Hawa watu ni waongo wakubwa hakuna holly spirit Wala holly sprite,nilishawahi ishi na mjomba mlokole nimemaliza kidato Cha nne tu nikaenda kwake kupumzika Ili nirefresh mind basi Kwa sababu Mimi nilikua Sina Imani na Hizi Abrahamic Religion since nipo kidato Cha pili ila yeye Alikua hajui nilivyo,
Jumamosi Moja akanambia aaah unajua kanisa letu Lina upako Sana na inabidi twende kwenye ibada ya maombezi,nilishindwa kumkatalia na kumuweka wazi juu nachokisimamia nilitaka bisha nikaona nitamdisapoint basi
Tukaondoka mapema pamoja na binadamu mpaka church
Kufika pale watu wamefurika Hata Kwa kukaa shida basi tukapata siti pale kibishi tulikuta wanaita kusifu na kuabudu kumeanza,
Baasi mchungaji akaingia akafungua ibada ya kukemea mapepo pale ila nikaona wanawake ndio wengi Sana wenye frustration zao wakianguka na kugala gala chini nikawa nazoom tu ule usanii
Mchungaji akaita hivyo holly spirit kwangu sikuona connection yoyote zaidi ya michosho tu
Basi Sasa kumbe mjomba Ile kunipeleka kwenye Lile kanisa lao alijua sijui nitakua na mapepo maaana binamu ndio alinifunulia Siri kusema eti kisa nimetoka Kwa bibi kijijini na bibi yangu namjua ana practice Sana tamaduni basi ankori akajua nitalipuka mapepooo niliyotoka nayo bush



Na ndio maana church alimwambia binamu akae karibu yangu maana lazima nitaanguka tu
Kile kitendo Cha Mimi kutoanguka na kua normal kama hakuna kitu limetokea kilimuudhi na kumdisapoint Ankori na kumkata mood Sana
Sasa Mimi nilivyogundua hivyo kesho yake jumapili tukaenda ibada kuu Ili nimuoneshe Mimi ni Mtu wa aina Gani ulivyofika Muda wa kumpandisha Roho mtakatifu nikasimama niki act kukemea mapepo Kwa Nguvu huku natembea tembea napishana nae nikimzoom naona ananiangalia na kupigwa na butwaa Sana
Tulivyo Rudi home akasema nimeona umempokea Roho mtakatifu mpaka unanena Kwa Lugha daa nimeshangaa nikamjibu aaaagh Mimi mbona niliokoka kitambo Sana na kule home nilipokua shule nilikua kiongozi wa maombi
Zote hizo zilikua ni fix na usaniitupu mpaka Leo anajua hivyo kunihusu ila ukweli naujua Mimi!
Covax





