Calculus problem solved using several different (alternative) methods

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,247
2,000
calculus ni nini?
Ni njia mojawapo ya kimahesabu inayotumia mbinu za integration (kuunganisha vilivyo vidogo vidogo na kuviweka pamoja na kupata kitukomojakikubwa) pamoja na differentiation (kinyume cha integration) katika kutatua matatizo ya kila siku ya mwanadamu.

Kwa mfano, mtu akipoteza mkono kwa bahati mbaya, anaweza akatengenezewa mwingine wa kuwa unafanya kazi wenyewe kama ule wa roboti. Kwa kifupi, haya mahesbau ndiyo yamewezesha hata roboti zikawepo na hivyo kurahisisha kazi za viwandani kama vile uunganishaji wa magari n.k.

Hesabu hizi pia zina matumizi mengine mengi tu hata kwenye uchumi, namna ya kupanga bei, kama wewe ni muuzaji ili uweze kupata faida na siyo hasara, au namna ya kununua bidhaa ili ukauze na kupata faida kubwa n.k. Ni mahesabu yanayotumika katika kumuwezesha mwanadamu aweze kufanya mambo kwa uhakika zaidi na kwa faida kubwa zaidi.

Zaidi ni kuwa katika biashara kwa mfano, ili uweze kujua faida ndogo kabisa kutokana na bidhaa zako ulizonazo kwenye stock au faida kubwa zaidi, unahitaji mahesabu ya aina hii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom