Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,487
- Thread starter
-
- #201
Mzee Mwakijiji,
Haya mathlan tukubali kwamba CCJ ni hao waliojitokeza ikiwa ni pamoja na wewe. Sawa kabisa, lakini mnashindwa kutuvuta kwa sababu moja kubwa. Nyie Kushindwa kuelewa TATIZO la wananchi hivi sasa ambalo ndilo linatangulia kabla ya hizo Itikadi zenu.
Nitakwambia tena na tena ili upate kunielewa vizuri natokea wapi.
Wengi wetu tunajiona kama wafungwa ndani ya gereza hili la chama CCM...Tunachokitaka ni kuondoka ktk hali hi ya ufungwa, na ndio maana nikatumia ule mfano wa ndege iloanguka kisiwani. Sasa unapokuja na idea ya kuroroka ni muhimu kwetu kusikia master Plan ya kutuwezesha ku escape toka kifungoni au kuondoka ktk adha za kisiwani hiki na kuwa HURU.
Sisi sote kwa ujumla wetu hapa JF tunataka kusikia mtaweza vipi kutuondoa ktk Utawala huu wa CCM na sio siasa za baadaye. Hata hao TANU chini ya na mwalimu Nyerere walitupa siasa za kujikomboa kwanza toka utawala wa mkoloni kabla ya itikadi za huo Ujamaa kuja miaka saba baadaye. Ndivyo wanavyofanya wana Mapinduzi wote duniani kutafuta support ya wananchi ili watoke ktk utawala unaowagandamiza.
Nachokiona mimi CCJ wanakuja na siasa za Itikadi kama vile nchi yetu haina matatizo, mkuu wangu sivyo wananchi wengi wanavyoitazama Tanzania ya leo..na kibaya zaidi viongozi na wanachama wa CCM wamekaa kama makaburu hawaoni shida hizi kwa sababu wao wako ktk hali nzuri ya kimaisha. Na kwa makosa ya wazi kabisa Utawala mzima unawanufaisha wale wanakubaliana nao kwa kuvaa magwanda ya Kijani kujionyesha wao ni watu tofauti kabisa na watawaliwa. Tofauti na makaburu, waliokuwa na Ubaguzi wa rangi sisi tunatumia ubaguzi wa mavazi na bendera za chama...na kwa bahati nzuri sii wananchi wengi wanakubali mfumo huu wa utengano.
Njia pekee ya CCJ kuweza kufanikiwa ni kuja na master Plan ya kuwakomboa wananchi toka gereza hili la CCM. Na ndio hapo tunapokuja na mchango wetu kwamba, hii great escape haiwezi kufanikiwa pasipo muungano wa makundi mengine yanayotaka pia kuondokana na kifungo hiki, pamoja na kwamba huko nje ya kifungo kila jumuiya inaweza kuwa na mipango yake. Walifanya Zimbabwe, South Africa nchi zote za Ulaya ya mashariki, Bosnia na majuzi tu Poland, Kenya, Zimbabwe tena na Liberia. Wote hawa walijenga mbinu za kukiondoa chama tawala pale wananchi hawakuwa na matumaini - Tumaini jipya kwa wananchi waliokosa Uhuru huanza na mbiu ya FREEDOM..na Uhuru hauwezi patikana pasipo wapinzani kuwa na nguvu moja japokuwa wana imani za kiitikadi tofauti..
Shukran, swali zuri sana..Mkandara,
a. kwanini muungano wa kuiondoa CCM umeshindikana sasa hivi miaka 15 tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi?
b. Kwanini muungano huo utamanike na uonekane unawezekana kwa ujio wa CCJ?
c. Kwanini vyama vilivyopo sasa (ukiondoa CCJ ambacho hakina itikadi, hakielewi matatizo ya wananchi na hakina mpango unaoeleweka wa ukombozi wa Mtanzania kutoka katika utumwa wa CCM) visiungane mara moja kwani tayari vina usajili wa kudumu na vina sera na mipango kamambe ya kuiondoa CCM?
