CAG Zanzibar aomba radhi kwa kulidharau Baraza la Wawakilishi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Zanzibar, Dkt. Othman Ali ameliomba radhi Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kusamehewa kufuatia kauli yake aliyoitoa ambayo ilionekana kuwabeza wajumbe wa baraza hilo.

Hivi karibuni wakati akiwakilisha ripoti ya CAG mwaka 2022/23, Dkt. Othman alinukuliwa akisema kamati za ukaguzi za baraza hilo hazina uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Pia soma > Zanzibar kazi ipo: CAG awajibu wawakilishi waliomtaka aombe radhi

---
Wiki moja baada ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Zanzibar, Dk Othman Abbas Ali kuliomba radhi kutokana na kauli yake kwamba halina uwezo, hatimaye ametekeleza agizo hilo.

Katika mkutano wa leo Jumatatu Juni 12, 2023 Spika wa Baraza hilo, Zubeir Ali Maulid baada ya kipindi cha maswali na majibu ameeleza kwamba tayari CAG amekiri kuwa kauli yake ilileta taharuki kwa hiyo anakiri kwamba alikosea.

"CAG amekiri kuwa maneno yake yameleta tafsiri mbaya hivyo amemuomba radhi mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, Kamati ya PAC na Kamati ya LAAC (Kamati za Kudhibiti Hesabu za Serikali) na waheshimiwa wajumbe wote wa baraza hili kwa ujumla," amesema Spika Zubeir huku wawakilishi wakigonga meza kama ishara ya kupongeza.

Spika Zubeir amesema kutokana na kitendo hicho alichokifanya CAG kufika katika ofisi za Spika na kutoa maelezo ya kuomba radhi kwa baraza, imemfanya (spika) akubaliane naye na ameridhishwa kutoa mwongozo wake kama alivyoombwa.

Baada ya kutoa mwongozo huo, Spika Maulid amesema kwa kuzingatia kanuni ya 64 (6) ya kanuni ya Baraza la Wawakilishi baada ya kutoa mwongozo huo aliagiza kusitisha mjadala wowote ndani na nje ya Baraza la Wawakilishi.

"Mjadala huu umefungwa itoshe tu kwa baraza hili kupokea taarifa ya CAG ya kuomba radhi na wajumbe mlichukue na kulipokea kama kilivyo," amesema.

Hatua hiyo ya kuomba radhi ilikuja baada ya wajumbe hao katika mkutano wa baraza hilo Juni 5, 2023 kuomba muongozo wa Spika wakimtaka CAG ombe radhi baraza lake tukufu kwa kuwaita wajumbe wake hawana uwezo.

Mwongozo huo uliombwa na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Juma Ali Khatib aliyesema CAG alitoa kauli zinazoonesha kulibeza na kulidharau baraza hilo tukufu hasa kupitia kamati zake kwamba hazina uwezo wa kufanyia kazi ripoti zake ikiwemo ripoti ya Tehama wakati CAG Abbas alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2021/22 Mei 3, 2023 Ikulu Zanzibar.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu itakuwa kuna watu wamemuweka chini na kumwambia kwamba haina tija kwake kubishana na watu wajinga najua radhi yake siyo ya dhati ila kwakuwa jamaa wanapenda sifa na kujikweza watu wamemshauri afunike kombe mwana haramu apite na mipenda sifa imejiona ni washindi.
 
CAG wa Zanzibar Dr Othman Ali ameliomba radhi Bunge la Nchi hiyo( BLW) kufuatia kauli yake ya awali kuleta mtafaruku

Spika wa Bunge la Zanzibar amelitaarifu Bunge kwamba CAG amekiri kufanya makosa na ameomba radhi

CAG alidai kuwa Bunge hilo halina Uwezo kauli iliyowauzi Wabunge hao
 
Source Mwananchi
alisemaje?
 
Hata mwanasheria mkuu Zanzibar aliomba radhi lakini alifukuzwa,Ndugai aliomba radhi lakini alifukuzwa
 
Bandari zetu zirudishwe
Huna pesa ya kununua hata kipakulia kontena bandarini kwako, ndiyo utakua na pesa ya kuvunja Mkataba ulio signiwa Dubai!!? Ukiimbiwa hizo gharama za kuvunja Mkataba ili Bandari irudi si utakufa ghafla na kisonono!!
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Zanzibar, Dkt. Othman Ali ameliomba radhi Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kusamehewa kufuatia kauli yake aliyoitoa ambayo ilionekana kuwabeza wajumbe wa baraza hilo.

Hivi karibuni wakati akiwakilisha ripoti ya CAG mwaka 2022/23, Dkt. Othman alinukuliwa akisema kamati za ukaguzi za baraza hilo hazina uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Pia soma > Zanzibar kazi ipo: CAG awajibu wawakilishi waliomtaka aombe radhi

---
Wiki moja baada ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Zanzibar, Dk Othman Abbas Ali kuliomba radhi kutokana na kauli yake kwamba halina uwezo, hatimaye ametekeleza agizo hilo.

Katika mkutano wa leo Jumatatu Juni 12, 2023 Spika wa Baraza hilo, Zubeir Ali Maulid baada ya kipindi cha maswali na majibu ameeleza kwamba tayari CAG amekiri kuwa kauli yake ilileta taharuki kwa hiyo anakiri kwamba alikosea.

"CAG amekiri kuwa maneno yake yameleta tafsiri mbaya hivyo amemuomba radhi mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, Kamati ya PAC na Kamati ya LAAC (Kamati za Kudhibiti Hesabu za Serikali) na waheshimiwa wajumbe wote wa baraza hili kwa ujumla," amesema Spika Zubeir huku wawakilishi wakigonga meza kama ishara ya kupongeza.

Spika Zubeir amesema kutokana na kitendo hicho alichokifanya CAG kufika katika ofisi za Spika na kutoa maelezo ya kuomba radhi kwa baraza, imemfanya (spika) akubaliane naye na ameridhishwa kutoa mwongozo wake kama alivyoombwa.

Baada ya kutoa mwongozo huo, Spika Maulid amesema kwa kuzingatia kanuni ya 64 (6) ya kanuni ya Baraza la Wawakilishi baada ya kutoa mwongozo huo aliagiza kusitisha mjadala wowote ndani na nje ya Baraza la Wawakilishi.

"Mjadala huu umefungwa itoshe tu kwa baraza hili kupokea taarifa ya CAG ya kuomba radhi na wajumbe mlichukue na kulipokea kama kilivyo," amesema.

Hatua hiyo ya kuomba radhi ilikuja baada ya wajumbe hao katika mkutano wa baraza hilo Juni 5, 2023 kuomba muongozo wa Spika wakimtaka CAG ombe radhi baraza lake tukufu kwa kuwaita wajumbe wake hawana uwezo.

Mwongozo huo uliombwa na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Juma Ali Khatib aliyesema CAG alitoa kauli zinazoonesha kulibeza na kulidharau baraza hilo tukufu hasa kupitia kamati zake kwamba hazina uwezo wa kufanyia kazi ripoti zake ikiwemo ripoti ya Tehama wakati CAG Abbas alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2021/22 Mei 3, 2023 Ikulu Zanzibar.

Chanzo: Mwananchi
Pamoja na kuomba radhi lakini ujumbe umefika
 
Back
Top Bottom