Case study kuhusiana na mjadala wa Katiba Mpya

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Hoja: la muhimu zaidi ni heshima kwa sheria, na kwa vile Katiba ni sheria mama, basi heshima husika iwe kwenye sheria zilizomo kwenye katiba.

Hali ilivyo sasa: ni kweli katiba iliyopo ina mapungufu mengi. Na ni kweli kuwa mapungufu hayo yanaathiri maeneo mbalimbali hususan haki za kisiasa/kidemokrasia.

Katiba yote ya sasa ina mapungufu?: Hapana. Kuna sheria nyingi tu katika katiba ya sasa ambazo ni mwafaka. Tatizo ni kwamba heshima kwa sheria ni changamoto kubwa kwa Watanzania. Kwahiyo hata sheria hizo "nzuri" zaishia kuonekana "mbaya" kwa sababu zinapuuzwa

Case study: kwa mujibu wa maelezo ya Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifoji majina wa wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho. Kufoji ni kosa la jinai. Hadi muda huu Chadema hawajafungua mashtaka dhidi ya tume ya Taifa ya Uchaguzi kutokana na forgery hiyo.

Tatizo lipo wapi? Ukisikiliza mjadala kuhusu Katiba mpya, focus ipo kwa watawala. Nguvu kubwa za Rais, Tume ya uchaguzi kutokuwa huru, nk. Lakini pengine kwa makusudi au kutojua, hakuna mjadala kuhusu "mapungufu ya watawaliwa." Mfano hai hapa ni huo wa NEC kuvunja sheria lakini wahanga wa uvunjifu huo wa sheria, Chadema hajachukua hatua za kisheria. Sasa hapo tatizo si katiba bali ni kupuuza sheria inayoweza kutoa haki stahili.

Logic ya wakati huo kwa Chadema: zama za Mwendazake, ingekuwa sawa na kupoteza muda kwa Chadema kwenda mahakamani kudai haki yao.

Logic ya sasa: huhitaji kuwa na upeo mkubwa wa kinachoendelea Tanzania kubaini kuwa zama zimebadilika haswa. Japo utaambiwa "kutenguliwa hukumu ya Mbowe na Mdude kuachiwa huru ni suala la kimahakama," ukweli wa wazi ni kuwa haya yasingewezekana katika zama za Mwendazake.

Kwa maana hiyo: kwa vile mazingira yaliyopo ni rafiki kudai haki, angalau kwa kigezo cha kesi hizo mbili, kwanini Chadema wasiiburuze mahakamani Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kosa la kufoji majina 19 ya wabunge wa viti maalum?

Katiba mpya inaingiaje hapa?: Naam kuna haja ya marekebisho ya sheria mbalimbali kandamizi. Endapo mabadiliko hayo ni lazima yafanyike kwa njia ya Katiba mpya, ni sawa. Endapo badala ya katiba mpya tunaweza kufanya marekebisho tu ya katiba, ni sawa pia. However, iwe ni marekebisho ya katiba au ujio wa katiba mpya, kasumba ya kupuuza sheria itafanya marekebisho ya katiba/katiba mpya kuwa tatizo kama ilivyo sasa.

Kama alivyosema Askofu Bagonza kuwa wanaovunja Katiba hii wanaweza pia kuvunja katiba mpya, nami nahitimisha kuwa wanaopuuzia kudai haki zao kipindi hiki cha "katiba yenye mapungufu" wanaweza pia kupuuzia kudai haki zao katika zama za "Katiba mpya."

Na mwisho kabisa, kama hatuwezi kuheshimiana sie wenyewe katika mjadala huu muhimu kwa mustakabali wa taifa letu, hiyo katiba mpya itaheshimiwa vipi maana asiye na heshima kwa mtu ana nafasi kubwa ya kutokuwa na heshima kwa kitu/vitu (eg Katiba).

