ila wananchi ndio waonganishe nguvu na kuunga mkono chama wanachoona kitawasaidia na kuepuka kugawa kura na kufanya viongozi wasiofaa kuendelea kuongoza
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hapa ndio napataga hasira au kisirani.... sasa wanalia nini? wameshalia kwa siku ngapi sasa? ni huruma za namba au vipi???

  Kiongozi ni jemedari, na yeye akianza kulialia sijui tutafika wapi??

  wakumbuke kupata kura ni zaidi ya kuhiji butiama na kulialia, they need to show us what they have got!!!

  +_)(*&^%$#$%^&*()
   
 7. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Binadamu wote tumeumbwa na feeling na tuna emotion hiv yo tuna react hajalishi wewe ni kamanda au ni infantry. Na wakipata hasira zitawajengea feeling ya kuwafanay wawe na uchungu na kuwa focused zaidi. Mimi nadhani ni jambo zuri kuwa wameenda kujazwa hasira Butiama. Hakuna aliyepata picha ya mkutano wao wa hadhara???
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sawa bana, ila kwangu huu ni usanii tu!!! i am tired with everybody using siasa kama platform ya kuendeleza watu, lakini wanatumia emotions badala ya strategies kutuonyesha watatuongozaje!!!

  Jiulize hao watu kabla ya kuwa CCJ walikuwa wapi? what have they done hata kwa kata zao tu? crying is not a solution, sanasana ni state ya mind ambayo inaonyesha umeshindwa kupata stable solution au a balanced state of emotion ndio mtu unaamua kunyesha mvua ya machozi as a way body inarelease hizo tensions na emotions

  sikumbuki kusikia nyerere alienda makaburi ya akina mamngungo, kinjeketile, isike, mkwawa na kuanza kulialia pale

  sorry that is my stand
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kulitembelea kaburi ni one thing but kulia? A decade after the man has died? Sasa na familia yake ifanyeje? Huu ni unafiki!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndugu yangu.. hii naona ndio cheap popularity, kutembelea butiama na kaburi safi sana, sasa haya machozi sijui ndio yatafuta madeni na kuondoa ufisadi??

  Nakumbuka pinda alilia na kushangaa lakini that hasnt changed anything kwenye matumizi ya serikali
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu you are exactly right. it's nothing but cheap publicity. If I was present I would have called them out. Wanaanza kuonyesha kuwa na wao ni politics as usual. Badala ya kutumia this early stage of their party kutangaza sera zao na kuattarct wanachama watakao kuwa ndiyo resource kuu ya chama wao wanaenda kumlilia mfu.

  It reminds of the the Bible(sorry kama mwenzangu si Mkristo) when Jesus was being tortured. Wanawake walipo anza kumlilia akageuka na kusema, "Msinililie mimi bali lilieni nafsi zenu na za watoto zenu." Sasa hao badala ya kulilia taifa ambalo ndiyo urithi kwa watoto wao wanamlilie Nyerere mh!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu yani siasa za tanzania zinabore sana... CCJ walianza kama "something good" lakini naona sasa wamekuwa kama vile vyama vyetu vya ruzuku na per diem!!
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Swali la kizushi CCJ wana website yao?

  Na wameainisha ILANI yao humo kwa website? Na mikakati mingine katika kuwakomboa watanzania katika hali ya kisiasa tuliyo nayo na kuja na mfumo mpya wa kizalendo zaidi na kimaendeleo?

  Kwa kipindi hiiki tulicho nacho nadhani ni bora pia watumie internet kujinadi kwa kasi kubwa tena isipunguwe iwe 240 per Hr nchi nzima, Ni wazo langu kwao pia

   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ngekewa, give yourself some psychological food for now but one day "THE TRUTH WILL SET YOU FREE"
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Hiki chama cha Lowassa hakiwezi kutusaidia lolote wa-Tanzania, wanaenda kulia nini wakati wao wametumwa tu na mafisadi! Hili taifa bwana usanii mpaka kwenye makaburi ya wenzenu!

  Respect.


  FMEs!
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Mar 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wanawazimu....Baraka za Nyerere haziombwi hivyo.
   
 17. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ya kulialia ni usanii... sikuhizi watu wameshtuka hawaibiwi kienyeji namna hiyo. Nyie CCJ hebu nendeni mkabuni mbinu nyingine... hii tumewashtukia!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tatizo mwanafalsafa..unazungumza kama unajua kilichowaliza ni nini. Unaona watu wanalia kwenye kabuli unafikiri wanamlilia Nyerere! Hawa nimeanza kuwapenda kwani they are doing all the good things I would have done kama ningeanzisha chama.. Wanajua wanachokitaka, wanafalsafa inayowaongoza na kinyume na wengi wanavyofikiria hawahitaji kigogo kuwa nyuma yao! Ni ajenda inayoelewekak na ambayo wanajua itawavutia Watanzania.

