Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,990
GS, ngoja nikae chini na kuchanganua matatizo ya sera za CHADEMA na ni kwanini ni kinyume na zile za CCJ. Kuamini vitu vile vile au kwa karibu haina maana mtatumia njia zile zile kwa sababu yote uliyoyasema kuhusu imani za Chadema yaweza kuwa ni imani ya CCM vile viile!
Mkuu hayo maswali yako yanachanganya kwa sababu wewe hutaki kusema malengo yako isipokuwa ya wengine. Sema wewe malengo ya CCJ kisha tuone kama kuna watu hawakubaliani nayo..Nijuavyo tunakubaliana na hoja zetu kama tunavyokubaliana na hizo za Chadema - REFORM inahitajika..Na sote hapa tumefikia kutoa ushauri wetu ni kwa sababu tunaamini katika vyama vyote wapo wananchama na watu wanaotaka mageuzi (changes) ambayo ndio msingi wa muungano huu.
Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika Nguvu na Mamlaka ya Umma (The Peoples Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao
Lengo la Ujamaa na Kujitegemea ni kuhakikisha kuwa uchumi wa Tanzania unamilikiwa na kuendeshwa na wananchi wenyewe kwa njia mbalimbali.
Nguvu na Mamlaka ya Umma ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
Dhana ya Sekta Binafsi ina maana pana zaidi kuliko ilivyo dhana ya
ubinafsishaji. Kimsingi ni dhana inayomaanisha kuwapa watu binafsi, yaani wananchi walio wengi fursa ya kumiliki na kuendesha uchumi moja kwa moja badala ya kupitia sekta ya dola.
Kama nilivyosema hapo awali hakuna chama Tanzania chenye itikadi, ila ni mawazo ya kutuwezesha kutoka ktk Umaskini. Mapungufu ya CCM sii mapungufu ya chama ila makosa ya viongozi wake wameshindwa kutuondoa ktk Umaskini..Navyojua mimi hili ndio chimbuko la vyama vyote vya Upinzani nchini kuzaliwa kwake.
Mzee Mtei kutokubaliana na Nyerere na Ujamaa haina maana ilikuwa itikadi ya kisiasa ila dhidi ya mfumo wa Uchumi. Mrema na NCCR haikuwa kupinga Ubepari bali kupinga mfumo wa Uongozi ktk kukuza uchumi wetu kwa kutumia wageni (Wakaburu). Hivyo hiyvo vyama vyote vimeundwa kwa kutazama zaidi mapungufu ya Uongozi na sio mapungufu ya Itikadi kwani hatujawahi kutumia itikadi yoyote kiutawala toka tumeacha Ujamaa.
Nadhani utarurahishia sote ukiweka malengo ya CCJ hapa ukumbini na vizuri zaidi ikiwa malengo hayo yatazungumzwa na wahusika (vyama vingine) zaidi yetu sisi kwani huko ndiko utapata majibu yenye kuthibitisha muungano huu utakuwa wa aina gani. Mkubaliane msikubaliane swala la ushindi dhidi ya CCM ni lazima kuwepo na UMOJA wenu ktk hatua za awali, kinyume cha hapo itakuwa kazi kubwa sana kuushawishi Umma ikiwa vyama vyote vinahadithia hadithi ile ile...Utawala wa CCM ni Mafisadi!
Really? This is certainly big news to me. I have to revisit my ideological class!!
MMM
Kuhusu hiyo hoja hapo juu, kuachiana majimbo ni kutathmini kila chama kinaelewa maeneo ambayo kinakubalika zaidi hivyo basi ni budi kuongeza juhudi huko kuliko kwenda kwenye majimbo ambayo chama kinajua wazi kuwa uwezo wa kushinda ni mdogo. Makubaliana hayo ni juu ya viongozi wa vyama husika kuamua ndio kukomaa kisiasa huko na mojawapo ya njia za kuwatoa CCM, as is now ni kuwa na uroho wa kisiasa yaani ni wazi majimbo mengine wanajua wazi kuwa CCM iko mbele na wanaona ni bora wote wakose...Kanuni za makubaliano ni wazi lazima waangalie nani zaidi ama kwa kutumia opinion polls au historical voting patern za maeneo husika. Ni lazima viongozi wakubali kuwa ili mabadiliko ya kweli yaje Tz ni muhimu kuwa na aina moja au nyingine ya ushirikiano kwenye upinzani, jinsi ilivyo sasa kwa upinzani kushika mamlaka ya dola ni kujidanganya tu na kuota ndoto za alinacha.