Mfano hai wa "kukoseana heshima" ni pale nguli wa sheria Prof Issa Shivji alipotoa angalizo kuhusu katiba mpya na kutanabaisha kuwa sio mwarobaini wa kutatua changamoto mbalimbali, baadhi ya "wasiopenda mawazo tofauti na yao" wamedai profesa huyo anazeeka vibaya. Wengine wameenda mbali na kumtusi kuwa "nafasi za u-DC zimejaa."

I stand to be corrected 🙏
 
Mojawapo ya umuhimu mkubwa wa Katiba mpya ni kwamba kutakuwa hakuna tena uporaji wa chaguzi. Chaguzi ziitakuwa za HAKI na HURU si za kupora kutumia Tume FAKE na mtutu wa bunduki kwani kupitia Katiba mpya tutakuwa na Tume huru ya uchaguzi na kama taratibu za uchaguzi zikiukwa na chama kilichoshinda basi matokeo yanaweza kabisa kufutwa na kuitishwa uchaguzi mpya kama ilivyotokea Kenya 2017.

Umenena kweli, suala la Katiba ni la wananchi wote,walio na vyama na wasio na vyama, wafanyabiashara,wasanii, watu wenye ulemavu, viongozi wa dini, vyombo vya habari n.k sote tunakubali Katiba ya sasa ina mapungufu na tumejitunza zaidi miaka 5 iliyoisha.

Mchakato unahitaji jumuishi ya makundi haya na ni mchakato wenye gharama na unaochukua muda ili ilitokane na matakwa ya wengi sio vikundi vya watu wachache tu, sasa wameshambiwa watakaa wajadiliane tena kila makundi lakini kuna watu wamelifanya kama ndio movement ya kisiasa.

Katiba mpya haiepukiki hatutaki tuliyopitia miaka mitano yajirudie akini ni mchakato wa kutumia muda na rasilimali. Katiba zinabadilishwa kadri mahitaji yanavyokuwa, kuna baadhi sijui wao nini hawakielewi, wao wanakuja na matusi na udhalilishaji
 
Na mijadala ya katiba mpya iwe huru, isifungamane na vyama vya siasa

Maana lengo la chama chechote cha siasa ni madalaka, si maslahi ya mwananchi

Kuna chama kinajifanya kiko mstari wa mbele kutafuta katiba mpya ila ukiwaangalia viongozi wake wote ni wezi na wenye tamaa ya madalaka

Sitegemei chama kama hiki kinaweza kutetea mwananchi.
 
Katiba mpya pia itakuwa na kipengele cha adhabu Kwa yeyote yule ambaye hatoiheshimu katiba kuanzia Rais na walio chini yake kwa kutozwa faini kubwa, kwenda jela au vyote kwa pamoja.
Katiba ya sasa iko kimya kuhusu Rais na wengine wote wanapokiuka katiba ya nchi. Na tumeyaona mengi sana yaliyofanywa na yule dhalimu mwendazake katika kuvunja katiba na sasa Samia anaendelea kuivunja katiba pamoja na Ndugai na Tulia Kwa kuendelea kuwakumbatia Wabunge haramu 19 na kuwalipa billions za walipa kodi kinyume na katiba.
 
Na mijadala ya katiba mpya iwe huru, isifungamane na vyama vya siasa

Maana lengo la chama chechote cha siasa ni madalaka, si maslahi ya mwananchi

Kuna chama kinajifanya kiko mstari wa mbele kutafuta katiba mpya ila ukiwaangalia viongozi wake wote ni wezi na wenye tamaa ya madalaka

