tatizo liko kwa Msajili.. na watu hawataki kuona tatizo hilo kwa sababu wanapenda kweli tatizo lingekuwa kwa CCJ.
Nilikesha jana kufuatilia suala hili kutoka pande zote na jaribio la msajili ni "kufanya uhakiki hewa" wakati tayari ameshafikia uamuzi. Hili ndilo lilikuwa lengo la kutoa kauli tofauti kati yake na Marmo (ambaye msajili yuko chini yake) ndani ya masaa 24. Lengo lilikuwa ni kuwachanganya wananchi na hivyo kutokutoa muda kwa CCJ kuwaandaa wananchi na kuelewana mfumo.
a. Msajili alisema hana fedha za kufanya uhakiki.. hakuna mtu anauliza hizi za sasa zimetoka wapi?
b. Walisema uhakiki hautafanyika na kuwa CCJ haitashiriki uchaguzi .. sasa wanafanya uhakiki ili kiwe nini?
Wengi humu mnaposikia "uhakiki" hata hamuulizi umefanywaje hadi kuzua malalamishi. Mnachukulia tu kuwa watu wamelalamika bure.
Nimefafanua sehemu nyingine labda nirudie hapa:
Msajili alitakiwa kufanya uhakiki wa wanachama 200 wa mkoa wa Dar.. kaenda Mwembeyanga na kukuta kuna wanachama wa kutoka matawi mbalimbali ya mkoa wa Dar. Yeye kachukua orodha ya watu wa maeneo ya Mwembeyanga na ni HAO TU ndio alioataka kuwahakiki. Wanachama wa CCJ kutoka sehemu nyingine wamekataliwa kwa sababu majina yao hayakuwepo kwenye "orodha ya mwembeyanga".. Hakutaka kuchukua orodha ya sehemu nyingine za Dar kulinganisha! Sasa anapotangaza kuwa watu hawapo kwenye orodha au majina yao hayaonekani ni kweli - in the wrong orodha.
Hii ndio sababu ya uongozi wa CCJ kutaka zoezi lisitishwe kwani "uhakiki wa mkoa" unapofanyika kama uhakiki wa kitu kimoja kunapoteza kabisa dhana nzima ya uhakiki. Cha kuudhi kama kawaida vyombo vya habari vimerudia tu kile kilichoripotiwa na Msajili baada ya kwenda kuuliza maswali ya muhimu kujua nini hasa kimetokea.
Mzee mwanakijiji,
Hamkujifunza hata vyama vingine vinafanyeje wakati wa kuhakiki majina? Inaelekea mmeenda kichwa kichwa labda mliona mnajua zaidi.
Inabidi mjifunze makosa na mafanikio ya walio watangulieni.
Hapa si ajabu mmefungwa goli na factors mbalimbali zikiwemo za CCM, CUF, CHADEMA, Msajili na wengine.
Mmejianika uchi barabarani na hata waliotaka kujiunga nanyi wanaweza kuficha sura zao.