  Uongozi ni uwezo mara zote siyo ahadi, siyo kutoa misaada, siyo cheap popularity ni kuweza kuchukua msimamo na watu wakajua msimamo huo. CCJ (SisiJUU).. ni chama ambacho kinafuata hatua zote muhimu za kuongoza mapambano ya kifikra kwenye sanduku la kura..

  Nakumbuka kisa cha kuteuliwa kwa Daudi kuwa Mfalme... Alipoenda Nabii Samwel kwenda kuwapaka mafuta watoto wa Yesse. Wakaletwa watoto saba wa kiume (vyama vilivyokomaa na vyenye uzoefu na majina makubwa).. Hadi alipokuwa tayari kumpaka mmoja wao mafuta BWANA akamwambia siyo "HUYU". Kila mmoja aliamini kabisa mfalme atakuwa ni mmoja wa hawa wazoefu na wanaosifiwa kijijini..

  Hadi pale Samweli akashangaa mwishoa akamuuliza Yesse "Yesse watoto wako wote ni hawa". Ndipo Yesse kiuvivu akasema "yeah kapo kamoja kanachunga ng'ombe huko sidhani kama hako kanaweza kuwa kafalme". Samweli akamwambie "mlete".

  Sasa.. tunaweza kucount watu out kwa sababu they don't fit in our own concept ya nani anaweza kutuongoza. Tunawapima na kuwaangalia majina yao wanajulikana vipi na kwa namna gani na wasiporidhisha tunasema hawa haiwezekani. Tungependa sana atakayetuongoza awe kutoka kwa wale Saba!!

  Well.. friends.. Here comes David!
   
 19. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji you are impossible! Kila ukichangia wengine hukosa cha kuandika maana yote unakuwa umeyasema.

  Chama hiki mie nimekipenda sana hata kabla hakijapata usajili wa kudumu. Ninachoweza kusema ni kwamba ninaona hawa waanzilishi wa chama hiki wanaipenda sana nchi yao. Wameona nchi inakwenda mrama na wao wameamua kujitokeza kujaribu, na bila shaka wanaweza kufanikiwa kuirudisha nchi pale inapostahili.

  Nakubaliana nawe kabisa kwamba hawa ndugu zetu hawamlilii Nyerere pale wanaililia Tanzania yetu! Wanalia, na bila shaka kimoyomoyo wanatoa madukuduku yao mbele ya kaburi la Mwalimu kana kwamba wanamuomba Mungu awasaidie na Mwalimu huko aliko awe nao katika safari ndefu na kazi ngumu ya kujaribu kulikomboa Taifa lililopotoka!

  Iko wapi heshima ya Tanzania ndani na nje ya nchi? Imetoweka! Leo hii mjumbe wa Tanzania kwenye mikutano ya Kimataifa akisimama kuongea nani anastuka na kutaka kusikiliza Tanzania inasema nini? Ndio kwanza wajumbe wanapata nafasi ya kutoka kwenda kunywa kahawa badala ya kuvuta sigara! Tanzania hivi sasa imekuwa ni dampo la bidhaa feki, eti ndio kwenda na wakati wa soko huria. Tumevitelekeza viwanda vyetu, tunacheza mdundiko na Wawekezaji wanaotuibia mali zetu. Iko wapi Tanzania yetu ambayo sote tulikuwa ni ndugu moja. Leo kuna matabaka. Mjukuu wangu mie ninayeishi Kitunda hawezi katu kupata mchumba kutoka Mbezi Beach maana wenzetu wale ni matawi ya juu na huku kwetu ni walalahoi wauza mayai! Wenzetu wamefikaje matawi ya juu, hakuna anayeuliza.

  Hawa viongozi wa CCJ wanalia kwa mengi jamani, tusiwabeze wala kuwapuuza!

  Sijui ni wewe Mzee au ni nani aliyesema kwamba si lazima kusimama jukwaani kuanza kujinadi ama kunadi sera. Naamini kwamba CCJ wanapata wafuasi kutokana na mawasiliano na wananchi kwa remote control – mawasiliano ya hisia zilizomo ndani ya mioyo ya wale ambao wanaona Tanzania inahitaji kukombolewa. Yeah, (SisiJUU)!
   
 20. K

  Kilian Senior Member

  #20
  Mar 20, 2010
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mzee mwanakijiji, tupo pamoja kabisa.
  Si busara kuanza kuwabeza hawa vingozi bila kujua exactly what is in their minds. Ati tu kwakuwa tulishachoshwa na wote waliopita na ahadi zao za uwongo, tunatoa hitimisho kwamba kila anayekuja ni yuleyule. Tuwape muda, si kwakuwaangalia na kuwabeza tu bali tuwasaidie kufikia lengo la ukombozi wa mtanzania, ambalo naona diyo angenda yoa kubwa.
  Tukiogopa kuwajaribu kwakuwapa nafasi naushirikiano ati tu kwasababu hawana majina makubwa, kamwe hatutapata nafasi ya kujua potentialities walizo nazo.
  Tusiwe waoga wakuanza.
   
Loading...