Sitegemei chama kama hiki kinaweza kutetea mwananchi.
Mijadala imeishafanyika na Warioba, ameenda kila kata ya nchi hii na kukusanya maoni kutoka katika makundi yote na jinsia zote,na ametumia zaidi ya Bilioni 120, mnataka mchakato upi na mawazo yapi tena jamani? Mbona kila siku tunarudishana nyuma. Au wengine mlikuwa hamfatilii? Mnatuchosha. Tatizo sio rasimu ya Warioba, tatizo lilianzia pale CCM walipoanza kuchomoa vipengele muhimu kutoka kwenye rasimu ya Warioba na kuchomeka vyao kulinda maslahi yao.. wapinzani kuona hivyo wakagoma, wakajitoa kwenye mchakato wakipinga uhuni huo.
Kinachotakiwa sasaiv ni kuitisha upya bunge la katiba na kuita makundi wakilishi kutoka kila sekta na jinsia kwa usawa, waanze upya kuipitia rasimu ya Warioba na hatimaye waipitishe iwe katiba mpya. Period!
 
👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👍🏽

Mijadala imeishafanyika na Warioba, ameenda kila kata ya nchi hii na kukusanya maoni kutoka katika makundi yote na jinsia zote,n ametumia zaidi ya Bilioni 120, mnataka mchakato upi na mawazo yapi tena jamani? Mbona kila siku tunarudishana nyuma. Au wengine mlikuwa hamfatilii? Mnatuchosha. Tatizo sio rasimu ya Warioba, tatizo lilianza pale CCM walipoanza kuchomboa vipengele muhimu kutoka kwenye rasimu ya Warioba na kuchomeka vyao.. wapinzani wakagoma, wakajitoa kwenye mchakato wakipinga uhuni huo.
Kinachotakiwa sasaiv ni kuitisha upya bunge la katiba na kuita makundi wakilishi kutoka kila idara kwa usawa, waanze upya kuipitia rasimu ya Warioba hatimaye waipitishe iwe katiba. Period!
 
Mojawapo ya umuhimu mkubwa wa Katiba mpya ni kwamba kutakuwa hakuna tena uporaji wa chaguzi. Chaguzi ziitakuwa za HAKI na HURU si za kupora kutumia Tume FAKE na mtutu wa bunduki kwani kupitia Katiba mpya tutakuwa na Tume huru ya uchaguzi na kama taratibu za uchaguzi zikiukwa na chama kilichoshinda basi matokeo yanaweza kabisa kufutwa na kuitishwa uchaguzi mpya kama ilivyotokea Kenya 2017.

Hebu Tumia Akili yko bro Tunaweza kuwa na Katiba mpya lkn uporaji ukawepo kwasbb Unaweza kuwa ba watawala wadiofata sheria hzo zlokuwa ndan ya katiba..
 
Hoja: la muhimu zaidi ni heshima kwa sheria, na kwa vile Katiba ni sheria mama, basi heshima husika iwe kwenye sheria zilizomo kwenye katiba.

Hali ilivyo sasa: ni kweli katiba iliyopo ina mapungufu mengi. Na ni kweli kuwa mapungufu hayo yanaathiri maeneo mbalimbali hususan haki za kisiasa/kidemokrasia.

Katiba yote ya sasa ina mapungufu?: Hapana. Kuna sheria nyingi tu katika katiba ya sasa ambazo ni mwafaka. Tatizo ni kwamba heshima kwa sheria ni changamoto kubwa kwa Watanzania. Kwahiyo hata sheria hizo "nzuri" zaishia kuonekana "mbaya" kwa sababu zinapuuzwa

Case study: kwa mujibu wa maelezo ya Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifoji majina wa wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho. Kufoji ni kosa la jinai. Hadi muda huu Chadema hawajafungua mashtaka dhidi ya tume ya Taifa ya Uchaguzi kutokana na forgery hiyo.

Tatizo lipo wapi? Ukisikiliza mjadala kuhusu Katiba mpya, focus ipo kwa watawala. Nguvu kubwa za Rais, Tume ya uchaguzi kutokuwa huru, nk. Lakini pengine kwa makusudi au kutojua, hakuna mjadala kuhusu "mapungufu ya watawaliwa." Mfano hai hapa ni huo wa NEC kuvunja sheria lakini wahanga wa uvunjifu huo wa sheria, Chadema hajachukua hatua za kisheria. Sasa hapo tatizo si katiba bali ni kupuuza sheria inayoweza kutoa haki stahili.

