Nilipoiona CCJ mwanzo, niliudharau na kuiona its a hoax, comming to put just another junk on the game ambalo tayari limeshajaa junks!. Alipoingia Mpendazoe, nikajua amekurupuka na kuhama CCM kwa jazba, nilipomsoma Mzee Mwanakijiji, ndipo nikapata shauku ya kweli kuanza kuiamini CCJ might be something realy, something serious and for realy war, japo mpaka sasa sijabahatika kujua ukweli wa who is who is a really CCJ, wanaambiana, wanaitana, na wanajiunga, huku wengine tukishawishiwa kwa ushawishi kuwa CCJ sasa ndio chama mbadala.
Tusiilaumu bure CCJ, kuna uwezekano Tendwa amewashtukiza (surprise check) hivyo walikuwa hawajajiandaa kama walivyo puliza baragumu, ila kama wakipata muda wa kujiandaa vizuri, they'll put their house in order kabla mgeni hajafika.
Lakini pia tusirule out uwezekano wa hii CCJ inayokaguliwa ndio CCJ halisi, achilia mbali CCJ ya kwenye ma Press Conference na wasemaji wake kibao. Kama hii inayoibuka ndio CCJ kweli na halisi, then I was not wrong. CCJ is a hoax!.
Mkuu Ndibalema,
ushahidi unao utaka hapa hutaukuta, wala usitegemee kuuona openly kama unvyotaka kuuona.
Kitu ninachoweza kukupa, labda ni kukumbusha kuwa sisiemu ndiyo iloshika serikali hivyo imemeza taasisi nyingi sana, ikiwa jeshi lapolisi, mahakama n.k vimeshikwa na serikali ya sisiemu; vipi kwa Tendwa?
Kwa macho ya nyama na masikio huwezi kuuona uchafu wa hiki chama, ni mpaka uruhusu fikra zako kuchungulia ndani zaidi, Bunge tu halina ubavu kwa sisiemu, tume za uchaguzi tu hazina ubavu kwa sisiemu awe Tendwa?
Usishangae akawa ana represent kile kilichoaandaliwa na sisiemu kwa manufaa yake, ila ushahidi unaotakuona hapa, mimi nina hakika huwezi kuupata kwa mtazamo wako.
WanaJF hapa msipate tabu CCM ni MAFIA wamewapa hela member wa CCJ ili wasitikee kwenye uhakiki, sasa mtu akipewa kama 200,000 unafikiri atakuja???
Bila shaka uko mkono wa CCM. Pengine tatizo ni kwamba CCJ ilivyokuwa launched ilitangazwa sana na kuonekana tishio (iwapo hili ni sahihi au la) kwa CCM. Nandiyo maana Msajili aliagizwa kukihakiki kwa kutumia darubini kali.
Mimi sidhani iwapo chama hicho kingeomba usajili kikawaioda tu kama vile vyama vingine uchwara -- ingepata bila kusita. Tusisahau mwaka 1994 wakati CUF ilipogomea kushiriki uchaguzi mdogo katika jimbo la Kwahani kulikuwa hakuna chama kingine kilichokubali kushiriki dhidi ya CCM, ambayo ilihofu mbele ya jamii la kimataifa kwamba nadharia nzima ya serikali yake kuanzisha kwa demokrasia ya vyama vingi ilikuwa mashakani katika zoezi la kwanza tu la demokrasia hiyo.
Inasikitisha kuona hawa CCJ wameshindwa kuorodhesha na kuhakiki wanachama wao 200 kwa Dar tu, ilhali ni wao ndio wamemladhimisha Tendwa aje kuwahakiki wako tayari na wanachama 2,000 Dar, acoording to their chairman. Sasa hapa mwenyekiti wao analalamika Tendwa hawezi kazi ilhali wanachama wao feki na real hawafiki hata 150 hapo mkutanoni. Na hata yeye na katibu wake hawana kadi!
Huu ni uzembe wa hali ya juu, period.
Kuna mtu awali alilinganisha na chama cha chemponda in 1994, sasa kweli wakati ule ccm ilikuwa inajaribu kulazimisha vyama vingi na kufungia macho those things, we are in 2010 tunataka responsible upinzani ambao wataweza kuorganise na kutetea jamii yenye watu takriban 40 million, sasa kama hata kuorganise watu 200 inakuwa taabu, jee siasa za kitaifa wataweza kweli?
Na sioni namna ccm inahusika na uanachama batili, ccj iombe ushauri cuf jinsi ya kuorodhesha wanachama na kuhakiki, wana uzoefu mkubwa hasa visiwani.
CCJ watoe kwanza kibanzi katika jicho lao kabla ya kuonesha boriti iliyokatika jicho la CCM!
