Cape Town, Afrika Kusini ingekuwa Tanzania, yote ingekuwa ni Hifadhi

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,409
8,911
Nimebahatika kutembelea miji mingi Duniani iliyoendelea nilichojifunza ni kwamba wazungu hawataki sisi tuendelee kwani wanachokifanya kwao kwetu wanakizuia, mifano mingi kuanzia kutenga maelfu ya square kilometers kwa ajili ya wanyama na “kutunza na kuhifadhi nature” mpaka uchafuzi wa mazingira, sisi ambao ni masikini ndio tunaotakiwa kutunza mazingira ambapo there is a catch, huwezi kuendelea bila ya polution, China, India au Brazili wamekataa mambo ya global warming ila sisi tunakatazwa kutumia hata makaa ya mawe au hata kujenga bwawa la kuzalisha umeme ili tusiharibu mazingira na ni ishu tunapigwa vita.

Ukiangalia mji kama Cape Town nchini AK ungekuwa Tanzania ingekuwa ni sehemu ya hifadhi ya wanyama na misitu na tungefurumushwa kupisha wanyama, lkn wazungu wao wanaishi Cape Town and its beautiful.

Wengi hawajui kwamba wakati wa ukoloni wa Ujerumani Ngorongoro crater haikuwa hifadhi waliitumia kwa ufugaji na makazi na hata kulikuwa na plani za kuleta makaburu ktk AK kuja kusettle ngorongoro crater, wazungu walivyoondoka wakasema ni hifadhi haturuhusiwi kuishi wala kufuga.

Mfano mwingine hai sasa hivi na misitu yetu haturuhusiwi au tumekubali kukatazwa kuitumia kwa chochote si kwa mbao wala asali kwa ajili ya sijui carbon credits, Amazon rain forest largest forest in the world lkn wazungu wa Brazil hawakatazwi au hawakubali kukatazwa kuitumia kimaendeleo sijui carbon credit wanalima, wanafuga wanakata mbao kwa maendeleo ila sisi ni no kwamba tutunze misitu.

Cape Town
1702710105055.jpeg


Rio Brazil
1702710830965.jpeg


1702710887532.jpeg


1702710782307.jpeg
 
Tunza misitu wewe....

Somalia wenyewe sahvi wanapanda miti...
Na nyie bila mjerumani kupanda miti kuanzia ikulu kule mitaa ya karimjee,kuelekea samora
Nyie msingepanda miti

Ova
 
Wanazijua akili zetu, isipowekwa limitation ya kukata miti watu watachoma mkaa mpaka misitu itakuwa jangwa.
 
Serikali ikiruhusu tukate miti nitaanza kuchoma mkaa mpaka ile miti ya pale Magogoni nitainunua
kazi ya kuchoma mkaa inalipa sana
 
Back
Top Bottom