Logic ya wakati huo kwa Chadema: zama za Mwendazake, ingekuwa sawa na kupoteza muda kwa Chadema kwenda mahakamani kudai haki yao.

Logic ya sasa: huhitaji kuwa na upeo mkubwa wa kinachoendelea Tanzania kubaini kuwa zama zimebadilika haswa. Japo utaambiwa "kutenguliwa hukumu ya Mbowe na Mdude kuachiwa huru ni suala la kimahakama," ukweli wa wazi ni kuwa haya yasingewezekana katika zama za Mwendazake.

Kwa maana hiyo: kwa vile mazingira yaliyopo ni rafiki kudai haki, angalau kwa kigezo cha kesi hizo mbili, kwanini Chadema wasiiburuze mahakamani Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kosa la kufoji majina 19 ya wabunge wa viti maalum?

Katiba mpya inaingiaje hapa?: Naam kuna haja ya marekebisho ya sheria mbalimbali kandamizi. Endapo mabadiliko hayo ni lazima yafanyike kwa njia ya Katiba mpya, ni sawa. Endapo badala ya katiba mpya tunaweza kufanya marekebisho tu ya katiba, ni sawa pia. However, iwe ni marekebisho ya katiba au ujio wa katiba mpya, kasumba ya kupuuza sheria itafanya marekebisho ya katiba/katiba mpya kuwa tatizo kama ilivyo sasa.

Kama alivyosema Askofu Bagonza kuwa wanaovunja Katiba hii wanaweza pia kuvunja katiba mpya, nami nahitimisha kuwa wanaopuuzia kudai haki zao kipindi hiki cha "katiba yenye mapungufu" wanaweza pia kupuuzia kudai haki zao katika zama za "Katiba mpya."

Na mwisho kabisa, kama hatuwezi kuheshimiana sie wenyewe katika mjadala huu muhimu kwa mustakabali wa taifa letu, hiyo katiba mpya itaheshimiwa vipi maana asiye na heshima kwa mtu ana nafasi kubwa ya kutokuwa na heshima kwa kitu/vitu (eg Katiba).

Mfano hai wa "kukoseana heshima" ni pale nguli wa sheria Prof Issa Shivji alipotoa angalizo kuhusu katiba mpya na kutanabaisha kuwa sio mwarobaini wa kutatua changamoto mbalimbali, baadhi ya "wasiopenda mawazo tofauti na yao" wamedai profesa huyo anazeeka vibaya. Wengine wameenda mbali na kumtusi kuwa "nafasi za u-DC zimejaa."

I stand to be corrected
Asante kwa Hoja nzur kabsa...
Hawa CDM kwasasa hawana hoja Mama Samiah kafanya vitu ambavyo vimewatoa kwenye Reli wanataka kusikika tu...
 
843B1763-BC6E-4FCD-A250-9ACA90A715BE.jpeg
 
Wewe ni mmoja kati ya wale waliolewa na utawala na "mama" wengi wenu mmekuwa mnatawaliwa na hisia zaidi ya uhalisia.

Unazungumzia mambo ya kudai Katiba kistaarabu wakati hao watawala hawaujui huo ustaarabu, unaonaje kama ungeanza kumwambia Samia afute ile kauli yake aliyoitoa Mbeya kuwa hata kama CCM isipochaguliwa itatangazwa mshindi?

- Kuhusu kuheshimu sheria, unadai kwamba hata kama Katiba Mpya ikija bado kuna uwezekano sheria nazo zitavunjwa.

Unasahau au hujui kwamba Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) iliweka miongozo kwa kila mtendaji kwenye ofisi ya serikali kuanzia Rais kwa nafasi yake atakuwa responsible kwa kila kosa atakalofanya, nini afanye akiwa ofisini na kipi kitampata asipotekeleza majukumu yake kisheria, wakati hii Katiba ya sasa inamzuia Rais kushtakiwa, Rais ni kama mfalme/ malaika.