Mimi hapa sioni mantiki ya CCJ kulalamikia Mkono wa CCM kwenye zoezi hili, ni wazi hakuna ushahidi na wala maelezo yao hayawezi kukidhi haja ya mtu mwenye kufikiri sawasawa, kuvurugika kwa lile zoezi CCJ have themselves to blame, there is no need of CCJ to start witch hunting in CCm or somewhereelse, the witch they are looking for is inside their part! Ni uzembe wao wenyewe, kama walishajua kuwa kuna mbinu chafu toka mwanzo si wangejiridhisha wenyewe kwanza kuwa kilakitu kiko sawa kabla ya kumuita Tendwa!
Ni upuuzi kwa CCJ kuendelea kuinyooshea kidole CCM kwa makosa yao wenyewe, mimi nahis CCJ wants to seek for public sympath by pointing a finger to CCM! Jamani not all evil doings are devils acts, some of them are from our own feelings and desire! Siipendi CCM, sio shabiki wa CCM, lakini kwa hili hapana!
Nasikia leo Mkoa wa Pwani! Duh wasipokuwa makini kwa kweli watapata tabu sana kusajiliwa
Walikuwa wanahangaika na kujibu matamko ya kwenye vyombo vya habari kwanza. Wekeni CVs za hawa viongozi wa muda wa CCJ. Mimi naona tatizo linaanzia kwa hawa.Wanababaika, wanahamanika, hawajiamini, hawazijui siasa za bongo, wanajifunzia UONGOZI hapa, sasa hivi.
...
Tungepata mtu wa CCJ atuthibitishie kuwa hili la majina feki ni kweli hujuma za CCM na Tendwa mwenyewe kutotaka wasishiriki uchaguzi mkuu ingekaa vizuri zaidi.
...
Mie kwenye Jambo au swala CCJ nalikalia mbali maana mh naiogopa siamini kama chama kilicho serious anyway ni mtazamo wangu tu
Ngoja kwanza Mwanakijiji amalizie usingizi, akiamka anaweza kusema kama ni hujuma au hawakujipanga!
Nadhani tatizo ni CCJ kwa kiasi kikubwa......
Majina ya kuhakikishwa huletwa na Chama chenyewe. Sasa hata huyo mwenyekiti wa CCJ hakuwa na kadi ili ahakikiwe anasema eti alipoteza wakati amenigwa pale Kariakoo (angeweza kuchukua kadi nyingine kwa mujibu wa taratibu za chama chao kwa kadi zinazopotea madhali alitoa taarifa polisi). Huyo Katibu Mkuu wao pia hakuweza kuhakikiwa. Hata wangehakiki watu wote pale Mwembe Yanga bado wasingefika 200! Huoni kuwa tatizo ni CCJ?
Kitu kimoja katika siasa za Tanzania, unapokuwa mpinzani unapaswa kuwa makini sana sana. CCJ wlaikwenda kuzindua chama MwembeYanga. Mpendazoe alikwenda kuchukulia kadi mwembe yanga. MwembeYanga ni TEMEKE na Temeke eneo la CUF. Kwa vyovyote vile kama CCJ hawakushirikiana na CUF (na ninaamini hivyo maana walijiona wao ndio wakombozi na kazi nyingine iliyofanywa na vyama vya upinzani toka mwaka 1992 ni bure) basi CUF ilipandikiza watu katika uanachama na ndio hayo yamewakuta. Hiyo ni Dar mtaona kwingine.
I have an experience with this. Mwaka 2007 CHADEMA tuliweka Mgombea Ubunge katika Jimbo la Tunduru baada ya Akukweti kufariki. Tunduru ni CUF strong hold lakini CHADEMA 'tuliamini' kuwa tunaweza kufanya mabadiliko. CUF walilalamika sana na hatukuwasikiliza. Wakaweka mtego. Kila kata tuliyokwenda wanachama wa CUF ndio walitupokea, wakachukua kadi za CHADEMA na kuunda uongozi na timu za kampeni. Tukafanya kampeni kabambe kabisa with a modern information system (ambayo pia tulitumia Tarime na chaguzi nyingine zote na hivyo kuwa chama cha kwanza kupata matokeo mapema kama tunashinda tunazuia wizi wa CCM).
Uchaguzi ukafika. Watu wakapiga kura. Tukapata kura 2000 tu. Kumbe watu wote tuliokuwa tunafanya nao kazi ni CUF na hawa 2000 kwa kweli ndio haswa walikuwa wafuasi wa CHADEMA kule Tunduru.
This is how CUF safeguard ngome zao. CCJ inaweza kuwa Hoax kama alivyosema Tendwa.
tatizo liko kwa Msajili.. na watu hawataki kuona tatizo hilo kwa sababu wanapenda kweli tatizo lingekuwa kwa CCJ.
.....