Mr Ngabu point yangu siyo nani tajiri au maskini kati ya Republican na Democratic, nachotaka kujua hapa kwetu TZ mtu akisema yuko Chama "A" na mwingine yuko chama "B" hawa watu wawili wanatofauti gani za kiitikadi zinazowafanya wawe kwenye vyama tofauti. Mfano mtu kukosa uteuzi wa chama chake na kuamua kukihama je kuhama kwake kunasababishwa na tofauti za kiitikadi au uchu wa madaraka? Mtu akiondolewa kwenye uongozi na kuhamia Chama kingine, je hapo amesukumwa na tofauti za kiitikadi au kusaka ajira?.Hiyo ni dhana potofu na propaganda za maliberali tu. Matajiri mabilionea wengi ni Democrats....
Come to think of this - Sheria ya Gharama za Uchaguzi.. Hivi hiyo kazi ya kuhakiki gharama zake wanaolipa ni kina nani kodi za wananchi? na inatarajiwa kiasi gani kitatumika!
Mkuu nadhani ungepitia kwanza tovuti yao na kusoma majukumu ya Tendwa na Ofisi yake kabla hatujaanza kumhukumu visivyo - HAPA
Written by Admin Wednesday, 27 June 2007 Statement of the Registrar of Political Parties
The main responsibilities of the office of the Registrar of Political Parties is to register political parties and monitor their administrative and political function in accordance with laws and regulations governing multiparty democracy in this country.
Major laws governing registration and monitoring of political parties are the constitution of the United Republic of 1977 and the Political Parties Act No. 5 of 1992. To-date there is eighteen political parties with permanent registration. These are CCM, CUF, CHADEMA, UMD, NLD, TLP, NCCR-MAGEUZI, CHAUSTA, JAHAZI ASILIA, TADEA, DP, FORD, NRA, SAU, DEMOKRASIA MAKINI, UDP, PPT-MAENDELEO UPDP.
The office is also responsible for aligning the political parties constitutions with the national constitution by ensuring political parties' constitutions do not overlap or ruin the interests and integrity of the mother constitution.
Other responsibilities of this office are to manage disbursement of government subvention to political parties, which have members of parliament and members in the local government councils and it also link the government with political parties.
The office is later responsible for receiving the returns on expenditure for analysis, scrutiny and publication of the audited Accounts for public consumption. The office is also expected to disclose any other sources financing to political parties. The office communicates to the public any information related to political parties and is also reports on National multiparty democracy by virtue of this position the office closely participates in monitoring and observation in all national electoral processes. The office hence serves as a link of the ruling party to the opposition parties.
The office is also held responsible for creating civic awareness to the public, which is implemented through educative seminars and workshops, and media, which has minimized political disputes amongst parties and within parties themselves. And this has also promoted good governance and enhancing democracy.
Mwanakijiji; I'm 100% not conviced;
Naamini CCJ=CCM B;
Ukiacha maneno ambayo hata kwenye kanga yapo; kupigania rushwa aliyeanzisha tena Mwembeyanga pale alitaja majina-jemedari yupo; ajenda zingine zote ziko exhausted already na vyama; ukiacha mikauli mbiu ambayo mie naona kila mahala ipo na haisaidii; nasema Chadema ndio chama ambacho kama hata hao CCJ wangekuwa seriuos wangejiunga huko kuleta mapambazuko maana hata kila kelele wanazopiga ziko exhaused. Samahani mwanakijiji mie sio mwanachama ila napenda mageuzi; naamini hii ni danganya toto; watu wahamishe maskio CCJ then waue vyama ambavyo falsafa zao zilianza kujulikana sasa kama za Chadema; naamini hivyo wengine mtanijuza zaidi nisiyojua
Mkuu wangu,
Katika hili la Usajili mkuu wangu tuliache kama lilivyo lakini kama utaniuliza mimi nitakwambia kwamba sioni kama mna nia njema kabisa..samahani lakini!