Zaidi umeenda kutupia malalamiko yako kwa Chadema kwamba hawakwenda mahakamani licha ya wao kudai kwamba palikuwepo na forgery kwenye lile suala la wale Covid 19, hapa umenishangaza, unataka Chadema waende mahakama ipi haki ikatendeke wakati mahakama sasa zimewekwa mfukoni na watawala?

- Rais hajawahi kuzungumza lolote kuhusu wale wanawake, yupo kimya licha ya nguvu na ushawishi alionao kwenye siasa za nchi, kitendo chake cha kukaa kimya kwenye hili suala kinaacha tafsiri kwamba anaridhika na uwepo wa wale wanawake kule bungeni kinyume cha sheria, licha ya kujinadi ni mpenda HAKI.

- Kule bungeni nako, Ndugai kila siku anawalinda wale wanawake licha ya kujua fika anavunja sheria inayotaka wabunge watoke kwenye chama cha siasa, licha ya Chadema kudai mara zote kwamba tayari walishamuandikia Ndugai barua kumjulisha kuhusu kuvuliwa uanachama wale wanawake 19.

Ndugai anadai Chadema hawajafuata taratibu wakati taratibu kam hizo zimewahi kufuatwa miaka ya nyuma na waliokuwa wabunge kufutwa uanachama.

Hapa tunaona kumbe ni watawala ndio wanaongoza kupuuza sheria zilizopo badala ya Chadema kama unavyodai wewe, hivyo Katiba Mpya ni muhimu ije kuwawajibisha viongozi wa aina hii na kuleta usawa kwa wote.

Wakati kwa "individuals" wa nchi hii na wapinzani wakishindwa kutii sheria, au wakati mwingine wakifuata sheria kinyume na mapenzi ya watawala hupelekwa mahakamani au jela kabisa ( sababu wameziweka mahakama mfukoni), kitendo chako cha kushindwa ku - address hii problem ni udhaifu mkubwa kwenye andiko lako.
 
Evarist Chahali,

..hoja yako ni nzuri, lakini naona umeichanganya na mfano mbaya ulipoleta suala la Chadema kutokwenda mahakamani kuhusiana na waliokuwa wanachama wao kujipeleka bungeni.

..mimi nadhani ungekuwa sahihi kama ungewashinikiza wabunge 19 ni kwanini wanahudhuria bungeni wakati chama chao kimewafukuza uanachama.

..Yuko mbunge mmoja alikiri bungeni kwamba amefukuzwa uanachama, na kitu cha kushangaza Naibu Spika akamkatiza hotuba yake na kumuelekeza afute kauli kuwa amefukuzwa uanachama.

..Pia wanaoweza kwenda mahakamani sio Chadema peke yao. Hata wabunge 19, Tume ya uchaguzi, Ofisi ya Spika, Msajili wa vyama vya siasa, wanayo dhima ya kulipeleka suala hili mahakamani ili liamuliwe kisheria.

..Kuhusu Chadema kutokwenda mahakamani inawezekana ni kutokana na UZOEFU wao na mahakama zetu. Kuna matukio mengi ya mahakama kuwaonea Chadema ama kwa kuwatia hatiani kwa makosa ya kubambikiwa, au kuamua mashauri kwa namna ya kukikandamiza chama hicho.

..Ni maoni yangu kwamba mhimili wa mahakama nao unapaswa kuhojiwa kama umekuwa ukitenda HAKI wakati wote. Kuna umuhimu wa mhimili huo kujitathmini utendaji wake na maadili yake.

..Naamini utendaji mbovu wa mahakama zetu ambazo zinashirikiana na wavunja sheria, na katiba, na hali hiyo imepelekea wananchi kukata tamaa kutafuta haki zao mahakamani.
 
Back
Top Bottom