CCJ ni mradi wa CCM

CCJ ni mradi wa CCM

Ramos

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2010
Posts
498
Reaction score
132
WanaJF mna maoni yeyote kuhusu hili?
Najaribu kujenga conclusion kuwa CCJ ni mradi wa CCM.

Najua kuwa CCM inafanya kila jitihada kuhakikisha haiondoki madarakani. Mojawapo wa mbinu wanazotumia ni 'wagawe uwatawale'. CCM wanajua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaokipinga chama chao hali inayohatarisha future yao katika siasa. yapo maeneo yanayoibukia kwa kasi katika kustawi kwa siasa za upinzani, moja wapo ikiwa kanda ya ziwa victoria. Kwa kuona na kutambua hatari hii inaonekana kundi moja la CCM (huwa naamini CCM ina makundi ma3) limeamua kuanzisha chama kitakachogawa nguvu ya upinzani nchini (hasa ya CHADEMA) kuhakikisha kuwa hakutakuwa na chama kitakachojenga nguvu ya kutisha.

Kama ni mfuatiliaji wa mambo ya CCJ utagundua kuwa chama hiki kimejijengea umaarufu mkubwa maeneo ya kada ya ziwa. Na pia utagundua kuwa huku ndiko CHADEMA kwa miaka ya karibuni imeanza kujizolea umaarufu na ukubaliwaji mkubwa.

Naamini CCJ kinaanzishwa katika mazingira ya ku-confuse akili za watanzania wapenda mabadiliko ambao wengi walishaanza kukifikiria CHADEMA kama chama muafaka ambacho kikiendelea kujipanga vizuri kitakuwa na uwezo wa kuchukua madaraka.

Nisiandike sana lakini pamoja na ushahidi mwangine wa kimazingira kama muda kilipoanzishwa, watu waliokianzisha na maeneo kinapojizatiti inatoa alarm kabisa kuwa CCJ ni chama mradi cha CCM...
 
WanaJF mna maoni yeyote kuhusu hili?
Najaribu kujenga conclusion kuwa CCJ ni mradi wa CCM.

Ndugu, mara nyingi hoja haijengwi kwa kuanza na hitimisho. Kwa kawaida tunaanza na utangulizi (intro/background) ambayo hueleza hali halisi, halafu hufuatiwa na smukumo , kwa nini unaamini yale unayotaka kuyaandika (rationale) n.k. Sasa unaporukia tu conclusion, inakuwa vigumu kuona kuwa huna lako jambo.

Ila kwa wakati huu watakuja na mengi kuwa huyu na wa yule na yule ni wa fulani. Kwa vyovyote kugawa ccm kujigawa haiwezi kuwa nafuu yake hata siku moja. Nafuu ni kufuata haki kwa wote na kurudisha sauti kwa umma, kitu ambacho hawawezi kwa kuwa tayari washakaliwa na walafi walao bila kunawa, na haka kapepo ka kutaka kuitawala nchi kifamilia. Walidhani wangeweza kutawala kwa miaka 100, ijayo ila sasa wanapata hofu kuwa hata miaka 5 tu, ishu ni nzito.

Sijui kama hayatatokea ya Thai, manake haya maguvu ya kuzuia hata kuandikishwa kwa vyama vilivyotimiza taratibu za kisheria, hayatoi picha nzuri huko tuendako.
 
hapana CCJ inafanya mambo kwa timing.. si unaona hatukutaka kumjibu Tendwa hadi hivi sasa. Basi matumbo yanawauma kwa sababu wamezoea vyama vingine kuwahi kutoa majibu.. sasa ule ukimya na jinsi ambavyo magazeti karibu yote ya leo yametoa habari ya CCJ "kutafakari" kauli za tendwa kinawasumbua.

Kesho nitadokeza...
 
hapana CCJ inafanya mambo kwa timing.. si unaona hatukutaka kumjibu Tendwa hadi hivi sasa. Basi matumbo yanawauma kwa sababu wamezoea vyama vingine kuwahi kutoa majibu.. sasa ule ukimya na jinsi ambavyo magazeti karibu yote ya leo yametoa habari ya CCJ "kutafakari" kauli za tendwa kinawasumbua.

Kesho nitadokeza...

Mhhhhh!
 
Kuna habari nimezipata sasa hivi hadi nasikia raha..

Duh! Mzee MM style yako ya "Nyeluuunyeluuuu" wakati mwingine huwa inafanya watu wawe na shauku kwelikweli, najua unaweza ianzishia thread mwaga nyuki mkuu. au na hii unaiwekea count down
 
ccm haitabiriki...na hata huyo mbunge aliyeingia inawezekana katumwa...alitumwa naibu waziri mkuu mzima ....aliyekuwa na uwezo wa kushinda urais[inasadikika alishinda] itakuwa mbunge????

mimi nitaamini upinzani utakaokuja na watu wapya kabisa ambao hawajawahi kuwa serikalini..kama vile kina nyerere walipokomboa nchi hawakuwa wamepata kuwa serikalini .......na kuna watu wengi tu hawajapata kuwa ccm wataweza kubadili mambo....kama ni kuchukua walio ccm wanaweza kuwakaribisha kwa utashi na sio hawa wa kujileta!!
 
Siamini kwamba CCj ni mradi wa CCM wala siamini kwamba CCJ ni tishio kwa CCM! Naweza kubashiri kuwa CCJ si CCJ!
 
ok... ndio maana hawataki kukipa usajili wa kudumu na kukupiga vita tangu mwanzo. Ufalme uliogawanyika wenyewe waweza vipi kusimama?
CCM ni wajanja sana wanapima upepo wakiona kitawasaidia watakipa wakiona vipi watakinyima kwa sababu ni chao.
 
Back
Top Bottom