Usajili wa CCJ unahitaji fedha za serikali kuendesha kampeni zake. Hali hii ni nchi maskini kabisa, nchi ambayo kila matumizi ya senti yake ni kumkwaza Mfanyakazi na Mkulima
. Nchi yenye vyama 18 na bado vingine vinazaliwa ni Ulevi na upumbavu mkubwa sana..
Vyama vyetu havina tofauti za kiiikadi 3 kubwa na sio vyama vyote vimezifuata hizi tatu. Wote wamejirundika ktk Progressive na Social Demokratic tofauti zao ni vichwa vya viongozi tu. Hivyo vyama vyetu vinatofautiana vichwa vya watu ktk Utekelezaji.
Mkuu hii ni hatari kubwa ya kupoteza maana ya Demokrasia, kama tulivyopoteza maana ya dini na Uhuru wa kuabudu. Madhehebu yameundwa kutokana na kutokubaliana na mawazo ya viongozi pamoja na kwamba kimsingi wote wanakubaliana na Gospel. Hii italeta matabaka ya wananchi hata kufikia watu kujiita wao wanaCCM bila kujali ni itikadi gani mwana CCM anapaswa kuifuata.
What's wrong with kina Mkapa, Lowassa na hata Kikwete ni wao kuishi nje ya mafundisho ya kiimani (itikadi) ya chama CCM. Kinachotakiwa kifanyike ni kuwafukuza waumini hawa uanachama wakaanzishe wao chama chenye imani tofauti, lakini mnapowakimbia nyie na kuwachia kanisa inatupa wasiwasi watu wengi nini haswa malengo ya kukimbia kanisa hilo..
Pia nimeona watu wakifukuzwa uanachama kwasababu hawakubaliani na kiongozi! Jamani chama ni Itikadi, huwezikumfukuza mtu uanachama kwa makosa nje ya itikadi ya chama. Ni sawa na kumfukuza mtu dini ati kwa sababu aligombana na Sheikh au Padri. Inachukua mtu kuvunja sheria za kiimani za dini au chama kufukuzwa na sio kukosana na kiongozi.
Hivyo mkuu wangu pengine mimi nipo at another level ya demokrasia kiasi kwamba siwezi kuelewa siasa za Bongo, lakini kwa kufahamu njaa iliyopo Bongo kuanzishwa kwa vyama vya siasa vingi ni moja ya matumizi mabaya ya kodi za wananchi..Vyama vingi vinajiandikisha kama njia ya ajira na kupata fedha za kutumia kwani Uchumi wa Tanzania (mzunguko wa fedha) huanza baada ya fedha hizi za Uchaguzi kutolewa.
The best option you guys had (Wanachama wa CCM) sio kukimbia chama isipokuwa kupambana na utawala huu dhalimundani ya chama CCM ktk uchaguzi wa ndani. Huu ulikuwa ni wakati wa kukisambaratisha chama toka ndani yaani hao kina Salim, Sitta na wengineo wagombee ndani ya chama against kundi hili la mashetani. Nina hakika kuna baraka za wazee wengi tu including Mzee Mwinyi na pia kuna laana za wachawi wengi against JK kina Mkapa, Sumaye na Lowassa. Hivyo vita ya ndani haiweza kuamlika kirahisi kwa sababu itakuwa vita ya vichwa (Uongozi)kuliko nyie kujitoa nje kukabiliana na chama kizima cha CCM...U dont need registration ya chama, vita ya ndani ibakie ndani na kufuli wekeni mlangoni hakuna kuamlia mtu..huku nje tuachieni sisi tulozoea kurusha mawe kisha tunaingia mitini..
Najua jinsi vyama vingine vilivyotulet down.. this is the best chance we have.. NN kwa muda wote huu umewahi kuniona lini napigia debe chama chochote cha siasa and why this?
Unajikatia pande au unataka tuamini kila unachoamni au kutaka kuamini?Najua jinsi vyama vingine vilivyotulet down.. this is the best chance we have.. NN kwa muda wote huu umewahi kuniona lini napigia debe chama chochote cha siasa and why this?