Kuhusu swala lako hapo juu ni wazi kuwa kama kungekuwa na chama kimoja cha upinzani chenye nguvu ni bora zaidi ya utitiri wa vyama bungeni hiyo ni wazi angalia Marekani (mainly 2 political parties )au hata UK (mainly 3 parties). Sasa hapa kwetu kweli inaumiza kichwa. Kama mtu unataka mageuzi (ng'oa CCM) halafu siku ya uchaguzi unapatwa na mchecheto nani niwape kura yangu CUF, Chadema, UDP au CCJ?
Hili halijajaribu hata chembe kujibu maswali yangu; umerudia rudia kile ambacho kimesharudiwa mara nyingi tangu mfumo wavyama vingi urudishwe tena.
Sasa u nafikiria kuwa na chama kimoja chenye nguvu kutawezekana kama msingi wa muungano ni kutokuunganisha vyama kabisa kuunda chama kimoja?
Wewe ushauri wako ni upi ili tuwe na upinzani ulio imara na wa kweli katika chaguzi zetu? Mimi nimeshatoa maoni yangu
Haiingii akilini kuwa kwenye kila jimbo on average CCM 50% na wasioipenda CCM ni 50%, sasa wale wasioipenda CCM wanavurugwa na utitiri wa vyama angalau 10, so at the end CCM on average wanashinda kwenye 90% ya majimbo.
Mkuu Mkandara wala usipoteze energy bure kwa huu wazimu sijui CCJ, sijui chama kingine kipya!!
Sisi watanzania tuliozaliwa kabla ya 1990 ni majuha na machizi, hivyo tuombe mungu kizazi hiki kipya kiwe na hekima.
Haiingii akilini kuwa kwenye kila jimbo on average CCM 50% na wasioipenda CCM ni 50%, sasa wale wasioipenda CCM wanavurugwa na utitiri wa vyama angalau 10, so at the end CCM on average wanashinda kwenye 90% ya majimbo.
Mchezo ungekuwa mzuri kama kuna chama kimoja tu cha upinzani, hivyo almost kila jimbo lingekuwa toss up, oooh no kwa wazimu wetu na kujifanya tunajua sana sijui itikadi, mara sera tuna vyama kama 10.
Issue namba moja ni CCM kushindwa kwanza, then in the future ndio mambo ya itikadi, sijui sera sijui wazimu upi mpya yaje. Sasa hivi ITIKADI NA SERA should be NGOA CCM, hakuna zaidi ya hapo.
Hivi mwenzetu unajua TANU walipomng'oa mkoloni walikuwa na mpango gani zaidi?Kweli wewe ni wa mwaka 1990! Hivi ukishaing'oa CCM bila kuwa na mpango wowote zaidi ya hapo nchi utaiendeshaje?
Hivi mwenzetu unajua TANU walipomng'oa mkoloni walikuwa na mpango gani zaidi?
Okay,W e got that advertisement.So what I need to know,The place where I can get the CcJ MEMBER CARD?
Ama kweli watu wanapenda debate. Mwanakijiji hiyo 50/50 ni maono tu ya juu juu nikimaanisha kuna watu wengi wameichoka CCM, lakini wanaona hakuna possibility ya kuingoa so at the end wanaipigia CCM kura shingo upande au hawapigi kura kabisa, kungekuwa na viable option ungeshaa lakini sitaki discussion ya nuts & bolts issue ni NGOA CCM.
Boramaisha, unauliza ukiingoa CCM, nchi utaendesha vipi?? What?? Hapa tulipo nchi inakwenda tu yenyewe bila muendeshaji, so anything else itakayofuata tu sheria say Watu walipe kodi, rushwa iondolewe, watu wawe appointed on merits, kipaumbele cha vitendo (ie budget) kwenye kilimo, Afya, elimu itakuwa step in the right direction.
Kujifanya wajuaji sijui ooh tunamipango hii sera hiii, itikadi hii ndio tutaishia humu humu kubishana na CCM kupiga magoli milele.
Haiwezekani kijiji kinashambuliwa na Simba hatari wanaokula mifugo na watu, badala ya issue kuwa namna ya kuua simba, wanakijiji wanakaa kubishana simba wakishauliwa mifugo itagawanjwa vipi au njia mpya za ufugaji, UA KWANZA SIMBA, mengine yatafuata.